Dk. Slaa akamata nyaraka ya siri ya serikali

Kuiba nyaraka za Serikali siyo kitu kizuri, lakini ikiwa ni kwa maslahi ya Taifa haina tatizo hebu fikiria bila wizi wa nyara za Serikali leo hii fedha za EPA zingekuwa zinarudishwa?? Bila wizi wa nyaraka za Serikali leo hii Lowassa angekaa pembeni? Leo hii Rostam, Kalamaghi na watu kama hao wangekuwa wapo wapi?? Hata kama una maslahi ni bora ukae kimya kuliko kukaa unalinda ugonjwa mkubwa uliolipata taifa letu?

Hoja yako ina msingi na ina mashiko. Ni suala la morality vs legality! Linahitaji mjadala mpana. Tupanue mjadala na wengine watupe maoni yao.
 
Huishi kusema ya ccm wewe mara nyaraka mara hiki , hv akili yako haina mambo mapya yakutufanya tukuamini? Staili yako ya uchochezi ndiyo inayonipa mashaka juu ya uwezo wako wa kutawala, huna tofauti na mpangaji wangu au mke wa jirani yangu ambaye ameruga mtaa kwa maneno ya uchochezi maana kutwa haongei ya kwake ni kusema wenzie tuu. Badilika slaa kama unaitaka tanzania.
 
Nchi hii tunacheza michezo ya hatari kweli. Hainiingii akilini kama tunaweza kuthubutu kushabikia kitendo cha mtu kuiba nyaraka ya serikali wenyewe tunasema 'akamata'. Kuiba nyaraka ya serikali ni jambo la hatari kwa uhai wa taifa lolote haijalishupi umefanywa na nani? Leo Dr. Slaa anaiba nyaraka ya Serikali na tunamshangilia.

Mbinu hii itatumika dhidi ya Serikali ya CHADEMA siku itakapojaaliwa kuingia madarakani. Mchezo huu ukiendelea, hakuna Serikali itakayotawala. Kitendo hiki kinadhoofisha Serikali na sio kitendo ch kushabikia hata kidogo, na ndio maana kuna sheria ya bunge dhidi ya kitendo hicho. Bahati nzuri Serikali yenyewe in huruma huruma hivi.

Lakini la pili ni kuwa, tunataka sasa kuhalalisha ushiriki wa watumishi wa umma kwenye siasa. Hii ni hatari nyingine. Kitendo cha kunajisi utumishi wa umma na siasa, aidha kusaidia Chama Tawala au Chama cha Upinzani ni kitendo cha hatari na kukemea. Watumishi wa umma wakifanya kazi kisiasa hakuna maendeleo yatakayopatikana na hatari ya hujuma aidha dhidi ya wapinzani au serikali inaweza kuwa kitu cha kawaida.

Sioni tatizo lolote kuhusu Waraka huo wa kukataza watumishi wa umma kutoshiriki shughuli za siasa. Waraka haukatazi mtumishi wa umma kuwa mwanachama, kinachokatazwa ni kuwa kiongozi wa chama au kufanya shughuli za chama cha siasa mahala pa kazi. Waraka huu unawasaidia pia CHADEMA kuliko tunavyotaka kuaminishwa.

Watumishi wa Umma wakiamua kutumika dhidi ya CHADEMA ustawi wa Chama hicho utakuwa mashakani. Inawezekana walioko kwenye utumishi wa umma wakawa CCM wengi kuliko CHADEMA kama ambavyo inawezekana pia wakawa CHADEMA wengi kuliko CCM. Lengo la Waraka huu ni kulinda maslahi ya umma wote na haki yao ya kupata haki na huduma kutoka katika utumishi wa umma bila kujali itikadi.

Pengine nielezwe humu ni nchi gani na wapi ambapo utumishi wa umma wanaruhusiwa kujihusisha na siasa za vyama mahala na wakati wa kazi? Kwa nini sisi tuwe wa kwanza?

Tusikubali kutumiwa kuhalalisha mbinu haramu kwa sababu tu ya kutaka kufikia maslahi yetu ya kisiasa. CHADEMA wakumbuke, mbinu hizo hizo zitatumika dhidi yao wakiwa madarakani.

Uwezo wako wa kufikiri ndo umekomea hapo ? au ni walewale wa kutumwa na magamba !
 
Waraka wowote wa serikali wenye lengo la kulinda maslahi ya umma wa watanzania utalindwa kwa nguvu zote.

Lakini waraka wowote wenye lengo la kuhujumu demokrasia na uhuru wa watu, tena uhuru wenyewe wa kikatiba haustahili kamwe kushabikiwa na mtu mwenye mapenzi mema na nchi hii, kwani waraka wowote wa aina hiyo unakuwa unakwenda kinyume cha katiba.

