zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,910
Ku generalize "Asians" na kuwaweka kundi moja nadhani si busara. Kwani mada inafananisha na wa Tanzania. Ikiwa tu tutafananisha "Africans" basi hapo ndio tufananishe Asians au Europeans na kadhalika. Si vyema kuifananisha au kufananisha wa Tanzania na watu wa Bara zima la Asia au Europe, haina mantiki.
Ikiwa nchi tu kama Tanzania, ina makabila na tabia, mila na hulka tofauti kwa karibu kila kabila, inakuwaje ufananishe na wa Asia? Ambao, kwa mfano mdogo tu, kuna wa China, wa Turuki, wa Hindi, wa Arabu, wa, wa, wa... Na kati ya hao kuna makabila tofauti, ambao wao kwa wao wanatofauti kubwa za kimila ki itikadi ki jamii na kadhalika.
Naona mtowa mada angetumia busara japo kidogo na kuanza kufananisha ki nchi na nchi na si kikontinenti na nchi.
Kwa ufupi tu, tumeshawahi kuona wa Tanzania wengi tu wenye asili ya kiarabu katika nyanja tofauti hapa Tanzania, na wengine ni maarufu sana. Na hali kadhalika kwa wa Tanzania wenye asili ya ki Hindi na ki Pakistan. Wenye asili ya ki Ingereza nao wapo lakini ni wachache sana, hali kadhalika kwa wenye asili za kigiriki, kijerumani.
Kwa hawa wa Tanzania wenye asili za nje ya bara la Afrika, utakuta ni wengi walioshika nyannja na nyadhifa mbali mbali katika Serikali kuliko wa Tanzania wenye asili za ki Afrika nje ya Tanzania.
Wengi wa waTanzania wenye asili ya ki Afrika nje ya Tanzania wako lakini, labda kwa kuogopa kubaguliwa hujichanganya na kujibandika makabila ya ki Tanzania na inakuwa vigumu kuwang'amuwa kwa urahisi kwa kuwa wengi wa waTanzania ni wenye asili ya kiAfrika.