Dkt. Ndugulile: Kutoza kodi Mapema kwenye Biashara za mitandaoni kutaua ajira za Vijana wengi na kudumaza e-Commerce

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,131
Mbunge wa Kigamboni, Dr Faustine Ndugulile ni kama amepingana na mbunge wa viti maalumu Neema Rugangira anayetaka biashara za mitandaoni zitozwe kodi.

Dkt. Ndugulile aliyewahi kuwa waziri wa Mitandao amesema kutoza kodi mapema kwenye biashara za mitandaoni kutauwa AJIRA za Vijana wengi na kudumaza mfumo wa Biashara Mtandao.

Dkt. Ndugulile ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter.

Maendeleo hayana vyama!
====
Mbunge wa Kigamboni, Faustine ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter kuhusu masuala ya kodi

Tanzania bado tuko nyuma sana katika biashara mtandao. Tunahitaji kukuza na kuilea e-commerce. Vijana wengi wamejiajiri kupitia mfumo huu. Kuanza kutoza kodi mapema kutadumaza mfumo huu na kuua ajira nyingi. Nguvu ielekezwe katika kuimarisha usalama na imani kwenye biashara hii.

Ni muhimu sana kuwa makini kwenye kodi za kidigitali. Mjadala uwe ni jinsi gani tunaweza kupata kodi toka kwa makampuni makubwa ya nje yanayofanya biashara mitandaoni pasipo kuleta athari kwa mteja wa mwisho ambao hutumia mitandao hii katika ubunifu, kujifunza na biashara.

Pia, soma:

1). Mbunge Neema Lugangira(Viti Maalum) ataka Biashara za Mtandaoni zianze kutozwa Kodi

Screenshot 2022-03-11 at 09.31.23.png
 
Mbunge wa Kigamboni Dr Faustine Ndugulile ni kama amepingana na mbunge wa viti maalumu Neema Rugangira anayetaka biashara za mitandaoni zitozwe kodi

Ni kweli kabisaa. Mhe. yuko sahihi.

Serikali itafute vyanzo vingine vya mapato.
 
Msomi analeta hoja bila kufanya utafiti na kuwa na data za kuitetea hoja yake.

Hata hizo biashara za mtandaoni hawazijui ni zipi wao wanakimbilia kwenye kodi tu.

Mifumo rafiki ya uwezeshaji wa hizo biashara mtandaoni hakuna, serikali inasubiri ujitutumue mwenyewe wao wanakuangalia tu, wakianza kuona matokeo wanachotaka ni kodi.

Hii nchi ngumu sana.
 
Mama akikopa mnalalamika, akitoza kodi mnalalamika, sasa afanyeje?

Kila mtu lazima alipe kodi, whether ana physical duka ama online duka.

Kinachotozwa kodi ni mapato na sio platform ya kufanyia biashara. Sasa unataka mtu mwenye mtaji wa milioni 10, anauza simu online stoku ya mzigo iko chumbani kwake asilipe kodi kisa anauza online na anapata mapato lakini aliekodi fremu na mtaji huo huo wa 10m na anafanya biashara hiyo hiyo ya kuuza simu alipe kodi kisa yeye hauzi online? Hizo ni akili ama mavi?

Kila mtu alipe kodi bila kujali anauza online ama anauzia nyumbani kwake.
 
Huyu mtakumbuka alipaisha Bei ya bundle kwa manufaa yake binafsi na manufaa ya mabeberu. Anafikiri tumesahau?

Sasa anajifanya Yuko upande wetu. Hatumtaki akae huko huko tigo Vodacom. Hata wakati wa kuomba Kura aende kwa wakurugenzi wa makampuni ya simu.

Apeleke mboga kwingine halafu anakuja kujipendekeza huku?

Akwendre huko...
 
Mbunge wa Kigamboni, Faustine ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter kuhusu masuala ya kodi

Tanzania bado tuko nyuma sana katika biashara mtandao. Tunahitaji kukuza na kuilea e-commerce. Vijana wengi wamejiajiri kupitia mfumo huu. Kuanza kutoza kodi mapema kutadumaza mfumo huu na kuua ajira nyingi. Nguvu ielekezwe katika kuimarisha usalama na imani kwenye biashara hii.

Ni muhimu sana kuwa makini kwenye kodi za kidigitali. Mjadala uwe ni jinsi gani tunaweza kupata kodi toka kwa makampuni makubwa ya nje yanayofanya biashara mitandaoni pasipo kuleta athari kwa mteja wa mwisho ambao hutumia mitandao hii katika ubunifu, kujifunza na biashara.
 
huyu hajatetea bali amekubaliana kuwa kuna biashara mitandaoni, harafu akatoa hoja kwa sasa bado kwani inaweza ua ajira za vijana, labda wataalam mtujuze kwenye mitandao inafanyika matangazo au wanauza na kununua?
 
Ndungulile akiwa waziri kwenye wizara husika hakuweza kukemea kodi kwa vijana wenye YouTube channels zao ambao basically wanamiliki gmail account.

Pia juzi nimemsikia akiiomba serikali iondoe tozo daraja la Kigamboni. Akiwa serikalini ilikuwa rahisi kwake kuweka hoja mezani kuliko sasa akiwa mbunge.
 
Mama akikopa mnalalamika, akitoza kodi mnalalamika, sasa afanyeje?

Kila mtu lazima alipe kodi, whether ana physical duka ama online duka.

Kinachotozwa kodi ni mapato na sio platform ya kufanyia biashara. Sasa unataka mtu mwenye mtaji wa milioni 10, anauza simu online stoku ya mzigo iko chumbani kwake asilipe kodi kisa anauza online na anapata mapato lakini aliekodi fremu na mtaji huo huo wa 10m na anafanya biashara hiyo hiyo ya kuuza simu alipe kodi kisa yeye hauzi online? Hizo ni akili ama mavi?

Kila mtu alipe kodi bila kujali anauza online ama anauzia nyumbani kwake.
Huu ndio ukweli sasa
 
Hii sio sawa,
Kila mmoja alipe kodi,
Kama wakiruhusu hilo basi na wengine nao
Wataleta vipoint vyao wasamehewe
 
Back
Top Bottom