Kama ccm wanaona hawawezi kuvumilia kuilinda katiba iliyopo japo mbovu lakini ina mazuri yake, basi wapeleke muswada bungeni kuvifuta vyama vya upinzani ili wabaki wao wenyewe.

Kusambaza waraka mikoani kutaka kuwatambua watumishi wa umma wanaoviunga mkono vyma vya upinzanbi ni dalili za wazi za kushindwa kwa serikali ya ccm kuwahudumia wananchi, na ni dalili za wazi za ccm kushindwa kuwashawishi watu kwamba ni chama cha kutumainiwa na wananchi. Hata wakiandika majina yao, wanaweza kurudisha kadi za vyama vya upinzani ili kunusuru ajira zao lakini ccm na serikali yake watambue kwamba hawawezi kuifuta chadema na vyama vingine vya upinzani kwenye mioyo ya watumishi hao!!

Nimependa opening statement yako. Sina tatizo na maoni yako. Naamini kuwa Serikali haiwezi kutoa Waraka inaosema kuwa wakaguliwe wafanyakazi wanaojihusisha na vyama vya upinzani. waraka unazungumzia kjihusisha na vyama vya siasa sio upinzani. Kwa kuwa Dr. Slaa anao na kama ana dhamira ya kweli, Waraka huo auweke hadharani na humu wale wenye kuamini hivyo wauweke hapa kwenye Jamiiforum. Kama Waraka unatamka wazi kuhusu vyama vya upinzani, hata mie ntangana mkono nanyi kuupinga.
 
Huishi kusema ya ccm wewe mara nyaraka mara hiki , hv akili yako haina mambo mapya yakutufanya tukuamini? Staili yako ya uchochezi ndiyo inayonipa mashaka juu ya uwezo wako wa kutawala, huna tofauti na mpangaji wangu au mke wa jirani yangu ambaye amevuruga mtaa kwa maneno ya uchochezi maana kutwa haongei ya kwake ni kusema wenzie tuu. Badilika slaa kama unaitaka tanzania uitawale.
 
Mimi siwafikirii madc, marc, na madas. Nazumgumzia watumishi wa kawaida tu kama walimu, makarani nk. kwa mfano kuna mwalimu wilaya moja ya iringa ni mwenyekiti wa uvccm wilaya na afisa utumishi na DED wake wameshindwa kumchukulia hatua. sasa fanya wewe jifanye ni mwenyekiti wa BAVICHA wilaya uone kazi yake. Serikali ya ccm wanawagandamiza watumishi lakini ujue asilimia 90 ya watumishi mioyo yao iko upinzani

Sasa unataka kusemaje? Ni halali kwa Mwalimu huyo kuwa mwenyekiti wa UVCCM? Si sahihi. Ni kosa na tunapaswa kuvumbua uozo kama huo. Atawafundisha wanafunzi siasa za ccm na anaweza pia kutoa upendeleo wa kisiasa.
 
Kwa nini waraka wa serikali kwa watumishi wa umma uwe siri?. Basi hiyo si siri tena ni njama na hujuma kwa upinzani nchi. Mapenzi, ushahabi na uanachama kwa chama chochote cha siasa uja kwa kufuata sera na mikakati inayotekelezeka na wala sio nyaraka za siri zenye malengo kandamizi.dalili za kuanguka kwa watawala ni pamoja na hizi..unaweza waforce ng'ombe kwenda kisimani lakin hauwezi kuwalazimisha kumywa maji . Ccm hauna la kufanya hakika umezeeka na umekataliwa na utaondoka kwa khali yoyote hile.
 
jk hawezi kuhutubia na watu wakasikiliza wakati mvua inanyesha(hapa ni mbalizi)


 
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk.Wilbrod Slaa, ameiumbua tena serikali ya Chama cha Mapinduzi(CCM) kwa kufichua waraka maalumu wenye lengo la kudhibiti na kufuatilia kwa makini nyendo za watumishi wa serikali wanaoshabikia vyama vya upinzani.

Akihutubia juzi katika mkutano wa hadhara uliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Nzovwe na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu, Dk. Slaa alisema waraka huo kupitia Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi ) unawataka Makatibu Tawala wa Mikoa yote nchini kufuatilia na kupeleka takwimu za wafanyakazi wanaojihusisha na siasa sehemu za kazi.

Alisema ili kutimiza azma hiyo wametakiwa kuorodhesha kila mtumishi kwa majina kamili, kazi anayofanya, cheo kazini, itikadi ya siasa na cheo alichonacho ndani ya chama husika lengo likiwa ni kuwapata watumishi wanachama wa vyama vya siasa pinzani nchini.

Dk. Slaa ambaye alikuwa akishangiliwa kila wakati na umati mkubwa watu, alisema hatua hiyo ya serikali ni ya hatari kubwa, na akaitaka kusitisha na kuacha kuwatisha wananchi walio huru ndani ya nchi yao.

