Diversity in Tanzania: Where are the Asian, Arab, European-Tanzanians?

Unatuchanganya, sidhani kama Nyerere, Mkapa, Mwinyi na Kikwete wamewahi kuwachagua hao minority kwa rangi kabila au dini zao, ila, nafahamu kuwa Nyerere alikuwa akichaguwa majority kwa Ukatoliki wao.

I wouldn't agree with that in red!, i really think you are pushing for a scapegoat! :focus:
 
Mfumo wetu umejengwa katika utaratibu wa kuigopa diversity badala ya kuikumbatia na kuitumia kuleta maendeleo. Ukiangalia hata kwenye sensa zetu hatutaki kabisa kujuana, hivyo kwa mtindo huo huwezi kuwa na mipango yoyote ya mendeleo kwa muktadha huo bali utafuta mtindo wa wale wanaojidhania ndio wengi kuhodhi kila kitu
 
Kwanza wana utayari? Ukiacha wahindi na waarabu wa zenj, wangapi huku bara wana lafudhi zetu? Ukiacha waarabu, ni watanzania wangapi wanafahamu kihindi? Ni wahindi wangapi tunaishi nao in the hoods? Kuna mtu kapanga nyumba moja na mhindi au mwarabu humu vitongojini mwetu? Kwa nini basi kufikiria kuwaweka kwenye nyadhifa ili wajichanganye na wazawa wakati wanajitenga kuanzia ngazi ya kitongoji na mtaa? Hawa watu wanakula na vipofu
 
Mwanakijiji,
Ukimalizana na suala hili naomba uingilie suala la makabila ya Tanzania. Tuna makabila zaidi ya 120. Je yote hayo yamewahi kuwakilishwa katika ngazi za juu katika serikali ya Tanzania?

Jasusi, naungana na wewe, tukishazipata sababu za hawa minority weupe kutokuwepo baadhi ya maeneo, tutawarudia na minority weusi na mfano mmoja ni huu hapa chini.

Tanzania tunamakabila dorminant tribes na pia kuna minority tribes, Sensa ya 1978 Wahadzabe waliofanikiwa kuhesabiwa ni 250 tuu, serikali ikawachukua kwa nguvu (abduction) watoto wavulana 4 toka kabila hilo ikawasomesha primary hakuna hata mmoja aliyefaulu, lakini ikawaingiza wote wanne Pugu Sekondari, wote walitoka na Div.0 lakini angalau walifanikiwa kuwabadili tabia kwa kustaarabika na kukubali kuvaa nguo.

Vijana hao wanne, walirudishwa maporini kwa jamii yao Wahdzabe ili wawabadilishe, huku support yenye supply ya mavazi na mambo ya kisasa ikiwa stand by ili wagaiwe. To start with wenzao walipowaona, waliwakimbia, iliwabidi hao wasomi wavue mavazi yao na kurudia asili yao ili wakubalike kwao, na badala ya kuwabadilisha wenzao, wao walirudia walikotoka. Sijajua kama kuna any follw up imegfanywa kuhusu watu hao ambao wazungu wanawahesabu kama endengered spicies!.

Wataturu, Wasandawe, Wabarbaig, Wabalungi na jamii za Wambulu, ndio wameweazunguka Wahadzabe, bado wanaishi misituni, hawavai nguo, hawalimu, wanakusanya matunda, hawana nyumba, wanaishi kwenye mashimo na viota ni Watanzania wenzetu, jee tunawasaidiaje?.
 
