Dokta Slaa aitisha Press Conference Iringa!

SIKU moja baada ya waziri wa Afrika Mashariki na mbunge wa jimbo la Urambo Mashariki Samwel Sitta kumrushia kombora mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe kuwa ,katibu mkuu wa Chadema Dkt Willbroad Slaa aibua tuhuma nzito dhidi ya waziri Sitta amwita msaliti .
Dkt Slaa amedai kuwa waziri Sitta ndie alikuwa katika makubaliano ya kuja kugombea uspika kupitia Chadema ila alisaliti pamoja na kukubaliana vizuri kuwa angekihama chama chake CCM.
Dkt Slaa alitoa tuhuma hizo leo mjini Iringa alipozungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya M.R alisema ilikuwa Mei mwaka 2010, Sitta ambaye hivi sasa ni Waziri wa Afrika Mashariki alipokutana na viongozi wa Chadema na kuonesha dhamira ya kujitoa CCM na kujiunga na chama chao ila alionyesha usaliti wa hali ya juu.
Alisema kuwa katika mazungumzo hayo yaliyoendelea kufanywa katika kipindi chote cha bunge la bajeti lililokuwa la mwisho kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Dk Slaa alisema katika masharti yake ya kujiunga na Chadema, Sitta ambaye kwa wakati huo alikuwa Spika, alitaka apewe nafasi ya kuwania urais kupitia chama hicho na vikao vilikuwa vikifanyika ofisini kwake Dodoma.
Alisema ameamua kutoa siri hiyo baada ya kiongozi huyo (Sitta) kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari juzi akidai kwamba Dk Slaa ni mtu pekee ndani ya Chadema ambaye ni tishio kwa urais katika uchaguzi ujao, huku akimponda Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kwamba ni mchezesha disco.
Hata hivyo alisdai kushangazwa na waziri Sitta kuanza kuzungumzia mambo ya watu badala ya kujibu hoja na kuwa Chadema haipendi kuzungumza habari za watu, inazunguma maendeleo. Kwa muda mrefu tumemuhifadhi Sitta lakini baada ya kupeleka mashambulizi sehemu isiyohusika sasa tunampiga ngumi za tumbo na uso

Dkt Slaa alisema kuwa wakati akitaka aandaliwe mazingira ya kujiunga na Chadema na kupewa nafasi ya kuwania urais, Sitta alidai ana kundi la wabunge zaidi ya 55 waadilifu kutoka katika chama hicho ambao angetoka nao pamoja CCM na kuhamia Chadema kabla ya bunge kuvunjwa.
Alisema kwa kuwa Chadema haina ubinafsi, ilihadi kuyafanyia kazi maombi yake ya kuwania urais kwa uzito mkubwa hata hivyo katika mazingira ya kushangaza aliwatelekeza.
Dk Slaa alisema Sitta ambaye uzoefu wake katika siasa na umakini wake katika kushughulikia maendeleo ya nchi umeanza kuwatia shaka watanzania, alisahau jinsi alivyowatelekeza kabla ya Uchaguzi Mkuu na baada ya uchaguzi huo akaja na hoja mpya kitaka Chadema wampe nafasi ya kuwania uspika kwa kile alichodai kuwepo kwa mizengwe ndani ya CCM.
Katika mazingira ya kushangaza badala ya kufikia uamuzi wake wa kuhamia Chadema kama dhamira yake ilivyomtuma, Sitta aliwatelekeza tena akidai kwamba atajiunga na chama hicho mpaka pale atakapokwenda jimboni kwake Urambo na kutangaza rasmi kujiondoa CCM.
Alisema kiongozi huyo aliyekuwa akitaka msaada wa viongozi wa Chadema ili afanikiwe kujiunga na chama hicho na hatimaye kupewa nafasi ya kuwania nyadhifa alizokuwa akitaka ameanza kuwatusi hadharani viongozi hao akiwemo Menyekiti wake Mbowe.
Alisema kauli inayotolewa na Sitta kwamba Mbowe ni mchezesha disco inadhihirisha jinsi asivyo makini jambo linalowafanya waanze kuitilia shaka elimu na uzoefu alionao katika kuendesha shughuli za serikali.

