Kila siku mnasema serikali dhaifu halafu hapo hapo mnaigopa hiyo serikali dhaifu.
Hapa ndo huwa mnafurahisha! Ushahidi ukiletwa kwenye makabrasha!
Kwani ile issue ya vinasa sauti Dodoma iliishia wapi?
Anasema anamtaka nani amhoji....! Au Ocampo..?
Katibu mkuu wa Chadema na aliyekuwa Mgomba wa urais mwaka 2010 kupitia chama cha CHADEMA ambacho ni chama kikuu cha upinzani na kinacho ongoza kwa umaarufu na kupendwa na watu wote hasa vijana Nchini tanzania na Nchi za jirani Dr.W.Slaa, amesema hatokubali kuhojiwa na polisi juu ya habari za kutishiwa kuuwawa kwa viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho kwa kile alicho dai kwamba hana imani na jeshi hilo la polisi.
Ni hayo tu.
Ritz,
Dr. Slaa ni dhaifu wa kiroho, kanisa katoliki limemsomesha na kumpa imani zote za kiroho; lakini kutoka na udhaifu wake wa kiroho alilikimbia kanisa na kujiingiza kwenye mambo ya dunia; sasa leo mtu kama huyu akipanda majukwaani kuishutumu serikali dhaifu utamuelewa? Roho yake imetaliwa na uongo wa kila aina ili mradi tu azma yake itimie; kila siku ni kutunga porojo ambao hazina kichwa wala miguu; ukiishiwa sera huishi kusema uwongo.
Chama
Gongo la mboto DSM
Jamani hii kauli ya Dr. Slaa kama ni yeye kasema kweli ni ya kisiasa tu. Polisi wanahaki ya kisheria ya kumhoji mtu yeyote wanayemhisi au kumdhani anataarifa ambazo zitaisaidia serikali katika kuendesha mambo yake na hasa taarifa zinahusu masuala ya usalama wa nchi. Hivyo Dr. anaweza kusema hatatoa ushirikiano wakati wa kumhoji. Hivihivi wanaweza hata wakatumia mbinu ambazo wanazijua wao tu kuhakikisha kuwa anatoa ushirikiano. Haki za binadamu na kuendesha serikali havikubaliani 100%. Tuache ushabiki hapa JF. tujitahidi kuwa wahalisia japo kidogo
Singo imegoma kuuzika, kwa hiyo anataka kuhojiwa na nani KGB au FBI.
hata kipindi kile anafichua juu ya epa mlisema hivyo hivyo kuwa naropoka....jeshi la polisi limeshapoteza credibility
Singo imegoma kuuzika, kwa hiyo anataka kuhojiwa na nani KGB au FBI.