Dkt. Slaa: Tusitegemee muujiza kwenye kitu kinachoitwa Katiba

Hivi huyu mzee kuhamia canada na lipumba kuhamia kigali shida ilikuwa nini hasa, na kilichowarudisha ni nini? kweli pesa inanunua utu.....
 
Kwani nani amemwambia kuwa wananchi wanataka katiba mpya ili iwaletee miujiza?
Ana maanisha kwamba katiba mpya haiwezi kubadilisha mahusiano kati ya wananchi na chama chochote cha siasa. Inabidi wajipange upya kisera ili waweze kuwashawishi wananchi
 
Na hapo utaambiwa aliteleza.Alijaribu kuficha ujinga wake kwa muda.Kwa kununuliwa kwa vipande vya pesa tu alionekana kabaki mtupu.

-Slaa alikejeli kupigwa risasi kwa Lissu na kusema ni kawaida tu hata mataifa mengine watu hupigwa risasi.Wakati yeye alikung'utwa rungu la mkono na polisi hadi Leo anatembea kama mkono ulibanikwa kwenye moto.

-Leo tena haitaki katiba mpya ilhali aliitaka akiwa CHADEMA!

Siwezi sema ni uzee.Kuna kitu hakijakaa sawa kichwani au ni laana ya usaliti.
Huyu mzee nikikumbuka kampeni zake za mwaka 2010 pale jangwan dah.
 
Sawa kila mtu ana uhuru wa kutoa maon na Dr slaa n moja ya wanasiasa wenye msimamo lakin sote tunajua anatafuta ulaji mpya baada ya chakula chake kuelekea ku expire
 
Ccm kwa kutunga upuuzi hamjambo na sijui kwanini?.alienda na ndege hahahaa. Lipumba alipelekwa Rwanda na nani? Na slaa alipelekwa Canada na nani? Slaa adi video zipo akiwa na mwakiembe na jinsi wanavyopanga watafanyaje Ile preas. Mkuu usituaminishe upuuzi wakati Kuna vitu tuliviona kwa macho yetu
Hawa walinunuliwa na nani?

Screenshot_20210916-123456.png
 
Huyu mzee nikikumbuka kampeni zake za mwaka 2010 pale jangwan dah.
Huyo jamaa alikuwa anawaza kuwa president na akakwama!Angetulia "yawezekana" angefaulu.Hawara yake aliyempiga "shuntama waitu" ndiye alimkwamisha.😝😝😝😂😂
 
"Ili chama cha siasa kipendwe na wananchi, hakina budi kuwa na agenda zinazogusa umma"

====

Balozi wa Tanzania nchini Sweden anayemaliza muda wake, Dk Wilbrod Slaa, amesema suala la Katiba Mpya ni muhimu, lakini linahitaji maandalizi ya kutosha na ya msingi.

Dk Slaa ameyasema hayo katika mahojiano yake na Mwananchi, ikiwa ni siku chache kabla ya kumaliza muda wake wa ubalozi nchini humo na kusema kuwa Katiba si jibu la kitu na Tanzania haiwezi kuacha kila kitu kwa ajili ya kuwa na Katiba Mpya.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini Ikulu Juni 28, Rais Samia aliulizwa kuhusu kuendeleza mchakato wa Katiba Mpya, lakini alionyesha kuliweka kando suala hilo akisema kuwa kwa sasa anataka kupata muda wa kuimarisha uchumi.

Akizungumzia suala hilo la Katiba, Dk Slaa alisema: “Tusitegemee muujiza kwenye kitu kinachoitwa Katiba, lakini inataka maandalizi mazuri, tunachotaka kukifanya sasa ni zimamoto. Unaweza kuandaa kitu nusu nusu ukapata madhara. Lakini hayo majibu yangu hayamaanishi kuwa Katiba si muhimu.’’

Kuhusu mwenendo wa siasa za upinzani kwa sasa, Dk Slaa alisema, asingependa kubeba mzigo wa kushauri akiwa nje ya siasa, lakini hata hivyo, jambo la msingi kwa chama siasa ni kuwa na ajenda.

