Dk. Slaa akamata nyaraka ya siri ya serikali

Naungana na wewe.

Hata ukipitia CV ya Padre Dr Slaa utaona kabisa wala hafai kuwa rais wa nchi kama Tanzania. yeye alifa zaidi kuwa PAPA wa wakatoliki. Na Cv yake inamsapoti kwa hilo.

wala ubwabwa utawajua kwa maneno yao tuu,.Baruruba umewahi kula shaba lililo mixiwa na pork.

ulijilambaje..!!!!.
 
Ahsante sana. Kama ulivyoweza kuipitia Cv yangu itakuwa ajabu sana mimi nikikataa au kulazimisha watu wasiniite Mchumi au Dr. Kwani hiyo ni haki yangu kwa sababu nimesomea mpaka kufikia hapo.

sasa vp mwenzetu utukataze tusimwite hivyo wakti Cv yake imejipambanua hivyo.
Kwani kumwita hivyo ni kosa? Mbona mchungaji Natse huyu ni mbunge anaitwa hivyo mpaka leo au mchungaji G Lwekatare na hata yule wa iringa mjini wanaitwa hivyo mpaka bungeni.

Tufafanulie bwana kosa li wapi?

Barubaru,

Tatizo lako kubwa na la msingi ni kwamba elimu yako haijakukomboa kifikra, kama bado unakuwa na mawazo kama mtu wa ngumbaru utawezaje kujinasibu kwamba una phd? hiyo elimu inakusaidia nini wewe binafsi na inainufaisha vipi jamii yako ya ukimbizini oman na kwa mababu zako unguja?

Kama huwezi kujipambanua na wenye elimu za ngumbaru, basi hakukuwa na umuhimu wowote wa wewe kwenda shule, hata kujiita mchumi ni bure tu kama alivyo raisi wa JMT mchumi lakini hajui chanzo cha umasikini wa nchi yake na hajui namna ya kuikwamua nchi yake toka kwenye umasikini, sasa ameipandisha nchi kuwa matonya namba tatu duniani!!
 
Naomba nikuulize swali kidogo tu-Kwako wewe ni halali wakuu wa mikoa kuwa wajumbe wa kamati za siasa za CCM?

Swali lako lingefaa kuwa, je, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ni viongozi wa siasa au watumishi wa umma? Jibu langu kwako ni kuwa Wakuu wa Mikoa ni viongozi wa kisiasa. Ndio maana wanatakiwa kulipwa kiinua mgongo kila baada ya miaka 5, ikiwa ameteuliwa tena anaendelea. Ndio maana katika Serikali ya Mkoa kuna mtu anaitwa Katibu Tawala wa Mkoa na Katibu Tawala wa Wilaya, hawa ndio watumishi wa umma. Wakuu wa Mikoa ni sawa na Mawaziri tu, na vigezo vyao vya kuteuliwa ni vya kisiasa.
 
Nchi hii tunacheza michezo ya hatari kweli. Hainiingii akilini kama tunaweza kuthubutu kushabikia kitendo cha mtu kuiba nyaraka ya serikali wenyewe tunasema 'akamata'. Kuiba nyaraka ya serikali ni jambo la hatari kwa uhai wa taifa lolote haijalishupi umefanywa na nani? Leo Dr. Slaa anaiba nyaraka ya Serikali na tunamshangilia.

Mbinu hii itatumika dhidi ya Serikali ya CHADEMA siku itakapojaaliwa kuingia madarakani. Mchezo huu ukiendelea, hakuna Serikali itakayotawala. Kitendo hiki kinadhoofisha Serikali na sio kitendo ch kushabikia hata kidogo, na ndio maana kuna sheria ya bunge dhidi ya kitendo hicho. Bahati nzuri Serikali yenyewe in huruma huruma hivi.

Lakini la pili ni kuwa, tunataka sasa kuhalalisha ushiriki wa watumishi wa umma kwenye siasa. Hii ni hatari nyingine. Kitendo cha kunajisi utumishi wa umma na siasa, aidha kusaidia Chama Tawala au Chama cha Upinzani ni kitendo cha hatari na kukemea. Watumishi wa umma wakifanya kazi kisiasa hakuna maendeleo yatakayopatikana na hatari ya hujuma aidha dhidi ya wapinzani au serikali inaweza kuwa kitu cha kawaida.

Sioni tatizo lolote kuhusu Waraka huo wa kukataza watumishi wa umma kutoshiriki shughuli za siasa. Waraka haukatazi mtumishi wa umma kuwa mwanachama, kinachokatazwa ni kuwa kiongozi wa chama au kufanya shughuli za chama cha siasa mahala pa kazi. Waraka huu unawasaidia pia CHADEMA kuliko tunavyotaka kuaminishwa.

Watumishi wa Umma wakiamua kutumika dhidi ya CHADEMA ustawi wa Chama hicho utakuwa mashakani. Inawezekana walioko kwenye utumishi wa umma wakawa CCM wengi kuliko CHADEMA kama ambavyo inawezekana pia wakawa CHADEMA wengi kuliko CCM. Lengo la Waraka huu ni kulinda maslahi ya umma wote na haki yao ya kupata haki na huduma kutoka katika utumishi wa umma bila kujali itikadi.

Pengine nielezwe humu ni nchi gani na wapi ambapo utumishi wa umma wanaruhusiwa kujihusisha na siasa za vyama mahala na wakati wa kazi? Kwa nini sisi tuwe wa kwanza?

Tusikubali kutumiwa kuhalalisha mbinu haramu kwa sababu tu ya kutaka kufikia maslahi yetu ya kisiasa. CHADEMA wakumbuke, mbinu hizo hizo zitatumika dhidi yao wakiwa madarakani.

Tukiiba waraka wa kumuua Sheba tusishangilie?. Hata kama CDM wataingia serikalini na kuibiwa nyaraka za namna hii tutashangilia! Kuna faida gani ya kuwa na serikali zenye nyaraka za kugandamiza wenye serikali?
 
Pumba mpya zimeanza! Bado hajaacha siasa maji taka?

Kama kweli ana nyaraka za siri za Serikali (kitu ambacho shida kuamini) inabidi ajieleze alikozitoa na kama ni kwa njia zisizo rasmi inabidi achukuliwe hatua kali za kisheria. Ujasusi dhidi ya Serikali ni kosa kubwa sana na adhabu zake ni kali sana kwa wote waliohusika. Sidhani kama atakuwa mjinga kiasi hicho, hii nna uhakika ni waandishi uchwara wanatafuta umaarufu kwa kuzuwa.

serikali legelege ya chama chako ndio inafanya siasa za maji ya chooni.

Katika serikali hii legelege ni nani mwenye uwezo wa kumkamata Dr. Slaa katika hili? walimtegeshea hadi vifaa vya kunasa mawasiliano yake kitandani hotelini dodoma, akastukia dili itakuwa hizi nyaraka zinazotumwa mchana kweupe.
 
Mwongo huyo, akawadanganye hukohuko kanisani alikokuwa akitumika, mzushi huyu siwezi kumuamini hata kidogo, tangu azushe issue ya kontena la kura, mfuko wa cement kuwa 5000 na mengine mengi simwamini huyu.

Sasa hapa kanisa linakujaje?
Mimi wewe sikujui wala imani yako siijui lakini kwa unavyoonyesha nina uhakika 100% imani yako ni ya uongo unamwabudu shetani bila kujua na unamwita mungu mwenyezi!!! na ndiyo maana imani yako ina mafundisho ya kinyume kinyume hizo ni daklili za shetani.
 
  • Thanks
Reactions: FEK
Acha unafiki wa kiccm, waraka unakuwa siri pale unapokuwa hujamfikia mlengwa, mlengwa wa waraka akishaupokea na kuusoma sio siri tena ila kinachobaki ni utekelezaji. Sasa uwezi kufanya utekelezaji kimya kimya inabidi ushirikishe watu wengine ndo hapa waraka unasomwa kwa wale wanaotakiwa kutekeleza. so, hapo hakuna siri tena.