Alisema kinachojaribu kufanywa na serikali ni kutaka kudhoofisha nguvu ya upinzani, jambo litakalosababisha kuzuka kwa vurugu.

“Mchezo huu si mzuri na hauwezi kuvumilika hata kidogo kwa kuwa nchi hii ni yetu sote na yenye kutawaliwa kwa mfumo wa vyama vingi na hawa watumishi wanaruhusiwa kuendesha siasa wakati wa nje ya kazi, kwa nini serikali iamue kutoa waraka huu?” alihoji.

Dk. Slaa alisema ndani ya waraka huo kuna maelekezo kuwa Katibu Tawala yeyote atakayeshindwa kutekeleza majukumu hayo aliyopewa na wizara basi jina lake litapelekwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ili ashughulikiwe ipasavyo.

Alisema CHADEMA itaendelea na maandamano nchi nzima kupinga baadhi ya mambo ya kifisadi ambayo serikali inayafanya na kamwe hawataogopa kufanya hivyo hata kama watakamatwa na polisi na kupelekwa mahakamani.

Aidha Dk. Slaa katika suala zima la uundwaji wa Katiba mpya alisema Chama cha Mapinduzi kupitia kikao chake cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kilitoa waraka uliowataka viongozi wa chama hicho ngazi zote kusimamia zoezi hilo katika kuhakikisha mawazo yote yatakayotolewa na wananchi yawe kwa manufaa ya CCM.

Alisema alifikiri kuwa mchakato wa Katiba ni kwa manufaa ya Watanzania wote kumbe CCM inauchukulia kwa manufaa yake na si ya wananchi.

“Tazameni, yaani haya ni mambo ya ajabu kabisa yanayofanywa na viongozi hawa, badala ya kujadili mambo ya mustakabali wa nchi juu ya hali ngumu ya maisha kwa wananchi, wao wanapanga ni jinsi gani watatekeleza azma yao ndani ya Katiba mpya kwa maslahi ya CCM na si ya Watanzania,” alisema.

SOURCE:TANZANIA DAIMA

na kwenye karatasi ya kura watawabanaje?
 
Huishi kusema ya ccm wewe mara nyaraka mara hiki , hv akili yako haina mambo mapya yakutufanya tukuamini? Staili yako ya uchochezi ndiyo inayonipa mashaka juu ya uwezo wako wa kutawala, huna tofauti na mpangaji wangu au mke wa jirani yangu ambaye amevuruga mtaa kwa maneno ya uchochezi maana kutwa haongei ya kwake ni kusema wenzie tuu. Badilika slaa kama unaitaka tanzania uitawale.

Umepata posho ya chakula leo?
 
kama kawaida amepewa na kanisa. Kwani kanisa lina mtandao mkubwa sana sio tu ndani ya Tz bali duniani kote.

Je mmesikia tamko la kanisa la Dr Slaa la DRC Kongo?

kazi kwenu.

Ujinga ni mzigo mzito kuliko kubeba kontena. Sasa wewe watu wanajadili hoja, tena ya Kisiasa, suala la kanisa linatoka wapi? Mimi nashangaa kwa nini nyie wamanga koko mnapenda sana vurugu. Tazama kule Somalia na Sudan mnavyouana. Sasa wewe uliye na uraia wa Qatar mambo ya uchochezi kwa Tanzania yanakunufaisha nini?

Ikiwa unaamini mizizi ya Uislamu ni huko uarabuni uliko, mbona basi na msiwe kioo cha mabadiliko kwa jamii ya kiislamu ya Tanzania badala yake umekuwa kama mwanamke wa kiswahili kutwa kucha kuzua mineno na kunung'unika? Hili suala la Dr.Slaa kufanya kazi ya kisiasa linahusika vipi na Kanisa kama sio umetumwa kuhakikisha unaleta ujinga wako ktk kila jambo linalozungumziwa hapa?
 
Sheba naona kaweka kajaribu kuelezea kireefuuu weee lakini at the end hakuna kilichoeleweka,labda uelewa wangu mdogo,ngoja nipite tu mimi
 
Huishi kusema ya ccm wewe mara nyaraka mara hiki , hv akili yako haina mambo mapya yakutufanya tukuamini? Staili yako ya uchochezi ndiyo inayonipa mashaka juu ya uwezo wako wa kutawala, huna tofauti na mpangaji wangu au mke wa jirani yangu ambaye amevuruga mtaa kwa maneno ya uchochezi maana kutwa haongei ya kwake ni kusema wenzie tuu. Badilika slaa kama unaitaka tanzania uitawale.

