Dokta Slaa aitisha Press Conference Iringa!

Mheshimiwa una tatizo la ufahamu tafuta Daktari, Umechemsha wewe kwa kupiga ramli badala ya kutuia hoja, si amini kuwa ni matokeo ya elimu ya kata, ila nashawishika uelewa wako una kasumba ya kupewa labda toka Lumumba. Anza kujikomboa kifikra ili hata unalosemaliwe na tija.

Katoka au kubaka CCM siyo suala, suala ni maamuzi ya busara kuachama na longo longo za mafsadi wanaomliki CCM. Sitta alibadili mawazo baada za kuona hana sifa ya kupata hata ukatibu kata wa CDM kwa unafiki wake.
Jadili hoja sio mimi. Nakushauri usome tena maneno ya Slaa, Sitta nafasi aliyo iomba hawakukataa.Ni Sitta mwenyewe ndio alibadili mawazo. Leo hii mnasema hafai wakati viongozi wenu walikua tayari kumpa cheo kikubwa CDM. Na kama Sitta kutaka kuhama CCM amekua mnafiki je hao walio hama watakua ni nini?
 
Hivi Sitta bado anaishi kwenye ile nyumba ya Spika? Pia ningetaka kujua kwanini Sitta aliona inafaa kujenga ofisi ya Spika jimboni kwake? Ina maana alikuwa amepanga kuwa Spika for life?
 
Kazi nzuri sana bt aache kuongea sana,hapatakuwa na tofauti kati yake na mropokaji
 
Congrats Dr. Slaa. Go on. Speak out with evidence si kama hao wanaobwabwaja hovyo!!!
 
images
images

Katika uchaguzi mkuu uliopita, Chadema kilikuja kutangaza mwanachama wa kumsimamisha kugombea kiti cha Urais mwishoni kabisa baada ya kumwangukia na kumsihi Dr. Slaa agombee ambaye alishachukua tayari form za kugombea ubunge katika jimbo lake la uchaguzi.

Hii inatoa taswira kamili ya kila ambacho Katibu Mkuu wa Chadema alichosema Samweli Sitta alikubaliana nao kuwa atagombea Urais kupitia Chadema, lakini akawaacha kwenye mataa dakika za majeruhi, na wakati huo huo alikuwa ndiye mwanzilishi wa CCJ.

Kipindi cha Kampeni katika uchaguzi Mkuu uliopita, Dr. Slaa mara kadhaa alimwanika Samweli Sitta kwamba si mkweli, mnafiki, ana tabia ya hadaa, hana msimamo, ni ndumila kuwili mambo ambayo leo ameamua kumwaga mtama kwenye kuku wengi. Ukweli huu Sitta hawezi kuukwepa maana wakati uli alikuwa akifanya kampeni makanisani kwa kisingizio cha kuwa mgeni wa mahafali vyuo vya dini na matukio mengine ya dini ili kuungwa mkono.

Kwa nafasi kadhaa Sitta aliwahi kutamka kwamba ametafutwa na vyama kadhaa vya upinzani agombee uraisi, na akasema urais ni isue nzito na kuu ya yeye kubombaniwa na vyama vya upinzani.

Kuna dalili kwamba pamoja na kutaka kugombea huko, alikuwa hajiamini na hakuamini kama anaweza kumshinda Kikwete, na hivyo kuishia kutorokea mitaani kuwakwepa Chadema aliowaahidia, na mwishoni kabisa Chadema wakafanya kama zima moto kumwangukia Dr. Slaa ambaye tunavyojua aliweza kumtikisa Kikwete hadi kuchanganyikiwa na kuanza siasa za udini.

Naweza kusema lilikuwa kosa lenye heri kwa Sitta kukimbilia mafichoni, kwani angegombea huenda Chadema kisingepata kukua na kukubalika kama Dr. Slaa alivyokijenga hadi sasa.

