Uongozi wa mkoa wa Arusha umelazimika kumleta Bongo Fleva, Diamond ili asaidie kukusanya watu wakati Rais Kikwete atakapohutubia umma wa mji wa Arusha siku ya alhamisi mchana.
Kikwete atazindua rasmi jiji la Arusha siku hiyo.
Vyanzo vya ndani vimebainisha kuwa jitihada za viongozi kuhamasisha mahudhurio zimekuwa zikigonga mwamba katika ngazi za kata kwani watu wengi wamekuwa wakisema wazi kuwa hawatakwenda Stadium!
Diamond ambaye ni kipenzi cha wanawake wengi hususan mabinti wa shule atasaidiana na za komedi kujaza uwanja kabla ya hotuba.
Wakati huo huo wasanii wa Arusha wameandamana hadi ofisi za meya wa jiji kupinga kuenguliwa kwenye tamasha hilo huku uongozi ukiwakumbatia ma bongo fleva wa Dar.
Let me believe that this is majungu ! Rais mzima atumie Diamond?......
Watu mnakurupuka san! Unafikiri kikwete hana wafuasi Arusha? Kumbken bdo kuna kata zinaongozwa na CCM na hata juz uchaguz wa daraja 2 ccm ilipata kura 1217 sasa hawa c wanampenda? Achen ndoto za abunuasi nyie, uwanja utajaa na kufurika tena kwaya zitakuepo! Mimi simkubl hata kidogo japo hainifanyi nitetee uongo
kwani kwenye huo uchaguzi wa daraja2 JK ndio aliekuwa anagombea? ushaur kwa JK apeleke wana hiphop watajaa.na mwana hiphop hawez kuwa CCM HATA siku moja.....
huendi kwa sababu hutaki kushuhudia uzinguzi wa jiji letu au ni kwa sababu kikwete ndio atakuepo?
\Kama pungu vileee, anazindua jiji, sasa wewe hutaki wakati huko ndiko unako ishi, mbona hueleweki. Baniani mbaya kiatu chake dawa. Mpenzi wa mama yako ni baba yako huyoooo, mama anaisikilizia, mtoto hujakua eeeheee.
Nipo mjini ila mimi na marafiki zangu hatutakanyaga katu hata wamlete 50 cent
Mie huwa napata wasi wasi sana na akili za watanzania na hasa watu wa arusha, kitu anacho kuja kufanya JK ni kwa faida yenu na vizazi vyenu, kumsusia mtu kuna maana gani sasa? hebu watanzania tupevuke akili zetu , kwani kwenye masuala ya maendeleo huwa hakuna uhasama. Na isitoshe hao mnao wakumbatia hawajawafanyia chochote na mwisho wa siku mnarudi kwa JK kumpigia magoti awafanyie hayo myatakayo
kuna siku niliwahi kusema kuwa kikwete akitaka kuja arusha lazima atengeneze mazingira rafiki na ninamhakikishia diamond akishuka tu watu wataanza kuondoka labda wafunge mageti kama mwaka juzi kwenye kampeni..
huyo diamond analipwa kiasi gani kwenda huko arusha...huyu diamond ana dili gani na jk/serikali? maana issues za chama/serikali anaitwaga yeye...mbona a town wana wanamuziki wengi tu kwanini wasiwatumie wao?
Kwa mimi mtu wa Arusha Kikwete kwangu ni laana; kushiriki kwenye laana kwa kuhudhuria kitu chake cho chote ni kujitakia laana. Afungue tu lakini Arusha itabaki kuwa ya watu wa Arusha ambao wamesalitiwa na Kikwete na CCM hadi mauaji!!!.
Mie nawashauri nendeni na kula burudani ya bure,hotuba zao zikianza mnateleza kama Kambale.Style kama ile ya Bungeni.
Mie nawashauri nendeni na kula burudani ya bure,hotuba zao zikianza mnateleza kama Kambale.Style kama ile ya Bungeni.