Dr. Mwakyembe na Dr. Slaa watishiwa kuuawa

Inawezekana ni kweli...kwa maelezo yake...halafu sidhani kama huku kwetu tuna maprofessional killers kama tunaowaona kwenye muvi...wengi ni vibaka wakawaida wenye njaa....hata hao wasomali huwa wanchukuliwa tu kwasababu ya hali yao kwao...sila, vita, ugaidi etc etc..i.e. wana experience ya kuua....

Hivi wale watu waliomwua Profesa wa sheria pale Dar ni akina nani.? Je angeshtukia mpango ulivyokuwa umesukwa akatoa kwenye gazeti watu wangemtukana kama walivyomtukana Mwakyembe. kuna kila sababu ya Mwakyembe kushtuka na hawezi kutengeneza tamthiliya ya namana hiyo na kutoa namba za kweli za magari
 
Bwana wee, hivi kwanza kifo cha Mwaikusa kimeishia wapi? Mbona awali walidai wamewakamata na tetesi zikasambaa eti ni wanyarwanda, yameishia wapi? Mi nina mpango wa kuanzisha intelligency binafsi!
 
Tatizo ni kwamba wengi kumbu kumbu zetu ni dhaifu sana, pengine ni kutokana na uwezo wa hard disc zetu? Wengi wetu tunajifanya hatuamini uchawi, lakini ni kwa sababu hatujaelewa msimamo wa maandiko tunayoyafuata kama ulivyosema hapo juu...na ndiyo sisi wenyewe na visomo vyetu tunaenda kutafuta protection ya namna hiyo...tunabisha bisha kwa sababu ya advantage ya mambo haya ya kishirikina hufanywa kwa siri...otherwise tungeumbuana sana.

Nashangazwa mno na ushabiki wako
 
Nilikuwepo uganda usiku na siku ya tukio la ugaidi lililofanywa na kundi la Al-shabab ambalo ni la waislamu wanaojiita wenye siasa kali na wenye lengo la kuleta sharia. Nilishuhudia maiti na vipande vya miili ya marehemu eneo hilo la Kyadondo. Uwezo wa kujilinda na makundi haya Uganda kama zilivyo nchi nyingine nyingi Africa hawana. Baada ya tukio ulinzi mkali ofizi za serikali wakisaidiwa na wamarekani uliimarishwa. Sheikh Ali Mahamud Rage.

Kundi hili ambalo liko affiliated na Al Qaida ni makundi yenye mission maalumu na yenye uwezo mkubwa wa fedha, uwezo, intelijinsia, wengi wa wafuasi wao ni wasomi na wenye high qualification kwenye IT, Engineering, weapons, planning etc. Huwa hawafanyi mashambulizi bila sababu, wakifanya husema bila uwoga kwani hufanya kwa mission maalumu.

Ukisoma kwa makini sana uwezo wao na mission zao, napata wasiwasina taarifa zilizojitokeza siku za karibuni kuwa wanataka wamuue Mwakyembe na Dr. Slaa! Mwakyembe alivyosema sikushtuka wote tunamjua. Issue kama zile ni za kusema na kufanya kimya kimya kwani makundi kama Al-Shabab huwa hawana siri na huwa wana declare interest zao. Pengine ni wasomali tu na sio Al –shabab, .Nimestuka na kauli ya Slaa eti haogopwi kuuawa na Al-Shabab nikacheka sana! Nilicheka sana , tena sana wauaji hawangaiki vile. Na Kama kungekuwa na failed attempt ingejulikana waziwazi! Kuna notable failed attempt ambazo huwa zinabuma na kuvuja vibaya, japo kama zile za kumuua rais zimefanywa siri sana na lakini kuna watu walikufa on spot.

Mwakyembe shughulika na polisi na maliza mambo yako na polisi bado tuna polisi wazuri wa kukusaidia. Slaa usikurupuke ulitakiwa kuwajua Al-shabab mapema na siyo kusema haugopi…huwa hawana muda na assassination ya mtu mmoja, huwa wanaua massive na unakaribisha kuuawa kwa raia wengi , kama hawa jamaa wataelekeza masikio yao kwenu .