Pili na kushangaa unaposema tusikubali kwa watumishi wa serikali kuwa viongozi wa vyama, hivi hii ni kwa upinzani pekee yake? mbona kuna watumishi wengi wa serikali ni viongozi wa ccm? wapo ambaoni wenyeviti wa umoja wa vijana ccm , wenyeviti wa wilaya, wajumbe wa kamati za siasa za wilaya na mikoa. kwanini kwa upande wa upinzani wa zuiwe?

wewe ni miongoni mwa magamba ambao unaona wakiruhusiwa ccm haitakuwa na chake

Ndugu,

Kama wako waumishi wa umma ambao ni viongozi wa ccm hilo ni kosa na wala makosa mawili hayahalalishi kosa lenyewe. Isije ikawa unawafikiria kichwani mwako ma DC na RC ambao ni viongozi wa kisiasa. Nazungumzia civil servants. Katika ngazi ya mkoa ni RAS na DAS na walio chini yao.

Aidha, kuhusu siri za serikali, sina haja ya kuanzisha ligi na wewe katika hili. Waraka ukiwa wa siri ni wa siri na sheria inayolinda hilo ipo si suala la wewe au mimi kupenda au kutopenda.
 
Wewe unayejua asiyefaa bila shaka unamjua/wajua wanaofaa...ni kina nani hao na wamefanya nini kwa taifa hili? Wapi wamepigania/tetea wanyonge na maskini wa taifa hili? Hebu waorodheshe hapa hao wanaofaa na sifa zao.

Huyo barubaru asikupe shida, anasumbuliwa na dhambi ya usaliti.

Kasomeshwa kwa kodi za watanganyika, akaajiriwa serikali ya Tanganyika lakini baada ya miaka kadhaa akafanya ufisadi na kukimbia mkono wa sheria na kwenda kwa wajomba zake oman.

Lakini kila siku yuko hapa JF kujadili masuala ya Tanganyika ilihali yeye si mtanganyika na wala hana msaada wowote kwetu na hata kwa ndugu zake aliowaacha kule matemwe.
 
Kaka kama huna uwezo wa kuandika kitu kinachoeleweka kwa wasomi nakushauri usifanye hivyo kwani unajiaibisha
wewe soma tuu yaliyoandikkwa labda utaelimika kidogo...,sio lazima umwage upupu wako hapa..

Msomi hujibu kwa hoja.
 
Nchi hii tunacheza michezo ya hatari kweli. Hainiingii akilini kama tunaweza kuthubutu kushabikia kitendo cha mtu kuiba nyaraka ya serikali wenyewe tunasema 'akamata'. Kuiba nyaraka ya serikali ni jambo la hatari kwa uhai wa taifa lolote haijalishupi umefanywa na nani? Leo Dr. Slaa anaiba nyaraka ya Serikali na tunamshangilia.

Mbinu hii itatumika dhidi ya Serikali ya CHADEMA siku itakapojaaliwa kuingia madarakani. Mchezo huu ukiendelea, hakuna Serikali itakayotawala. Kitendo hiki kinadhoofisha Serikali na sio kitendo ch kushabikia hata kidogo, na ndio maana kuna sheria ya bunge dhidi ya kitendo hicho. Bahati nzuri Serikali yenyewe in huruma huruma hivi.

Lakini la pili ni kuwa, tunataka sasa kuhalalisha ushiriki wa watumishi wa umma kwenye siasa. Hii ni hatari nyingine. Kitendo cha kunajisi utumishi wa umma na siasa, aidha kusaidia Chama Tawala au Chama cha Upinzani ni kitendo cha hatari na kukemea. Watumishi wa umma wakifanya kazi kisiasa hakuna maendeleo yatakayopatikana na hatari ya hujuma aidha dhidi ya wapinzani au serikali inaweza kuwa kitu cha kawaida.

