David Kafulila ajivua uanachama CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Mkandara,
Hizo ulizoandika hapo sio sifa za kiongozi aliyetaka apewe nchi na sasa anaongoza chama chenye vijana waliomzidi elimu.

Kwa nini basi anaendelea kung'ang'ania madaraka kama anaongozwa na wapambe, anafikia maamuzi mazito bila kuyadadisi na sio inteligent?
Hayo maswalio uliouliza juu ya Mbowe yaulize tena kuhusu Kikwete tuone majibu utakayopata.
 
Teh teh teh teh
amini na kuambia 2010 atakepata ubunge kutoka chadema ,huyo mtu hata angekuwa chama cha genge mkeni mitomingi angelipata ubunge.

This is great; absolute great. Na ni evalution checklist kwa Chadema, waone kuwa Chadema ni chama au!

Great to be quoted though
 
Mpaka leo ishu za ruzuku,ukabila, ufamilia, demokrasia chafu, hazijapata majibu.Tulisema wee kafulila huyo anaondoka, unafikiri amewarudisha nyuma kiasi gani?

Mkuu Waberoya hayo Mambo uliyoyataja hapo yametolewa Ufafanuzi mwingi akuna Kitila, Zitto na hata Kafulila wamejibu tuhuma hizo kwa Hoja, sasa sijui ulikuwa unataka majibu gani mkuu

WANGWE: DEMOKRASIA BILA NIDHAMU NI FUJO
Na David Kafulila:
Nimekuwa kimya kwa muda mrefu bila kuzungumzia kinachoitwa mgogoro ndani ya CHADEMA. Ni wazi kwamba kwa wanaonifahamu hali hii itakuwa imewashangaza. Wapo wanaoweza kusema bila shaka ni kwasababu kinachoitwa mgogoro wenyewe unakihusu chama ninachoshiriki kukijenga nikifikiri na kuendelea kuamini kuwa kinayo fursa ya kusukuma mabadiliko makubwa ya kisiasa na utawala wa nchi yetu kama tunavyoendelea kuona.

Lakini ukweli wa kimya changu ulitokana na fikra kuwa, kwakuwa misingi ya hoja iliyobainishwa na Mh Chacha Wangwe haikuwa na ukweli wa mantiki na nyakati. Nakwamba kilichokuwa kikijengwa na Chacha zilikuwa ni hisia za ujinga wa ubaguzi, basi sikudhani kama hisia hizo zingeweza kutaka kusimama akilini mwa watu wanaoishi katika nchi inayokabiliwa na changamoto nyingi za msingi ambazo kwa ujumla wake zinaelezea umasikini wa jamii hii.

Nikiri kwamba kwasababu binadamu tumeumbwa kwa kusahau. Nilisahau kuwa uongo unoporejewa mara kwa mara hugeuka ukweli wa watu.Nilisahau kuwa siasa zinajengwa kwa mitazamo, na hisia(za uongo au kweli) ni moja ya vichocheo vya mitazamo.

Kuna nadharia nyingi kuzungumzia kadhia hii; mwelekeo, historia, na kinachoendelea ndani ya CHADEMA sanjari na mikanganyiko ya kisiasa inayoendelea nchini hasa baada ya CCM kupoteza mwelekeo na matumaini kwa watanzania baada ya kushindwa vita dhidi ya ufisadi.

Wengine wanaweza kushangaa kwanini nimesema “kinachoitwa” mgogoro. Hii inatokana na ukweli kuwa wapo wanaoamini kuwa mgogoro kwa chama cha siasa ni tofauti za kisiasa baina ya kambi mbili zinazohitirafiana, ambazo kimsingi zinakuwa zinakaribiana kwa ushawishi ndani ya chama kama ilivyokuwa kwa NCCR mageuzi, ambapo kambi mbili zenye nguvu na ushawishi mkubwa katika siasa za ndani na nje ya chama, ya Mabere Marando ilitofautiana na kambi ya Lyatonga Mrema.

Mtazamo huo unajenga hoja kuwa kwa mazingira ya CHADEMA pengine mgogoro wa msingi ungejitokeza kama magwiji wa siasa za CHADEMA kama Freeman Mbowe, Dk Willibrod Slaa na Kabwe Zitto wangekuwa wamehitirafiana katika masuala ya msingi kuhusu uendeshaji wa siasa na chama. Hii inatokana na ukweli kuwa hawa ni viongozi ambao angalau unaweza kujua wanasimamia nini kwa mwelekeo wa Taifa hili kwa sasa na huko tuendako.Na heshima zao zimejengeka katika misingi hiyo.

Hali ya sasa ambapo kinachoitwa mgogoro kinabainisha kambi mbili. Ya Mh Chacha Wangwe peke yake dhidi ya ile ya Freeman Mbowe, Dk Willibrod Slaa na Kabwe Zitto inajenga mashaka kwa wachambuzi wa mambo wa siasa hasa tukijua wazi kuwa Mh Chacha pengine kwa bahati mbaya hajapata fursa ya kubainisha maono yake kama kiongozi wa kitaifa(stateman). Siwezai kumlaumu katika hili, natambua mchango wake na ninaelewa kuwa kila kitu ni mchakato,na mchakato ni suala la muda.

Nimelazimika kusema hayo kwanza ili kubainisha taswira ya kinachoitwa mgogoro kabla ya kuchambua hoja za msingi zinazobainishwa katika hisia hizo za mgogoro.Najua zinaweza kuwa hisia na maoni ya watu tu, lakini umuhimu wake unatokana na ukweli kuwa siasa zinajengwa na mitazamo,najua wanasiasa wengi wasio na sifa wametumia hisia na hata hofu za uongo kuangusha na kuingiza tawala nyingi madarakani tawala nyingi duniani.



Kuna mambo manne ningependa kujadili kabla ya mwisho wa makala yangu kuhusiana na kadhia. Kwanza ni hoja ya matumizi ya ruzuku, Ukabila, Udikteta na maamuzi ya Kamati Kuu kuhusu kusimamishwa kwa Makamu Mwenyekiti Chacha Wangwe.

Chacha ni rafiki yangu. Ni kiongozi wangu wa mkoa. Najua kuwa Chacha anapenda demokrasia na uhuru kuliko kitu chochote katika siasa. Hili ni jambo jema. Lakini tatizo lake ni kukosa uongozi wa pamoja ambao chimbuko lake ni nidhamu.

Ni muhimu wanaomshauri Chacha Wangwe wakampa somo kuwa kazi ya kujenga uongozi mmoja katika chama ni kutekeleza kwa dhati kanuni ya demokrasia na nidhamu ndani ya chama.Chama chetu lazima kiendeshwe kwa misingi ya kidemokrasia kila ngazi.Wajumbe wa vikao lazima wawe huru na sawa katika kuyajadili masuala. Uhuru huu uheshimu maoni ya wachache lakini usiathiri kanuni ya wengi wape maana lazima mjadala ufike mwisho na uamuzi kufanywa.

Nadharia ya nidhamu ndani ya chama inatokana na ukweli kuwa chama ni chombo cha kutenda, na kutenda kama kitu kimoja.Nakwamba nidhamu ni pamoja na kuwajibika kwa maamuzi ya kikao kinachokuhusu. Uamuzi wa Chacha kukaidi na kubeza uamuzi wa Kamati Kuu ambayo yeye(Chacha ) ni mjumbe ni kielelezo cha namna asivyo muumini wa kweli wa demokrasia.

Ni ukweli kuwa nidhamu bila demokrasia ni udikteta. Lakini ni ukweli pia kuwa demokrasia bila nidhamu ni fujo.Kanuni ya demokrasia na nidhamu ndiyo inayokiwezesha CHADEMA kuwa chama cha kidemokrasia na papo hapo kuwa kuwa taasisi ya kusimamia mageuzi ya kisiasa nchini kutokana na nidhamu inayokipa uongozi na msimamo mmoja katika vitendo.

Wanaojua vizuri historia ya CHADEMA wanakiri kuwa kuna mabadiliko makubwa yamefanywa kuitaasisi CHADEMA chini ya Freeman Mbowe na ndio sababu Chama kinafanikiwa katika malengo mengi sasa. Huko nyuma malengo mengi ya chama hayakuweza kutekelezwa moja ya sababu ikiwa ni udhaifu wa baadhi ya viongozi kuhusiana na nidhamu, demokrasia wanaitaka lakini palikuwa na kulegalega kuhusu nidhamu.

Imekwishajadiliwa na kupitishwa kwenye Kamati Kuu, Baraza Kuu na Mkutano Mkuu kuwa Chama kiendelee kutumia helkopta kwenye oparesheni maalumu ya kisiasa kama kampeni. Uamuzi huu ulifikiwa baada ya majadiliano ndani ya vikao hivyo ambavyo vyote Chacha ni mjumbe. Lakini baada ya vikao anakutana na waandishi wa habari na kudai kuwa yeye anapinga matumzi ya helkopta na mbaya zaidi anasema hayo ni matumizi mabaya ya ruzuku.Anasahau kuwa yeye alipokuwa Kaimu Makamu Mwenyekiti aliwajibika kusimamia maazimio ya vikao vya chama na kwamba anapopingana na maazimio ya vikao ni sawa na kuomba kujiuzulu!

Agosti13,2006 wakati wa uzinduzi wa Chama na Mkutano Mkuu, Mh Mbowe alisisitiza sana umuhimu wa viongozi wote kuhakikisha wanasimamia majukumu ya chama tunayojiwekea ili kufikia malengo yale.lakini ni wazi kuwa bila kusimamia kanuni ya nidhamu na demokrasia, tamko hilo haliwezi kutekelezwa katika ngazi yoyote. Ndio maana ilikuwa muhimu sana kumsimamisha Chacha ili kujipa nafasi ya kutekeleza malengo ya chama ambayo kimsingi yanatafsiri nafuu ya maisha kwa watanzania wengi.

Kwa mfano, Mh Chacha anazungumza hadharani kuwa ruzuku ya chama haiendi mikoani. Lakini anasahau kuwa Kamati Kuu ilisha agiza kuwa kila mkoa ufungue akaunti utumiwe sh 100,000/=(laki moja kwa mwezi). Je Chacha anaweza kutoa mfano wa mkoa uliokwisha fungua akaunti na haujatumiwa pesa hiyo?..Sio hayo, kila wilaya yenye diwani na zile za makao makuu ya mkoa ziilikwishaagizwa kufungua akaunti ili zitumiwe sh 200,000/= kwa mwezi tangu mwaka 2007.

Na ikumbukwe kuwa CHADEMA kinapata ruzuku ya kiasi cha takribani milioni60 kwa mwezi,dhidi ya CCM inayopata ruzuku ya bilioni1.2 kwa mwezi(takribani mara20 ya ile ya CHADEMA). Ruzuku ya CCM kwa mwezi ni takribani sawa na jumla ya ruzuku ya CHADEMA kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu.

Zaidi ya fedha hizo kutumwa, Chama kinatengeneza vifaa vya uenezi kama vitabu, bendera,nk na kusambaza wilayani bure ili kuhakikisha chama kinafanya kazi. Viongozi wa taifa wanafanya ziara mikoani mara kwa mara.Kwa mfano, kwa miezi miwili tangu mei2008, Viongozi wamefanya ziara mikoa mbalimbali. Zitto Kabwe amefanya ziara ya Chama Tanga kwa siku nne, na Kigoma kwa wiki mbili. Ilhali Dk Slaa emefanya ziara Singida na Manyara., Ni bahati mbaya kwamba wakati wengine wanaendelea kujenga chama wengine wanahaha huku na kule kutafuta jinsi ya kubomoa badala ya kwenda bungeni au mikoni kufanya kazi.

Wakati Mh Chacha Wangwe anasema CHADEMA imeshindwa kufanya kazi Dar es Salaam , anasahau kuwa mpaka sasa kuna timu ya kuhamasisha chama mkoa wa Dar es Salaam , na wanatumia fedha za chama. Wamefungua matawi Temeke na sasa wanaendelea Kigamboni. Mh Chacha anafahamu hilo kwasababu imeripotiwa kwenye Kamati Kuu ambayo yeye ni mjumbe. tayari zaidi ya matawi ishirini yamefunguliwa Temeke, Kinondoni na yanaendelea kufunguliwa Kigamboni kwa fedha hiyo ya ruzuku na msaada wa makao makuu. Si katai Mh Chacha kutaka uenyekiti, lakini muhimu ni awe mkweli. Aseme mambo ya hakika kwasababu CHADEMA imejijengea heshima ya kuwa na viongozi wanaozungumza hoja kwa vielelezo. Hali sasa ambapo anajikuta anazungumza mambo yasiyo na hakika alimradi kuusaka uenyekiti sio ustaarabu na ni hatari kwa demokrasia nchini. Ni vema akabainisha sifa zinazomfanya afae kuwa Mwenyekiti badala ya kutafuta kuungwa mkono kwa kubomoa chama kwani inamvunjia heshima.

Ni ukweli usiopingika kuwa kama chama, CHADEMA kinakabiliwa na Changamoto nyingi za kujijenga yenyewe na wakati huo huo kuthibiti mwelekeo wa Taifa kikiwa na wabunge 11 na madiwani 100 nchi nzima. Na sababu hiyo inayopelekea kulega kwa nyakati Fulani katika maeneo Fulani. Lakini ukweli huo hauwezi kuondoa ukweli mwingine kuwa kuna hatua kubwa imepigwa katika kufikia mpango mkakati wa chama 2005-2010 hasa katika eneo la kuiondolea serikali uhalali wa kisiasa kwa kusimamia vema kwenye vyombo vya maamuzi kama bunge.

Ni ukweli pia kuwa kumekuwepo na Changamoto ya kutuma ruzuku mikoani katika nyakati Fulani kutokana na mwenendo wa siasa za wakati huo.Huo ndio ukweli unaojulikana kwa Kamati kuu, Baraza Kuu ambapo kote Mh Chacha ni mjumbe mwenye haki na uhuru wa kuhoji na kushawishi maazimio, misimamo na mwelekeo. Kwa mfano, isingetarajiwa kuwa chama kipeleke ruzuku mikoani wakati wa uchaguzi wa Kiteto ambao ulikuwa ukihitaji zaidi ya sh milioni40 kati ya 60 za ruzuku.

Jambo moja ni kweli kwamba sasa CHADEMA inakubalika kila kona ya nchi. Kazi iliyofanywa na CHADEMA tangu sakata la Buzwagi likiongozwa na Kabwe Zitto,likifuatiwa na hili vita dhidi ya Ufisadi chini ya Dk Slaa mpaka leo sambamba na utendaji mahiri wa wabunge wa CHADEMA vimekuwa sababu kubwa ya mahitaji hayo. Changamoto pekee ni namna kufikia watanzania wote, tena mara kwa mara ili waone kuwa CHADEMA kipo pamoja nao. Naam! Changamoto ni nyingi lakini muhimu ni kwamba CHADEMA kipo kwenye mstari sahihi.

Mwandishi wa makala hii ni Afisa Habari wa CHADEMA.Lakini haya ni maoni yake binafsi kama mwanachama.
Anapatikana kwa
email: davidkafulila@yahoo.com
Cell: 0786 22 48 48.

Sasa mkuu wangu Eng. waberoya sijui unataka nani ajibu na umuamini
 
kama wewe ulivyokwenda kuwavuruga CUF.HIVI UNAJUA HAPO ULIPO UMEKALIA KUTI KAVU?MWENZAKO AKINYOLEWA WEWE TIA MAJI.MBOWE NI DIKTETA NAWE IKO SIKU YAKO.UMEFIKIA WAPI KWENYE MCHANGO WA WAKILI.WEE JAMAAA KWA KUOMBA SIKUWEZI.
Niliamua kutokuwa najibu ujinga wako maana wewe ulithibitisha ni kanda mbili kweli yaani hata akili yako ni ya ****ni kweli kama ulivyo wewe.
Unajaribu kukisia mi ni nani lakini huwezi kunijua ng'o! Kama mimi unadhani ni Lwakatare umepiga chini.
Yawezekana wewe ni Makamba maana kwa style ya maneno yako umekaa kimakamba makamba. Pumba tupu:D
 