Sijajua lengo la kuwaingiza al-shabab ni kuwatisha watanzania au kuwakaribisha, mkiwawekea njia kweli watakutana na wengine waliojichokea maisha na kutawala eneo la maziwa makuu, wanataka sharia, huku wengine wanataka kadhi, hivi hamuoni kuwa mnawakaribisha??

Hivi akina Slaa na mwakyembe hawa jamaa wakiamua kufanya mambo nani wa kuwazuia? Ya Gongo la Mboto na Mbagala yanatosha, waaacheni, msiwataje tena, hatuna uwezo wa kuwahimili na wakiingia watatuonea mpaka basi!!

I repeat kama Al-Shabab wanataka kuwaua akina Mwakyembe na Slaa wangekuwa wamefanya hivyo siku nyingi na wao wenyewe wangetuambia kwa nini wameamua wawaue! I dont think so unless kama hawa watu waliwazuia al-shabab kwenye mission zao. Kwa uwezo wao hawana muda wa kutumia magari yenye number na kujulikana na Mwakyembe! kumbuka I can prove that they are highly trained.

Sina muda kuwa kupitia kila sentensi ya taarifa ya mwakyembe, ila ina maswali mengi sana, na inaweza kumuweka kwenye kundi la kuwa naye ni mtu hatari..unafanya biashara gani??

Richmond na Dowans mpaka sasa wajuzi wa mambo wanajua imekula kwenu, mmeshindwa, tunaangalia movie inaendaje
 
Gama nikijaribu kuunganisha thread zako nadhani nakufahamu, sielewi ni kwanini haukubaliani kabisa na watu wa namna ya Mwakyembe,ikitokea ishu ya Sita unapuuza na kuongea hovyo,likizungumzwa la mwakyembe,slaa,na wengine wa type hiyo unakuja tofauti kabisa,likiandikwa jema la kumsifu JK au RA,au EL basi utaandika vyema kweli,sio siri ni wewe.. Kwa vp mtu unakataa ukweli wazi wazi hivi hapana ni wewe tuweke wazi.. Kwa vp mtu umuite mzushi kwa kuhofia maisha yake,..na kutetea ya binadamu mwenzake
 
Mheshimiwa, maelezo yaliyotolewa na Dr, yanajitoshereza; hakusema wahusika wana bifu yeyote na Al-Shabab bali kundi hilo limekodiwa kutoa huduma hiyo ya kutoa watu roho. Kwakuwa wamekodiwa, bila shaka walio wakodi wanataka kazi hiyo itekelezwe kwa kuzingatia masharti fulani, ikiwa ni pamoja na kufanyika kwa siri. Kulingana na maelezo yalizotolewa kuwa ya kina, kuna kila sababu polisi kuyapa madai hayo uzito unao stahili.
 
Ni maradhi tuu na yanaitwa schizophrenic paranoia. Kama ni kweli hao alshabab ni "al-qaeda affiliates" basi hawawezi kukodiwa na mtu yoyote, serikali yoyote kwa ajili ya kupata pesa. Alqueda hawana historia ya kufanya mashambulizi ili kupata pesa kwa hiyo madai yanayotolewa kwamba al-shabab wamekodiwa kuwashambulia ni ya uongo, na yana lengo la kujinufaisha kisiasa.
 
