Dr. Slaa, Mbowe waweka historia Kilombero!

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA kimeacha historia ambayo ni vigumu kufutika katika uzinduzi wa operesheni Sangara kanda ya kati uliofanyika Ifakara-Kilombero jana.

Katika mkutano huo ulikusanyika umati mkubwa kuwahi kushuhudiwa katika wilaya hiyo kwa miaka ya karibuni.

Akihutubia maelfu kwa maelfu ya wananchi katika mkutano huo jana, ikiwa ni sehemu ya Operesheni Sangara awamu ya pili, Kiongozi mkuu wa upinzani nchini ambaye pia ni Katibu mkuu wa CHADEMA Dk.Wilbroad Slaa aliyeambatana na viongozi wakuu wa chama hicho, akiwemo Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe, alisema kuwa Serikali ya CCM imekuwa na kiburi cha kuwatisha wanaotaka kutetea maslahi ya wananchi huku ikifungia hata vyombo vya habari kama Mwanahalisi.

"Serikali ina nguvu ya kuvifungia vyombo vya habari kwa sheria dhalimu ya magazeti ya mwaka 1977, lakini kamwe haitaweza kuzuia kina Dr Slaa kupiga kelele'' alisema kiongozi huyo. Dk. Slaa ambaye alikuwa akishangiliwa kwa nguvu na halaiki hiyo huku anga likihanikizwa kwa kelele za RAIS....RAIS...RAIS...., aliongeza kuwa, kuanzia sasa CHADEMA itaanzisha mapambano kwa ajili ya haki ya Watanzania.

Akizungumza katika mkutano huo, Mbowe alisema umati uliokusanyika unaonesha namna wakazi wa Kilombero walivyomthamini aliyekuwa mbunge wa viti maalumu, marehemu Regia Mtema.

Mbowe aliomba jina la uwanja wa Ifakara libadilishwe na kuitwa Uwanja wa Ukombozi, na kwamba hali hiyo iwe chimbuko la ukombozi kwa Mkoa wa Morogoro.
Aliwataka wakazi wa Kilombero kuacha kulalamika na badala yake wachukue hatua kwa kuachana na CCM na kujinga na CHADEMA.

Katika mkutano huo maelfu ya wananchi walijiunga na CHADEMA wengi wao wakiwa ni kutoka CCM.Mara baada ya mkutano huo baadhi ya watu walionekana wakifuta machozi huku wakisema wanaamini bado siku chache tu CHADEMA kuingia madarakani na kukomboa watanzania kiuchumi.

Mbali na Dk. Slaa na Mbowe, viongozi wengine waliokuwa katika msafara huo ni Joshua Nassar (Arumeru Mashariki), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Hamad Yusuph (Naibu Katibu Mkuu Zanzibar), Suzan Kiwanga (Viti Maalumu), Joyce Mukya (Viti Maalumu) na wengine wa makao makuu.

Source: Majira/Tanzania Daima/Nipashe

attachment.php

attachment.php

attachment.php
 
Attachments

  • Nyomi.JPG
    Nyomi.JPG
    88.6 KB · Views: 5,916
  • Mbowe.JPG
    Mbowe.JPG
    95.1 KB · Views: 5,709
  • Dk.Slaa.JPG
    Dk.Slaa.JPG
    89.7 KB · Views: 5,561
Molemo akili yako finyu sana hivi Kilombero ina wakazi wangapi mpaka iweke historia ambayo haiwezi kufutika katika Taifa ambalo linawakazi takribani mil. 40? historia ambayo haiwezi kufutika ni Dr. Slaa na wenzake kuigeuza Chadema saccos mkumbushe deni alilikopa saccos linatkiwa lilipwe.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Kazi nzuri sana! wananchi wanahitaji kutiwa matumain, kuonyeshwa nini cha kufanywa ili waweze kupambana na hali ngumu za maisha!!
 
[Tuntemeke mwingine]Molemo akili yako finyu sana hivi Kilombero ina wakazi wangapi mpaka iweke historia ambayo haiwezi kufutika katika Taifa ambalo linawakazi takribani mil. 40? historia ambayo haiwezi kufutika ni Dr. Slaa na wenzake kuigeuza Chadema saccos mkumbushe deni alilikopa saccos linatkiwa lilipwe.

Chama
Gongo la mboto DSM[/QUOTE]
 
Mkuu Chama na Tuntemeke,
Mlisema wabunge wa cdm wamegoma kuhudhuria mikutano ya Ifakara kwa sababu wana madai ya milioni mbili mbili zao. Hawa kina Nassari, TL(Jembe), Sugu, Mukya na Kiwanga kwa uchache, hawahusika na madai yenu?