"Sita anataka kutuambia kwamba watu wanaocheza disco wakiwemo mawaziri wengi tu wanaokutwa kwenye kumbi za burudani wanatenda dhambi na ni uhalifu kufanya hivyo?," alisema.
Alisema kama biashara hiyo ya Mbowe inafanywa kinyume na sheria za nchi, serikali inasubiri nini kufuta leseni yake.
Kuhusu uongozi na namna ya kupata viongozi ndani ya chama hicho, Dk Slaa alisema sio kazi ya Sitta akuwapangia utaratibu.
"Sitta hajui kwamba duniani hakuna chuo cha kusomea uwaziri, ukatibu mkuu, na hajui kwamba Mwalimu Julius Nyerere hakuwa na uzoefu wakati akipewa madaraka ya kuongoza taifa hili na kwamba hata wasaidizi wake nao walipata uzoefu baada ya kupata madaraka," alisema.
Alisema Sitta ni kiongozi mnafiki na atakumbukwa zaidi alipokuwa Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwasababu kuna hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wabunge wa upinzani kuhusu ufisadi alizizima.
Alisema kuzimwa kwa hoja hizo ikiwemo ya Mkataba uliogubikwa na utata wa Buzwagi, unadhihirisha jinsi naye alivyotumia madaraka yake vibaya kwa kujenga ofisi ndogo ya Spika ambayo yeye aliita ya mbunge jimbo kwake Urambo.
Alisema wakati serikali imeridhia ofisi za wabunge zijengwe kwa kiasi cha fedha kisichozidi Sh Milioni 40 kwa kuzingatia upatikanaji wa fedha, ofisi hiyo ya Urambo ilijengwa kwa Sh Milioni 350.
"Kauli zinazotolewa na Sitta kuhusu chama chetu zinadhihirisha jinsi alivyomnafiki na asivyofaa jambo lililosababisha hata CCM wamemnyime nafasi ya kuwania kugombea kwa mara nyingone tena nafasi ya Uspika," alisema.
Dk Slaa na viongozi mbalimbali wa chama hicho wako mkoani hapa, wakisubiri waanza mikutano yao ya vugugugu la mabadiliko walilolipa jina la M4C baada ya kuzuiwa na jeshi la Polisi kufanya mikutano yao katika kipindi chote cha sensa.
Wakati huo huo Dkt Slaa ameshindwa kutolea ufafanuzi juu ya kiasi cha fedha walizotenga kwa ajili ya mikutano yao ya M4C inayoendelea hapa nchi huku akiishia kudai kuwa fedha zinazotumika ni fedha zinazotokana na ruzuku ya serikali na michango ya wananchi bila kutaja kiasi hicho cha fedha.
 
Movie ndo imeanza, naona Mh. Samwel Sitta umeanzisha vita. Hakika hufai kuwa Rais!
 
M4C IRINGA MJINI NI TAREHE 9.9.2012. Polisi wamepigwa bit kali sana!
 
Hii hoja sitta akipenda kuimaliza ataipangua kirahisi sana.atasema ni kweli alitaka kugombea ursis kupitiachadema ila aliona atapata shida kupanga safu kwa kuwa bench lipo shallow.
 
M4C mpaka imalize mikoa yote tutajua mengi na ccm itakua ndo inaaga madarakani. We r sick n tired of these bloodsuckers.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
***** huooo... Hadi makalioni sasa.. Huyu ndiye Dr wa ukweli bwana .. Tupe raha raia wako.. Hapa niko Shwaaaaaariii.. Dr u make my day... God bless u
 
Kumbe ndo maana alikuwa anaendesha bunge namna ile. naona alitaka kuuwa chama hili agombee kiulaini. Aisee Sitta siyo mchezo. Mzee wa standard na speed. Kumbe ni speed ya madaraka.
 
Ni kuhusu M4C Iringa baada ya mvutano mkubwa na polisi. Tegemeeni Updates ya yatakachojili!

