DC Kyobya wa Kilombero ashauri Kituo Kipya Cha Umeme kuitwa "Samia Ifakara Substation"

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,064
49,751
DC Kyobya Dunstan wa Kilombero ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Kituo hicho kipya na kuwasha umeme Ifakara.

Kituo hicho kilichogharimu Bilioni 25 ni maalumu Kwa Ajili ya kuleta umeme mkubwa wa uhakika kwenye Wilaya 3 na kuchochea shughuli za Viwanda vya Kilimo.

Hongera Serikali ya awamu ya 6,Kazi iendelee

=====
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) imewasha Kituo cha Kupoza na Kusambaza Umeme cha Ifakara ambacho kimegharimu shilling bilioni 25.

Akiwasha kituo hicho ambacho kimelenga kuongeza uwekezaji na uanzishaji wa viwanda kwa upatikanaji wa umeme wa uhakika, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Dunstan Kyobya ameshauri kituo hicho kiitwe Samia Ifakara Substation.

Ameipongeza REA na EU kwa kuhakikisha kituo kimekamilika na kuwashwa kwani kinaenda kumaliza matatizo ya umeme katika wilaya ya Kilombero, Malinyi na Ulanga ambayo ni maeneo ya kimkakati ya kilimo na viwanda.

“Tunategemea kuongeza uwekezaji kwa kuanzisha viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo na vile vya kuchakata madini” amesema Kyobya.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Jones Olotu amesema kuwashwa kwa kituo hicho kunaongeza upatikanaji wa umeme na hivyo kuwawezesha wananchi kukuza na kuboresha hali zao za kiuchumi kwa kufungua biashara mbalimbali kwa uwepo wa umeme wa uhakika katika maeneo hayo.

Naye Mbunge wa Kilombero, Aboubakar Asenga amewataka wananchi wa Jimbo hilo kuchangamkia fursa ya upatikanaji wa umeme mkubwa kwa kuzalisha kwa wingi na kuanzisha viwanda vikubwa kama vya kukausha na kukoboa mpunga ili kuongeza thamani zao hilo linalolimwa kwa wingi katika eneo hilo.

Meneja wa Mradi huo kutoka REA, Mhandisi Romanus Lwena amesema ujenzi wa kituo hicho ulianza 2020 ambapo kinazalisha kV 220 za umeme baada ya wananchi wa maeneo hayo kuwa wanapata umeme mdogo wa kV 33 uliokuwa unasababisha kukatika mara kwa mara.

Meneja Miradi ya Nishati wa EU, Mhandisi Francis Songela amesema kituo hicho kipo katika eneo la kimkakati la Mpango wa Kukuza Kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania , SAGCOT ambapo Mradi huo unaenda kuleta mapinduzi ya kilimo na viwanda.

View: https://youtu.be/Nnv80pGEd0k?si=5UvuY13s8LSkmnVr
 
Naunga mkono hoja kwa asilimia zote kabisa ,maana Rais wetu mpendwa anastahili kabisa kutokana na juhudi zake kubwa ambazo amekuwa akizifanya usiku na mchana kuhakikisha kuwa Taifa linakuwa na mwanga muda wote na wananchi wanaendelea na shughuli zao pasipo kikwazo cha aina yoyote ile.
 
Siungi mkono Kwa kuwa kituo hicho ni kidogo sana, utafutwe mradi mkubwa wenye sura ya Nchi uitwe jina lake.
Mfano: "Samia Muungano Bridge"' /au "The tunnel of Samia" (kama ni Barabara chini ya bahari)
(Kuunganisha Zanzibar na Tanganyika)
 
Naunga mkono hoja kwa asilimia zote kabisa ,maana Rais wetu mpendwa anastahili kabisa kutokana na juhudi zake kubwa ambazo amekuwa akizifanya usiku na mchana kuhakikisha kuwa Taifa linakuwa na mwanga muda wote na wananchi wanaendelea na shughuli zao pasipo kikwazo cha aina yoyote ile.
Promax
 
Back
Top Bottom