Dk Slaa ambaye aliwahi kuwa Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa Chadema na mgombea wa urais kupitia chama hicho alisema, ili chama cha upinzaji kipendwe na wananchi hakina budi kuwa na ajenda zinazogusa umma.

“Mkienda kwenye ajenda zisigusa umma Watanzania hawatawatazama, hata kama mngekuwa na Katiba Mpya kesho,” alisema na kuongeza:

“Hili Taifa tunahitaji kulibeba wote, kila mmoja ana mchango wake unaohitajika; kila mmoja anatakiwa kurekebisha dosari zilizopo, robo tatu ya dosari zilizopo, lakini kila mmoja afanye kazi eneo lake.”

Dk Slaa alisema wapinzani nao ni Watanzania, lakini upinzani haupo Tanzania peke yake, hata nchi zilizoendelea zina upinzani.

“Hata nchi za Ulaya zina upinzani na bado zinapaza sauti kuhusu haki za binadamu, hivi wangapi mnajua Denmark iliwahi kupelekewa watunza amani’?” alisema.

Mwananchi lilimuuliza pia ikiwa bado ana nia ya kugombea urais, alisema:

“Hotuba yangu Septemba Mosi 2015 mnaikumbuka. Usitafute uchawi. Mimi ni mwanasiasa anayejua siasa, ambaye akishatoa kauli habadiliki habadiliki, labda kulingana na mazingira, sina nia ya kurudi katika ‘actual’ politics” (siasa majukwaani).

Kadhalika Dk Slaa alipoulizwa kuhusu maoni ya wadau kwamba demokrasia na haki za binadamu zinakandamizwa nchini hasa pale Jeshi la Polisi linapowazuia wafuasi wa vyama vya upinzani, huku likiwaruhusu wa chama tawala, Dk Slaa alisema msingi mkubwa ni kujua sheria na taratibu za nchi zinataka nini.

“Ni muhimu kujiuliza je, hii haki tunazolalamikia kwa wengine, je, mimi nipo sawa? Utanyoosha kidole kimoja kwa mwingine na vidole vitatu vinakugeukia wewe ni muhimu kama Taifa kutafuta mustakabali wa pamoja,” alisema

Alisema wakati akiwa kwenye siasa, Halmashauri ya Karatu, ilitaka kufutwa kwa barua, lakini hakufanya mgogoro wala kugombana bali kama chama waliangalia sheria inasema nini.

“Nafikiri kila mmoja akicheza vizuri mahali pake kwa umakini, mengine yote ya kuvurugana hayatakuwepo. Watanzania tujue haki zetu, tuna nafasi pana lakini hatuzitumii,” alisema

Dk Slaa aliongeza na kusema, hata bila Katiba Mpya wakati ule akiwa mbunge wa Karatu, alishirikiana na wananchi na kupigania haki iliyosababisha hiyo isifutwe.

Wanawake na uongozi

Kuhusu Rais Samia kuonyesha nia ya kugombea tena urais 2025, alisema:

“Ukitaka kunyanyua jinsia, ni suala lisilokuja kwa miujiza, hapa Tanzania mnaona ni jambo la ajabu lakini hapahapa Sweden, wanawake wanashika nafasi za juu, hata Finnland waziri mkuu ni mwanamke na Denmark waziri mkuu ni mwanamke.”

Dk Slaa alisema wanawake wameiva kwa kuwa katika nafasi za juu za uongozi, na kwamba Rais Samia ameiweka Tanzania katika ramani ya kimataifa.

“Mama alichosema, ni kwamba anatekeleza maazimio ya mkutano wa Beijing, kwa kuichukua ajenda ya miaka 20 iliyopita, tangu mwaka ule hatukupata mtu makini wa kumuunga mkono mama Getrude Mongela, lakini sasa Samia ametekeleza yale maazimio.”alisema

Pamoja na kugusia demokrasia, upinzani na masuala ya jinsia, aidha, Dk Slaa alizungumzia kile kinachosemwa na baadhi ya watu kuhusu tofauti ya uongozi kati ya Rais Samia na mtangulizi wake.

“Mama Samia ametembea katika nyayo za JPM.Kwa mfano, kuhusu chanjo ya Covid-19, ameunda timu ya watalaamu ambao walifanya uchunguzi kuhusu ubora na kujiridhisha kabla ya kuitumia,” alisema

Alisema hata hayati John Magufuli alisema ni muhimu kujiridhisha kwanza kwa kufanya utafiti kabla ya kuleta chanjo hiyo.

Kuhusu safari za nje ya nchi za Rais Samia, Dk Slaa alisema huo ulikuwa ni utaratibu uliokuwepo tangu awali kwa hayati Magufuli kufanya kazi za ndani, huku Samia akifanya za kidiplomasia.

“Mimi sijaona tofauti. Pia usisahau kuwa viongozi wawili hawatafanana kwa asilimia 100, iwe ni kwa kauli, kimtazamo , upole au ukali. Hata siku moja hawawezi kufanana kwa kila kitu,”alisema

Chanzo: Mwananchi.
Spidi ya Dr. Slaa kudai katiba mpya akiwa Chadema ilikuwa kubwa kuliko sasa akiwa CCM. Kiuhalisia na kwa maoni yangu, madai ya katiba mpya yanachagizwa na changamoto za kisiasa (hasa wanazopata wapinzani) kwa 75% zaidi kuliko changamoto za kiuchumi na kijamii. Nijuavyo, katiba ni agenda mtambuka, madai yake yanapaswa kwenda mbali zaidi ya siasa. Naamini siyo rahisi leo kwa wanasiasa hasa wa upinzani kuacha kuakisi madai ya katiba mpya kwenye siasa na kuyaakisi kwenye masuala ya uchumi-jamii. Chagizo za madai ya katiba mpya zina msingi wake kwenye agenda ya uchaguzi kwa asilima kubwa (hata Kenya Raila alifanya hivi hivi japo hakufanikiwa kuingia ikulu ambapo hata baada ya kupata katiba mpya aliyoiasisi yeye bado hakuridhika na kutulia, hii inadhihirisha kwamba kumbe katiba ni mtambuka zaidi ya kwenda ikulu). Ni ukweli kwamba leo hii akitokea kiongozi Tz atakayehakikisha usawia katika uwanja wa siasa za uchaguzi na demokrasia, madai ya katiba mpya yatachukuwa kasi ndogo bila ya kujali kwamba taifa bado lina changamoto kubwa za uchumi-jamii.

Ni maoni yangu sawa na ibara ya 18(1) ya katiba ya JMT ya 1977 (kama ilivyorekebishwa 2005).
 
Hata humu anaogopa kuingia kule Twitter account yake iko dormant. Anajua hana hoja ndiyo sababu anahofia mijadala mtandaoni kama alivyokuwa anashiriki miaka ya nyuma.

Huyu naye ni spent force, hana lolote kichwani. AAkifanya mchezo anarudi Bongo kulim bamia maana huku hakuna supermarket atafanya kazi kama Canada! Ignore this nonsense man
 
Wazee aina ya Slaa ni zaidi ya laana maana sio mfano bora kwa jamii.

1. Alikikana kiapo cha kanisa kwa ajili ya tamaa za mwili tuu.
2. Aliwakana mke na watoto wake kwa sababu ya mwanamke mwingine kimada.
3. Alikikana chama na vile alivyopigania kwa kushawishiwa kwa vipande vya fedha na ahadi ya nafasi kuponya tumbo lake na mchumba wa uzeeni.
4. Alimkebehi mwenzake waliyekuwa naye kikazi na kirafiki (Lissu) alipofanyiwa shambulizi lenye lengo la kumuua likaishia kumlaza kitandani zaidi ya mwaka, operesheni 25 na ulemavu juu.

Je, mzee wa aina hiyo anafaa kuwa mfano mwema katika jamii?

Kuna watu wanafanya reference kuwa alipokuwa Chadema alifanya hiki na kile so what? Sii alikuwa analipwa mshahara na marupurupu kibao?