Nahitimisha kwa kusema Samweli sitta ni ndumila kuwili, ni sawa na kinyonga anayejigeuza rangi kutegemeana na mazingira aliyo nayo, na akisha toka hapo hutaamini alivyobadilika rangi, labda amebaki na sura tu lakini rangi yake hubadilikabadilika. Sitta kigeugeu, ana tamaa ya madaraka, anajikweza, na pengine yaliyosababishwa yeye kuenguliwa na CCM kugombea uspika ni tabia hiyo ambayo wanaCCM waliona anaweza kuwageuka baadaye na pengine kutolinda masilahi ya chama. CCJ mwasisi halisi ni Sitta, akina Nape walitumiwa tu, na walipona wameingizwa kicha kichwa wakaamua nao kusepa.
 
nina uhakika nimesoma kuliko wewe.

Hahaa wala sitakubisha kwa hilo, lakini elewa moja ya serikali iliyowahi kuwa na maprofesa wengi na ikafeli kwa mda mchache ni ya Binaisa wa Uganda, ya pili ni ya Jakaya Kikwete na ccm yake,

Kumbuka ccm imejaa madaktari feki na maprofesa original na feki na imefeli kupindukia.

Lakini kumbuka zaidi, moja ya serikali iliyoundwa na DJ maarufu zaidi barani afrika na mwenye elimu ya yakiraia kabisa ndugu Andry Rajoelina baada ya kumung'oa Marc Ravalomanana, ndio iliyoleta mapinduzi na machipuko huru ya taifa la Madagascar, na leo nitaifa linalokua kidemokrasia na kiuchumi kwa kasi nzuri barani afrika.

Kwahiyo usomi si tiketi ya mema ya dunia, bali msaada wa tatu wa msukumo wa mema ya dunia.

1. Ubinadamu, 2. Utu, 3. Elimu
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hahaa wala sitakubisha kwa hilo, lakini elewa moja ya serikali iliyowahi kuwa na maprofesa wengi na ikafeli kwa mda mchache ni ya Binaisa wa Uganda, ya pili ni ya Jakaya Kikwete na ccm yake,

Kumbuka ccm imejaa madaktari feki na maprofesa original na feki na imefeli kupindukia.

Lakini kumbuka zaidi, moja ya serikali iliyoundwa na DJ maarufu zaidi barani afrika na mwenye elimu ya yakiraia kabisa ndugu Andry Rajoelina baada ya kumung'oa Marc Ravalomanana, ndio iliyoleta mapinduzi na machipuko huru ya taifa la Madagascar, na leo nitaifa linalokua kidemokrasia na kiuchumi kwa kasi nzuri barani afrika.

Kwahiyo usomi si tiketi ya mema ya dunia, bali msaada wa tatu wa msukumo wa mema ya dunia.

1. Ubinadamu, 2. Utu, 3. Elimu
Sasa kwanini unliniambia nirudi shule?
Dogo na wewe magwanda yashaanza kukuwasha nini?
Kayafue!!
 
Kwa Undani wa Kinachojiri Iringa Pitia hii Link

Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima

Kitu kamili ni hiki hapa:

DR SLAA AMTOLEA UVIVU WAZIRI SAMWEL SITTA, AFICHUA SIRI NZITO KATI YAKE NA SITTA





Katibu mkuu wa Chadema Dkt Slaa akionyesha baadhi ya vielelezo kwa wanahabari leo mjini Iringa

Dkt Slaa akiwa katika mkutano wake na wanahabari mkoa wa Iringa katika ukumbi wa Hoteli ya M.R


SIKU moja baada ya waziri wa Afrika Mashariki na mbunge wa jimbo la Urambo MasharikiSamwel Sitta kumrushia kombora mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe kuwa ,katibu mkuu wa Chadema Dkt Willbroad Slaa aibua tuhumanzito dhidi ya waziri Sitta amwita msaliti.

Dkt Slaa amedai kuwa waziri Sitta ndie alikuwa katika makubaliano ya kuja kugombea uspikakupitia Chadema ila alisaliti pamoja na kukubaliana vizuri kuwa angekihama chama chake CCM.