You know all these problems could be sorted by intermarriages... the this differences will be diluted:teeth:.... Just kidding
 
Mwanakijij
Hebu soma hii:
Marehemu Mzee Bori Lilla wakati mmoja alikuwa miongoni mwa walioteuliwa kufanya selection ya vijana wa form4 kwenda form6 enzi za Mwl.Nyerere.Kilicho mshangaza ni kuona vijana wenye majina ya kiislam walikuwa na division 1 na 2 yakiwekwa kando ili hata yasiweze kujadiliwa na hatimaye kupatiwa selection.Alipouliza kulikoni wenzie wakamshangaa wakamuuliza kwani wewe ni mgeni hujui taratibu zetu? Kutokana na jina lake waliomteua hawakujua dini yake wakagundua kwamba yalifanyika makosa makubwa,kwani siku zote huo ndio ulikuwa utaratibu wa baraza la mitihani kuwabagua waislam ktk elimu kwa makusudi huku ikisingiziwa kwamaba Waislam hawapendi kusoma au hawana akili.Sasa kama Waislam ambao sio minority walibaguliwa kiasi hicho sio ktk elimu tu bali hata ajira,unadhani hali itakuwaje kwa hao minority?
 
You know all these problems could be sorted by intermarriages... the this differences will be diluted:teeth:.... Just kidding
VoiceOfReason, intermariages zipi na nani?, labda tufanya kama zile za Zanzibar baada ya mapinduzi ya 64 kwa waafrika kujitwalia mabinti wa kiarabu na kuwaoa kwa nguvu, forceful marriages, wahindi wana caste system ndani ya mioyo yao, na wale walio oa ngozi nyeusi, kwao wametengwa na jamii zao. Hata wale madada wa kihindi wanaofanya ile biashara kuu ya wadada ya usiku, wateja wao ni wahindi tuu, wakati dada zetu wateja wao ni yoyote. Hizi nitermariages zitatoka wapi?.

Take a close note, hata intermariages nyingi za kiarabu ni baba Mwarabu mama ngozi nyeusi, ni aghlabu sana kukuta baba ngozi nyeusi mama Mwarabu, ukiondoa zile za Zanzibar. Tena afadhali ya wazungu mara mia, wenzetu waliopelekwa huko , waliruhusiwa ku procreate, walipolekwa Arabu na Barahindi, wote walihasiwa kwanza wasije wakanajisi pure race za wenyewe!.

Angalia wanafunzi wanaosoma India uniambie ni wangapi wamerudi na wake wa Kihindi, compare na Watanzania waliosoma kwa Wazungu, walivyoryudi na wamama wa kizungu. Sio ubaguzi wa segregation ni ubaguzi wa discrimination na ndicho kinachoendelea, tukubali, tukatae, tunabaguana.
 
Mzee Mwanakijiji, hakuna any divesity plan au inclusion strategy yoyote simply because these people are not there.

Hawa wenzetu hawaombi kazi serikali, hao unaowaona kwenye siasa, ni watu wenye biashara zao, uwaziri hata wa bure hawataki.

Mahali pekee ambapo bado wapo ni Mahospitali na kwenye tasnia ya sheria kama wanasheria na wengi ni maadvocate.

Zamani nilidhani hawana interest na kazi zetu, niko jengo moja mjini lina ofisi za balozi kadhaa, nimegundua most of the local staff, ndio hawa wenzetu, waajiri wa kimataifa wamejiaminisha hawa wenzetu ni watu wenye bidii zaidi na ni waaminifu zaidi kuliko akina sisi.

Uakuja wewe na degree yako ya chuo kikuu, unapewe kazi ya advisory na take home ya M.3 plus, unaridhika kwa sababu level ya serikalini unaijua, bali utashindwa kushangaa unapokutana na mfanyakazi mwenzako form 1V leaver akifanya clerical job na take home ya M.5 simply beause ni light skinned!.

Nilitembelea hapo UN nikafuatilia kidogo quota systeam ya ajira. Ajira zetu sisi Watanzania ziko chini ya Eastern Africa and the Horn of Africa. Nikakuta surprise surprise, karibu wajiriwa wote ni Wasomali, Wanda na Wakenya, kwenye portion ya Tanzania, nafasi zimejazwa na wenzetu hawa. Vivyo hiyo ofisi za UN pale Geneva, na sio UN peke yake, hata kwenye mashirika yake, portion ya Watanzania kwenye ILO, FAO Rome, pia zimejazwa na wenzetu hawa.