Winners never quit and quiters never win!!!!! tutaona kama huko aendako atashinda. Wish angebaki CHADEMA akajisahihisha akaomba msamaha kwa Katibu Mkuu wake akajiandaa kuwa kiongozi wa chama badala ya kuwa mtumishi wa chama makao makuu. Si vyema kumpoteza hata mwanachama mmoja kwa sasa ila anatakiwa akubali kuwa alikosea na abadilike vinginevyo kokote atakapo kwenda atafukuzwa na Ubunge wa Kigoma kusini atabakia kuuota!!
 
Samahanini jamani, nasikitika kuwataarifu kuwa yule aliyekuwa Ofisa
Habari wa Chadema Kafulila kajivua uanachama leo. Chakujiuliza chama
hiki kinaelekea wapi?
Yaani kujitoa kwa Kafulila ndiyo tujiulize chama kinaelekewa wapi? Mbona unakuza mambo wewe mtu?
 
Hivi huyu bwana kosa lililomfanya mpaka avuliwe wadhifa wake lilikuwa nini? Tusije tukamhukumu bila kujua kisa hasa ni nini. Isije kuwa alionewa ki kweli na kusababisha yeye kufikia hatua hii.

Hakuvuliwa wadhifa wake bali hakuteuliwa tena baada ya muda wake wa kuwa kwenye kurugenzi ya habari kwisha!
 
Pombe za bure mbaya mpaka unakosa akili..unatetea wavunjifu wa democrasia...lol
Tumaini lisilokuwa Tumaini. chumvi ikikosa ladha inafanywa nini zaidi ya kutupwa kwenye jaa ikanyagwe na vichaa na wapita njia??
 
Mkuu Waberoya hayo Mambo uliyoyataja hapo yametolewa Ufafanuzi mwingi akuna Kitila, Zitto na hata Kafulila wamejibu tuhuma hizo kwa Hoja, sasa sijui ulikuwa unataka majibu gani mkuu



Sasa mkuu wangu Eng. waberoya sijui unataka nani ajibu na umuamini

Kama uko Chadema then you are different! hakuna matusi wala kejeli kwenye post zako-Bravo, people need to know, asante kwa majibu mazuri,nakutakieni kila laheri uchaguzi mwakani, kura yangu ya urais itaenda Chadema, kama lisipotokea zengwe la kunikatisha tamaa!
 
huyu kijana ana upeo mdogo sana katika kuchanganua mambo...nimemwona akihojiwa jana kwenye tv. Chadema walikuwa na wakati mgumu kufanya kazi na mtu kama huyu.lol
 
Mkuu Waberoya hayo Mambo uliyoyataja hapo yametolewa Ufafanuzi mwingi akuna Kitila, Zitto na hata Kafulila wamejibu tuhuma hizo kwa Hoja, sasa sijui ulikuwa unataka majibu gani mkuu



Sasa mkuu wangu Eng. waberoya sijui unataka nani ajibu na umuamini


Yona aliitwa kwenda ninawi akaitwa tena yeye kwa kujifanya mjanja akapanda mtumbwi kuelekea anakokujua ,akiwa ndani ya mtumbwi akazama baharini akatokea samaki mkubwa akammeza na alipokuwa tumboni mwa samaki alijuta sana kwa kitendo chake cha ukaidi na akamlilia sana aliyemwita.

Mwitaji akasikia kilio cha Yona na akayasikia matubio yake akamwamulu yule samaki akamteme yona ktk ufukwe wa ninawi, na yona katemwa na samaki ktk ufukweni ninawi na akaanza kazi rasmi ya yule aliyemwita.
Ukaidi kwa mwanadamu ni kitu cha kawaida ili mwanadamu aitikie mwito halisi lazima apewe msukoseko .
 
kule kigoma kusini ngoma ni droo kati ya CHADEMA na NCCR nahisi ndio maana anaweza kwenda huko kwani ndani ya CHADEMA walikuwa wagombea wawili yeye na Musilim Hassanal ambaye alienda kule kushiriki uchaguzi wa vijiji.
Kama maneno haya ni ya kweli, THEN nakubali kuwa kimkakati ZITTO ni muelewa. CHADEMA ni chama maarufu cha kisiasa kwa wapiga kura lakini kina wawakilishi wachache bungeni, why? CUF haiizidi CHADEMA kwa umaarufu kwa wapiga Kura lakini kina wabunge Kibao bungeni, kwanini? CHADEMA kina ajenda zenye tija lakini haziwezi kubebwa bungeni kwa nguvu inayostahili kwasababu wana idadi ndogo ya wabunge, na wabunge wa upinzani walio wengi (CUF) hawajazipa priorities ajenda za CHADEMA. Kwa hiyo sasa kama Kafulila alikuwa ni potential candidate huko Kigoma na kama kukua kwa CHADEMA huko Kigoma kusini kunachangiwa kwa kiasi kikubwa na Mh. Kafulila basi NCCR-Mageuzi itapata mwakilishi kutoka Kigoma mwakani na CHADEMA wamelipoteza jimbo lao la uhakika na mwakilishi mmoja bungeni.

Hili Ni kosa la kimkakati, Nakubalina na Zitto kuwa huu haukuwa wakati muafaka kumfukuza Mh. Kafulila kutoka kwenye nafasi yake, kwani kunaathiri CHAMA kiukuaji. Ni kweli CHADEMA itabaki kama ilivyokuwepo bila Kafulila lakini it will take long time for its VISION "kushika dola" to be realized. Mpingeni Zitto mnavyoweza, lakini nadhani ni wakati muafaka wa kukubali kuwa Mawazo ya Zitto ni mtaji mkubwa sana ndani ya CHADEMA.

Nimesoma post za viongozi wanaochangia humu kutoka CHADEMA, ujengaji hoja hasa wanapojibu maswali magumu "sensitive questions" wapo so emotional, wanapersonalize, wanatoka nje ya mada mara nyingi, At least Zitto na Dr. Slaa wamekuwa watu wa hoja. I doubt we shall have to wait mpaka siku mtu mwingine anaongoza CHADEMA kuweza kukubalika kwa baadhi ya sisi watanzania ambao bado hatuna Itikadi.
 
Kama maneno haya ni ya kweli, THEN nakubali kuwa kimkakati ZITTO ni muelewa. CHADEMA ni chama maarufu cha kiasiasa kwa wapiga kura lakini kina wawakilishi wachache bungeni, why? CUF sio haiizidi CHADEMA kwa umaarufu kwa wapiga Kuara lakini kina wabunge Kibao bungeni, kwanini? CHADEMA kina ajenda zenye tija lakini haziwezi kubebwa bungeni kwa nguvu inayostahili kwasababu wana idadi ndogo ya wabunge, na wabunge wa upinzani walio wengi (CUF) hawajazipa priorities ajenda za CHADEMA. Kwa hiyo sasa kama Kafulila alikuwa ni potential candidate huko Kigoma na kama kukua kwa CHADEMA huko Kigoma kusini kunachangiwa kwa kiasi kikubwana Mh. Kafulila basi NCCR_ Mageuzi itapata mwakilishi kutoka Kigoma mwakani na CHADEMA wamelipoteza jimbo lao la uhakika.

Hili Ni kosa la kimkakati, Nakubalina na Zitto kuwa huu haukuwa wakati muafaka kumfukuza Mh. Kafulila kutoka kwenye nafasi yake, kwani kunaathiri CHAMA kiukuaji. Ni kweli CHADEMA itabaki kama ilivyokuwepo bila Kafulila lakini it will take long time for its VISION "kushika dola" to be realize. Mpingeni Zitto mnavyoweza lakini, lakini nadhani ni wakati muafaka wa kukubali kuwa Mawazo ya Zitto ni mtaji mkubwa sana ndani ya CHADEMA.

