Dr. Slaa aitolea nje serikali ya Tanzania

Katibu mkuu wa Chadema na aliyekuwa Mgomba wa urais mwaka 2010 kupitia chama cha CHADEMA ambacho ni chama kikuu cha upinzani na kinacho ongoza kwa umaarufu na kupendwa na watu wote hasa vijana Nchini tanzania na Nchi za jirani Dr.W.Slaa, amesema hatokubali kuhojiwa na polisi juu ya habari za kutishiwa kuuwawa kwa viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho kwa kile alicho dai kwamba hana imani na jeshi hilo la polisi.
Ni hayo tu.

Akitaka atake asitake atahojiwa tu, hao vibaraka zake wa nchi za nje walio mwambia alete uzabi zabina wa maneno ya uwongo waje wamsaidie, kwani kwa hili hatoki hata chembe.

Anasema anamtaka nani amhoji....! Au Ocampo..?

Hapo red kama mkiweza mleteni......hili jeshi la police hatuna imani nalo kabisa......afu Ocampo atakuja kumhoji JK siku moja manake ana mengi ya kujibu!
 
Dr Slaa unahitajia mkutano kutoa na kuhubiri imani hio ,na isitoshe huna imani na jeshi la polisi na pia huna imani na mahakama ni mambo ambayo wananchi watapenda wayasikie kupitia kwenye mikutano na sio vipembeni .

Huo ni msimamo wake hata angetolea barabarani ujumbe umefika hutaki acha
 
Katibu mkuu wa Chadema na aliyekuwa Mgomba wa urais mwaka 2010 kupitia chama cha CHADEMA ambacho ni chama kikuu cha upinzani na kinacho ongoza kwa umaarufu na kupendwa na watu wote hasa vijana Nchini tanzania na Nchi za jirani Dr.W.Slaa, amesema hatokubali kuhojiwa na polisi juu ya habari za kutishiwa kuuwawa kwa viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho kwa kile alicho dai kwamba hana imani na jeshi hilo la polisi.
Ni hayo tu.

Wenye akili tumeshapata jibu. Madai yao ni ya uongo
 
Kila siku mnasema serikali dhaifu halafu hapo hapo mnaigopa hiyo serikali dhaifu.
 
huyu mzee bora aludie fani yake tu

Acha kuweweseka wewe, tangu ahojiwe walipokuta vinasa sauti kwenye kitanda chake akiwa mbunge kuna taarifa gani hilo jeshi la polisi limetoa? Atahojiwa vipi na majambazi hao hao wanaotaka kumtoa roho! Hata huhitaji elimu kubwa kujua polisi wetu wanatumiwa na ccm
 
Hata mimi sina Imani na Jeshi la Polisi, unless watupe kwanza matokeo ya uchunguzi wao wa kufikirika kuhusu vile vinasa sauti alivyotegeshewa Dr Slaa Hotelini Dodoma.

Tuache kubwabwaja, siwezi nikawa na Imani na Polisi hawa hawa akina Zombe wazee wa Mabwepande. nchi za wenzetu vyombo vya dola vipo huru na ndio maana vinaaminika na raia wote na kila mtu anaweza kuhojiwa.
 
Akitaka atake asitake atahojiwa tu, hao vibaraka zake wa nchi za nje walio mwambia alete uzabi zabina wa maneno ya uwongo waje wamsaidie, kwani kwa hili hatoki hata chembe.

Watanzania wana roho ngumu kweli kweli, bado wana imani na jeshi la polisi
 
Akitaka atake asitake atahojiwa tu, hao vibaraka zake wa nchi za nje walio mwambia alete uzabi zabina wa maneno ya uwongo waje wamsaidie, kwani kwa hili hatoki hata chembe.

Hapa ndo huwa mnafurahisha! Ushahidi ukiletwa kwenye makabrasha!

Kwani ile issue ya vinasa sauti Dodoma iliishia wapi?
 
Kila siku mnasema serikali dhaifu halafu hapo hapo mnaigopa hiyo serikali dhaifu.

Hakuna cha woga bali imani imetoweka. Nadhani hujapitwa na msemo wa KICHAA KAPEWA RUNGU ndivyo ilivyo serikali yako inapiga mwenye hatia na asiye na hatia hadi ambaye anataka kusaidia
 
Nadhani ni utashi wa mtu kuamua kama anakwenda kufungua kesi au la. Tumeona wengi wanapigwa lakini wanaamua kutokwenda kushitaki au kutoa maelezo Police. Utashi huo huathiriwa na mfumo wa kisheria na haki itolewayo na mahakama.

Mifumo ya namna Polisi na Mahakama vinavofanya kazi, havijengi imani kuwa haki inatendeka. Mke wangu alitishiwa kuuawa na pamoja na kutoa taarifa Police na hata mtu kujulikana, ikawa ni Polisi wakimwambia mke "tumemuonya asitoe vitisho". Ndipo nilipomaliza kabisa imani yangu na Police!!

Wengi tunaona Dr. Slaa anafanya vibaya lakini nadhani anatumia haki yake.
 
Na wewe umekosea kidoooogo Mkuu, sio Ulaya, America, Asia, Australia, bali hata Mungu na Malaika wanakipenda hicho chama, na ndio maana Sisi tuna Mungu, wao wana walichonacho.
Hata wewe umekosea, siyo Mungu na malaika tu....bali hata shetani na mabaya yake yote lakini akisikia neno CDM na viongozi wake basi huwa anafurahi sana na anajikuta ile mipango yake mibaya aliyoipanga dhidi ya CDM anasamehe na
badala yake anawarushia CCM....chezea Chadema wewe!
 
Back
Top Bottom