Katibu Mkuu cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amesema Chadema imejipanga kuufumua mfumo wa elimu Tanzania ulioshindwa na kuunda upya pindi watakapounda serikali mpya mwaka 2015. Hayo aliyasema katika mahali ya darasa la saba ya shule ya Queen's English Medium Schools iliyopo Ukonga katika hotuba iliyosisimua wengi iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Kitivo cha Elimu(DUCE) na Mshauri wa masuala ya elimu wa Chadema Dr Kitila Mkumbo.
Ifuatayo ni summary ya hotuba hiyo;
Kwanza alitoa udhuru kwamba Dr Slaa amemtuma amwakilishe kwani yupo kwenye kampeni za uchaguzi wa madiwani. Aliupongeza uongozi wa shule hiyo kuweza kumwalika Katibu Mkuu wa Chadema kuwa mgeni rasmi na wamedhihirisha kuwa viongozi wote ni sawa bila kujali ni CCM au upinzani. Shule hiyo ilizinduliwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa DSM John Guninita na mahali ya mwaka jana mgeni rasmi alikuwa naibu Waziri Mh Mahanga.
Pia aliupongeza uongozi wa shule hiyo kwa elimu nzuri wanayotoa kwani mwaka jana walipata cheti cha ushindi na manispaa ya Ilala kwa kufaulisha wanafunzi wote. Na pia alisema ubora wa shule hiyo unathibitishwa na hotuba, mihadhara na maigizo kwa lugha ya kiingereza yaliyotolewa na wanafunzi wa shule hiyo. Watoto wadogo wa darasa la tano walitoa hotuba nzuri sana kuelezea sababu za umaskini Tanzania na pia watoto wengine waliweza kutoa mhadhara kwa ufasaha kuhusu digestive system na pragnancy.
Akielezea sera ya elimu ya Chadema Dr Mkumbo alisema mfumo wa elimu uliopo sasa si mzuri sana na idadi ya watoto wanaopata elimu bora hasa kupitia shule binafsi ni chini ya asilimia moja. Alisema mfumo wa elimu katika shule za umma una matatizo makubwa sana na nchi imegawanywa katika matabaka mawili ya wale wanaomudu elimu nzuri katika shule binafsi na wale wanaosoma shule za umma ambapo elimu inayotolewa huko ni duni sana na walimu wamekata tamaa. Alisema Chadema imejipanga kuurekebisha mfumo wa elimu na pia kuhakikisha elimu katika shule za umma inakuwa bora. Alielezea mambo yafuatayo kuwa ni baadhi ya mambo ya kwanza Chadema kuyarekebisha mara tu watakapochukua dola.
(i) watoto wataanza shule mapema zaidi kwani kwa sasa watoto wanakuwa haraka zaidi. Alisema kwa sasa watoto wanaingia shule wakiwa wamechelewa na hivyo wanachelewa pia kuanza kazi pindi wanapomaliza masomo yao. Moja ya sera za Chadema ni kuhakikisha watoto wanaanza shule wakiwa na miaka mitano na nusu hadi sita. Pia alisema sera ya Chadema ni kuwa na miaka minane kwa elimu ya shule ya msingi ambapo watoto watakuwa wamesoma hadi masoma ya kidato cha pili yanayotolewa sasa. Pia elimu ya sekondari itakuwa kwa miaka minne yaani itakuwa ni kuanzia kidato cha tatu cha sasa hadi kidato cha sita. Baada ya hapo watoto watajiunga vyuo vikuu na ufundi na itawezekana vijana kumaliza vyuo wakiwa na miaka 21 na kuanza kazi mapema kuliko ilivyo sasa.
(ii) Sera ya Chadema ni kuweka mkazo katika elimu ya kujitegemea na stadi za ufundi. Alisema elimu ya nadharia itapewa minofu na elimu ya vitendo na pia elimu ya kujitegemea ili vijana wanaomaliza shule wawe wabunifu zaidi kuliko ilivyo sasa.
(iii) Chadema imepania kuirudisha heshima ya mwalimu iliyopotea. Alisema mwalimu aliyekata tamaa hawezi kutoa elimu bora bali atawafundisha watoto kukata tamaa. Alisema Chadema itawalipa walimu vizuri, itawapatia nyumba na vitendea kazi ili kurudisha heshima ya walimu. Alisema heshima ya mwalimu ni heshima ya taifa.
(iv) Chadema itaimarisha lugha ya Kiingereza kwani kwa sasa watoto wengi wa Kitanzania wametengwa na lugha hiyo. Alisema watoto wanaosoma shule za mfumo wa kiingereza wanaweza kuizungumza lugha hiyo vizuri huku maelfu ya watoto wanaosoma shule za umma wakiwa wametengwa na kuachwa yatima. Alisema kwa sasa hata Wanyaruanda wanawazidi watoto wa kitanzania kwa kuzungumza kiingereza na kusema tutakuwa tunajidanganya kuwa kiingereza sio muhimu wakati sasa ndio imekuwa lugha kubwa ya mawasiliano hasa kwenye makampuni makubwa na kwenye nyanja ya kimataifa. Alisema sera ya Chadema ni kuhakikisha watoto wanazungumza kiswahili vizuri lakini pia kuhakikisha wanamudu lugha ya kiingereza. Alishangaa imekuwaje Rwanda iliyotoka kwenye vita muda mfupi uliopita kutuzidi katika nyanja za elimu, afya na huduma za jamii katika takwimu za hivi karibuni.
(v) Chadema imepania kuvunja matabaka ya elimu ambayo ni tishio kwa umoja wa taifa na kuhakikisha mtoto anayesoma shule ya serikali hatakuwa na tofauti na yule anayesoma shule binafsi.
Alimaliza hotuba yake kwa kuupongeza tena uongozi wa shule hiyo na kuahidi kiasi cha shilingi laki tano katika kusaidia maendeleo ya shule hiyo ambayo inasaidia pia kusomesha bure watoto yatima.
Kwa mawasiliano wa uongozi wa shule hiyo piga no 0719 604156