Dkt Slaa alitoa tuhuma hizo leo mjini Iringa alipozungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya M.R alisema ilikuwa Mei mwaka 2010, Sitta ambaye hivi sasa ni Waziri wa Afrika Mashariki alipokutana na viongozi wa Chadema na kuonesha dhamira ya kujitoa CCM na kujiunga na chama chao ila alionyesha usaliti wa hali ya juu.

Alisema kuwa katika mazungumzo hayo yaliyoendelea kufanywa katika kipindi chote cha bunge la bajeti lililokuwa la mwisho kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Dk Slaa alisema katika masharti yake ya kujiunga na Chadema, Sitta ambaye kwa wakati huo alikuwa Spika, alitaka apewe nafasi ya kuwania urais kupitia chama hicho na vikao vilikuwa vikifanyika ofisini kwake Dodoma.

Alisema ameamua kutoa siri hiyo baada ya kiongozi huyo (Sitta) kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari juzi akidai kwamba Dk Slaa ni mtu pekee ndani ya Chadema ambaye ni tishio kwa urais katika uchaguzi ujao, huku akimponda Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kwamba ni mchezesha disco.

Hata hivyo alisdai kushangazwa na waziri Sitta kuanza kuzungumzia mambo ya watu badala yakujibu hoja na kuwa Chadema haipendi kuzungumza habari za watu, inazunguma maendeleo. Kwa muda mrefu tumemuhifadhi Sitta lakini baada ya kupeleka mashambulizi sehemu isiyohusika sasa tunampiga ngumi za tumbo na uso

Dkt Slaa alisema kuwa wakati akitaka aandaliwe mazingira ya kujiunga na Chadema na kupewa nafasi ya kuwania urais, Sitta alidai ana kundi la wabunge zaidi ya 55 waadilifu kutoka katika chama hicho ambao angetoka nao pamoja CCM na kuhamia Chadema kabla ya bunge kuvunjwa.

Alisema kwa kuwa Chadema haina ubinafsi, ilihadi kuyafanyia kazi maombi yake ya kuwania urais kwa uzito mkubwa hata hivyo katika mazingira ya kushangaza aliwatelekeza.

Dk Slaa alisema Sitta ambaye uzoefu wake katika siasa na umakini wake katika kushughulikia maendeleo ya nchi umeanza kuwatia shaka watanzania, alisahau jinsi alivyowatelekeza kabla ya Uchaguzi Mkuu na baada ya uchaguzi huo akaja na hoja mpya kitaka Chadema wampe nafasi ya kuwania uspika kwa kile alichodai kuwepo kwa mizengwe ndani ya CCM.

Katika mazingira ya kushangaza badala ya kufikia uamuzi wake wa kuhamia Chadema kama dhamira yake ilivyomtuma, Sitta aliwatelekeza tena akidai kwamba atajiunga na chama hicho mpaka pale atakapokwenda jimboni kwake Urambo na kutangaza rasmi kujiondoa CCM.

Alisema kiongozi huyo aliyekuwa akitaka msaada wa viongozi wa Chadema ili afanikiwe kujiunga na chama hicho na hatimaye kupewa nafasi ya kuwania nyadhifa alizokuwa akitaka ameanza kuwatusi hadharani viongozi hao akiwemo Menyekiti wake Mbowe.

Alisema kauli inayotolewa na Sitta kwamba Mbowe ni mchezesha disco inadhihirisha jinsi asivyo makini jambo linalowafanya waanze kuitilia shaka elimu na uzoefu alionao katika kuendesha shughuli za serikali.

"Sita anataka kutuambia kwamba watu wanaocheza disco wakiwemo mawaziri wengi tu wanaokutwa kwenye kumbi za burudani wanatenda dhambi na ni uhalifu kufanya hivyo?," alisema.