Nimesoma post za viongozi wanaochangia humu kutoka CHADEMA, ujengaji hoja hasa wanapojibu maswali magumu "sensitive questions" wapo so emotional, wanapersonalize, wanatoka nje ya mada mara nyingi, At least Zitto na Dr. Slaa wamekuwa watu wa hoja. I doubt we shall have o wait mpaka siku mtu mwingine anaongoza CHADEMA kuweza kukubalika kwa baadhi ya sisi watanzania ambao bado hatuna Itikadi.
CUF hawana mbunge hata mmoja TZ bara wote hao wanatoka zanzibar!!
 
Si kosa kwake kuamua kusuka au kunyoa. zote ni khiari zake. Ila cha msingi ajipange vizuri na kuangalia wapi pahala sahihi atupe kete yake kwani msimu unakaribia.
 
Kama maneno haya ni ya kweli, THEN nakubali kuwa kimkakati ZITTO ni muelewa. CHADEMA ni chama maarufu cha kiasiasa kwa wapiga kura lakini kina wawakilishi wachache bungeni, why? CUF sio haiizidi CHADEMA kwa umaarufu kwa wapiga Kuara lakini kina wabunge Kibao bungeni, kwanini? CHADEMA kina ajenda zenye tija lakini haziwezi kubebwa bungeni kwa nguvu inayostahili kwasababu wana idadi ndogo ya wabunge, na wabunge wa upinzani walio wengi (CUF) hawajazipa priorities ajenda za CHADEMA. Kwa hiyo sasa kama Kafulila alikuwa ni potential candidate huko Kigoma na kama kukua kwa CHADEMA huko Kigoma kusini kunachangiwa kwa kiasi kikubwana Mh. Kafulila basi NCCR_ Mageuzi itapata mwakilishi kutoka Kigoma mwakani na CHADEMA wamelipoteza jimbo lao la uhakika.

Hili Ni kosa la kimkakati, Nakubalina na Zitto kuwa huu haukuwa wakati muafaka kumfukuza Mh. Kafulila kutoka kwenye nafasi yake, kwani kunaathiri CHAMA kiukuaji. Ni kweli CHADEMA itabaki kama ilivyokuwepo bila Kafulila lakini it will take long time for its VISION "kushika dola" to be realize. Mpingeni Zitto mnavyoweza lakini, lakini nadhani ni wakati muafaka wa kukubali kuwa Mawazo ya Zitto ni mtaji mkubwa sana ndani ya CHADEMA.

Nimesoma post za viongozi wanaochangia humu kutoka CHADEMA, ujengaji hoja hasa wanapojibu maswali magumu "sensitive questions" wapo so emotional, wanapersonalize, wanatoka nje ya mada mara nyingi, At least Zitto na Dr. Slaa wamekuwa watu wa hoja. I doubt we shall have o wait mpaka siku mtu mwingine anaongoza CHADEMA kuweza kukubalika kwa baadhi ya sisi watanzania ambao bado hatuna Itikadi.

Heshima kwako Mbogela.

Nimesoma post nyingi sana kuhusiana na hii mada kwa kweli dada/kaka Mbogela uko juu sana sijui ni kwanini hauko kwenye safu ya uongozi wa CHADEMA,ungewasaidia sana kuachana na siasa za kukurupuka na zisizo na maslahi kwa chama hasa kipindi hiki kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.


 
CUF hawana mbunge hata mmoja TZ bara wote hao wanatoka zanzibar!!
kwani Zanzibar sio Tanzania? ni sawa na mtu aseme CHADEMA ina wabunge wengi kutoka Kilimanjaro na haina mbunge hata mmoja kutoka Zanzibar. Wanapopiga kura bungeni haijalishi ni mbunge wa kutoka Mtwara Corridor au Kanda ya ziwa, Kutoka nyanda za juu kasikazini au nyanda za juu kusini, ni idadi ya wabunge wa bunge la JMT. Kwa hiyo ninachosema hapa ni kuwa Makakati wa kuongeza wabunge bungeni ungekuwa ni mkakati wenye tija kwa CHADEMA na unaotekelezeka.

