Dr. Slaa, Mbowe waweka historia Kilombero!

Ndiyo majibu yenu, hamna sera tena. Nchi haItatawalika kwa majungu, fitina na uzushi kweli? Subiri ZITTO achukue nchi 2015 kama u-chagga utakuwemo tena ndani ya CDM na majungu yenu hayo.

ukiona mtu anazungumzia ukabila kwenye urais anatatizo kwenye elimu aliyopata au hajawahi kutoka kijijini kwao akakutana na watanzania na walimwengu wengine mimi sijali rais mchagga, muha, msukuma, msandawe, mhazabe ninataka raisi atakayeweza kusimamia rasilimali za nchi ipasavyo kutuondolea umaskini huu unaonuka,. kama ni Zitto, well, kama slaa well hata kama ni wewe fine tupate mtu wa kutunasua hapa kwani makabila wanayotoka Nyerere, Mwinyi,Mkapa na Kikwete yana unafuu gani kuliko makabila ambayo hayajawahi kutoa rais?Tatizo sio rais tatizo ni mfumo, ondoa tongotongo za ukabila na udini angalia utaifa kwa upana wake!
 
Huyu jamaa haimwenei kabisa, tunamjua lema, ni kamanda wa ukweli, Arusha adabu tele ameifanya, ibadilike kimtazamo na kifikra-------Long live CHADEMA, long live COMMANDER LEMA

Zitto atakujaje kwenye movement for chaggaz(m4c)kwani ye mchagga?hauoni wameenda viongoz wakaskazini pekee?slaa na mbowe!macho huoni hata kusikia hausikii ?zitto kamanda wa ukweli siasa kwake ni maisha sio kama hao chaggaz wanafanya siasa za dharura,na kugeuza chama saccos!slaa kwishney sasaivi,na nchi hatuwezi mpa mchagga,so the answer for 2015 is ZZK.kaza buti powertiller zitto we are with you!
 
Wewe si umeolewa huko Kaskazini, sina haja ya kujua ulichokiandika.

Dume la kuoa liolewe?. Labda wewe kakuoa mr Dhaifu. Hoja hiyo imekushinda,basi jibu hii:-KWANINI ccm ILIMLISHA SUMU Dr Mwakyembe na KUZIKA MISALABA KULE SUMBAWANGA 2010?.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA kimeacha historia ambayo ni vigumu kufutika katika uzinduzi wa operesheni Sangara kanda ya kati uliofanyika Ifakara-Kilombero jana.

Katika mkutano huo ulikusanyika umati mkubwa kuwahi kushuhudiwa katika wilaya hiyo kwa miaka ya karibuni.

Akihutubia maelfu kwa maelfu ya wananchi katika mkutano huo jana, ikiwa ni sehemu ya Operesheni Sangara awamu ya pili, Kiongozi mkuu wa upinzani nchini ambaye pia ni Katibu mkuu wa CHADEMA Dk.Wilbroad Slaa aliyeambatana na viongozi wakuu wa chama hicho, akiwemo Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe, alisema kuwa Serikali ya CCM imekuwa na kiburi cha kuwatisha wanaotaka kutetea maslahi ya wananchi huku ikifungia hata vyombo vya habari kama Mwanahalisi.

“Serikali ina nguvu ya kuvifungia vyombo vya habari kwa sheria dhalimu ya magazeti ya mwaka 1977, lakini kamwe haitaweza kuzuia kina Dr Slaa kupiga kelele'' alisema kiongozi huyo. Dk. Slaa ambaye alikuwa akishangiliwa kwa nguvu na halaiki hiyo huku anga likihanikizwa kwa kelele za RAIS....RAIS...RAIS...., aliongeza kuwa, kuanzia sasa CHADEMA itaanzisha mapambano kwa ajili ya haki ya Watanzania.

Akizungumza katika mkutano huo, Mbowe alisema umati uliokusanyika unaonesha namna wakazi wa Kilombero walivyomthamini aliyekuwa mbunge wa viti maalumu, marehemu Regia Mtema.

Mbowe aliomba jina la uwanja wa Ifakara libadilishwe na kuitwa Uwanja wa Ukombozi, na kwamba hali hiyo iwe chimbuko la ukombozi kwa Mkoa wa Morogoro.
Aliwataka wakazi wa Kilombero kuacha kulalamika na badala yake wachukue hatua kwa kuachana na CCM na kujinga na CHADEMA.

