Dr. Mwakyembe na Dr. Slaa watishiwa kuuawa

likitumika kama toilet haliwezi kuumiza? (utani) .kuhusu mwakyembe mimi simuungi mkono achague moja kuwa moto au baridi pia kama kweli ni mpigania haki kwanini aongope kwani kina dr silaa sio watu yeye achague kama anaogopa kufa amwombe radhi rostam.

Hili si suala la kuungwa mkono, ni suala la maisha yake. Hivi ukiletewa taarifa kuwa jirani yako anatafuta sumu ya mamba kukuwekea kwenye kisima chako, unanyamaza kimya ili uonekana baridi au motomoto? Ama kweli mkuki kwa nguruwe! Kawaida, ni mtu kwenda Polisi ili wachunguze! Mbezeni Mwakyembe mnavyotaka, Kamati aliyoiongoza itabaki katika historia ya nchi hii kuwa chachu ya mabadiliko ya kisiasa nchini. Maadui anao lukuki, tunawajua, ndiyo maana wengine tunamwombea!
 
Tumejenga taifa la watu wazushi. Daktari wa PhD anazusha. Alizusha mambo mengi akiwa mwenyekiti wa kamati teule ya bunge na uzushi wake unatugharimu hadi leo. Akatuaminisha kwamba Richmond na Dowans ni moja na kwamba zote zina mikono ya RA na EL. leo hii haya yote yamethibitika kuwa ni uongo na anafanya hivi ili kujiepusha na kitanzi cha uzushi wake.

Ni bahati tu kwamba watanzania ni wavivu wa kukumbuka, tumeshasahau na bado tunamuona Mwakyembe shujaa. Mtu huyo huyo kwa sababu ya uzushi wake huo aliposikia Tanesco wanataka kuinunua mitambo ya Dowans akafanya press conference na kuliambia taifa ni bora nchi iwe gizani kuliko kuinunua mitambo hiyo, sasa hivi tuko gizani na kazi iliyofanywa na kamati yake imeligharimu taifa karibu shilingi bilioni 100, mitambo ipo haiwashwi kisa ni uchochezi dhidi ya nishati ya umeme uliojengwa na mwakyembe na wahuni wenzake.

Mzushi huyu akaja tena na uongo mwingine alipopata ajali ambayo hakuna shaka ilitokana na uzembe wa dereva wake, akadai kulikuwa na lori lililokuwa likitaka kuwagonga na dereva wake alipokwepa ndipo gari likaacha njia na yeye akapata ajali. Uchunguzi wa polisi ulipofanyika ikabainika kwamba wakati ajali ikitokea alikuwa amelala na wala hakuliona lori alilokuwa akilisema...hakika huyu ana PhD ya uzushi.

Sasa kazusha jipya eti anataka kuuawa na akaandika barua kutoa ushahidi wa kutunga wa kuunga unga mambo na kuwataja watu na namba za magari mengi akijifanya ana mtandao unaompa taarifa za kila kinachotokea. Ana bahati tu kwamba tuna jeshi la polisi la wasanii ambalo linashindwa kumbana atoe ushahidi wa kina wa maelezo yake ambayo hakuna shaka yatathibitisha kuwa ni ya uzushi.

Anafanya hivi lili EL na RA waonekane ni wauaji...ajenda yake ile ile ya kuwazushia na kuwachafua wengine kwa malengo machafu ambayo ufadhili wake unatambulika kuwa ni wa wahuni wachache walio ndani ya idara moja nyeti. Ni aibu kuwa na naibu waziri tena mwenye PhD wa kiwango duni kama Mwakyembe.

Uzushi wake umelifanya taifa kupiga maktaimu na kujadili hoja moja kwa miaka minne sasa, uzushi wake umeliingiza taifa gizani na sasa anatengeneza uzushi mwingine unaoweza kuligharimu jeshi la polisi, idara ya usalama wa taifa, serikali, chama chake na watanzania kwa ujumla. Mwakyembe ni mtu hatari, ni mtu wa kuogopwa kama ukoma. Huyu mtu ana pepo baya, anapaswa kuangaliwa na kuchungwa sana

Hivi haya unaandika ukiwa matikas au soba. When you are not in a position to think dont join the great thinkers.

Wewe unataka tujadili nini zaidi ya maslahi ya taifa letu. Wewe yaani sina neno la kukuita.
 
Kwa sababu ni mawazo yako sitaki kukusema ila wewe ni wa kuogopwa kama UKIMWI inawezekana na wewe umo kwenye ujinga huu unaofanywa na mafisadi.
 
Kweli Mwakyembe mzushi msema kweli ni Hosea aliyesema Richmond haina tatizo na akaishia kusifiwa kwa kazi nzuri.
 
POLE Dr.
ILA NAZANI UMEPITIWA KIDOGO KWA KUTUMIA HEADED PAPER YA SERIKALI WAKATI ISSUE YENYEWE NI KAMA PERSONAL VILE JAPO WEWE NI WAZIRI
 
Madai ya Mhe. Mwakyembe ni ya msingi lazima yafanyiwe kazi na IGP pamoja na Jeshi lake!
Mwakyembe ni Professional Lawyer kwenye level ya Doctor HAWAWEZI KULETA MADAI AU TUHUMA ZA VIJIWENI!!!
Katika madai yake ANA VIELELEZO: Kuna NAMBA ZA MAGARI ZIMETAJWA TENA MAGARI YA SERIKALI (ST-X na SM)! Je, ina maana hizi namba za MAGARI NI ZA BANDIA? Je,Police wanahitaji SIKU NGAPI KUJUA GARI NAMBA FULANI LIKO WAPI KWELI??????????

Kwa Greal Thinkers hizi habari ZINAUKWELI KWA NAMNA FULANI. Mimi naamini kuwa plot ya kumwangamiza Dr.Mwakyembe na wengine waliotajwa kwenye list kama Dr. Slaa zina ukweli. Naamini kuna watu ndani ya CCM na Serikali yake HAWALALI USINGIZI KWASABABU YA MISIMAMO YA KINA DR. SLAA,MWAKYEMBE,na wale wote ambao NI TISHIO KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA URAHISI-2015!!!

Ni mtu mpuuzi na mjinga tu anaweza kupingana na ukweli huu. Kwa wale wanaobisha au kupuuza haya maneno,there is a day watakuja kuamini kuwa ni habari za ukweli but it will be too late!!!

Hivi watu wanategemea nini kutoka kwa mtu kama RA,EL,AC(Mzee wa vijisenti). These guys are very dangerous,they can kill or do anything for the sake of their own benefits.
 
Ni maradhi tuu na yanaitwa schizophrenic paranoia. Kama ni kweli hao alshabab ni "al-qaeda affiliates" basi hawawezi kukodiwa na mtu yoyote, serikali yoyote kwa ajili ya kupata pesa. Alqueda hawana historia ya kufanya mashambulizi ili kupata pesa kwa hiyo madai yanayotolewa kwamba al-shabab wamekodiwa kuwashambulia ni ya uongo, na yana lengo la kujinufaisha kisiasa.

Hivi wewe unadhani pesa wanazo pata kuendeshea mission zao wanatoa wapi?,hao ndio wanao itwa maharamia wa kisomali watekaji wa meli na watalii huko kenya,then wana demand madola
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom