Dkt. Slaa: Tusitegemee muujiza kwenye kitu kinachoitwa Katiba

Hakuna anayetegemea "muujiza" na katiba mpya. Kinachotakiwa ni katiba inayozuia mtu kuwa mungu juu ya watu waliomweka kwenye madaraka na kuwageuza kuwa mateka wake.
Katiba hiyo ikiwepo, huyo mtu akiisigina hatua zitachukuliwa juu yake, ziwe za kisheria au vinginevyo, kwa sababu yeye atakuwa ni mhalifu.

Huyo Dr Mihogo hana 'credibility' yoyote aliyobaki nayo kuwaambia waTanzania nini cha kufanya. Yeye ni mfano sahihi ya watu ambao hawana soni mbele za watu waliomwamini, na ni mfano mzuri wa viongozi wanaotakiwa kufungwa gavana na katiba iliyo bora.

Ila ninakubaliana na hayo yaliyoandikwa kwenye huo mstari mmoja hapo juu.

"Ili chama cha siasa kipendwe na wananchi, hakina budi kuwa na agenda zinazogusa umma".

Sasa awaeleze waTanzania kama CCM hii inazo agenda hizo!

Ingekuwa hivyo wasingeng'ang'ania katiba wanayoitumia kuwanyanyasa wananchi.
Now that wameshamtoa ubalozini… yuko chama gani?

Maana alijivuruga sana
 
Kama hii katiba iliyopo inakiukwa wazi wazi namna hii na hamna lolote la maana linalofanyika kupinga ukiukwaji huo, hiyo katiba mpya inahitajika ili iweje?

Mara karibu zote ambapo katiba imeonekana kukiukwa, hakuna cha maana ambacho wananchi tumefanya zaidi ya kujimwambafy humu kwenye mitandao.

Hakuna aliyethubutu kuingia barabarani na kupinga. Hakuna aliyefungua kesi mahakamani. Tumelia lia tu humu mitandaoni.

Sasa hiyo katiba mpya tukiipata, ikikiukwa ndo itatuwezesha kupata ujasiri wa kupinga kukiukwa kwake?

Nimeanza kudhani pengine tatizo letu si katiba mpya pekee. Tatizo letu kubwa ni sisi wenyewe. Tunaachia tu mambo yaende hata kama yapo kinyume na katiba.

A new constitution will not be worth the paper it’s written on if we allow and let the one we have to be breached with impunity!
 
Ni Nani anataka kumsikiliza Dr mihogo

Nani anaetaka msikiliza jamaa alieshikwa akili na mkewe

He is finished
 
Wazee aina ya Slaa ni zaidi ya laana maana sio mfano bora kwa jamii.
1. Alikikana kiapo cha kanisa kwa ajili ya tamaa za mwili tuu.
2. Aliwakana mke na watoto wake kwa sababu ya mwanamke mwingine kimada.
3. Alikikana chama na vile alivyopigania kwa kushawishiwa kwa vipande vya fedha na ahadi ya nafasi kuponya tumbo lake na mchumba wa uzeeni.
4. Alimkebehi mwenzake waliyekuwa naye kikazi na kirafiki (Lissu) alipofanyiwa shambulizi lenye lengo la kumuua likaishia kumlaza kitandani zaidi ya mwaka, operesheni 25 na ulemavu juu.
Jee mzee wa aina hiyo anafaa kuwa mfano mwema katika jamii?
Kuna watu wanafanya reference kuwa alipokuwa Chadema alifanya hiki na kile so what? Sii alikuwa analipwa mshahara na marupurupu kibao?
Na alipwaye mshahara anapaswa kufanya nini kama sio kazi at his best performance?
Atuache tuna mengi ya muhimu sana
TUWEKANE SAWA
Lowassa hakuja bure CHADEMA bali alikuja kwa fedha yake ambbayo ni hiyo Tsh 10 Billion. Mkakati wa UPINZANI mwaka 2015 ilikuwa through UKAWA.

Kwa Rais wa Muungano Dr Slaa alikuwa tayari popular kuliko mgombea yeyote yule. Mbowe na CDM walitumia muda wao wote wa 2008 hadi 2015 kumpakaza matope Lowassa kuwa ni FISADI kwa ile kashfa ya RICHMOND. Isingekuwa rahisi kimpokea hivihivi kwa kisingizio kuwa eti ndiye mgombea pekee anayeweza kuishinda CCM kwa mwaka ule. Huo ulikuwa ni uwongo tu kutetea hiyo fedha waliyochukua kwa Lowassa na kugawana na Baba mkwe wake Mtei na mgombea wa ZNZ Maalim Seif.

Hawa akina Lissu na Mnyika walipata kiasi cha mboga tu kufunga mdomo. Ukitaka ushahidi tafuta zile picha mtoto wa Mbowe alikuwa anasafiri First Class kwenye Emirates Air kwenda Hongkong kati ya September na December 2015. Alikwenda kuweka hela kwenye akaunti iliyopo benki ya HSBC.

Na hiyo ndiyo sababu iliyomchefua Dr Slaa na Prof Lipumba ambao jamii inawaona ni wasaliti wa UPINZANI mpaka sasa. Ni fedha tu no more
 
Hakuna anayetegemea "muujiza" na katiba mpya. Kinachotakiwa ni katiba inayozuia mtu kuwa mungu juu ya watu waliomweka kwenye madaraka na kuwageuza kuwa mateka wake.
Katiba hiyo ikiwepo, huyo mtu akiisigina hatua zitachukuliwa juu yake, ziwe za kisheria au vinginevyo, kwa sababu yeye atakuwa ni mhalifu.

Huyo Dr Mihogo hana 'credibility' yoyote aliyobaki nayo kuwaambia waTanzania nini cha kufanya. Yeye ni mfano sahihi ya watu ambao hawana soni mbele za watu waliomwamini, na ni mfano mzuri wa viongozi wanaotakiwa kufungwa gavana na katiba iliyo bora.

Ila ninakubaliana na hayo yaliyoandikwa kwenye huo mstari mmoja hapo juu.

"Ili chama cha siasa kipendwe na wananchi, hakina budi kuwa na agenda zinazogusa umma".

Sasa awaeleze waTanzania kama CCM hii inazo agenda hizo!

Ingekuwa hivyo wasingeng'ang'ania katiba wanayoitumia kuwanyanyasa wananchi.
Kama mtu hajakuelewa hapa, aelezwe kwa kilugha chake.
 
Mkulima mvivu mwenye njaa anayelalamikia mpini wa jembe hata ukimpa trekta atapata sababu ya kulalamika mwishowe njaa haitamuacha sababu ni mvivu.
 
Ukitaka kunyanyua jinsia, ni suala lisilokuja kwa miujiza, hapa Tanzania mnaona ni jambo la ajabu
Kwanini wanawake wanalipwa ujira mdogo kuliko wanaume kwa kazi ileile kama kweli kuna usawa!!!?
 
Back
Top Bottom