Mwakyembe, toboa siri kama ulivyoahidi, ...au tuendelee kusubiri?

dazu

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
365
76
Mnamo mwezi Octoba mwaka jana tulipata taarifa kupitia mtandao huu wa jf kwamba "Mbunge wa Kyela na Naibu waziri wa Miundombinu Dr Harrison Mwakyembe ametamka maneno magumu akiwa kwenye matibabu nchini India,Mwakyembe amesema akirudi salama atamwaga yote yanayomsibu bila kuficha hata nukta moja maana amechoka na hawezi kuvumilia tena..." Sasa naona ni muda mrefu tangu amerejea toka India na bado yuko kimya, vipi afya yake haijaimarika hivyo tuendelee kusubiri au amebadili mawazo?
 
Labda amepona kabisa na hivo hataki mengine yamtokee kwa kupasua jipu.
 
...Kishasema kwamba yeye hatii neno ameiachia Serikali ambayo inadaiwa inafanya uchunguzi. Hii Serikali yenyewe iliyojaa mafisadi kweli ichunguze mbaya wake kapewa sumu na nani!!!? Ngoja tusubiri lakini mimi naamini tutasubiri hadi 2015 Serikali inamaliza muda wake hakutakuwa na ripoti au kama itatolewa ripoti ya uchunguzi huo basi itajaa usanii wa hali ya juu na hitimisho litakuwa hakuna ushahidi wa kutosha unaoonyesha Mwakyembe kapewa sumu.
 
Mnamo mwezi Octoba mwaka jana tulipata taarifa kupitia mtandao huu wa jf kwamba "Mbunge wa Kyela na Naibu waziri wa Miundombinu Dr Harrison Mwakyembe ametamka maneno magumu akiwa kwenye matibabu nchini India,Mwakyembe amesema akirudi salama atamwaga yote yanayomsibu bila kuficha hata nukta moja maana amechoka na hawezi kuvumilia tena..." Sasa naona ni muda mrefu tangu amerejea toka India na bado yuko kimya, vipi afya yake haijaimarika hivyo tuendelee kusubiri au amebadili mawazo?

hana lolote huyo, siku zote amekuwa ni kuwatishia mafisadi wa nchi hii, wakirudisha mapigo yeye CHALI. Safari hii hawatamruhusu kwenda India kutibiwa, watamfanyia kweli
 
Usitegemee lolote mkuu,ndo zake kuficha mambo huyo Nnyampala,,hukumbuki hata report ya richmond alificha some of ingredients?
 
..........amesema amemwachia Mungu, na sisi tunasema aliyoficha kwenye Richmond report tunamwachia Mungu.
 
hana lolote huyo, siku zote amekuwa ni kuwatishia mafisadi wa nchi hii, wakirudisha mapigo yeye CHALI. Safari hii hawatamruhusu kwenda India kutibiwa, watamfanyia kweli

Hapo kwenye red, wamfanyie mara ngapi? Huyu wameshamalizaiana naye wanangojea siku na saa.
 
Back
Top Bottom