Desprospero
JF-Expert Member
- Feb 1, 2023
- 887
- 2,201
Wajumbe, aliyekuwa Rais wa JMT Dk. John Pombe Magufuli alifariki tarehe 17/3/2021 hapo Mzena kisha Samia Suluhu Hassan kutangaza kifo chake saa 5:57 usiku "akiwa ziarani Tanga".
Baada ya hapo aliyekuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alitawazwa kuwa Rais wa JMT. Katiba yetu inaelekeza kuwa Rais atakuwa madarakani kwa miaka 5 (si minne wala sita) na kama atataka kugombea tena kwa awamu ya pili na ya mwisho basi ataomba ridhaa kwa chama chake.
Katiba imeweka bayana kuwa Rais ataacha Urais kwa (1) kufariki
(2) Kuumwa na kushindwa kutekeleza majukumu yake na (3) kwa kujiuzulu. Katiba haisemi kwamba Rais akipatwa na hayo matatu let's say ndani ya miaka minne basi atakayemrithi atamalizia awamu yake (marehemu).
Naamini hii ndiyo maana uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan umetambuliwa kama Awamu ya Sita na si ya Tano. Kama ni hivyo basi, tutakuwa hatujamtendea haki Rais Samia Suluhu Hassan endapo tutafanya uchaguzi Mkuu Oktoba mwakani Jumapili ya mwisho maana haitokidhi matakwa ya Katiba ya miaka mitano madarakani.
Kwa hiyo tuheshimu Katiba na haki ya Samia tufanye uchaguzi mwezi machi 2026 siku aliyoapishwa. Ova!