Mfano kama CHADEMA mwakani wanapata wabunge asilimia 60 na Mh. JK anashinda kwa asilimia 60 kwenye nafasi ya urais. Je hoja ya kuwa na waziri Mkuu kutoka Chadema haitakuwa na nguvu? Au uundwaji wa serikali ya mseto hautakuwa bayana? Kama unafuatilia sana matamshi ya viongozi wa CHADEMA utaona kabisa ni nani anaona mwenendo wa CHADEMA kwa kipimo sahihi na anaweka mikakati sahihi, ni huyu Mh. Anayekataa siasa za kuvizia na anapenda siasa za kujipanga. Ndio maana kwa hili naungana naye kuwa Inawezekana CHADEMA hawana mkakati wa kushika dola. Hata Mzee mwanakijiji ameshawaonya several times kwenye masuala mbali mbali kuwa hawaoneshi kama wapo serious kutaka kushika dola kweli.
 
CUF hawana mbunge hata mmoja TZ bara wote hao wanatoka zanzibar!!

Chukua mfano ungekuwa ni mwanasiasa ambaye huna chama kwa mfano lakini unauwezo mzuri wa kuongoza na kushawishi. Sasa tutakupa kazi ya uenezi wa chama, Tukikuambia uchague unataka tukupe uenezi utachagua lipi kati ya haya.
1. Kuitangaza na kuijengea image nzuri CUF Tanzania bara na tutakupima kwa idadi ya wanachama utakao wasajili na idadi ya washindi wa nafasi za kisiasa kwenye duru mbali mbali za uchaguzi.
2. Kuitangaza na kuipa kuikuza CHADEMA Tanzania Visiwani na utapimwa kwa usajili wa wanachama na idadi ya washindi wa viti mbali mbali wakati wa chaguzi

Pia ndugu yangu naomba nikuambie, wengi walimpinga mzee mwanakijiji kwenye ile thread aliyouliza CHADEMA wamefanya nini kuaminiwa kushika dola, wapingaji wakasema wafanye nini wakiwa Chama cha upinzani? wao walidhani mwanakijiji anauliza kama wamefanya kazi za ujenzi wa barabara, umeme, miradi ya maji, kilimo nk.

Wengine tunaona tofauti, tulimuelewa Mzee mwanakijiji tofauti, Chama cha upinzani kinapimwa kwa msukumo na mbinyo kinaotoa kwa serikali kutekeleza majukumu ambayo serikali inapaswa kuyafanya kwa wanachi wake. Kwa mfano kama CHADEMA wangekuwa na wabunge wengi bungeni leo hii hoja ya EPA ambayo waliasisi ingekuwa ilishafungwa siku nyingi. Na hili ndilo wanachi tungewapima nalo. Sasa hivi wao na ajenda yao ya ufisadi imekosa ufanisi wa kuwapimia na matokeo yake Anna kilango, Selelii, Mwakyembe wanachukua Credit kwa hiyo.

Kama CHADEMA wangekuwa na wabunge wakutosha bungeni, leo hii suala la Richomnd isingekuwa ajenda ya CCM ana kamati za Mwinyi, ingekuwa ni ajenda ya watanzania, Leo hii tungekuwa tunajua kwa uhakika huduma za shirika la reli zinamwelekeo gani, na kama wenzetu wa kanda ya ziwa watasafiri krismass kwenda nyumbani kwa usafiri wa uhakika?

CHADEMA wanapaswa kuwa na mkakati wa makusudi wa kushika dola, hata ndani ya baraza la mawaziri kuna kutofautiana, kama Rais atakuwa wakati wote analazimisha hoja zake zipite bila kujali hoja za mawaziri wake basi serikali hiyo itakuwa ya "one man show" na matokeo yake Rais ansimamishwa barabarani kwasababu wanachi wanataka matuta kwenye bara bara kuzuia magari yasiende kasi, kitu ambacho hata mwenyekiti wa kitongoji angeweza kukimaliza.

CHADEMA lazima wakubali it was not a right time to make a move they made, CHAMA kitatulia hakutakuwa na choko choko kama kilivyokuwa kimetulia wakati wa uenyekiti wa Edwin Mtei, wakati wa Bob Makani lakini je kitafika nchi ya ahadi (Kuongoza dola)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom