Safari_ni_Safari
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 23,268
- 17,101
Mbunge wa Kyela na Naibu waziri wa Miundombinu Dr Harrison Mwakyembe ametamka maneno magumu akiwa kwenye matibabu nchini India,Mwakyembe amesema akirudi salama atamwaga yote yanayomsibu bila kuficha hata nukta moja maana amechoka na hawezi kuvumilia tena...
Akaendelea kusema Watanzania waendelee kumuombea maana anaendelea vyema na Allah akimsaidia akanyanyuka kitandani basi wategemee siri nzito ambayo haikuwai kufahamika Tanzania....
Hii imekuwa ni baada ya kuibuka kwa hoja nzito kuwa kuna Watanzania wanataka kuuwawa akiwemo Dr Harrison Mwakyembe,hoja yangu ngoja tusubiri tuone mambo yatakuwaje baada ya kufika,naamini Mungu mkubwa atamnyanyua toka kitandani.
Get well soon Dr Harrison Mwakyembe and Prof Mwandosya...
Huyu hatarudi