Kweli ndugu, tunatakiwa kuwajua hawa watu kwanza kabla ya kusema haya mambo ya aibu sana,
 
Suala hapa ni udini au? maana Membe na Mwandosya si anti-government sasa kwanini wahusishwe. Maana ukiangalia majina kwenye orodha hiyo utagundua kuwa ni wakristo wote.
 
diehard: kwa hiyo unamuunga mkono dr harison mwakyembe kuwa wataalam wa mauaji toka alshabaab wameletwa nchini ili kumuua yeye?! Wakisaidiwa na jeshi la polisi?!, wakisaidiwa na wizara yake?!, wakisaidiwa na kampuni kubwa ya ujenzi hapa nchini?!, wakisaidiwa na karani wa bunge?!, wakisaidiwa na mchawi maarufu wa hiko songea?!. Brigade yote hiyi kwa ajiri ya mwakyembe na bado hawajaweza kutekeleza?, na yeye ameweza kupata taarifa za ndani kabisa ya mpango huo kwa 100%.............. Hii ni CRAP.,na kama kweli mwakyembe ametoa taarifa hizi basi tumpeleke mirembe haraka sana. BTW anamtafutia ujiko Slaa.

more than crap! shame upon him
 
Nilikuwepo uganda usiku na siku ya tukio la ugaidi lililofanywa na kundi la Al-shabab ambalo ni la waislamu wanaojiita wenye siasa kali na wenye lengo la kuleta sharia. Nilishuhudia maiti na vipande vya miili ya marehemu eneo hilo la Kyadondo. Uwezo wa kujilinda na makundi haya Uganda kama zilivyo nchi nyingine nyingi Africa hawana. Baada ya tukio ulinzi mkali ofizi za serikali wakisaidiwa na wamarekani uliimarishwa. Sheikh Ali Mahamud Rage.

Kundi hili ambalo liko affiliated na Al Qaida ni makundi yenye mission maalumu na yenye uwezo mkubwa wa fedha, uwezo, intelijinsia, wengi wa wafuasi wao ni wasomi na wenye high qualification kwenye IT, Engineering, weapons, planning etc. Huwa hawafanyi mashambulizi bila sababu, wakifanya husema bila uwoga kwani hufanya kwa mission maalumu.

Ukisoma kwa makini sana uwezo wao na mission zao, napata wasiwasina taarifa zilizojitokeza siku za karibuni kuwa wanataka wamuue Mwakyembe na Dr. Slaa! Mwakyembe alivyosema sikushtuka wote tunamjua. Issue kama zile ni za kusema na kufanya kimya kimya kwani makundi kama Al-Shabab huwa hawana siri na huwa wana declare interest zao. Pengine ni wasomali tu na sio Al –shabab, .Nimestuka na kauli ya Slaa eti haogopwi kuuawa na Al-Shabab nikacheka sana! Nilicheka sana , tena sana wauaji hawangaiki vile. Na Kama kungekuwa na failed attempt ingejulikana waziwazi! Kuna notable failed attempt ambazo huwa zinabuma na kuvuja vibaya, japo kama zile za kumuua rais zimefanywa siri sana na lakini kuna watu walikufa on spot.

Mwakyembe shughulika na polisi na maliza mambo yako na polisi bado tuna polisi wazuri wa kukusaidia. Slaa usikurupuke ulitakiwa kuwajua Al-shabab mapema na siyo kusema haugopi…huwa hawana muda na assassination ya mtu mmoja, huwa wanaua massive na unakaribisha kuuawa kwa raia wengi , kama hawa jamaa wataelekeza masikio yao kwenu .

Sijajua lengo la kuwaingiza al-shabab ni kuwatisha watanzania au kuwakaribisha, mkiwawekea njia kweli watakutana na wengine waliojichokea maisha na kutawala eneo la maziwa makuu, wanataka sharia, huku wengine wanataka kadhi, hivi hamuoni kuwa mnawakaribisha??

Hivi akina Slaa na mwakyembe hawa jamaa wakiamua kufanya mambo nani wa kuwazuia? Ya Gongo la Mboto na Mbagala yanatosha, waaacheni, msiwataje tena, hatuna uwezo wa kuwahimili na wakiingia watatuonea mpaka basi!!

I repeat kama Al-Shabab wanataka kuwaua akina Mwakyembe na Slaa wangekuwa wamefanya hivyo siku nyingi na wao wenyewe wangetuambia kwa nini wameamua wawaue! I dont think so unless kama hawa watu waliwazuia al-shabab kwenye mission zao. Kwa uwezo wao hawana muda wa kutumia magari yenye number na kujulikana na Mwakyembe! kumbuka I can prove that they are highly trained.

