Dr. Slaa aitolea nje serikali ya Tanzania

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Katibu mkuu wa Chadema na aliyekuwa Mgombea wa urais mwaka 2010 kupitia chama cha CHADEMA ambacho ni chama kikuu cha upinzani na kinacho ongoza kwa umaarufu na kupendwa na watu wote hasa vijana Nchini tanzania na Nchi za jirani Dr.W.Slaa, amesema hatokubali kuhojiwa na polisi juu ya habari za kutishiwa kuuwawa kwa viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho kwa kile alichodai kwamba hana imani na jeshi hilo la polisi.
Ni hayo tu.
 
Katibu mkuu wa Chadema na aliyekuwa Mgomba wa urais mwaka 2010 kupitia chama cha CHADEMA ambacho ni chama kikuu cha upinzani na kinacho ongoza kwa umaarufu na kupendwa na watu wote hasa vijana Nchini tanzania na Nchi za jirani Dr.W.Slaa, amesema hatokubali kuhojiwa na polisi juu ya habari za kutishiwa kuuwawa kwa viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho kwa kile alicho dai kwamba hana imani na jeshi hilo la polisi.
Ni hayo tu.
Umekosea kidogo Mkuu hapo kwenye Rangi siyo nchi za jirani tu mpaka Ulaya America Asia Australia na wengine wanakipenda hicho chama
 
pamoja na hayo.Umeandika taarifa hii kwa ushabiki mno mpaka mtu wa kawaida anaelewa wewe uko katika itikadi gani! Na kupoteza reputation ya kuwa jf!
 
kama wao nao wanaongozwa na Dhaifu hawana jipya.....hawana hadhi ya kumuoji dr:israel:
 
Singo imegoma kuuzika, kwa hiyo anataka kuhojiwa na nani KGB au FBI.
 
Dr Slaa unahitajia mkutano kutoa na kuhubiri imani hio ,na isitoshe huna imani na jeshi la polisi na pia huna imani na mahakama ni mambo ambayo wananchi watapenda wayasikie kupitia kwenye mikutano na sio vipembeni .
 
Singo imegoma kuuzika, kwa hiyo anataka kuhojiwa na nani Kubenea au Mwanakijiji.
Wale waliomhoji Samwel Sita na Mwakyembe na kuleta ripoti. Au wale waliohoji kuuawa kwa wafanyabiashara ya Madini na kuja na taarifa ya Zombe kuhusika kisha mahakamani wakaambiwa wakamlete muuaji na pale hakuna muuaji!

 
Anasema anamtaka nani amhoji....! Au Ocampo..?
Amesema wapeleke kesi mahakamani ili yeye akatoe ushahidi mbele ya mahakama. Inaonekana anataka kumwaga mchele kwenye kuku wengi. Bila shaka ana ushahidi wa kutosha. Lakini hata hivyo sidhani kama hiyo kauli yake itafanya kazi, maana Nchimbi amesema suala la ulinzi wa mtu si la hiari, serikali inaweza kutumia nguvu kumpa ulinzi au kumlazimisha aisaidie polisi kulichunguza jambo hilo. Nafikiri siasa za bongo zimefika pazuri. Kama serikali ingeamua kujikausha na kujifanya haijasikia, ingeweza kulimaliza jambo hili kirahisi sana, lakini ikishaanzisha malumbano tu, ndo itajiweka kwenye wakati mgumu zaidi.
 
Katibu mkuu wa Chadema na aliyekuwa Mgomba wa urais mwaka 2010 kupitia chama cha CHADEMA ambacho ni chama kikuu cha upinzani na kinacho ongoza kwa umaarufu na kupendwa na watu wote hasa vijana Nchini tanzania na Nchi za jirani Dr.W.Slaa, amesema hatokubali kuhojiwa na polisi juu ya habari za kutishiwa kuuwawa kwa viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho kwa kile alicho dai kwamba hana imani na jeshi hilo la polisi.
Ni hayo tu.

Ni kweli acha akatae manake hii serikali dhaifu ya JK hata haijulikani nani police nani alshababu.....anaeza kwenda kwa mahojiano afu akajikuta msitu wa pande akiwa hana meno wala kucha!......asiende asee!
 
Back
Top Bottom