Na alipwaye mshahara anapaswa kufanya nini kama sio kazi at his best performance?

Atuache tuna mengi ya muhimu sana
Alipokuwa CHADEMA alikuwa adui mkubwa sana wa CCM. Alitajwa kama ajenti wa Vatican mwenye misheni ya kuhakikisha Tanzania inatawaliwa na "mfumo Katoliki". Hapa JF mada za kumponda zilivunja rekodi. Aliitwa daktari wa kanoni, mzinzi, n.k. Hata Mbowe alisahaulika kama kiongozi wa chama. Alivyohamia CCM tu watu walewale wanadai CHADEMA na upinzani vilikufa Slaa "alipotimuliwa" CHADEMA. Wanadai alipoondoka nao wakaamua "kuachana na siasa"; "bora kutawaliwa na CCM". Wanamtukuza kama ndio "mpinzani pekee wa kweli aliyepata kutokea Tanzania"! This is pure BS!
 
Ana maanisha kwamba katiba mpya haiwezi kubadilisha mahusiano kati ya wananchi na chama chochote cha siasa. Inabidi wajipange upya kisera ili waweze kuwashawishi wananchi
Unaamini katika hilo aliloongea?Kijamaa halafu kizee kisanii.Let him rot in hell!😂😂😂😂
 
"Ili chama cha siasa kipendwe na wananchi, hakina budi kuwa na agenda zinazogusa umma"

====

Balozi wa Tanzania nchini Sweden anayemaliza muda wake, Dk Wilbrod Slaa, amesema suala la Katiba Mpya ni muhimu, lakini linahitaji maandalizi ya kutosha na ya msingi.

Dk Slaa ameyasema hayo katika mahojiano yake na Mwananchi, ikiwa ni siku chache kabla ya kumaliza muda wake wa ubalozi nchini humo na kusema kuwa Katiba si jibu la kitu na Tanzania haiwezi kuacha kila kitu kwa ajili ya kuwa na Katiba Mpya.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini Ikulu Juni 28, Rais Samia aliulizwa kuhusu kuendeleza mchakato wa Katiba Mpya, lakini alionyesha kuliweka kando suala hilo akisema kuwa kwa sasa anataka kupata muda wa kuimarisha uchumi.

Akizungumzia suala hilo la Katiba, Dk Slaa alisema: “Tusitegemee muujiza kwenye kitu kinachoitwa Katiba, lakini inataka maandalizi mazuri, tunachotaka kukifanya sasa ni zimamoto. Unaweza kuandaa kitu nusu nusu ukapata madhara. Lakini hayo majibu yangu hayamaanishi kuwa Katiba si muhimu.’’

Kuhusu mwenendo wa siasa za upinzani kwa sasa, Dk Slaa alisema, asingependa kubeba mzigo wa kushauri akiwa nje ya siasa, lakini hata hivyo, jambo la msingi kwa chama siasa ni kuwa na ajenda.

Dk Slaa ambaye aliwahi kuwa Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa Chadema na mgombea wa urais kupitia chama hicho alisema, ili chama cha upinzaji kipendwe na wananchi hakina budi kuwa na ajenda zinazogusa umma.

“Mkienda kwenye ajenda zisigusa umma Watanzania hawatawatazama, hata kama mngekuwa na Katiba Mpya kesho,” alisema na kuongeza:

“Hili Taifa tunahitaji kulibeba wote, kila mmoja ana mchango wake unaohitajika; kila mmoja anatakiwa kurekebisha dosari zilizopo, robo tatu ya dosari zilizopo, lakini kila mmoja afanye kazi eneo lake.”

Dk Slaa alisema wapinzani nao ni Watanzania, lakini upinzani haupo Tanzania peke yake, hata nchi zilizoendelea zina upinzani.

“Hata nchi za Ulaya zina upinzani na bado zinapaza sauti kuhusu haki za binadamu, hivi wangapi mnajua Denmark iliwahi kupelekewa watunza amani’?” alisema.

Mwananchi lilimuuliza pia ikiwa bado ana nia ya kugombea urais, alisema:

“Hotuba yangu Septemba Mosi 2015 mnaikumbuka. Usitafute uchawi. Mimi ni mwanasiasa anayejua siasa, ambaye akishatoa kauli habadiliki habadiliki, labda kulingana na mazingira, sina nia ya kurudi katika ‘actual’ politics” (siasa majukwaani).

Kadhalika Dk Slaa alipoulizwa kuhusu maoni ya wadau kwamba demokrasia na haki za binadamu zinakandamizwa nchini hasa pale Jeshi la Polisi linapowazuia wafuasi wa vyama vya upinzani, huku likiwaruhusu wa chama tawala, Dk Slaa alisema msingi mkubwa ni kujua sheria na taratibu za nchi zinataka nini.

“Ni muhimu kujiuliza je, hii haki tunazolalamikia kwa wengine, je, mimi nipo sawa? Utanyoosha kidole kimoja kwa mwingine na vidole vitatu vinakugeukia wewe ni muhimu kama Taifa kutafuta mustakabali wa pamoja,” alisema

Alisema wakati akiwa kwenye siasa, Halmashauri ya Karatu, ilitaka kufutwa kwa barua, lakini hakufanya mgogoro wala kugombana bali kama chama waliangalia sheria inasema nini.

“Nafikiri kila mmoja akicheza vizuri mahali pake kwa umakini, mengine yote ya kuvurugana hayatakuwepo. Watanzania tujue haki zetu, tuna nafasi pana lakini hatuzitumii,” alisema

Dk Slaa aliongeza na kusema, hata bila Katiba Mpya wakati ule akiwa mbunge wa Karatu, alishirikiana na wananchi na kupigania haki iliyosababisha hiyo isifutwe.

Wanawake na uongozi

Kuhusu Rais Samia kuonyesha nia ya kugombea tena urais 2025, alisema:

“Ukitaka kunyanyua jinsia, ni suala lisilokuja kwa miujiza, hapa Tanzania mnaona ni jambo la ajabu lakini hapahapa Sweden, wanawake wanashika nafasi za juu, hata Finnland waziri mkuu ni mwanamke na Denmark waziri mkuu ni mwanamke.”

Dk Slaa alisema wanawake wameiva kwa kuwa katika nafasi za juu za uongozi, na kwamba Rais Samia ameiweka Tanzania katika ramani ya kimataifa.

“Mama alichosema, ni kwamba anatekeleza maazimio ya mkutano wa Beijing, kwa kuichukua ajenda ya miaka 20 iliyopita, tangu mwaka ule hatukupata mtu makini wa kumuunga mkono mama Getrude Mongela, lakini sasa Samia ametekeleza yale maazimio.”alisema

Pamoja na kugusia demokrasia, upinzani na masuala ya jinsia, aidha, Dk Slaa alizungumzia kile kinachosemwa na baadhi ya watu kuhusu tofauti ya uongozi kati ya Rais Samia na mtangulizi wake.

“Mama Samia ametembea katika nyayo za JPM.Kwa mfano, kuhusu chanjo ya Covid-19, ameunda timu ya watalaamu ambao walifanya uchunguzi kuhusu ubora na kujiridhisha kabla ya kuitumia,” alisema

Alisema hata hayati John Magufuli alisema ni muhimu kujiridhisha kwanza kwa kufanya utafiti kabla ya kuleta chanjo hiyo.

Kuhusu safari za nje ya nchi za Rais Samia, Dk Slaa alisema huo ulikuwa ni utaratibu uliokuwepo tangu awali kwa hayati Magufuli kufanya kazi za ndani, huku Samia akifanya za kidiplomasia.

“Mimi sijaona tofauti. Pia usisahau kuwa viongozi wawili hawatafanana kwa asilimia 100, iwe ni kwa kauli, kimtazamo , upole au ukali. Hata siku moja hawawezi kufanana kwa kila kitu,”alisema

Chanzo: Mwananchi
Baba Mushumbushi Bana
 
Back
Top Bottom