Tukirudi hapa nyumbani, ni wenzetu hawa hawa ndio wenye upper hand kwenye tenda zote kubwa kumbwa. Toka tenda ya supply ya vifaa vya Jeshi, Rada, Helcopter, Ndege ya rais mpaka local partner wa Kalamazoo, na sasa national ID project, ni hawa hawa wenzetu.

Tunazo production company lukiki hapa nchini zinazomilikiwa na wazawa, tenda zote za promotion ya Utalii, zinakwenda kwa wenzetu hawa. Wao ndio wamiliki wakubwa wa biashara zote kubwa kubwa nchini, hata ukijitahidi ukafungua ka travel agent kako, tenda zote za travel, advertising na promotion, zinakwenda kwao.

Japo siungi mkono juhudi zozote za kuwabagua, natamani tungefanya affinmative action ya wazawa kushika biashara kubwa kama walivyofanya wenzetu kule South Afrika. Leo jijini, Dar kunaibuka maghorofa ya kutisha kila kukicha, na yote ni ya wenzetu hawa. Kariakoo wameishaimaliza sasa wamehamia Ilala na Magomeni, wakitununua na kutuhamisha, wakati kungekuwa na affimative action, tungeingia nao ubia.

Sasa jeshini hawapo tena, polisi hawapo na wala serikali hawaombi kazi, tutawasaidiaje, ila pia kitu funny ajabu, wenzetu pia hawavunji kabisa sheria, hawapo mahabusu za polisi, wala magerezani, na ni impaka ilipoibuka EPA, baada ya serikali kujua wenzetu hawa wapo, wakakarabati kwanza gereza la Ukonga kuweka vyumba VIP vyenye viyoyosi, plasma big screen TV, shower za hot water, na kutoa tenda kwa 5 star hotel kuprovide outside catering, eti hawawezi kula ugali na maharage, sio vyakula vyao vya asili.

Enzi za Dr. Leader Starring, Joan Wickens, Derreck Bryson, All Noor Kassum, Amiri Jamal are over, hizi sasa ni nyakati zetu, sisi na Bagamoyo yetu japo bado ni wao ndio wanaotujengea!.

Heshima kwako Pasco,

Mkuu bandiko lako liko juu sana yaani umemaliza kila kitu.
 
Mwanakijij
Hebu soma hii:
Marehemu Mzee Bori Lilla wakati mmoja alikuwa miongoni mwa walioteuliwa kufanya selection ya vijana wa form4 kwenda form6 enzi za Mwl.Nyerere.Kilicho mshangaza ni kuona vijana wenye majina ya kiislam walikuwa na division 1 na 2 yakiwekwa kando ili hata yasiweze kujadiliwa na hatimaye kupatiwa selection.Alipouliza kulikoni wenzie wakamshangaa wakamuuliza kwani wewe ni mgeni hujui taratibu zetu? Kutokana na jina lake waliomteua hawakujua dini yake wakagundua kwamba yalifanyika makosa makubwa,kwani siku zote huo ndio ulikuwa utaratibu wa baraza la mitihani kuwabagua waislam ktk elimu kwa makusudi huku ikisingiziwa kwamaba Waislam hawapendi kusoma au hawana akili.Sasa kama Waislam ambao sio minority walibaguliwa kiasi hicho sio ktk elimu tu bali hata ajira,unadhani hali itakuwaje kwa hao minority?
Wee KALAMAZOO, usitake kuileta tena hapa hii sumu kuwa Waislamu walibaguliwa!.
Kazi ya baraza la mitihani ni kusahihisha mitihani na kutoa maksi, kama hao wanafunzi wa Kiislamu walishapata Div 1 haiwezekani wasichaguliwe form V. Selection haifanywi na baraza la mitihani, inafanywa na wakuu wa sekondari zenye A-Level.

