Dr. Mwakyembe: Nikirudi nitamwaga yote kwa watanzania nimechoka sasa....

Daud Ballali alisema hivyo hivyo, na akaacha video na documents kibao. Walionavyo walipima upepo, wakaona yote ya nini wakati mtu tayari yuko futi 6 chini? Wanakula bata kwa kwenda mbele. Hujawahi kujiuliza wapi alipo Anna Mganda-Ballali, na kwa nini hasemi kitu? Mkono na Maregesi je?
 
Kama kawaida yake kutudanganya watanzania , "mara mkiendelea nitalipuka"! Sasa anasema akirudi salama atasema kitu......!

ha ha ha ha ha ......!

Mwakwembe ni mchumia tumbo kama wengine na alichakachua ripoti ya Richmond kuwalinda watu fulani kama alivyokuja sema mwenyewe "Au tuseme kila kitu ambacho tuliacha kwa kulinda heshima ya serikali".

Lakini kama
mtanzania lazima tumwombee nafuu mapema kadri iwezekanavyo na Mungu ampe maisha marefu.
 
Dunia ina mambo mengi na maisha ni fumbo. Mwenyezi Mungu pekee ndio ndio ajuaye fumbo hilo. Kama taarifa hii ni kweli,bas hiyo ndo dalili kubwa ya watu ambao wako 'close to death' . Nina ushahidi wa dalili hizi . Tumwombee Mungu,lisilowezekana kwa binadamu,kwa Mungu linawezekana .
 
Kama nilivyosema mwanzo kwa SITTA leo narudia kwa Mwakyembe, Namheshimu saana lakini Mbuzi aliyefungwa kamba huishia kulia mee!
Kama ilivyo kwa Sitta, Mwakyembe alipewa unaibu wa Sitta ili kumtuliza....Wote walipoteza imani yangu kwao pale walipokubali kuapishwa!! Hapo wakawa 'wamefungwa kamba' . Wangechagua kuwa ma 'freelance' ndani ya CCM hapo ningeendelea kuwa na imani nao!
 
Jamani nimesikia kwenye dondoo za magazeti toka gazeti la nipashe kuwa hali yake si shwari. Jamani hili ni kweli? Tunaomba mtujuze mliojirani na huyu mheshimiwa kwani tunaachwa gizani.
 
Juzi tuliambiwa Lowassa amewaita waandishi wa habari anataka "kupasua jipu". Akaishia kutoa bla bla tu, alipoulizwa khs Dowans na Richmond ambayo ndo tulidhani ndo ajenda yake kuu, akaishia kusema ataongea baadae wakati ukifika. Tusije shangaa Mwakiyembe akirudi kutuambia bla bla zile zile. This is politics!!!!!!!
 
Get well soon....ila ni sababu ipi ilimfanya afanye siri kwa maslahi ya nani na leo aseme atasema ?
 
Alisema wapi? Akiwa nanani? Muda gani? kwanini? Kunatatizo fulani katika taarifa hii. Naheshimu Mwakyembe, lakini naamini si mkurupukaji wa kiasi hiki.
 
Si azitoe huko huko kama alivyotamka haya. Zitatufikia tutazipata. Sasa anatafuta makubwa huyu kaka
si atulie jamani!
 
Si azitoe huko huko kama alivyotamka haya. Zitatufikia tutazipata. Sasa anatafuta makubwa huyu kaka
si atulie jamani!

...kamwachia Mungu jamani, japo Mungu kampa nafasi lakini hatimizi ahadi yake.
 
Mwakyembe ni mmoja ya wanasiasa waoga, watu wasio makini wenye kupenda kujipendekeza sn na hiz ni tabia za jamii ya wanyaki wengi wanatabia hz... Sitarajii kuwa atakuja na jipya huyu anaogopa kivuli chake mwenyewe ni kiongoz mnafiki 2 km walivyo ccm wengi hawana jipya. Hata hivyo anabaki kuwa ndugu yangu Mungu mwenye uweza wote amponye na kumtia nguvu... Aludi kyela wanamhitaji.
Tunashukuru kwamba kapona , lakini hakuna anayemhitaji Kyela
 
Mbunge wa Kyela na Naibu waziri wa Miundombinu Dr Harrison Mwakyembe ametamka maneno magumu akiwa kwenye matibabu nchini India,Mwakyembe amesema akirudi salama atamwaga yote yanayomsibu bila kuficha hata nukta moja maana amechoka na hawezi kuvumilia tena...

Akaendelea kusema Watanzania waendelee kumuombea maana anaendelea vyema na Allah akimsaidia akanyanyuka kitandani basi wategemee siri nzito ambayo haikuwai kufahamika Tanzania....

Hii imekuwa ni baada ya kuibuka kwa hoja nzito kuwa kuna Watanzania wanataka kuuwawa akiwemo Dr Harrison Mwakyembe,hoja yangu ngoja tusubiri tuone mambo yatakuwaje baada ya kufika,naamini Mungu mkubwa atamnyanyua toka kitandani.

Get well soon Dr Harrison Mwakyembe and Prof Mwandosya...
Huyu jamaa aliugua ukimwi wa kupukutika ngozi akadai amelishwa sumu, hopeless
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom