Dr. Ulimboka apelekwa nje kwa matibabu zaidi...

Hakukuwa na haja ya kuanzisha uzi kwa swala dogo kama hilo, bila shaka ukisoma maantiki ya uzi wangu utaona sikuwa eneo la tukio bali nilipewa taarifa tu,

Na kama ijulikanavyo kimang'amuzi, taarifa ya kupewa hubadilika kadri inavyosafiri umbali/idadi ya watu!

Mazingira ya safari ya matibabu ya Dr Ulimboka nayo yalichangia usiri wa wapi anakwenda kutibiwa, maana madokezo ya serikali yalikuwa India huku madaktari wakiwa na siri yao ya Afrika kusini!

Nilipopewa taarifa na chanzo changu kilinieleza kuwa ni India!

Nadhani mapaka hapo umenielewa ndugu, hivyo nawaomba mods iondoeni hii thread haina mafaa kwa nchi,jf na wanajf kwa ujumla!



Yericko Nyerere!
Ninakukubali katika thread zako & post zako Kamanda wetu!
Nami nimeisoma vizuri sana kabla ya kugandisha uzi huu Kamanda wangu!

Na hata mwishoni mwa thread nimependa sana usielewe tofauti Kamanda wangu kwn ni sehemu tu ya marekebisho yetu jukwaani!

Hata Mi mwenyewe ninaelewa haupendi pale unapofungu thread halafu member wa kurekebishwa ikawa ni wewe mwenyewe.
Pole sana Kamanda wetu na usielewe vingine kwani tunajenga pamoja.

Na hilo ktk aya ya mwisho la kumtaka Mods waiondoshe uzi huu Mi siiafiki maana wakati mwingine utakuwa makini sana kufuatilia yaliyojiri na hata kuedit ikiwezekana Kamanda wetu!


Pamoja sana!


Uwe na wakati mzuri!
 
Yes, people have eyes and you are bloody blind! Wait and I mean wait, you will soon be able to see. In the unlikely event that you do not happen to see, I strongly recommend that you fly to India and get your eyes checked. I like your use of words 'giant' soma ka historia ka karibuni Libya, Misri... walijiita ma 'giant' Unatia kichefuchefu wewe!
 
Taarifa zilizonifikia hivi punde kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa JK Nyerere Dar, nikuwa kiongozi wa madaktari aliyetekwa na kujeruhiwa na watu wanaohisiwa kwa 99.5% kwa ni serikali (TISS) nikuwa anapelekwa nchini India kwa matibabu

Kuna sehemu nimesoma wameandika kapelekwa Afrika Kusini. Which is which now?
 
Aliyekanusha,ana logic.Coz tungejua yuko Indian kumbe yuko South.Au India ndo South?Tunashkur kw kutujuza Wakuu
 
Y.nyerere alikurupuka kuleta Habari za kusikia tu.. bila kuzithibitisha.. now swallow ur pride and admit.ulikosea..
 
My dog! Huu uandishi unatupa shida kweli.


Hivi kwa nini kila mtu na kaugonjwa kake lazima apelekwe India?

kaugonjwa? Kidney failure si kaugonjwa

Hawa madokta waliogoma wameshindwa kweli kumsaidia mwenzao?

Hawajashindwa hawana vifaa.


na kama wameshindwa kumtibu mtu aliyejeruhiwa na kipigo, kuna haki gani kwao kugoma kama matatizo kama hayo tu lazima watu wapelekwe nje ya nchi.

Hapo sijakuelewa sijui una maana gani.


Ni wakati sasa sisi wananchi tuanze kuuliza hawa madokta wetu wanatibu nini sasa kama kila mtu mwenye kauwezo kidogo tu, anaenda India.

Talk for yourself the rest of us know.

Tuliwasomesha ili watusaidie na kama wako kwenye mgomo sasa ina maana hawako busy ya vile,

Tatizo la lugha na pengine sarufi.


basi wamtibu mwenzao kuonyesha uwezo wao na ili kuhalalisha waongezewe posho, kwa nini apelekwe nje?

Upeo wako mdogo sana unasikia hoja zikitolewa lakini hata huelewi maana yake.
Hata mpika chipsi mashuhuri anahitaji vifaa ili apike chipsi zake.
Ukimpa Viazi,kikaango, kijiko, mkaa -kuni au gesi ukashindwa kumpa mafuta na chumvi badala yake ukampa maji na sukari hata ajitahidi vipi hawezi kukaanga chipsi zikawa chipsi.
kila shughuli inahitaji vifaa ufundi pekee bila vifaa ni lawama tu.

 
Nakubaliana na wewe. Tumuombee Mungu apone arudi kuwatibu hao aliowaacha hoi katika mgomo aliouanzisha ..."ikiwa atawakuta bado wako hai....! Hypocrisy ...
Mshahara + Mazingira ya kazi havirizishi. Madaktari wamegoma just like you would expect workers to do. What is the government doing? Does it care?
 
Go safe doctor and come back alive and healthy!we are continuing the sruggle, Aluta continua!!
 
