Dr. Slaa aitolea nje serikali ya Tanzania

Sikubaliani na wewe, Hizo sheria ni Mbwembwe tu, kama ni kulindwa kama unahainisha kwenye sheria hii, mnalinda watu kwa kutumi msitu wa mabwe pande? Acha Utani kwa maisha ya watu wewe, Mwakyembe, Mengi, Mwandosha, Kubenea, Kolimba, Kombe wote wamelindwa?

Huna haja au hata swifa ya kukubaliana na mimi. Mimi naomba ukubaliane na Katiba yenu ambayo mumeitunga wenyewe na kuweka sharia za kuwaongoza kama jamii. Hilo ndio la msingi.

Kumbuka kuwa muna kila haki ya kufanya mabadiliko ya sharia zenu pindi mnapoziona haziendani na wakti na kwa mahitaji ya wakti ule.

Kucheza na Sharia ni kucheza na Doula na hapo lazima nguvu za Doula zitakusulubu. Ndio maana tena kwa kinywa kipana sana nasema Dr Slaa pamoja na kubobea katika Canon Law (ambayo nazo zinasisitiza umuhimu wa kutwii sharia) anatakiwa afuate sharia zenu na sio kufanya mzaha na sharia hizo.

kama kiongozi alitakiwa kuwa ni wa kupigiwa mfano kwa kufuata sharia hizo.

 
Huna haja au hata swifa ya kukubaliana na mimi. Mimi naomba ukubaliane na Katiba yenu ambayo mumeitunga wenyewe na kuweka sharia za kuwaongoza kama jamii. Hilo ndio la msingi.

Kumbuka kuwa muna kila haki ya kufanya mabadiliko ya sharia zenu pindi mnapoziona haziendani na wakti na kwa mahitaji ya wakti ule.

Kucheza na Sharia ni kucheza na Doula na hapo lazima nguvu za Doula zitakusulubu. Ndio maana tena kwa kinywa kipana sana nasema Dr Slaa pamoja na kubobea katika Canon Law (ambayo nazo zinasisitiza umuhimu wa kutwii sharia) anatakiwa afuate sharia zenu na sio kufanya mzaha na sharia hizo.

kama kiongozi alitakiwa kuwa ni wa kupigiwa mfano kwa kufuata sharia hizo.


wewe kilaza si ulishaaga humu jamvini na ukaandika shairi la kwaheri .... kitu gani kimeku;;washa
 
Dk.+Peter+Slaa+%28wa+kwanza+kulia%29+akizungumza+na+wanahabari+leo+makao+makuu+ya+chama+hicho.JPG





Na Ninaeli Masaki



11th July 2012




Asema washughulike na kesi za zamani kwanza
Aeleza kuwa Kamati Kuu imelaani vitisho kwao




Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amesema hatakwenda polisi kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano kwa sababu Jeshi hilo limekuwa na desturi ya kumfanyia mahojiano katika matukio mbalimbali, lakini hawayafanyii kazi.

Dk. Slaa alitoa kauli hiyo kufuatia agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, alilotoa kwa Jeshi la Polisi juzi la kuwahoji viongozi wote wa Chadema waliosema wanatishiwa maisha na vyombo vya usalama.

Katibu Mkuu huyo alirejea matukio mbalimbali yaliyotokea kipindi cha nyuma likiwemo lile la Aprili mwaka huu katika uchaguzi mdogo wa kata ya Kirumba, ambapo wabunge wawili wa chama hicho mkoani Mwanza, Highness Kiwia (Ilemela) na Salvatory Machemli (Ukerewe), walivamiwa na kushambuliwa na mapanga na watu waliosadikika kuwa wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema jana asubuhi alipokea simu kutoka makao makuu ya jeshi hilo iliyomtaka kufika polisi ili kufanyiwa mahojiano, lakini alisema hayupo tayari kufanyiwa mahojiano mengine mpaka pale watakapofanyia kazi yale ambayo walishawahoji katika kipindi kilichopita.

"Ofisa mmoja wa makao makuu ya polisi alinipigia simu leo asubuhi (jana) akinitaka niende polisi, lakini nimekataa. Siwezi kwenda kwa sababu yapo mahojiano mengi ambayo walinifanyia baada ya matukio kadhaa yaliyohusisha chama chetu kutokea na hawajayafanyia kazi, wayashughulikie hayo kwanza," alisema Dk. Slaa.

Aidha, Dk. Slaa ameitaka serikali kufanya uchunguzi wa kina ili kupata ukweli wa taarifa ya baadhi ya viongozi wa chama hicho kutishiwa maisha na vyombo vya usalama badala ya kutafuta kujua aliyetoa taarifa hiyo.

"Kazi ya serikali na vyombo vya usalama ni kulinda amani, walichotakiwa kufanya mara tu baada ya kupata taarifa hizi ni kufanya uchunguzi ili kupata ukweli na siyo kutafuta kumjua aliyetoa taarifa hizo," alisema Slaa.

Alisema taarifa yao ya awali kuhusu kuwindwa kwa viongozi wa Chadema, walisema kuwa wanawatambua baadhi ya maofisa usalama wanaohusika ambao aliwataja kwa majina ya Zoka na Rama na kwamba mmoja kati yao amekuwa akifuatilia nyendo za Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.

Dk. Slaa aliongeza kuwa kamati kuu ya chama hicho imelaani kitendo cha kutaka kudhuriwa kwa viongozi hao na kwamba mpango huo ni wa kuhatarisha amani ya nchi. "Kamati kuu imelaani kitendo cha kutaka kudhuru viongozi wake na imelaani pia mpango wowote uliopo ambao unalenga kuhatarisha amani ya nchi," alisema.

Jumapili iliyopita uongozi wa juu wa Chadema uliitisha mkutano na waandishi wa habari na kueleza kuwa baadhi ya viongozi waandamizi wa chama chao wanawindwa na watu wanadaiwa kuwa ni usalama wa taifa.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freema Mbowe, alisema viongozi hao ni pamoja na Dk. Slaa, Mnyika na aliyekuwa Mbunge wa arusha Mjini, Godbless Lema.

Alisema mipango hiyo inahusisha kuuawa kwa sumu au kuwapelekea majambazi kwa nia ya kuwaua.

OPERESHENI SANGARA II YAIVA

Wakati huo huo, Dk. Slaa ametangaza kuwa chama hicho kinatarajia kuanza mpango wa nchi nzima wa 'Operesheni Sangara' awamu ya pili, kwa lengo la kuimarisha na kujenga chama itakayohusisha mikoa mitano.

Alisema operesheni hiyo itafanyika kwa siku 44 katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Singida na Manyara na kwamba vijiji 4,000, kata 806 na majimbo 44 vitafikiwa.






CHANZO: NIPASHE
Ni vizuri kufanya hiyo operation part ii ila sasa nasubiri operation papa ng'oa mafisadi.
 
Asante Rais, raiti wasingechakachua matokeo leo watanzania tusingekuwa hapa. Dr. Slaa mungu akulinde sana uwape matumaini watoto wetu na taifa kwa ujumla, maana kauli yenu ya bungeni iliniuma sana kwamba sisi tunakopa maisha ya wajukuu zetu ambao hawajazaliwa tunakula sasa.
 
Naona Dr sasa anatafuta umaarufu zaidi baada ya kuona sasa umaarufu wake unazidi kushuka siku hadi siku. Hana jipya la kuwaeleza wananchi wa Tanganyika zaidi ya propaganda na ubishi uso maana.

Hajui kuwa anajiaibisha yeye na taaluma yake aliyobobea ya Canon Law
.

Hivi wewe Barubaru si uliaga kuwa unaondoka jf?......kimekurudisha nini tena?.....wewe pia unajiaibisha na taaluma yako ya madrasa alnuur kwa kupost visivyoeleweka humu!
 
Last edited by a moderator:
Naona Dr sasa anatafuta umaarufu zaidi baada ya kuona sasa umaarufu wake unazidi kushuka siku hadi siku. Hana jipya la kuwaeleza wananchi wa Tanganyika zaidi ya propaganda na ubishi uso maana.

Hajui kuwa anajiaibisha yeye na taaluma yake aliyobobea ya Canon Law
.
Hii ni nini sasa!!mbona sioni kitu hapa!!wewe umeshasema wewe kwenu ni Nchi ya kigeni ya Zanzibar unafuatiliani mambo ya "tanganyika" weye?
 
wameshikwa pabaya wanaanza kujistukia .WALIDHANI MCHONGO WAO HAUTAFICHUKA NA WAJARIBU WAONE KUTISHIA KUMWAGA TENA DAMU YA MWANA CDM
 
:A S-baby:kwan dokta ma silaha bado ana ndoto ya kuongoza nchi hiii??hahahaha,,labda tanzania zanzibar...
 
Wapi matokeo ya Waziri Mwakyembe alipomuandikia barua IGP lakini matokeo yake ikawa kuwekewa sumu?

Wapi matokeo ya vinasa sauti bungeni??

Serikalo ingetaka kuaminika ingekuwa inatoa ripoti kwa wananchi baada ya kuunda tume, vonginevyo inakuwa kama ni kuwa enjoy hawa jamaa kama wanaujua ukweli au laaaah halafu wanaishia kutupia kapuni na kuanza kutafuta leakage imetokea wapi!!!!

Ni bora Dr. alivyogoma kuhojiwa maana haina maana kama watu wanakwenda kukudhalilisha!!!!
 
