Diwani wa Kata ya Sombetini (CCM, Arusha) ahamia CHADEMA

Wanaanza mmoja mmoja.but cdm iwe makini tusije tukawa tunawafungulia zizi fisi wenye uchu tukidhani ni kondoo wenzetu, mwishowe tukakuta zizi halina kitu zaid ya mabaki ya mifupa na kinyesi cha chokaa.

Hasante gfsonwin,

CDM wanao mtiani kama walikuwa hawajajitayisha. Hawa wanaorukia jahazi la CDM wana lengo gani? Je wameafikiana na Falsafa pamoja na Sera za CDM? Wameisoma katiba ya CDM na kuilukubali? Miaka nenda rudi walikuwa wapi? Ninasema CDM wawe makini wanapowapokea wakimbizi, wadandiaji na ma-stoways na rejects wa kisiasa. CDM inaweza ikajikuta inatumika kama launching pad ya kuhitimisha ndoto za wazamiaji.
Wakati huu miaka mitatu kabla ya um nilitegemea CDM inamfahamu na kumtayarisha kila mgombea wa udiwani, ubunge - majimbo yote ya uchaguzi Tanzania. Nilitegemea sasa hivi CDM ipo vijijini kuwaeleza watz jinsi CCM ilivyo-hijack mchakato wa kutengeneza katiba mpya na kuwaongoza watz wafanyeje kurekebisha hili. Nilitegemea CDM wanayo skeleton ya katiba mpya ambayo watanzania wangetumia kama reference wakati wanajadiri katiba mpya itakuwaje.
Sifikirii kama haya ni too much wishing - kama kuna mwanaCDM amenisikia naomba anikosoe.
 
jamani kama ni kweli naamin kwa wsle wenye dini kama mimi ni maombi ya kufunga ya lema kwa siku saba yanajibiwa Mungu atukuzweee!!!!?
 
Hayawi ,hayawi sasa yanakuwa anguko kuu la ccm sasa linatimia mungu akiwa upande wetu hakuna alie juu yetu
 
Breaking News,
Diwani wa Kata ya Sombetini Mh. Alphonce Mawazo amejiengua kutoka CCM na kuhamia CHADEMA, samahani tutakatisha matangazo ya moja kwa moja kutoka Bungeni na kujiunga na Sunrise redio kusikiliza mahojiano maalum.
 
CCM wengi mjini Arusha wameonyesha ya kujiengua na kujiunga Chadema,wanasubiri mkutano wa CDM siku yo yote kuanzia sasa,
 
CCM, kwishney huko Arusha wangejua wasingeleta zengwe kwenye kesi ya Lema, nawomba Pro CCM watoe comments zao kuhusu hili anguko la CCM Ausha
 
Mawazo alikuwa ni diwani wa sombetini ameondoka ccm na kujiunga na cdm, kweli arusha kumekucha na mwaka huu tutashuhudia mengi.
source sunrise radio arusha.
 
Breaking News,
Diwani wa Kata ya Sombetini Mh. Alphonce Mawazo amejiengua kutoka CCM na kuhamia CHADEMA, samahani tutakatisha matangazo ya moja kwa moja kutoka Bungeni na kujiunga na Sunrise redio kusikiliza mahojiano maalum.

Simu za aina gani zina uwezo wa kupata matangazo ya arushamambo online?
 
CCM, kwishney huko Arusha wangejua wasingeleta zengwe kwenye kesi ya Lema, nawomba Pro CCM watoe comments zao kuhusu hili anguko la CCM Ausha

Bado watasema kwamba wanatekeleza maagizo ya Kamati kuu, mpaka wale wasafi wote watoke huko. Kamati kuu ilishindwa kuwatoa wale wachafu (MAGAMBA), hivyo ikaagiza wale wasafi watoke ili wawaachie gamba lao.
 
Hizi ndizo dalili za gamba kumalizika, na mwendo wa makada wa CCM kuhamia CDM si kwa Arusha pekee bali muda si mrefu toka sasa kuna kada almaarufu wa CCM Iringa naye atabwaga manyanga na kujiunga Chadema, kwa wakati huu anajipanga huku cdm mkoa wa Iringa ikiandaa protocol pamoja na siku maalumu ya kumpokea, Magamba chaliii.

naamini kuwa vuguvugu la ukombozi kwa mtanzania haliko mbali
 
Back
Top Bottom