Kazi mnayo mwaka huu
 
Molemo akili yako finyu sana hivi Kilombero ina wakazi wangapi mpaka iweke historia ambayo haiwezi kufutika katika Taifa ambalo linawakazi takribani mil. 40? historia ambayo haiwezi kufutika ni Dr. Slaa na wenzake kuigeuza Chadema saccos mkumbushe deni alilikopa saccos linatkiwa lilipwe.

Chama
Gongo la mboto DSM

"Katika mkutano huo ulikusanyika umati mkubwa kuwahi kushuhudiwa katika wilaya hiyo kwa miaka ya karibuni."

Hata kama wewe una mwendo kasi wa kukashifu wenzio basi usiwe mvivu wa kusoma! msome taratibu huyu bwana utaelewa anachokizungumzia! put your mind into gear before shooting off like a loose canon!
 
Molemo akili yako finyu sana hivi Kilombero ina wakazi wangapi mpaka iweke historia ambayo haiwezi kufutika katika Taifa ambalo linawakazi takribani mil. 40? historia ambayo haiwezi kufutika ni Dr. Slaa na wenzake kuigeuza Chadema saccos mkumbushe deni alilikopa saccos linatkiwa lilipwe.

Chama
Gongo la mboto DSM
Amesema kwa ngazi ya eneo hilo kijografia na sio Taifa. Kweli nakuambia sikutukani hata kama unalazimisha.
 
Molemo akili yako finyu sana hivi Kilombero ina wakazi wangapi mpaka iweke historia ambayo haiwezi kufutika katika Taifa ambalo linawakazi takribani mil. 40? historia ambayo haiwezi kufutika ni Dr. Slaa na wenzake kuigeuza Chadema saccos mkumbushe deni alilikopa saccos linatkiwa lilipwe.

Chama
Gongo la mboto DSM

kwa akili ya kawaida tu kama msikitini wnakuja waumii wastani wa ishirini halafu siku hio wakaja 25 kati ya waislam waliopo mfano wapo 30 kijijini .....maanake nini kimehasabu? au wewe kuvunja record ni mpaka idadi ya watu iwe wengi kama dar au mwanza
tumia akili na elimu yako kufikiri kuliko kukariri

Nahisi ww ndo unamatatizo ukisoma vizuri hakuna sehem amesema haiwezi futika katika taifa. Ila kasema ni vigumu kufutika katika uzinduzi wa Operesheni Sangara. Ushabiki usikufumbe Macho
 
Chama akili yako narrow sana Chadema ni chama cha siasa siyo saccos

Ahaaa haa wewe ndiye mwenye akili finyu ikiwa kama viongozi wanajikopesha pesa za chama hapa ni siasa au saccos

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Molemo akili yako finyu sana hivi Kilombero ina wakazi wangapi mpaka iweke historia ambayo haiwezi kufutika katika Taifa ambalo linawakazi takribani mil. 40? historia ambayo haiwezi kufutika ni Dr. Slaa na wenzake kuigeuza Chadema saccos mkumbushe deni alilikopa saccos linatkiwa lilipwe.

Chama
Gongo la mboto DSM

Mkuu usiwe mvivu wa kufikiri na kusoma embu soma vizuri mdau alichokiandika alf ndo urudi tena kuchangia.
 
kwa akili ya kawaida tu kama msikitini wnakuja waumii wastani wa ishirini halafu siku hio wakaja 25 kati ya waislam waliopo mfano wapo 30 kijijini .....maanake nini kimehasabu? au wewe kuvunja record ni mpaka idadi ya watu iwe wengi kama dar au mwanza
tumia akili na elimu yako kufikiri kuliko kukariri

Ahaa samahani nilisahau naongea na wanazi wa chadema UK mmefungua tawi watu walikuwa takriban 15 lakini kwenu walikuwa wengi sasa hata Kilombero watu 200 kwenu inaweza kuwa historia.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Molemo akili yako finyu sana hivi Kilombero ina wakazi wangapi mpaka iweke historia ambayo haiwezi kufutika katika Taifa ambalo linawakazi takribani mil. 40? historia ambayo haiwezi kufutika ni Dr. Slaa na wenzake kuigeuza Chadema saccos mkumbushe deni alilikopa saccos linatkiwa lilipwe.

Chama
Gongo la mboto DSM

Mtalia sana hadi kufika twenti fiftini, kanyaga twende!
 
Back
Top Bottom