Sina muda kuwa kupitia kila sentensi ya taarifa ya mwakyembe, ila ina maswali mengi sana, na inaweza kumuweka kwenye kundi la kuwa naye ni mtu hatari..unafanya biashara gani??

Richmond na Dowans mpaka sasa wajuzi wa mambo wanajua imekula kwenu, mmeshindwa, tunaangalia movie inaendaje
kaka umemaliza yooooote, i think JF shd have people of ur calibre,sio watu wanao comment tuu bila kufanya tafakuri pana! hongera sana
 
Tumejenga taifa la watu wazushi. Daktari wa PhD anazusha. Alizusha mambo mengi akiwa mwenyekiti wa kamati teule ya bunge na uzushi wake unatugharimu hadi leo. Akatuaminisha kwamba Richmond na Dowans ni moja na kwamba zote zina mikono ya RA na EL. leo hii haya yote yamethibitika kuwa ni uongo na anafanya hivi ili kujiepusha na kitanzi cha uzushi wake.

Ni bahati tu kwamba watanzania ni wavivu wa kukumbuka, tumeshasahau na bado tunamuona Mwakyembe shujaa. Mtu huyo huyo kwa sababu ya uzushi wake huo aliposikia Tanesco wanataka kuinunua mitambo ya Dowans akafanya press conference na kuliambia taifa ni bora nchi iwe gizani kuliko kuinunua mitambo hiyo, sasa hivi tuko gizani na kazi iliyofanywa na kamati yake imeligharimu taifa karibu shilingi bilioni 100, mitambo ipo haiwashwi kisa ni uchochezi dhidi ya nishati ya umeme uliojengwa na mwakyembe na wahuni wenzake.

Mzushi huyu akaja tena na uongo mwingine alipopata ajali ambayo hakuna shaka ilitokana na uzembe wa dereva wake, akadai kulikuwa na lori lililokuwa likitaka kuwagonga na dereva wake alipokwepa ndipo gari likaacha njia na yeye akapata ajali. Uchunguzi wa polisi ulipofanyika ikabainika kwamba wakati ajali ikitokea alikuwa amelala na wala hakuliona lori alilokuwa akilisema...hakika huyu ana PhD ya uzushi.

Sasa kazusha jipya eti anataka kuuawa na akaandika barua kutoa ushahidi wa kutunga wa kuunga unga mambo na kuwataja watu na namba za magari mengi akijifanya ana mtandao unaompa taarifa za kila kinachotokea. Ana bahati tu kwamba tuna jeshi la polisi la wasanii ambalo linashindwa kumbana atoe ushahidi wa kina wa maelezo yake ambayo hakuna shaka yatathibitisha kuwa ni ya uzushi.

Anafanya hivi lili EL na RA waonekane ni wauaji...ajenda yake ile ile ya kuwazushia na kuwachafua wengine kwa malengo machafu ambayo ufadhili wake unatambulika kuwa ni wa wahuni wachache walio ndani ya idara moja nyeti. Ni aibu kuwa na naibu waziri tena mwenye PhD wa kiwango duni kama Mwakyembe.

Uzushi wake umelifanya taifa kupiga maktaimu na kujadili hoja moja kwa miaka minne sasa, uzushi wake umeliingiza taifa gizani na sasa anatengeneza uzushi mwingine unaoweza kuligharimu jeshi la polisi, idara ya usalama wa taifa, serikali, chama chake na watanzania kwa ujumla. Mwakyembe ni mtu hatari, ni mtu wa kuogopwa kama ukoma. Huyu mtu ana pepo baya, anapaswa kuangaliwa na kuchungwa sana

