Gaijin
JF-Expert Member
- Aug 21, 2007
- 11,812
- 5,289
Sir Leem, nimeelezea kuhusu wenzetu hawa kuwa ni vibarua tuu kule Dubai wakati hapa kwetu ni waheshimiwa sana!. Pia nemesema hapa kwetu wanachagua kazi zenye hadhi fulani ndizo wanafanya hivyo kwa hapa Tz wao ni watu wa maana sana kufikia hata kiwango ilipojulikana wanahusika EPA, gereza la Ukongo likakarabatiwa na kufungwa AC ili kuwaacomodate waheshimiwa hawa!
Sababu pekee ya kutumika wenzetu hawa ni kuwa wako too cheap, you can pay them the minimum of minimum na kazi ikafanyika. Kwa sasa, ni gharama ndogo zaidi kutengenezea India,tangazo zuri la TV kuliko kutengenezea hapa. Its cheaper kutibiwa India kuliko kutibiwa Ulaya, yaani wazungu sasa wanafiri toka Ulaya kwenda India kufuata matibabu. Hata gharama za uwakili India ni cheaper kuliko ulaya, hivyo wateja wa ulaya, wanawafuata malawyer wa India.
Naomba nikurudishe kidogo kwenye historia, jee unajua ni kwa nini Wahindi ni wengi Afrika ya Mashariki na wamejikita kibiashara zaidi?. Hao unaowaona, wengi wao, haswa mababu zao, walikuja tangu enzi za German East Africa kama makuli wa kutengeneza reli ya kati, mishahara waliolipwa ndio wakajengea maghorofa unayayaona miji yote reli ilikopita. Hivyo mwanzo walikuwa makuli wakati sisi tungali bado tukiishi gizani. Sasa wao ndio wafanya biashara wakubwa hapa kwetu, ukuli wa nini tena?, kibao kimetugeukia sasa sisi wenye nchi ndio makuli wao, ndio watumishi wao na wao ndio mabwana zetu mpaka serikali yetu nasi wenye nchi ndio watwana wao.
Nawaombeni sana sana sana, msije mkanitafsiri mimi kuwa ni racist, no, its about values. Hapa hufanya nguma zao za Bhagra pale Nkurumah Street, ukitaka kuingia kwanza hapo hapo mlangoni, unakataliwa!. Wana baa zao, maja wapo ni pale Odeon, kwenye jengo la DTV, wahuduma wa hizo bar ni waswahili wenzetu, nenda kaingie, huhudumiwi ng'o!. Wao ndio wateja wakubwa wa dada zetu wa usuku kwenye ma night club, nenda kwao uonekana unahangaika na vibinti vyao!. Yule Mtanzania aliyeuwawa Dheli, sababu haukusemwa na haitasemwa, we acha tuu. Mimi nimekaa New Dheli, mambo mengine ya huko kwao kuhusu wenzetu hawa, wee acha tuu! hapa kwetu ndio wafalme wetu!.
Pasco unataka watu wasikuite mbaguzi wakati kwenye post yako kumesheheni alama za ubaguzi huo.
Unatukumbusha historia kuwa mababu zao ndio waliokuja na kuwa makuli, lakini hapo hapo unawatenga kwa kusema 'sisi wenye nchi' ikimaanisha kuwa huamini/huwachukulii kuwa hapa ni kwao.
Baadae kidogo unasema "wao wanachukua wanawake wetu, lakini ukenda kwao..."
Kwao wapi?