Naomba nisizungumzie brain power ya Waislamu na Wakristo, nenda nchi za Kiislamu, ukiondoa Uturuki, kwa vile iko ulaya, nenda middle east yote, angalia ma expart ni wakina nani, you'll be surprised karibu wote ni wazungu Wakristo, na miongoni mwa hao Wazungu, Wayahudi ndio wanaoongoza dunia nzima kwa mabingwa wa sayansi akiwemo Albert Enstain.

Kama ungeniambia baraza la mitihani wanakula njama za kuzifelisha shule za Kiislamu kwa kuzipa low marks ili Waislamu waonekane wajinga wajinga, labda ningekuelewa, hili la mwanafunzi Mwuislamu mwenye Div.1 na hajachaguliwa kwenda A-level lingekuweko, si mngelipigia kelele mpaka mbinguni?.
 
I noticed a funny thing wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu nchini. Ilikuwa ni vigumu sana kuona Watanzania Wahindi ama Wazungu wakija kusikiliza sera za Wagombea Uraisi na Ubunge. Maana yake ni kwamba wao yoyote ambaye angechaguliwa ni sawa tu. Iwapo watu hawa hawajali hata mwenendo wa Kisiasa wa Nchi yao unavyokwenda, Iweje leo tuwatake Viongozi wetu waumize Vichwa vyao kutafuta njia za kuwajumlisha kwenye taasisi za uongozi wa nchi ambao mwingi unaanzia kwa kuwa Muwakilishi wa Watu?
 
Pasco.....ninataka upanue mawazo yako kidogo........hivi hizo tenda za Rada, za ID, na zinatoka Serikalini........lakini unafikiri wanaotoa hizo tenda ni nani Wahindi au........Mimi ni MTanzania kama wewe mwenye uchungu na nchi hii kama wewe.......nimezaliwa Bongo.......siijui India ilivyo so inabidi nihukumiwe kwa rangi yangu.......nataka niseme kitu kimoja ......Watanzania tuna hulka ya kulaumu vikundi vya watu lakini uozo upo katika kila sekta nchini......pale Muhimbili ni madaktari so called Wazawa ambao wamepewa hela na Serikali kusoma wanaokandamiza wananchi maskini kwa kutowapa huduma zinazohitajika au kuomba pesa chini ya meza........pale Trafiki hupati stika ya Usalama barabarani mpaka uache chochote ili gari yako ikaguliwe juu kwa juu.....ukienda Ardhi ndio usiseme........ukija kwa Mramba, Mgonja hao wote ni wahindi pia.........Ufisadi hauna rangi....wapo WAhindi wanaoimaliza nchi sikatai lakini jamani hata so called tunaowaita wazawa pia wanaitafuna nchi yetu.........Barrick Gold Mine ilikuwa sio ya muhindi na mkataba upande wa Serikali hakusaini muhindi.....so mimi ni MTanzania full stop....na nina uhakika rangi ya mtu haimaanishi wewe ni fisadi bali roho yako........
 
Kaka mimi ninafanya kazi na watanzania mia nne sijasiki mtu akiomba ruhusa kazini anaenda kumsikiliza Mpendazoe au Mahanga wakati ndio walikuwa wagombea jimboni tunapofanya kazi..........Jiulize ni wangapo wanaoenda kwenye mikutano.........kupiga kura tu watu walikuwa chini ya asilimia hamsini.........tusinyooshe vidole kwa watu pindi hata sisi tuna ya kujibu mengi......
 
HAWANA UCHUNGU NA TAIFA HILI ZAIDI YA KUTAKA KUNYONYA RASILIMALI ZAKE.......! wanajipendelea wao kwa wao tu
 
Angalia wanafunzi wanaosoma India uniambie ni wangapi wamerudi na wake wa Kihindi, compare na Watanzania waliosoma kwa Wazungu, walivyoryudi na wamama wa kizungu. Sio ubaguzi wa segregation ni ubaguzi wa discrimination na ndicho kinachoendelea, tukubali, tukatae, tunabaguana.

Kweli kabisa ndugu... nilikuwa UK huko kuna cases nyingi za wapakistan (wazazi na ndugu) kuwauwa mabinti sababu wamependa mtu wa kabila tofauti au class tofauti na walivyotaka wenyewe... Am sure kama mtu mweusi akioa mpakistan Binti atatengwa if she is lucky.. lakini kama ana bahati mbaya watamuua eti kwa sababu amewatia aibu... (OOh God..... I think we have open a Pandora's Box)
 
Kaka mimi ninafanya kazi na watanzania mia nne sijasiki mtu akiomba ruhusa kazini anaenda kumsikiliza Mpendazoe au Mahanga wakati ndio walikuwa wagombea jimboni tunapofanya kazi..........Jiulize ni wangapo wanaoenda kwenye mikutano.........kupiga kura tu watu walikuwa chini ya asilimia hamsini.........tusinyooshe vidole kwa watu pindi hata sisi tuna ya kujibu mengi......

Unaonyesha jinsi usivyowajua waTZ wenzako. Kwa sababu tu unafanya kazi na 400 na hukuona hata siku moja mtu akiomba ruxa kwenda kusikiliza kampeni za wabunge uliotaja basi una-conclude kuwa hakuna aliyekwenda! Ningeweza kumaka 'How naive!' lakini basi. Niseme tu kuwa katika hao chini ya aslimia 50 waliopiga kura waTZ wa kiasia walikuwa asilimia ngapi kiasi cha kumfanya mteule a-sit up na ku-take note kwamba this is one minority group that I have to choose someone from on my cabinet ama nafasi yoyote ya Uongozi???
 
Pasco.....ninataka upanue mawazo yako kidogo........hivi hizo tenda za Rada, za ID, na zinatoka Serikalini........lakini unafikiri wanaotoa hizo tenda ni nani Wahindi au........Mimi ni MTanzania kama wewe mwenye uchungu na nchi hii kama wewe.......nimezaliwa Bongo.......siijui India ilivyo so inabidi nihukumiwe kwa rangi yangu.......nataka niseme kitu kimoja ......Watanzania tuna hulka ya kulaumu vikundi vya watu lakini uozo upo katika kila sekta nchini......pale Muhimbili ni madaktari so called Wazawa ambao wamepewa hela na Serikali kusoma wanaokandamiza wananchi maskini kwa kutowapa huduma zinazohitajika au kuomba pesa chini ya meza........pale Trafiki hupati stika ya Usalama barabarani mpaka uache chochote ili gari yako ikaguliwe juu kwa juu.....ukienda Ardhi ndio usiseme........ukija kwa Mramba, Mgonja hao wote ni wahindi pia.........Ufisadi hauna rangi....wapo WAhindi wanaoimaliza nchi sikatai lakini jamani hata so called tunaowaita wazawa pia wanaitafuna nchi yetu.........Barrick Gold Mine ilikuwa sio ya muhindi na mkataba upande wa Serikali hakusaini muhindi.....so mimi ni MTanzania full stop....na nina uhakika rangi ya mtu haimaanishi wewe ni fisadi bali roho yako........
nooresh, kwanza karibu jf, uwepo wako humu ni muhimu sana hata kwa divesity ya jf.

Naomba read me in between the lines, hoja ya Mzee Mwanakijiji ameuliza kwa nini minority ya wenzetu hawaonekani serikalini, mawizani au hata nafasi za kuteuliwa?.

Mimi nikamjibu, wenzetu hawa, hawaonekani, hata hao wachache waliongia bungeni, wameingia tuu lakini wana biashara zao, uwaziri hata wa bure, hawautaki!.

Nikasema, japo hao ni minority na haonekani kwa nafasi za uteuzi, lakini ndio hao wenye upprer hand kwenye kazi za maana mashirika ya kimataifa na ubalozini, nikataloe mfano nafahamu graduate fulani mwenye masters yake ya MBA, analipwa M.3 na ofisi hiyo hiyo, mwenzetu mmoja toka kundi la minority analipwa M.5, hivyo sio kweli kuwa hawapo kabisa, bali hawapo kwenye low paying jobs na wamejazana kwenye high paying jobs kama UN na mashirika yake.

Nikamalizia kwa kutolea mfano enzi za Nyerere, wakati huo, kina Amir Jamal, Al Noor Kassum, Dr. Leader Starring, Dereck Bryson, Joan Wickens, kuwa enzi hizo sasa zimepita, sasa tuko katika enzi za hao minority ndio wamekamata kila kitu and infact sisi ni watumishi wao, tangu rais wetu mpaka watoto wetu na watoto wa watoto wetu!.

Sijasema sio Watanzania, ndio maana nawaita wenzetu japo siulizi fedha zote wanazochuma, wanaivest wapi ili hali wanaishi kwenye viota vyao vya NHC?.

Ni kweli, watoa tenda wote ni sisi, ila tenda zote huangukia kwao, mind well, wao n i middle men tuu, huku tukiwa na nafasi ya kununua direct lakini tunawang'ang'ania hawa middle men, najua unajua ni kwanini!.

Mimi wala sijasema wenzetu wanaitafuna nchi, bali wamebahatika kuzaliwa na silver spoon hivyo wanakula top layer na sisi tunaambulia kilichobakia!.

Nilikwenda Dubai, huko nikakuta wenzetu hawa ndio mahouse girls, makuli, wabeba zege na kazi zote za ajabu ajabu, niliporudi hapa, nililisema hili mahali jinsi wenzetu hawa walivyo Dubai, na jinsi wenzetu hawa walivyo Tanzania, nearly ingenicost my job, maana nami nilikuwa natumika kwao.

Ufisadi ni ufisadi tuu, hauna rangi, hauna dini, hauna kabila, kwenye thread za kuwalaani mafisadi, mimi ni mmoja niliowasifu waliofisidi na kuporomosha ma-housing estates kwamba angalau wamefanya kitu cha kuonekanika hata wakiitwa siku ya siku, wataviacha hapa kwetu hivyo walivyofisidi, lakini wenzetu hata wakifisidi, hizo proceed za ufisadi wanaziinvest wapi?.

Divesity ni namna kumanage utofauti wetu, yaani tunakubali tuu tofauti, tufanya kazi ya ujenzi wa taifa letu kwa umoja, pamoja na utofauti wetu, lakini the facts inabaki pale pale, tuko tofauti!.
 
Ili mjadala huu uwe mzuri ni vizuri tukajua watu wenye asili ya nje wenye rangi isiyo nyeusi kwa maana ya wazungu,waarabu na wahindi ni asilimia ngapi ya idadi ya Watanzania?Sensa yetu ya Tanzania kwa bahati mbaya huwa haiulizi rangi wala dini kwa hiyo inakuwa vigumu sana kuwa idadi ya wenye dini na rangi Tanzania!
Lakini wadadisi huwa wanakisia tu kuwa hawa wenye rangi nyeupe wanaweza kuwa asilimia moja ya watanzania kwa hiyo kama tupo Milioni 40 that means hawa weupe wanaweza kuwa kama laki 4 hivi ya population.Ina maana ushiriki wao katika sekta mbali mbali inaweza kuwa hivyo hivyo ya asilimia moja.
Kwa mfano kama tuna askari 50000 thats means asilimia moja ya ni 500 hivi sasa sijui kama kama wanaweza fika askari 500 wenye asili ya kiarabu wa kiasia!
Ila nahisi katika ubunge wanaweza zidi asilimia moja.katika uwaziri kipindi hiki hakuna ila kipindi kililcho pita alikuwepo Megji na Abood(ana asili ya kiarabu) naibu waziri wa Afrika mashariki!kwenye Ukuu wa Mkoa namuona mmoja Mkuu wa Mkoa wa Lindi nahisi ana asilia Ya kihindi!Kwa ukuu wa wilaya mmmh!sina takwimu!
Sasa sijui kwenye sekta zingine kama wanafika asilimia moja
Sijui idadi ya wafungwa kama wanafika asilimia moja,nk nk