Sioni tatizo lolote kuhusu Waraka huo wa kukataza watumishi wa umma kutoshiriki shughuli za siasa. Waraka haukatazi mtumishi wa umma kuwa mwanachama, kinachokatazwa ni kuwa kiongozi wa chama au kufanya shughuli za chama cha siasa mahala pa kazi. Waraka huu unawasaidia pia CHADEMA kuliko tunavyotaka kuaminishwa.

Watumishi wa Umma wakiamua kutumika dhidi ya CHADEMA ustawi wa Chama hicho utakuwa mashakani. Inawezekana walioko kwenye utumishi wa umma wakawa CCM wengi kuliko CHADEMA kama ambavyo inawezekana pia wakawa CHADEMA wengi kuliko CCM. Lengo la Waraka huu ni kulinda maslahi ya umma wote na haki yao ya kupata haki na huduma kutoka katika utumishi wa umma bila kujali itikadi.

Pengine nielezwe humu ni nchi gani na wapi ambapo utumishi wa umma wanaruhusiwa kujihusisha na siasa za vyama mahala na wakati wa kazi? Kwa nini sisi tuwe wa kwanza?

Tusikubali kutumiwa kuhalalisha mbinu haramu kwa sababu tu ya kutaka kufikia maslahi yetu ya kisiasa. CHADEMA wakumbuke, mbinu hizo hizo zitatumika dhidi yao wakiwa madarakani.

Hivi Nape ni kiongozi wa Umma?
 
Ndugu yangu Sheba utaniwia radhi kwa lugha nitakayoitumia kupingana na hoja zako.

1. Usifikri Dr. Slaa ni mjinga na wala Watanzania ni wajinga. Unapaswa kuelewa kipi hasa kinachostahili kuwa siri ya serikali katika maana halisi na kipi hakistahili. Ipo sheria zinazotumika kulinda siri za serikali na hivyo anayezitoa na anayesitumia anastahili kushtakiwa kwa mujibu wa sheria hizo( kwa sasa sina muda wa kuzirejea). Mwamvuli wa sheria hizo usitumike kutuletea uposhaji kama wa kwako. Dr. Slaa hata siku moja hatashtakiwa kwa sheria hizo kwa maana yako ya uelewa wa siri za serikali. Hizo zinazotajwa kuwa ni siri ya serikali ilistahili kuitwa upumbavu wa serikali.

Wakati fulani Dr. Slaa alipokuwa mbunge alisema anazo nyaraka za serikali na ushahidi kuhusu wizo wa EPA na Richomodn nk. Aliibuka waziri mmoja kwamba Dr. Slaa atachukuliwa hatua za kisheria kwa kukutwa na nyaraka za serikali. Upande mwingine Spika akasema kuwa ushahidi wa Dr. Slaa ni feki kwa sababu ameutoa kwenye mitandao. Kuhusu kushtakiwa, Dr. Slaa aliwaambia wakamshtaki lakini hakuna hata mmoja aliyefanya hivyo. kwa suala la Richmond hakuna asiyefahamu yaliyotokea. Hakuna mahala popote duniani ambapo wizi unaendeshwa na serikali halafu useme ni siri isipokuwa hapa Tanzania.

Matumizi ya serikali yanapitishwa na bunge katika vikao vya bajeti, huu uchukuaji wa fedha kutoka benki kuu kwa ajili ya matumizi yasiyoeleweka ndiyo siri ya serikali? Bwana Sheba kama una akili ambayo imeacha kufikiri tafadhali usitumie kutoa mawazo kama hayo kwa Watanzania wenzako. Hakuna Mtanzania mwenye akili timamu atakayekubalina na upumbavu wako.

Waraka wa serikali kwa Makatibu Tawala kuhusu suala la kuandikisha watumishi na vyama vyao ni aina ya upumbavu mwingine wa serikali. Watumishi wanaongozwa na kanuni na miongozo ya kiutumishi. Maagizo kama hayo hayana sifa ya kuwa nyaraka za siri za serikali kwa sababu yana malengo mabaya na yana harufu ya Chama tawala kinachotamani kubaki madarakani kwa nguvu na siyo kwa ridhaa ya wananchi. Kama kanuni za utumishi hazikutaka watumishi watoe taarifa zao za uanachama katika vyama vya siasa, kumetokea nini hadi makatibu tawala waagizwe kufanya kazi ya kishushushu kazi ambayo hata TISS imewashinda kuifanya kwa ajili ya maslahi ya umma?

Kila mwananchi analo jukumu la kuilinda serikali iliyo halali. Kwa sasa Serikali hii ya CCM inaonekana haipo kwa ajili ya maslahi ya umma na wautu hawana hamu ya kuiona inaishi. Kama serikali inaamua kuwanyanyasa wananchi iliopaswa kuwatumikia kuna mategemeo yoyote ya kulindwa. Ni serikali ipi duniani iliyo kwa ajili ya wananchi wake inawaacha wezi wa mali za umma wanashindwa kupelekwa hata mahakamani? Ni serikali ipi inayodai wananchi waipelekee ushahidi wa wizi wa fedha za umma kama vile yenyewe haina vyombo vya kuweza kuwajua? Ni serikali gani duniani iliyo kwa ajili ya maslahi ya umma inashindwa kuwashtaki watuhumiwa hata pale ilipopelekewa ushahidi?

Ndugu Sheba, hiyo siri ya serikali unayoitaka iwe siri haistahili kuwa siri kwa wananchi wa Tanzania. Hivi wewe (mke) ukilietewa siri ya mkuwa mumeo ana hawara utaichuliaje? Huyo aliyekuletea siri utamwona ni mtu mbaya? Kwa mantiki hiyo, kama Wananchi wa Tanzania ndiyo wanye mamlaka ya mwisho juu ya nchi yao, unadhani siri inayohusu serikali kuwaibia wananchi mali zao na kuibaka demokrasi yao inastahili kuwa siri, na kuwa ni kitu kibaya wananchi kuifahamu?

Asante sana kwa mtazamo wako.
 
Ahsante sana. Kama ulivyoweza kuipitia Cv yangu itakuwa ajabu sana mimi nikikataa au kulazimisha watu wasiniite Mchumi au Dr. Kwani hiyo ni haki yangu kwa sababu nimesomea mpaka kufikia hapo.

sasa vp mwenzetu utukataze tusimwite hivyo wakti Cv yake imejipambanua hivyo.
Kwani kumwita hivyo ni kosa? Mbona mchungaji Natse huyu ni mbunge anaitwa hivyo mpaka leo au mchungaji G Lwekatare na hata yule wa iringa mjini wanaitwa hivyo mpaka bungeni.

Tufafanulie bwana kosa li wapi?
Maajabu mengine haya hapa! Kumbe huna hata uwezo wa kuelewa mambo madogo hivi! Au ni tatizo la kukariri vitu kama kasuku?! Sijawahi kuona cv yako wala hakuna mahali nimeandika kuwa nimewahi kuiona hiyo cv... Pia hakuna mahali nimekukataza wewe wala mwingine yeyote hapa kumuita vyovyote vile, kwanza nikukataze mimi kama nani?! Ikiwa una dini yoyote, naamini inakufundisha kuwa uongo ni dhambi,utajitendea haki sana kama utatambua kuwa umenisingizia uongo mara mbili kwenye bandiko lako hili... (kwamba nimeipitia cv yako na kuwa nimekukataza kumuita Dr Slaa 'padri')Vinginevyo, endelea na kazi za 'baba' wa uongo kama unaona inalipa!!!
 
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk.Wilbrod Slaa, ameiumbua tena serikali ya Chama cha Mapinduzi(CCM) kwa kufichua waraka maalumu wenye lengo la kudhibiti na kufuatilia kwa makini nyendo za watumishi wa serikali wanaoshabikia vyama vya upinzani.

Akihutubia juzi katika mkutano wa hadhara uliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Nzovwe na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu, Dk. Slaa alisema waraka huo kupitia Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi ) unawataka Makatibu Tawala wa Mikoa yote nchini kufuatilia na kupeleka takwimu za wafanyakazi wanaojihusisha na siasa sehemu za kazi.

Alisema ili kutimiza azma hiyo wametakiwa kuorodhesha kila mtumishi kwa majina kamili, kazi anayofanya, cheo kazini, itikadi ya siasa na cheo alichonacho ndani ya chama husika lengo likiwa ni kuwapata watumishi wanachama wa vyama vya siasa pinzani nchini.

Dk. Slaa ambaye alikuwa akishangiliwa kila wakati na umati mkubwa watu, alisema hatua hiyo ya serikali ni ya hatari kubwa, na akaitaka kusitisha na kuacha kuwatisha wananchi walio huru ndani ya nchi yao.

Alisema kinachojaribu kufanywa na serikali ni kutaka kudhoofisha nguvu ya upinzani, jambo litakalosababisha kuzuka kwa vurugu.

“Mchezo huu si mzuri na hauwezi kuvumilika hata kidogo kwa kuwa nchi hii ni yetu sote na yenye kutawaliwa kwa mfumo wa vyama vingi na hawa watumishi wanaruhusiwa kuendesha siasa wakati wa nje ya kazi, kwa nini serikali iamue kutoa waraka huu?” alihoji.

Dk. Slaa alisema ndani ya waraka huo kuna maelekezo kuwa Katibu Tawala yeyote atakayeshindwa kutekeleza majukumu hayo aliyopewa na wizara basi jina lake litapelekwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ili ashughulikiwe ipasavyo.

Alisema CHADEMA itaendelea na maandamano nchi nzima kupinga baadhi ya mambo ya kifisadi ambayo serikali inayafanya na kamwe hawataogopa kufanya hivyo hata kama watakamatwa na polisi na kupelekwa mahakamani.

Aidha Dk. Slaa katika suala zima la uundwaji wa Katiba mpya alisema Chama cha Mapinduzi kupitia kikao chake cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kilitoa waraka uliowataka viongozi wa chama hicho ngazi zote kusimamia zoezi hilo katika kuhakikisha mawazo yote yatakayotolewa na wananchi yawe kwa manufaa ya CCM.

Alisema alifikiri kuwa mchakato wa Katiba ni kwa manufaa ya Watanzania wote kumbe CCM inauchukulia kwa manufaa yake na si ya wananchi.

“Tazameni, yaani haya ni mambo ya ajabu kabisa yanayofanywa na viongozi hawa, badala ya kujadili mambo ya mustakabali wa nchi juu ya hali ngumu ya maisha kwa wananchi, wao wanapanga ni jinsi gani watatekeleza azma yao ndani ya Katiba mpya kwa maslahi ya CCM na si ya Watanzania,” alisema.

SOURCE:TANZANIA DAIMA

Acha utumwa wa mawazo kaka. Kinachozungumziwa hapa ni SIASA MAHALI PA KAZI na sio SIASA WAKATI WA KAZI. Wewe ungetumia akili yako vizuri kufikiri, ungegundua ni nini CCM wanaogopa na ndio maana wanatunga sera za ajabu. Nakupa mfano wa walimu: wana matatizo mengi na serikali imeyafumbia macho kwa muda mrefu. Kwa kuwa imani yao kwa serikali imeshuka, si ajabu ukawasikia now and then wakisema hili na lile kuhusu harakati za CDM na ukombozi wa wanyonge. Hili ndilo linaloiumiza kichwa CCM na serikali yake.

Kuhusu suala la Nyaraka, Dr.Slaa hajaiba waraka na hana nafasi ya kuiba waraka wowote ule serikalini. Kinachotokea ni kwamba yeye huletewa nyaraka hizi zenye nia chafu na watu waliojitolea kuinusuru hii nchi . Kinachoisumbua CCM ni mbinu chafu dhidi ya wananchi na ndio maana nyaraka hizi zinaitwa za siri, lkn ukiangalia sababu za kuwa ni siri ni UBAYA WA MAUDHUI YAKE. Hivi kwa akili yako, unafikiri mtu mwenye akili timamu atlichukia suala hili ikiwa hata Nyaraka za EPA nazo zilipatikana hivi hivi?

Kama unaamini agizo hili ni jema na lina msingi mzuri wa kuimarisha ustawi wa jamii, ni vipi lisitolewe kama Government Notice kwenye gazeti la serikali badala yake uwe waraka wa siri?

Ndugu yangu wewe unaathiriwa na u-CHAMA zaidi ya Utanzania. Juzi hapa tumeoneshwa waraka mwingine tena umeandikwa na CCM badala ya serikali kwenda kwa wahisani kuelezea muendelezo wa lile sakata la EPA just kuwaridhisha ilhali kwenye field fedha zenyewe hazipo hata zile zilizorudishwa zimetafunwa tena. Tuendelee kucheka na serikali au kuungana kuiumbua kwa mabaya yake?
Kama wewe unafaidika na ufisadi baba, tusamehe. Kwangu mimi ni sawa kabisa kwani serikali inatakiwa iwe kwa ajili ya wananchi na sio wananchi kuitukuza kwa kila madudu inayofanya. Nani anaipa serikali haki ya kuwapangia wananchi vyama vya kuvifuata?

Ni nini kitu kipya hapa? Mbona huu waraka ni wa siku nyingi? ya kwamba Mtumishi haruhusiwi kushabikia au kutumikia siasa. ndiyo maana ukitaka mambo ya siasa unaachia ngazi kwanza? naona watu wanachanganya mtumishi wa umma na yule wa siasa, wakuu wa Mikoa/wilaya, Mawaziri, wabunge ni viongozi wa siasa siyo wa umma. sema wabongo tunasahau haraka sana na tunashabikia kwa matukio. tukio fulani likiwepo watu wanashabikia sana na likipita wanasahau kabisa
 
Pumba mpya zimeanza! Bado hajaacha siasa maji taka?

Kama kweli ana nyaraka za siri za Serikali (kitu ambacho shida kuamini) inabidi ajieleze alikozitoa na kama ni kwa njia zisizo rasmi inabidi achukuliwe hatua kali za kisheria. Ujasusi dhidi ya Serikali ni kosa kubwa sana na adhabu zake ni kali sana kwa wote waliohusika. Sidhani kama atakuwa mjinga kiasi hicho, hii nna uhakika ni waandishi uchwara wanatafuta umaarufu kwa kuzuwa.

Kwa kiasi fulani wewe unajulikana kama miongoni mwa wadini wachache wanye uwezo wa kuchangia mada

zenye manufaa kwa taifa, hivyo acha kujidhalilisha na kujishusha.
 
Umesahau Arusha alivyobambwa kajificha kwenye maspika? Umesahau na Mwenyekiti alivyolazwa "centro". Unanchekesha!

Umesahau kwamba hata EPA mlisema ni uzushi na uongo lakini leo hii kila kitu kiko peupee.

Na usisahau kwamba kila waraka wa kifisadi mnaouandika unamfikia na hamuwezi kumkamata wala kumshtaki kwa kuwa na waraka wa "siri" wa serikali legelege.
 
Nchi hii tunacheza michezo ya hatari kweli. Hainiingii akilini kama tunaweza kuthubutu kushabikia kitendo cha mtu kuiba nyaraka ya serikali wenyewe tunasema 'akamata'. Kuiba nyaraka ya serikali ni jambo la hatari kwa uhai wa taifa lolote haijalishupi umefanywa na nani? Leo Dr. Slaa anaiba nyaraka ya Serikali na tunamshangilia.

Mbinu hii itatumika dhidi ya Serikali ya CHADEMA siku itakapojaaliwa kuingia madarakani. Mchezo huu ukiendelea, hakuna Serikali itakayotawala. Kitendo hiki kinadhoofisha Serikali na sio kitendo ch kushabikia hata kidogo, na ndio maana kuna sheria ya bunge dhidi ya kitendo hicho. Bahati nzuri Serikali yenyewe in huruma huruma hivi.

Lakini la pili ni kuwa, tunataka sasa kuhalalisha ushiriki wa watumishi wa umma kwenye siasa. Hii ni hatari nyingine. Kitendo cha kunajisi utumishi wa umma na siasa, aidha kusaidia Chama Tawala au Chama cha Upinzani ni kitendo cha hatari na kukemea. Watumishi wa umma wakifanya kazi kisiasa hakuna maendeleo yatakayopatikana na hatari ya hujuma aidha dhidi ya wapinzani au serikali inaweza kuwa kitu cha kawaida.

Sioni tatizo lolote kuhusu Waraka huo wa kukataza watumishi wa umma kutoshiriki shughuli za siasa. Waraka haukatazi mtumishi wa umma kuwa mwanachama, kinachokatazwa ni kuwa kiongozi wa chama au kufanya shughuli za chama cha siasa mahala pa kazi. Waraka huu unawasaidia pia CHADEMA kuliko tunavyotaka kuaminishwa.

Watumishi wa Umma wakiamua kutumika dhidi ya CHADEMA ustawi wa Chama hicho utakuwa mashakani. Inawezekana walioko kwenye utumishi wa umma wakawa CCM wengi kuliko CHADEMA kama ambavyo inawezekana pia wakawa CHADEMA wengi kuliko CCM. Lengo la Waraka huu ni kulinda maslahi ya umma wote na haki yao ya kupata haki na huduma kutoka katika utumishi wa umma bila kujali itikadi.

Pengine nielezwe humu ni nchi gani na wapi ambapo utumishi wa umma wanaruhusiwa kujihusisha na siasa za vyama mahala na wakati wa kazi? Kwa nini sisi tuwe wa kwanza?

Tusikubali kutumiwa kuhalalisha mbinu haramu kwa sababu tu ya kutaka kufikia maslahi yetu ya kisiasa. CHADEMA wakumbuke, mbinu hizo hizo zitatumika dhidi yao wakiwa madarakani.

serikali ni nani? umetumwa? hata chadema wakiingia madarakani wafanyiwe hivyo hivyo maana vitu vikienda kwa uwazi na usawa nani atatoa hizo nyaraka za serikali, jaribu kuthink outside the box
 
kama kawaida amepewa na kanisa. Kwani kanisa lina mtandao mkubwa sana sio tu ndani ya Tz bali duniani kote.

Je mmesikia tamko la kanisa la Dr Slaa la DRC Kongo?

kazi kwenu.

Udini utakuua, acha kuleta udini kila kukicha.
 
Magu FULL na Wasira kule Igunga wakiwa watumishi wa Umma walikuwa wanafanya nini? days of confusion for Magamba.
 
Ndugu,

Kama wako waumishi wa umma ambao ni viongozi wa ccm hilo ni kosa na wala makosa mawili hayahalalishi kosa lenyewe. Isije ikawa unawafikiria kichwani mwako ma DC na RC ambao ni viongozi wa kisiasa. Nazungumzia civil servants. Katika ngazi ya mkoa ni RAS na DAS na walio chini yao.

Aidha, kuhusu siri za serikali, sina haja ya kuanzisha ligi na wewe katika hili. Waraka ukiwa wa siri ni wa siri na sheria inayolinda hilo ipo si suala la wewe au mimi kupenda au kutopenda.

Mimi siwafikirii madc, marc, na madas. Nazumgumzia watumishi wa kawaida tu kama walimu, makarani nk. kwa mfano kuna mwalimu wilaya moja ya iringa ni mwenyekiti wa uvccm wilaya na afisa utumishi na DED wake wameshindwa kumchukulia hatua. sasa fanya wewe jifanye ni mwenyekiti wa BAVICHA wilaya uone kazi yake. Serikali ya ccm wanawagandamiza watumishi lakini ujue asilimia 90 ya watumishi mioyo yao iko upinzani
 
Back
Top Bottom