Nimesoma maelezo yako, kwa kifupi yamejaa chuki binafsi. Lakini hilo si lengo langu la kuandika.
Ila nataka nikuulize, Kwa hiyo wewe unaona Mwakyembe kujitetea na tisho la kuuliwa ni hatari kuliko TISHO LA AKINA ROSTAM AZIZ NA LOWASSA KUITAFUNA NCH?. SIKIA EWE MWANA SISIEMU MASLAHI, WATU HATARI KATIKA NCHI HII NI ROSTAM AZIZ KWA AJILI YA UWIZI WAKE, NA KIKWETE KWA AJILI YA KUCHEKA NA MAFISADI NA KUWAKUMBATIA. HAWA WATU NDIYO WANAO FANYA NCHI IWE KATIKA HALI YA WASI WASI. WANASINGIZIA CDM NA DR. SLAA ILI KUWAPUMBAZA WANANCHI. LAKINI WANANCHI HAWADANGANYIKI MAANA WANAJUA FIKA DR. SLAA HAJAWAHI INGIA MIKATABA YA WIZI WA DOWANS, DR. SLAA HAJAPANDISHA GHARAMA ZA MAISHA N.K N.K.
KIFUPI NIHITIMISHE KUWA SIKU ZENU ZINAHESABIKA.
 
diehard: kwa hiyo unamuunga mkono dr harison mwakyembe kuwa wataalam wa mauaji toka alshabaab wameletwa nchini ili kumuua yeye?! Wakisaidiwa na jeshi la polisi?!, wakisaidiwa na wizara yake?!, wakisaidiwa na kampuni kubwa ya ujenzi hapa nchini?!, wakisaidiwa na karani wa bunge?!, wakisaidiwa na mchawi maarufu wa hiko songea?!. Brigade yote hiyi kwa ajiri ya mwakyembe na bado hawajaweza kutekeleza?, na yeye ameweza kupata taarifa za ndani kabisa ya mpango huo kwa 100%.............. Hii ni CRAP.,na kama kweli mwakyembe ametoa taarifa hizi basi tumpeleke mirembe haraka sana. BTW anamtafutia ujiko Slaa.

Wewe ndiyo unayetoa crap,
Kimsingi this is a very serious allegation, lakini cha kushangaza watuhumiwa wote hamna aliye kanusha upeplelezi wa Dr Mwakyembe.
Hivyo sisi tuna kila sababu ya kuamini hilo. Maana kama hayo yasingejili, basi watu wangejitokeza kusema hatukwenda Songea, hatukulala Morogoro, hatukupanda gari ya Vodacom na Caspian. Lakini woote hao wako kimya. wanajua kuwa mwakyembe ana ushahidi wa kutosha. Na mwaka huu lazima kieleweke.
 
Jamani ukiangalia vizuri,hii taarifa imeletwa hapa kupitia gazeti la fisadi,kwaio vipaumbele vya habari vimeenda kwenye swala la ushirikina ili msimuelewe dr kama kusudio lao.
Tungejaribu kupata barua halisi aliyoandika dr tuone ukweli wa mambo!

Tusikurupuke jamani, phd huipati ukiwa bingwa wa kukurupuka;huyu ni analyst wa mambo. Sio uDr wa heshima huu. Tafadhali
Yani kweli Phd holder anakuwa na imani za namna hii.....eti kuna watu hapa wanaamini kabisa kuwa ni kweli alitaka kulogwa.du last week citizen waliandika kuwa tanzania inaongoza africa mashariki kwa imani za kishirikina
 
Kuna wangapi humu wanamkumbuka Katibu mkuu wa CCM Mh. Marehemu Harace Kolimba? Kuna yeyote anayekumbuka kifo chake kilivyokuwa na utata na jinsi muhimbili walivyojichanganya na autopsy yake?? Ni sumu inayosadikika kupewa ilikuwa wapi kama si Dodoma??? Hivi kuhusu uchawi, hata ukiwa msomi unakuzuia kuelewa kama uchawi upo ama haupo?? Katika Biblia Uchawi umetajwa( Mnamkumbuka Simon Mchawi ktk kitabu cha Matendo ya mitume?).. Bila shaka hata kwenye kitabu cha kiislam pia umetajwa. Hao wanaosema asiamini uchawi na kama watu wameenda kwa mganga asiseme??? Mfano asiposema na akauliwa kweli nani atakuwa mzembe?? Kila rakheli.