Katika mkutano huo maelfu ya wananchi walijiunga na CHADEMA wengi wao wakiwa ni kutoka CCM.Mara baada ya mkutano huo baadhi ya watu walionekana wakifuta machozi huku wakisema wanaamini bado siku chache tu CHADEMA kuingia madarakani na kukomboa watanzania kiuchumi.

Mbali na Dk. Slaa na Mbowe, viongozi wengine waliokuwa katika msafara huo ni Joshua Nassar (Arumeru Mashariki), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Hamad Yusuph (Naibu Katibu Mkuu Zanzibar), Suzan Kiwanga (Viti Maalumu), Joyce Mukya (Viti Maalumu) na wengine wa makao makuu.

Source: Majira/Tanzania Daima/Nipashe

attachment.php


attachment.php

attachment.php

Lazima waende kuwashangaa kwa mbwembwe zao ambazo hazina vitendo.
 
Lazima waende kuwashangaa kwa mbwembwe zao ambazo hazina vitendo.

Jibu maswali haya: 1.Kwanini ccm ilimlisha sumu Dr Mwakyembe? 2.Kwanini ccm iliizika misalaba Sumbawanga 2010? 3.Kwanini ccm inachoma makanisa Znz na kuwasingizia Uamsho wanaojitafutia Uhuru wa nchi yao?. 4.Kwanini Alhaji Mrisho(ccm)-SULEIMAN-AHMED-RAMADHAN-ABDALLAH=kutekwa Dr STEVEN?.
 
Molemo akili yako finyu sana hivi Kilombero ina wakazi wangapi mpaka iweke historia ambayo haiwezi kufutika katika Taifa ambalo linawakazi takribani mil. 40? historia ambayo haiwezi kufutika ni Dr. Slaa na wenzake kuigeuza Chadema saccos mkumbushe deni alilikopa saccos linatkiwa lilipwe.

Chama
Gongo la mboto DSM
Hivi kauli ya kusema CCM dhaifu haimaanishi kuwa "wanachama na wafuasi wake ni dhaifu vile vile"?
 
[Tuntemeke mwingine]Molemo akili yako finyu sana hivi Kilombero ina wakazi wangapi mpaka iweke historia ambayo haiwezi kufutika katika Taifa ambalo linawakazi takribani mil. 40? historia ambayo haiwezi kufutika ni Dr. Slaa na wenzake kuigeuza Chadema saccos mkumbushe deni alilikopa saccos linatkiwa lilipwe.

Chama
Gongo la mboto DSM
[/QUOTE]

mkuu mbona unatoa machozi sana!
 
Molemo akili yako finyu sana hivi Kilombero ina wakazi wangapi mpaka iweke historia ambayo haiwezi kufutika katika Taifa ambalo linawakazi takribani mil. 40?
Chama
Gongo la mboto DSM

Wacha ujuha wewe jamaa kasema hivi:
Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA kimeacha historia ambayo ni vigumu kufutika katika uzinduzi wa operesheni Sangara kanda ya kati uliofanyika Ifakara-Kilombero jana.

Wewe endelea tu kutumia kichwa chako kufugia nywele
 
Wacha ujuha wewe jamaa kasema hivi:
Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA kimeacha historia ambayo ni vigumu kufutika katika uzinduzi wa operesheni Sangara kanda ya kati uliofanyika Ifakara-Kilombero jana.

Wewe endelea tu kutumia kichwa chako kufugia nywele

wewe pimbi umechelewa kwenye mjadala wenzako wamekimbia

Chama
Gongo la mboto DSM
 
mkuu ni wote kama mwenyekiti ni dhaifu basi kachaguliwa na wanachama dhaifu!
wajinga wanachaguana!

Kuna dhaifu mmoja anadai kutojua msingi wa hoja ya yangu. Nashukuru kwa ufafanuzi huu. Ujumbe umefika kwa mhusika.
 
Umeuliza swali au unataka ufafanuzi?

Chama
Gongo la mboto DSM
Akili ni nywele japo haimaanishi kuwa kila mwenye nywele anatumia vizuri nywele zake. Kama unazitumia vizuri ungeweza kujua kama ni swali au jibu. Hata darasa la kwanza wanajua kiashiria cha swali ni nini. Nakutakia Kazi njema ya kutumika.
 
Akili ni nywele japo haimaanishi kuwa kila mwenye nywele anatumia vizuri nywele zake. Kama unazitumia vizuri ungeweza kujua kama ni swali au jibu. Hata darasa la kwanza wanajua kiashiria cha swali ni nini. Nakutakia Kazi njema ya kutumika.

Kama hoja unaye dhaifu wa kiroho Dr. Slaa, CCM nguvu moja tu !

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Back
Top Bottom