Dk Ulimboka alisafirishwa kwa gari la kubebea wagonjwa la kampuni ya AAR. Alipofika uwanjani, alisafirishwa kwa ndege ya kukodi ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini, akisindikizwa na watu watatu.

DK Ulimboka akiongea kwa shida kuelezea ilikuwaje.mov - YouTube





Dk Chitega alisema hadi kufikia jana, walikuwa wamepata fedha zilizokuwa zikihitajika kwa ajili ya matibabu yake. Juzi madaktari hao walisema wanahitaji Dola za Marekani 40,000 (Sh63.2 milioni) ili kumtibu mwenzao nje ya nchi.:peep:
 

Attachments

  • Dk.Ulimboka.jpg
    Dk.Ulimboka.jpg
    61.3 KB · Views: 33
Je akikuta huko alikopelekwa nako kuna akina Dr. Ulimboka wa huko wanaendesha mgomo. Mbona hajawakumbuka Watz waliokosa huduma hospitali hapa Tz kutokana na mgomo.
 
vitendea kazi hakuna kaka hata vipimo muhimu hakuna na ndio msingi mkuu wa mgomo kuwa mazingira ya kazi yaboreshwe na vipimo vingi ambavyo ndio vinatupeleka india bei yake ni sawa na land cruser V8;kama la nape na chemba...
hilo ndio dai nambari 1 ktk mgomo “ wanahitaji supana za kufanyia kazi”” injini wanaweza kutengeneza vizuri sana kuliko nje ya nchi tatizo supana za kufungulia na kuchunguzia injini, au unataka wafungue na meno???
k
 
Hofu yangu, baada ya Dr. Ulimboka kupigwa, kulikuwa na uzi uliwekwa hapa jukwaani kuwa mmojawapo wa waliohusika katika kumtesa, alikuwa ni jamaa wa TISS na mmojawao alitoroshwa kwenda Afrika Kusini ambapo atapangiwa kazi maalum.

Sasa leo Dr. Ulimboka anapelekwa huko tena si ndo wanarahisisha namna ya kummaliza haraka. Kwani aliyependekeza kuwa Dr. Ulimboka apelekwe SA ni nani?

Serikali au madaktari wenyewe, hapo sina ujuzi wowote. Lakini ni hofu yangu tuu.
 
vitendea kazi hakuna kaka hata vipimo muhimu hakuna na ndio msingi mkuu wa mgomo kuwa mazingira ya kazi yaboreshwe na vipimo vingi ambavyo ndio vinatupeleka india bei yake ni sawa na land cruser V8;kama la nape na chemba...
hilo ndio dai nambari 1 ktk mgomo “ wanahitaji supana za kufanyia kazi”” injini wanaweza kutengeneza vizuri sana kuliko nje ya nchi tatizo supana za kufungulia na kuchunguzia injini, au unataka wafungue na meno???
k

sembuli; Night Allowances, Call Allowance na Ongezeko la Mishahara to 3.5M
Then yanakuja
 
Last edited by a moderator:
vitendea kazi hakuna kaka hata vipimo muhimu hakuna na ndio msingi mkuu wa mgomo kuwa mazingira ya kazi yaboreshwe na vipimo vingi ambavyo ndio vinatupeleka india bei yake ni sawa na land cruser V8;kama la nape na chemba...
hilo ndio dai nambari 1 ktk mgomo “ wanahitaji supana za kufanyia kazi”” injini wanaweza kutengeneza vizuri sana kuliko nje ya nchi tatizo supana za kufungulia na kuchunguzia injini, au unataka wafungue na meno???
k

sembuli; Night Allowances, Call Allowance na Ongezeko la Mishahara to 3.5M
Then yanakuja hayo ya vitendea kazi
 
Last edited by a moderator:
Naamini katika nguvu ya umma, wembe ni ule ule, Madaktari mtakaoandamana naye chonde chonde ulinzi kwa kipenzi chetu Dr. Ulimboka uwe kama wa siafu, wasipungue watu kando yake.

Majangili/Majasusi hayana mpaka yanaweza kufika mpaka huko. Najua mnajua jukumu lenu, tunakumbushana tu wapendwa mfike salama, Mungu aliye muumba Dr. Ulimboka na sisi wote awatangulie.

Sisi tupo nyuma yenu kwa sala na dua. Amina.
 
Hadha Min Fadhil Rhabi.

Lakini hatuna imani na Madaktari watakaomuhudumia huko nje ya nchi maana wanaweza kupewa maagizo na TISS wasimtibu vizuri ili afie huko na hatimae kupoteza ushahidi wa tuhuma za mauaji zinazowang'ang'ania!
Umechanganya madawa hapa mkuu,
"ushahidi wa tuhuma za mauaji"? ama ni "ushahidi wa tuhuma za jaribio la mauaji"?

TISS hawawezi kupoteza ushahidi wa tuhuma za mauwaji kwasababu Dr. anaenda huko akiwa mzima, fanya marekebisho.
 
Back
Top Bottom