Alisema kama biashara hiyo ya Mbowe inafanywa kinyume na sheria za nchi, serikali inasubiri nini kufuta leseni yake.
Kuhusu uongozi na namna ya kupata viongozi ndani ya chama hicho, Dk Slaa alisema sio kazi ya Sitta akuwapangia utaratibu.

"Sitta hajui kwamba duniani hakuna chuo cha kusomea uwaziri, ukatibu mkuu, na hajui kwamba Mwalimu Julius Nyerere hakuwa na uzoefu wakati akipewa madaraka ya kuongoza taifa hili na kwamba hata wasaidizi wake nao walipata uzoefu baada ya kupata madaraka," alisema.

Alisema Sitta ni kiongozi mnafiki na atakumbukwa zaidi alipokuwa Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwasababu kuna hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wabunge wa upinzani kuhusu ufisadi alizizima.

Alisema kuzimwa kwa hoja hizo ikiwemo ya Mkataba uliogubikwa na utata wa Buzwagi, unadhihirisha jinsi naye alivyotumia madaraka yake vibaya kwa kujenga ofisi ndogo ya Spika ambayo yeye aliita ya mbunge jimbo kwake Urambo.

Alisema wakati serikali imeridhia ofisi za wabunge zijengwe kwa kiasi cha fedha kisichozidi Sh Milioni 40 kwa kuzingatia upatikanaji wa fedha, ofisi hiyo ya Urambo ilijengwa kwa Sh Milioni 350.

"Kauli zinazotolewa na Sitta kuhusu chama chetu zinadhihirisha jinsi alivyomnafiki na asivyofaa jambo lililosababisha hata CCM wamemnyime nafasi ya kuwania kugombea kwa mara nyingone tena nafasi ya Uspika," alisema.

Dk Slaa na viongozi mbalimbali wa chama hicho wako mkoani hapa, wakisubiri waanza mikutano yao ya vugugugu la mabadiliko walilolipa jina la M4C baada ya kuzuiwa na jeshi la Polisi kufanya mikutano yao katika kipindi chote cha sensa.

Wakati huo huo Dkt Slaa ameshindwa kutolea ufafanuzi juu ya kiasi cha fedha walizotenga kwa ajili ya mikutano yao ya M4C inayoendelea hapa nchi huku akiishia kudai kuwa fedhazinazotumika ni fedha zinazotokana na ruzuku ya serikali na michango ya wananchi bila kutaja kiasi hicho cha fedha.
 
Sasa naweza kuunganisha doti jinsi wanasiasa wetu wanavyojiuza. Rafiki yangu mmoja (ni askari wa JW) aliwahi kunieleza Zitto alivyokuwa akifanya vikao tata hapa Dar na Dom na akina Rostam na Sitta so kuna mengi tutasikia baada ya Dokta kutoa kifuniko cha tanuru la ukweli
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Swala ni uadilifu na kuchapa kazi, tunacholia tz ni wizi uliokithiri pamoja na hamna mipango yoyote ya kushughulikia jambo hilo
 
Ni kuhusu M4C Iringa baada ya mvutano mkubwa na polisi. Tegemeeni Updates ya yatakachojili!

SISIEMU ni chama hatari sana sana kinapandikiza udini,ukabila na mauaji Tanzania,Chama hiki 2010 kilikataliwa sana mijini,lakini kwa sasa mpaka vijijini ndani ndani huko Maswa,Meatu,Bukombe,Ukerewa n.k.,wote wazee kwa vijana wamekikataa hawakitaki tena,hawataki hata kukisikia wanasema 2015 lazima wakichinjie baharini.
 
SISIEMU ni chama hatari sana sana kinapandikiza udini,ukabila na mauaji Tanzania,Chama hiki 2010 kilikataliwa sana mijini,lakini kwa sasa mpaka vijijini ndani ndani huko Maswa,Meatu,Bukombe,Ukerewe n.k.,wote wazee kwa vijana wamekikataa hawakitaki tena,hawataki hata kukisikia wanasema 2015 lazima wakichinjie baharini.
 
Back
Top Bottom