Dr. Ulimboka apelekwa nje kwa matibabu zaidi...

Hivi kwa nini kila mtu na kaugonjwa kake lazima apelekwe India? Hawa madokta waliogoma wameshindwa kweli kumsaidia mwenzao? na kama wameshindwa kumtibu mtu aliyejeruhiwa na kipigo, kuna haki gani kwao kugoma kama matatizo kama hayo tu lazima watu wapelekwe nje ya nchi. Ni wakati sasa sisi wananchi tuanze kuuliza hawa madokta wetu wanatibu nini sasa kama kila mtu mwenye kauwezo kidogo tu, anaenda India. Tuliwasomesha ili watusaidie na kama wako kwenye mgomo sasa ina maana hawako busy ya vile, basi wamtibu mwenzao kuonyesha uwezo wao na ili kuhalalisha waongezewe posho, kwa nini apelekwe nje?

Hapo kwenye red jibu ni rahisi sana. Ujuzi wanao lakini vifaa hawana. Nafikiri ni sehemu ya madai yao pia. Labda tupitie kwa umakini madai yao kabla hatujaanza kuwashutumu. Mbona mara nyingi tu watu wanaenda hospitali wanaambiwa unahitaji operesheni fulani lakini hapa nchini vifaa hivyo havipo au havifanyi kazi kwahiyo ni lazima kwenda nje.
 
Hivi kwa nini kila mtu na kaugonjwa kake lazima apelekwe India? Hawa madokta waliogoma wameshindwa kweli kumsaidia mwenzao? na kama wameshindwa kumtibu mtu aliyejeruhiwa na kipigo, kuna haki gani kwao kugoma kama matatizo kama hayo tu lazima watu wapelekwe nje ya nchi. Ni wakati sasa sisi wananchi tuanze kuuliza hawa madokta wetu wanatibu nini sasa kama kila mtu mwenye kauwezo kidogo tu, anaenda India. Tuliwasomesha ili watusaidie na kama wako kwenye mgomo sasa ina maana hawako busy ya vile, basi wamtibu mwenzao kuonyesha uwezo wao na ili kuhalalisha waongezewe posho, kwa nini apelekwe nje?

Sijajua elimu yako na ufahamu wako
Imesemwa mara zote hakuna vifaa tiba MNH na hospitali karibu zote nchini, ndiyo maana inalazimka kumpeleka nje
 
Dah, soo sad! Hii leo imenitoa machozi! Get Well Soon Man. Mungu anakupenda daima!
For security reasons ilikuwa lazima ukatibiwe nje kwani kuanzia jumatatu kinanuka! Mungu awatangulie wadai haki wote!
 
Namfahamu aliyefuta post yangu we Wacha tu na mimi nitawakodi askari kanzu wanaowashughulikia watu, si wanataka mpunga tu .. .... ..... .... *khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

BTW tutarudi kwenye sport very soon.
 
Nakubaliana na wewe. Tumuombee Mungu apone arudi kuwatibu hao aliowaacha hoi katika mgomo aliouanzisha ..."ikiwa atawakuta bado wako hai....! Hypocrisy ...
 
Mungu endelea kunyoosha mkono wako wa haki na uendelee kutenda maajabu kwa tunayoyashuhudia kwa Dr.Ulimboka.
 
siasa ikijaa mioyoni mwa wataalamu matokeo yake ndo haya! people do hate CCM. ......after failling to ouster from power they try every way round to make sure the giant falls
Bad enough some cut their own hands thinking by doing that the giant will fall (MAJIMAJI WAR IDEA)
They kill their own voters and innocent to create bad image of the giant......forgeting that PEOPLE DO HAVE EYES
 
Aliripoti ktk post ya tatu ama ya nne jana mchana kuhusu Dr Ulimboka:

Namnukuu:

Yericko Nyerere:
(Taarifa zilizonifikia hivi punde toka uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jk Nyerere ni kuwa kiongozi wa madaktari aliyetekwa na kujeruhiwa na watu wanaohusishwa kwa 99.5% kuwa ni (TISS) nikuwa anapelekwa Nchi India kwa matibabu:) MWISHO WA KUMNUKUU.

Habari nilizozipata kupitia mitandao kadha ni kwamba Dk Steven Ulimboka amepelekwa Nchi South Africa kwa matibabu zaidi hasa ya ubongo.

Na hakika MUNGU ni mkubwa kwani ameshafika S/Africa salama salimin.

Na nimependa tu nimerekebishe huyu Member wetu na asinielewe vibaya.
 
So Mods plz, ni mwamini nani ni nani wananigeukia vigeugeu............:noidea::noidea:
 
Hakukuwa na haja ya kuanzisha uzi kwa swala dogo kama hilo, bila shaka ukisoma maantiki ya uzi wangu utaona sikuwa eneo la tukio bali nilipewa taarifa tu,

Na kama ijulikanavyo kimang'amuzi, taarifa ya kupewa hubadilika kadri inavyosafiri umbali/idadi ya watu!

Mazingira ya safari ya matibabu ya Dr Ulimboka nayo yalichangia usiri wa wapi anakwenda kutibiwa, maana madokezo ya serikali yalikuwa India huku madaktari wakiwa na siri yao ya Afrika kusini!

Nilipopewa taarifa na chanzo changu kilinieleza kuwa ni India!

Nadhani mapaka hapo umenielewa ndugu, hivyo nawaomba mods iondoeni hii thread haina mafaa kwa nchi,jf na wanajf kwa ujumla!
 
Huna nidhamu kbs. Hv unajua maana ya kudai haki? Mgomo wa madaktari unahusianaje na Chadema kama si prejudice zako tu! Waza km aliyeenda shule bhana.

Tuwasamehe sana hawa wanaotoa mawazo yasiyo na vichwa wala miguu - mawazo viwiliwili. Tukumbuke hata hawa viongozi wetu wadhaifu wamekwenda shule tena kwa pesa za mlala hoi Mtanzania; tukawaamini na kuwachagua watuongoze, badala yake angalia wanayotufanyia. Tatizo kubwa ni kwamba hawa wote wanapungukiwa na hekima na wataendelea kutuchelewesha kuikomboa nchi yetu. Tuwe na uvumilivu na kuwaelimisha taratibu ili wasiwe wepesi wa kudanganyika na kushindwa kutumia akili ya kuzaliwa. Dr Ulimboka tunakuombea na tunawaombea ndugu zako wa karibu na madaktari wetu wapendwa wanaoipenda nchi yao. Mungu ibariki Tanzania na tubariki wote wenye nia njema na hii nchi ili siku moja tuikomboe. Tunakuomba ee BABA uilete karibu siku hii ya ukombozi.
 
Back
Top Bottom