Kama nakufahamu vile? Au hiyo picha siyo yako?
 
likitumika kama toilet haliwezi kuumiza? (utani) .kuhusu mwakyembe mimi simuungi mkono achague moja kuwa moto au baridi pia kama kweli ni mpigania haki kwanini aongope kwani kina dr silaa sio watu yeye achague kama anaogopa kufa amwombe radhi rostam.

Mama mkubwa kweli umekua mpaka graph curve ya growth inashuka sawia na akili, RA ni wakuangukiwa na Dr kweli? Kwa taarifa yako siku yakitokea machafuko wa kwanza kukimbia bongo ni RA mtakaofanywa mbaya ni nyie masalia yake, endelea kujigonga kwake atakufanya uwe mfuta viatu wake akepe japo Megawatt 0.0001 uuze upunguze umaskini, njaa, maradhi na ujinga.
 
Kama kawaida yako unaropoka tu halafu utakuja kufikiria baadaye. Kweli kwa akili yako unadhani gazeti la mtanzania lipoteze muda wake tena kuweka front page hii story (peke yake) kama hamuna kitu. Mwakyembe amewaandikia police, mtanzania wameamua kuiwahi kwenye gazeti.

Ngoja niwabandikie hapa hiyo story kama ilivyo kwenye gazeti la leo mjionee wenyewe

For your information, gazeti la Mtanzania halisomwi na wengi na liko sokoni kimkakati tu: kumtetea Rostam, Lowassa na mtoto wake (Fred) & cohorts wao pale wanapotuhumiwa - kazi yake ni kuwajengea utetezi; kuwashughulikia wale wote ambao ni anti-ufisadi kwa kejeli, matusi na tuhuma za kupikwa na ku-sponsor hata wachangiaji kwenye JF ili kuzima kelele fulani; ku pre-empt stories zozote zinazoweza kuathiri maslahi ya wakubwa hao k.m. gazeti la RAIA MWEMA lilipokuwa linafuatilia taarifa za kipolisi London kuhusu mtoto wa Lowassa (Fred) kuwa anajihusisha na biashara ya fedha haramu, Mtanzania iliwahi siku moja kabla na kusema Lowassa na familia yake wanaonewa sana na kusingiziwa. Hatua hiyo ilifuatiwa na watumishi wa ndani wa Rostam akina Balile kwenda kiwanda cha uchapishaji na kuununua mzigo wote wa RAIA MWEMA ambao waliuharibu baadaye.

Hilo ndilo linaloonekana sasa kwa habari hiyo ya Mwakyembe na wenzake kutengenezewa njama za kuuawa. Badala ya kuliachia Jeshi la Polisi lipeleleze, Mtanzania wanaandika habari juu ya barua ya Mwakyembe waliyoipata Polisi na kuanza kumbeza mlalamikaji na kubeza alichokiandika! Wanadiriki hata kudanganya kuwa hata "wasomi na wanasiasa wamshangaa na kumbeza". Ukisoma gazeti lao humkuti msomi wala mwanasiasa yeyote wakimnukuu! Ni porojo tu za akina Balile na Bashe wakifuata maelekezo-fisadi ya akina Rostam, Lowassa. Wanaishia kusema taarifa za Mwakyembe Polisi huwa ni za utata maana hata alipopata ajali, alisingizia kugongwa wakati dereva wake alikuwa na makosa ya kwenda mwendo wa kasi! Kama ni hivyo, kwa nini dereva hakufunguliwa mashtaka ya kuendesha gari kwa uzembe? Kwa nini Polisi wasitoe taarifa hiyo kwa mhusika mpaka gazeti la Rostam liwasemee?
Ukiisoma habari ya Mtanzania ukalinganisha na habari ya MwanaHalisi kuhusu suala hili, unauona waziwazi umamluki wa gazeti la Mtanzania.
 
Back
Top Bottom