Dr.Slaa haitaji kura za watu wasioweza kufikiri kama wewe. Ulitaka aseme nini zaidi ya kuyasema yale yanayotukwamisha? Uchochezi ni nini kwako? Mtu akiwa anaiba dirishani kwako tukaja kukuambia fulani anakuibia nenda ukamkamate utatuita sisi wachochezi au walinzi wa mali zako?

Wewe ndio mwenye akili kama za mke wa jirani yako na ndio maana ameweza kuwagombanisha, hujui kulinganisha mambo wala kupambanua yenye kuhusika na jambo lingine. Hii nchi ni yetu wote, utamwambia vipi Dr.Slaa aseme yanayomhusu, kwani nchi haimuhusu?

Kwa hiyo kwa tafsiri yako ya Buguruni unakoishi, Dr.Slaa alifanya uchochezi alipoibua ufisadi wa EPA kwa hiyo angewaacha waibe yeye aendelee na mambo yake, hayo hayamhusu?

Nikiwa na mtoto mwenye akili kama zako, nabadilishana na sahani ya wali nakula najua sina mtoto. Pumba square
 
Dawa ni moja tu! Kiongozi dikteta,atukimbize mchakamcha tutaacha kukalia maneno tu na mbinu chafu za kisiasa
 
Huishi kusema ya ccm wewe mara nyaraka mara hiki , hv akili yako haina mambo mapya yakutufanya tukuamini? Staili yako ya uchochezi ndiyo inayonipa mashaka juu ya uwezo wako wa kutawala, huna tofauti na mpangaji wangu au mke wa jirani yangu ambaye amevuruga mtaa kwa maneno ya uchochezi maana kutwa haongei ya kwake ni kusema wenzie tuu. Badilika slaa kama unaitaka tanzania uitawale.


Ukweli wa Dr umekugusa na wewe, na huu ndo mwisho wenu enyi vibaraka vya magamba.
 
Mimi ni CHADEMA na ni mtumishi wa umma waanze na mimi..shit!!
Mimi pia. Wasichokifahamu watu kama kina Sheba na Kupinduka (sijui kwa kuwa hawajawahi kuwa watumishi wa umma) ni kwamba Kanuni za Utumishi wa umma za mwaka 2003 na sheria yake ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa mwaka 2007, Scheme of Service na Kanuni za kudumu za mwaka 2009 zinaeleza wazi kuwa, Mtumsihi wa Umma ana ruhusiwa kuwa mwana chama wa chama cha siasa lakini asitoe huduma kwa ubaguzi au kwa itikadi za siasa.

Asifanyie siasa kazini, asitumie nyaraka za ofisi kwa manufaa ya kisiasa wala asivae sare za vyama katika mazingira ya kazi. Je huo waraka wa nini tena?

Kama wanataka wajaribu kufuatilia kama hawataambulia pressure maana ukweli ni kwamba asilimia 90 ya watumishi ni "Wapinzani" hata kama wengine hawana vyama na wala hawapo Chadema.
 
nchi hii tunacheza michezo ya hatari kweli. Hainiingii akilini kama tunaweza kuthubutu kushabikia kitendo cha mtu kuiba nyaraka ya serikali wenyewe tunasema 'akamata'. Kuiba nyaraka ya serikali ni jambo la hatari kwa uhai wa taifa lolote haijalishupi umefanywa na nani? Leo dr. Slaa anaiba nyaraka ya serikali na tunamshangilia.

.

mkuu naona umechemka, hii sio nyaraka ya serikali, ni nyaraka ya ccm. Halafu kama ni kitu haramu slaa angekuwa lupango hivi sasa. Hivi huoni kama unafanana na passport ya ccm??
 
Dr.Slaa haitaji kura za watu wasioweza kufikiri kama wewe. Ulitaka aseme nini zaidi ya kuyasema yale yanayotukwamisha? Uchochezi ni nini kwako? Mtu akiwa anaiba dirishani kwako tukaja kukuambia fulani anakuibia nenda ukamkamate utatuita sisi wachochezi au walinzi wa mali zako?

Wewe ndio mwenye akili kama za mke wa jirani yako na ndio maana ameweza kuwagombanisha, hujui kulinganisha mambo wala kupambanua yenye kuhusika na jambo lingine. Hii nchi ni yetu wote, utamwambia vipi Dr.Slaa aseme yanayomhusu, kwani nchi haimuhusu?

Kwa hiyo kwa tafsiri yako ya Buguruni unakoishi, Dr.Slaa alifanya uchochezi alipoibua ufisadi wa EPA kwa hiyo angewaacha waibe yeye aendelee na mambo yake, hayo hayamhusu?

Nikiwa na mtoto mwenye akili kama zako, nabadilishana na sahani ya wali nakula najua sina mtoto. Pumba square
Mkuu achana na huyo, maana hata hajui alicho ''comment'', hapo nilipo bold ni sawa kabisa.
 
Back
Top Bottom