SIKU moja baada ya waziri wa Afrika Mashariki na mbunge wa jimbo la Urambo Mashariki Samwel Sitta kumrushia kombora mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe kuwa ,katibu mkuu wa Chadema Dkt Willbroad Slaa aibua tuhuma nzito dhidi ya waziri Sitta amwita msaliti .
Dkt Slaa amedai kuwa waziri Sitta ndie alikuwa katika makubaliano ya kuja kugombea uspika kupitia Chadema ila alisaliti pamoja na kukubaliana vizuri kuwa angekihama chama chake CCM.
Dkt Slaa alitoa tuhuma hizo leo mjini Iringa alipozungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya M.R alisema ilikuwa Mei mwaka 2010, Sitta ambaye hivi sasa ni Waziri wa Afrika Mashariki alipokutana na viongozi wa Chadema na kuonesha dhamira ya kujitoa CCM na kujiunga na chama chao ila alionyesha usaliti wa hali ya juu.
Alisema kuwa katika mazungumzo hayo yaliyoendelea kufanywa katika kipindi chote cha bunge la bajeti lililokuwa la mwisho kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Dk Slaa alisema katika masharti yake ya kujiunga na Chadema, Sitta ambaye kwa wakati huo alikuwa Spika, alitaka apewe nafasi ya kuwania urais kupitia chama hicho na vikao vilikuwa vikifanyika ofisini kwake Dodoma.
Alisema ameamua kutoa siri hiyo baada ya kiongozi huyo (Sitta) kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari juzi akidai kwamba Dk Slaa ni mtu pekee ndani ya Chadema ambaye ni tishio kwa urais katika uchaguzi ujao, huku akimponda Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kwamba ni mchezesha disco.
Hata hivyo alisdai kushangazwa na waziri Sitta kuanza kuzungumzia mambo ya watu badala ya kujibu hoja na kuwa Chadema haipendi kuzungumza habari za watu, inazunguma maendeleo. Kwa muda mrefu tumemuhifadhi Sitta lakini baada ya kupeleka mashambulizi sehemu isiyohusika sasa tunampiga ngumi za tumbo na uso

Dkt Slaa alisema kuwa wakati akitaka aandaliwe mazingira ya kujiunga na Chadema na kupewa nafasi ya kuwania urais, Sitta alidai ana kundi la wabunge zaidi ya 55 waadilifu kutoka katika chama hicho ambao angetoka nao pamoja CCM na kuhamia Chadema kabla ya bunge kuvunjwa.
Alisema kwa kuwa Chadema haina ubinafsi, ilihadi kuyafanyia kazi maombi yake ya kuwania urais kwa uzito mkubwa hata hivyo katika mazingira ya kushangaza aliwatelekeza.
Dk Slaa alisema Sitta ambaye uzoefu wake katika siasa na umakini wake katika kushughulikia maendeleo ya nchi umeanza kuwatia shaka watanzania, alisahau jinsi alivyowatelekeza kabla ya Uchaguzi Mkuu na baada ya uchaguzi huo akaja na hoja mpya kitaka Chadema wampe nafasi ya kuwania uspika kwa kile alichodai kuwepo kwa mizengwe ndani ya CCM.
Katika mazingira ya kushangaza badala ya kufikia uamuzi wake wa kuhamia Chadema kama dhamira yake ilivyomtuma, Sitta aliwatelekeza tena akidai kwamba atajiunga na chama hicho mpaka pale atakapokwenda jimboni kwake Urambo na kutangaza rasmi kujiondoa CCM.
Alisema kiongozi huyo aliyekuwa akitaka msaada wa viongozi wa Chadema ili afanikiwe kujiunga na chama hicho na hatimaye kupewa nafasi ya kuwania nyadhifa alizokuwa akitaka ameanza kuwatusi hadharani viongozi hao akiwemo Menyekiti wake Mbowe.
Alisema kauli inayotolewa na Sitta kwamba Mbowe ni mchezesha disco inadhihirisha jinsi asivyo makini jambo linalowafanya waanze kuitilia shaka elimu na uzoefu alionao katika kuendesha shughuli za serikali.

“Sita anataka kutuambia kwamba watu wanaocheza disco wakiwemo mawaziri wengi tu wanaokutwa kwenye kumbi za burudani wanatenda dhambi na ni uhalifu kufanya hivyo?,” alisema.
Alisema kama biashara hiyo ya Mbowe inafanywa kinyume na sheria za nchi, serikali inasubiri nini kufuta leseni yake.
Kuhusu uongozi na namna ya kupata viongozi ndani ya chama hicho, Dk Slaa alisema sio kazi ya Sitta akuwapangia utaratibu.
“Sitta hajui kwamba duniani hakuna chuo cha kusomea uwaziri, ukatibu mkuu, na hajui kwamba Mwalimu Julius Nyerere hakuwa na uzoefu wakati akipewa madaraka ya kuongoza taifa hili na kwamba hata wasaidizi wake nao walipata uzoefu baada ya kupata madaraka,” alisema.
Alisema Sitta ni kiongozi mnafiki na atakumbukwa zaidi alipokuwa Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwasababu kuna hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wabunge wa upinzani kuhusu ufisadi alizizima.
Alisema kuzimwa kwa hoja hizo ikiwemo ya Mkataba uliogubikwa na utata wa Buzwagi, unadhihirisha jinsi naye alivyotumia madaraka yake vibaya kwa kujenga ofisi ndogo ya Spika ambayo yeye aliita ya mbunge jimbo kwake Urambo.
Alisema wakati serikali imeridhia ofisi za wabunge zijengwe kwa kiasi cha fedha kisichozidi Sh Milioni 40 kwa kuzingatia upatikanaji wa fedha, ofisi hiyo ya Urambo ilijengwa kwa Sh Milioni 350.
“Kauli zinazotolewa na Sitta kuhusu chama chetu zinadhihirisha jinsi alivyomnafiki na asivyofaa jambo lililosababisha hata CCM wamemnyime nafasi ya kuwania kugombea kwa mara nyingone tena nafasi ya Uspika,” alisema.
Dk Slaa na viongozi mbalimbali wa chama hicho wako mkoani hapa, wakisubiri waanza mikutano yao ya vugugugu la mabadiliko walilolipa jina la M4C baada ya kuzuiwa na jeshi la Polisi kufanya mikutano yao katika kipindi chote cha sensa.
Wakati huo huo Dkt Slaa ameshindwa kutolea ufafanuzi juu ya kiasi cha fedha walizotenga kwa ajili ya mikutano yao ya M4C inayoendelea hapa nchi huku akiishia kudai kuwa fedha zinazotumika ni fedha zinazotokana na ruzuku ya serikali na michango ya wananchi bila kutaja kiasi hicho cha fedha.
 
Hii hoja sitta akipenda kuimaliza ataipangua kirahisi sana.atasema ni kweli alitaka kugombea ursis kupitiachadema ila aliona atapata shida kupanga safu kwa kuwa bench lipo shallow.

Angalia mtiririko wa hoja 1. msaliti wa chama chake, 2. anatafuta madaraka si uongozi 3. wakati anajua ubabaishaji na mizengwe ya CCM hachukui hatua. 4 Hajagundua kwa nini CCM wanamhitaji;ni kwa kumtumia kama mgambo wanaotangulizwa na jeshi wakati wa mapambano.

Ana haki ya kuzipangua hoja hata kwa upuuzi
 
Kumbe ndo maana alikuwa anaendesha bunge namna ile. naona alitaka kuuwa CCM ili agombee kiulaini. Aisee Sitta siyo mchezo. Mzee wa standard na speed. Kumbe ni speed ya madaraka. Lakini naona ni makini maana CCJ ni yeye na sasa Chadema. Mwaka 2015 CCM muonee huruma jamani angalau agombee.
 
Sitta ameanza kufa taratibu na bahati mbaya wenzake wanaanzaga kufa macho, miguu kugoma n.k yeye anaanza kufa UBONGO....magamba wamekwisha , hata huyu aliekua anaonesha dalili njema kumbe nae ni mahututi wa kupelekwa MILEMBE.
 
huwa nasema kila siku Sita ni fisadi tu tizama hapa tegeta masite{NYAISHOZI}amehodhi aridhi kubwa wala hakuna kitu anaifanyia zaidi ni kijishule tu hapa ndio kafungua cha msingi huyu nae ni fisadi tu.
 
Siasa ni mchezo mchafu. Kwa lugha mbofumbofu alizozitoa Sitta kwa viongozi wa chadema huwezi kuamini kwamba huko nyuma aliweza kukaa nao meza moja tena kirafiki na kupanga mipango ya 'kuihujumu' ccm. Kweli tumbo halina mshindani!
 
evidence ya kutaka kuuliwa uliziona? Evidence ya silaha za ccm uliziona? Labda kama ulienda mahakamani akaja kukuonyesha.

Hebu niambieni,ameleta jipya gani leo? Katika yote yanayo endelea kwenye siasa anakuja kujibishana na Sitta. Haya mambo ya mipasho ni kazi ya kina lema.

Sijawahi ona wala kusikia wanaenda mahakamani ili apeleke ushahidi kule.
Ingekuwa uongo si wangeenda na kufungua kesi? Toka list of shame mwembeyanga hadi leo hakuna aliyeenda mahakamani hata mmoja!
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom