Dokta Slaa aitisha Press Conference Iringa!

SIKU moja baada ya waziri wa Afrika Mashariki na mbunge wa jimbo la Urambo Mashariki Samwel Sitta kumrushia kombora mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe kuwa ,katibu mkuu wa Chadema Dkt Willbroad Slaa aibua tuhuma nzito dhidi ya waziri Sitta amwita msaliti .
Dkt Slaa amedai kuwa waziri Sitta ndie alikuwa katika makubaliano ya kuja kugombea uspika kupitia Chadema ila alisaliti pamoja na kukubaliana vizuri kuwa angekihama chama chake CCM.
Dkt Slaa alitoa tuhuma hizo leo mjini Iringa alipozungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya M.R alisema ilikuwa Mei mwaka 2010, Sitta ambaye hivi sasa ni Waziri wa Afrika Mashariki alipokutana na viongozi wa Chadema na kuonesha dhamira ya kujitoa CCM na kujiunga na chama chao ila alionyesha usaliti wa hali ya juu.
Alisema kuwa katika mazungumzo hayo yaliyoendelea kufanywa katika kipindi chote cha bunge la bajeti lililokuwa la mwisho kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Dk Slaa alisema katika masharti yake ya kujiunga na Chadema, Sitta ambaye kwa wakati huo alikuwa Spika, alitaka apewe nafasi ya kuwania urais kupitia chama hicho na vikao vilikuwa vikifanyika ofisini kwake Dodoma.
Alisema ameamua kutoa siri hiyo baada ya kiongozi huyo (Sitta) kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari juzi akidai kwamba Dk Slaa ni mtu pekee ndani ya Chadema ambaye ni tishio kwa urais katika uchaguzi ujao, huku akimponda Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kwamba ni mchezesha disco.
Hata hivyo alisdai kushangazwa na waziri Sitta kuanza kuzungumzia mambo ya watu badala ya kujibu hoja na kuwa Chadema haipendi kuzungumza habari za watu, inazunguma maendeleo. Kwa muda mrefu tumemuhifadhi Sitta lakini baada ya kupeleka mashambulizi sehemu isiyohusika sasa tunampiga ngumi za tumbo na uso

Dkt Slaa alisema kuwa wakati akitaka aandaliwe mazingira ya kujiunga na Chadema na kupewa nafasi ya kuwania urais, Sitta alidai ana kundi la wabunge zaidi ya 55 waadilifu kutoka katika chama hicho ambao angetoka nao pamoja CCM na kuhamia Chadema kabla ya bunge kuvunjwa.
Alisema kwa kuwa Chadema haina ubinafsi, ilihadi kuyafanyia kazi maombi yake ya kuwania urais kwa uzito mkubwa hata hivyo katika mazingira ya kushangaza aliwatelekeza.
Dk Slaa alisema Sitta ambaye uzoefu wake katika siasa na umakini wake katika kushughulikia maendeleo ya nchi umeanza kuwatia shaka watanzania, alisahau jinsi alivyowatelekeza kabla ya Uchaguzi Mkuu na baada ya uchaguzi huo akaja na hoja mpya kitaka Chadema wampe nafasi ya kuwania uspika kwa kile alichodai kuwepo kwa mizengwe ndani ya CCM.
Katika mazingira ya kushangaza badala ya kufikia uamuzi wake wa kuhamia Chadema kama dhamira yake ilivyomtuma, Sitta aliwatelekeza tena akidai kwamba atajiunga na chama hicho mpaka pale atakapokwenda jimboni kwake Urambo na kutangaza rasmi kujiondoa CCM.
Alisema kiongozi huyo aliyekuwa akitaka msaada wa viongozi wa Chadema ili afanikiwe kujiunga na chama hicho na hatimaye kupewa nafasi ya kuwania nyadhifa alizokuwa akitaka ameanza kuwatusi hadharani viongozi hao akiwemo Menyekiti wake Mbowe.
Alisema kauli inayotolewa na Sitta kwamba Mbowe ni mchezesha disco inadhihirisha jinsi asivyo makini jambo linalowafanya waanze kuitilia shaka elimu na uzoefu alionao katika kuendesha shughuli za serikali.