Mkuu barubaru, wewe ni mwanazuoni kiasi. Jaribu kuangalia swala hili bila kumhusisha Dr Slaa, jaribu kunagalia historia ya nchi yetu na jaribu kutafuta tafiti zilizofanywa kuhusu imani ya watanzania kwa mahakama na polisi. Kweli unaweza kuamini kwamba kama kuna mkono wa wakubwa Polisi watafanya lolote? Kumbuka first degree murder ya Dito, polisi wote mpaka RPC walikuwa wanaogopa kumkamata, angalia wezi wa EPA wanatesa tu, tell me kama kweli waliompiga Ulimboka watakamtwa au la (siamini kama ni uslama wa taifa), labda mmoja wao au wawili wao walitumiwa. Siwezi kupingana na Slaa hata kidogo, akienda Polisi hakuna litakalofanyika, sana sana ndio atakuwa anawarahisishia kazi wauaji. Kumbuka ya Mwakyembe habari zilianzahivi hivi kwenye mtandao kuwa atawekewa sumu, aliripoti polisi, lakini still sumu aliwekewa. Sasa ukienda kuwaambia maana yake nini? Kilichopo ni kujichukulia hatua za ulinzi binafsi.

Bongolander,

Ahali yangu. Mimi nikiangalia taaluma ya Dr Slaa na hao wenzake naona wazi wanacheza na Sharia zenu. Hebu nikupe kidogo nini sharia zenu zinazungumza kuhusu Serikali. Nitazibainisha hapa chini uone Dharau ya Dr na wenzake kuhusu sharia zenu.

Ukisoma Sharia na 15 ibara 6 ya mwaka 1984 inazungumza wazi Seikali yenu
8​

.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata
misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo -​
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikaliitapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwawananchi kwa mujibu wa Katiba hii;(b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;

Na ukirejea kwenye haki sawa mbele ya sharia. Soma Katiba yenu Sharia na 15 Ibara 6 ya mwaka 1984 na Sharia na 4 ibara 6 ya mwaka 1984 na ile ya Sharia na 3 ibara 5 ya mwaka 2000. Zimeweka bayana kabisa na kusema hivi
13​
.-(1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki,
bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sharia


(3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya yawatu yatalindwa na kuamuliwa na Mahakama na vyombovinginevyo vya Mamlaka ya Nchi vilivyowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.


Kwa mantiki hiyo sioni kwanini Dr apambane na sharia. kama wanaona hawazitaki kwanini wasishinikize zibadilishwe.
Sasa sioni kwa nini mtaalamu wa sharia na wenzake wanacheza na hizi sharia walizojitungia wenyewe ili ziwaongoze. kama wanaziona hazifai wanayo nafasi kubwa kushinikiza kubadilishwa


 
Amesema wapeleke kesi mahakamani ili yeye akatoe ushahidi mbele ya mahakama. Inaonekana anataka kumwaga mchele kwenye kuku wengi. Bila shaka ana ushahidi wa kutosha. Lakini hata hivyo sidhani kama hiyo kauli yake itafanya kazi, maana Nchimbi amesema suala la ulinzi wa mtu si la hiari, serikali inaweza kutumia nguvu kumpa ulinzi au kumlazimisha aisaidie polisi kulichunguza jambo hilo. Nafikiri siasa za bongo zimefika pazuri. Kama serikali ingeamua kujikausha na kujifanya haijasikia, ingeweza kulimaliza jambo hili kirahisi sana, lakini ikishaanzisha malumbano tu, ndo itajiweka kwenye wakati mgumu zaidi.
"Ulinzi wa mtu si hiari, serikali inaweza kutumia nguvu kumpa mtu ulinzi au kumlazimisha aisaidie Polisi kuchunguza jambo" alisema Mh. Nchimbi. Hapo kwenye red pananikumbusha Dr. Ulimboka..........aaah napita tuu.
 
Kafanya jambo la maana sana ,kucha na meno ni vitu ambavyo hutakiwi uvipoteze kibwege ***** labda watumie nguvu kama walivyomfanya DR Uli!
 
Ahojiwe na nani tena??polisi wa tz hawa hawa tunaowajuwa waliochukua jukumu la kuchunguza ajali ya Mwakyembe pale iringa halafu ikaweje???hawa hawa akina kova waliombambikiza kesi ya kupika iliyomhusu yule mtangazaji ta TBC nani jina lake vile teh teh teh,hawa hawa ambao bosi wao mkuu alisha wahi kusema ukiwakamata watuhumiwa wa wizi wa EPA nchi haitatawalika teh teh teh hivi mnashawishika kuna polisi hapa au polisi uchwala wachumia matumbo???????ovyo kabisa.
 
Soma ujumbe ila si umeuelewa ? Washwawashwa mna shida sana kila sehemu zinawasha sijui tuwasaidiaje ?

Mpuuzi mkubwa sana wewe....acha ukibaraka na umbumbu....umeshafanywa msukule na ccm mpaka umekosa hata chembe ya utashi....even if Dr slaa akifa,afungwe or athurike atabaki kuwa the memorable icon of this nation than ur fellow idiot......He manage to make nation awerenance na leo unatawala using his shadow....anawapeleka puta that why kila kukicha slaa....hajawai zusha lolote zaidi ya kuubiri ukweri....imagine without him the list of shem ingejulikana vp?EPA nao ni uzushi?....think twice na acha kuwa kibaraka na mwenye fikra finyu....
 
Back
Top Bottom