Kuhusu Ndg yangu Pasco kueleza kuwa umewaona vibarua wenye asili ya kihindi Dubai lakini Tanzania hukuwaona ili jambo halihitaji kuwaza sana leo Dubai mradi mmoja wa burj khalifa jengo refu duniani limegharibu 1.5 billion dollar sasa lazima viabrua waletwe kutoka India pakistan na kwinngine.Tanzania asilimia 80% hawana ajira nani aje toka India awe kibarua huku kuna vibaru hawana ajira na wanalipwa elfu 3 kwa siku?Simpe logic
 
Sir Leem, nimeelezea kuhusu wenzetu hawa kuwa ni vibarua tuu kule Dubai wakati hapa kwetu ni waheshimiwa sana!. Pia nemesema hapa kwetu wanachagua kazi zenye hadhi fulani ndizo wanafanya hivyo kwa hapa Tz wao ni watu wa maana sana kufikia hata kiwango ilipojulikana wanahusika EPA, gereza la Ukongo likakarabatiwa na kufungwa AC ili kuwaacomodate waheshimiwa hawa!

Sababu pekee ya kutumika wenzetu hawa ni kuwa wako too cheap, you can pay them the minimum of minimum na kazi ikafanyika. Kwa sasa, ni gharama ndogo zaidi kutengenezea India,tangazo zuri la TV kuliko kutengenezea hapa. Its cheaper kutibiwa India kuliko kutibiwa Ulaya, yaani wazungu sasa wanafiri toka Ulaya kwenda India kufuata matibabu. Hata gharama za uwakili India ni cheaper kuliko ulaya, hivyo wateja wa ulaya, wanawafuata malawyer wa India.

Naomba nikurudishe kidogo kwenye historia, jee unajua ni kwa nini Wahindi ni wengi Afrika ya Mashariki na wamejikita kibiashara zaidi?. Hao unaowaona, wengi wao, haswa mababu zao, walikuja tangu enzi za German East Africa kama makuli wa kutengeneza reli ya kati, mishahara waliolipwa ndio wakajengea maghorofa unayayaona miji yote reli ilikopita. Hivyo mwanzo walikuwa makuli wakati sisi tungali bado tukiishi gizani. Sasa wao ndio wafanya biashara wakubwa hapa kwetu, ukuli wa nini tena?, kibao kimetugeukia sasa sisi wenye nchi ndio makuli wao, ndio watumishi wao na wao ndio mabwana zetu mpaka serikali yetu nasi wenye nchi ndio watwana wao.

Nawaombeni sana sana sana, msije mkanitafsiri mimi kuwa ni racist, no, its about values. Hapa hufanya nguma zao za Bhagra pale Nkurumah Street, ukitaka kuingia kwanza hapo hapo mlangoni, unakataliwa!. Wana baa zao, maja wapo ni pale Odeon, kwenye jengo la DTV, wahuduma wa hizo bar ni waswahili wenzetu, nenda kaingie, huhudumiwi ng'o!. Wao ndio wateja wakubwa wa dada zetu wa usuku kwenye ma night club, nenda kwao uonekana unahangaika na vibinti vyao!. Yule Mtanzania aliyeuwawa Dheli, sababu haukusemwa na haitasemwa, we acha tuu. Mimi nimekaa New Dheli, mambo mengine ya huko kwao kuhusu wenzetu hawa, wee acha tuu! hapa kwetu ndio wafalme wetu!.
 
cabinet+tanganyika.jpg
 
Back
Top Bottom