“Sita anataka kutuambia kwamba watu wanaocheza disco wakiwemo mawaziri wengi tu wanaokutwa kwenye kumbi za burudani wanatenda dhambi na ni uhalifu kufanya hivyo?,” alisema.
Alisema kama biashara hiyo ya Mbowe inafanywa kinyume na sheria za nchi, serikali inasubiri nini kufuta leseni yake.
Kuhusu uongozi na namna ya kupata viongozi ndani ya chama hicho, Dk Slaa alisema sio kazi ya Sitta akuwapangia utaratibu.
“Sitta hajui kwamba duniani hakuna chuo cha kusomea uwaziri, ukatibu mkuu, na hajui kwamba Mwalimu Julius Nyerere hakuwa na uzoefu wakati akipewa madaraka ya kuongoza taifa hili na kwamba hata wasaidizi wake nao walipata uzoefu baada ya kupata madaraka,” alisema.
Alisema Sitta ni kiongozi mnafiki na atakumbukwa zaidi alipokuwa Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwasababu kuna hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wabunge wa upinzani kuhusu ufisadi alizizima.
Alisema kuzimwa kwa hoja hizo ikiwemo ya Mkataba uliogubikwa na utata wa Buzwagi, unadhihirisha jinsi naye alivyotumia madaraka yake vibaya kwa kujenga ofisi ndogo ya Spika ambayo yeye aliita ya mbunge jimbo kwake Urambo.
Alisema wakati serikali imeridhia ofisi za wabunge zijengwe kwa kiasi cha fedha kisichozidi Sh Milioni 40 kwa kuzingatia upatikanaji wa fedha, ofisi hiyo ya Urambo ilijengwa kwa Sh Milioni 350.
“Kauli zinazotolewa na Sitta kuhusu chama chetu zinadhihirisha jinsi alivyomnafiki na asivyofaa jambo lililosababisha hata CCM wamemnyime nafasi ya kuwania kugombea kwa mara nyingone tena nafasi ya Uspika,” alisema.
Dk Slaa na viongozi mbalimbali wa chama hicho wako mkoani hapa, wakisubiri waanza mikutano yao ya vugugugu la mabadiliko walilolipa jina la M4C baada ya kuzuiwa na jeshi la Polisi kufanya mikutano yao katika kipindi chote cha sensa.
Wakati huo huo Dkt Slaa ameshindwa kutolea ufafanuzi juu ya kiasi cha fedha walizotenga kwa ajili ya mikutano yao ya M4C inayoendelea hapa nchi huku akiishia kudai kuwa fedha zinazotumika ni fedha zinazotokana na ruzuku ya serikali na michango ya wananchi bila kutaja kiasi hicho cha fedha.

Sijaipenda hii approach. Haioneshi kama imetamkwa na PhD
 
Wameshasema kuwa uwaziri hauna experiance! hata mwalimu hakuwa na uzoefu wa kuwa raisi na pia timu yake haikuwa na uzoefu wakati wanapewa madaraka mwaka 1961. au mkuu haujaona hoja hii?
Hii hoja sitta akipenda kuimaliza ataipangua kirahisi sana.atasema ni kweli alitaka kugombea ursis kupitiachadema ila aliona atapata shida kupanga safu kwa kuwa bench lipo shallow.
 
evidence ya kutaka kuuliwa uliziona? Evidence ya silaha za ccm uliziona? Labda kama ulienda mahakamani akaja kukuonyesha.

Hebu niambieni,ameleta jipya gani leo? Katika yote yanayo endelea kwenye siasa anakuja kujibishana na Sitta. Haya mambo ya mipasho ni kazi ya kina lema.

ulitaka anyamaze?
 
Si tulisikia alikua ametegea kuhamia ccj.au alitega kwingi?
Huyu sita anatisha kama kuna ukweli wowote hapa.
 
Serikali ya ccm isihangaike na chadema, kufanya hivyo nikutangaza rasmi kuwa ipo tayari kuwa chama cha upinzani Tanzania, Nawaomba wanachadema wenzangu furahieni pindi muonapo serikali inahangaika na chadema
 
Hizi kweli ni ngumi za uso na tumbo!... Sita hana msimamo!.. mara CCJ, CCM na CDM!...
 
Mbona slaa mwenyewe alihama CCM baada ya kupigwa chini? Mtei alikua chama gani?Kuhama chama ni jambo la kawaida kabisa. Sitta alibadili mawazo baada za kuona msimamo wa chama na ndio maana amekuja na kusema CDM hakuna kiongozi.
Slaa amechemsha hapo. Watu walitegemea atazungumzia matumizi ya M4C.
 
Mbona slaa mwenyewe alihama CCM baada ya kupigwa chini? Mtei alikua chama gani?Kuhama chama ni jambo la kawaida kabisa. Sitta alibadili mawazo baada za kuona msimamo wa chama na ndio maana amekuja na kusema CDM hakuna kiongozi.
Slaa amechemsha hapo. Watu walitegemea atazungumzia matumizi ya M4C.

Mheshimiwa una tatizo la ufahamu tafuta Daktari, Umechemsha wewe kwa kupiga ramli badala ya kutuia hoja, si amini kuwa ni matokeo ya elimu ya kata, ila nashawishika uelewa wako una kasumba ya kupewa labda toka Lumumba. Anza kujikomboa kifikra ili hata unalosemaliwe na tija.

Katoka au kubaka CCM siyo suala, suala ni maamuzi ya busara kuachama na longo longo za mafsadi wanaomliki CCM. Sitta alibadili mawazo baada za kuona hana sifa ya kupata hata ukatibu kata wa CDM kwa unafiki wake.
 
Mbona slaa mwenyewe alihama CCM baada ya kupigwa chini? Mtei alikua chama gani?Kuhama chama ni jambo la kawaida kabisa. Sitta alibadili mawazo baada za kuona msimamo wa chama na ndio maana amekuja na kusema CDM hakuna kiongozi.
Slaa amechemsha hapo. Watu walitegemea atazungumzia matumizi ya M4C.
Ni lini ccm kwa miaka 50 iliwahi kuanika matumizi yake?
 
Back
Top Bottom