Polisi yachunguza tukio la Watu watatu kuuawa baada ya kudaiwa kuiba Bodaboda eneo la Pugu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linachunguza tukio la mauaji ya watu watatu lililotokea tarehe 7 Februari, 2024 majira ya saa 9 (tisa) usiku huko eneo la Pugu Kisumo Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.

Watu hao waliouwawa na kundi la watu kwa kuwashambulia na silaha za jadi, wanadaiwa kukutwa wakiwa na pikipiki namba MC. 520 EBV aina ya Boxer Nyeusi iliyoporwa kwa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Husein Mohamed Simba (28) mwendesha bodaboda wa kijiwe ‘F’ cha Pugu Kinyamwezi anayeishi Viwege kwa Mpemba. Inadaiwa kabla ya kumpora, walimshambulia na baadae kumtupa pembezoni mwa barabara.

Tukio hilo linaelezwa kufanyika tarehe 7 Februari, 2024 majira kati ya saa 6 -7 usiku huko eneo la Pugu Kinyamwezi kaburi moja baada kumkodi bodaboda huyo.

Ufuatiliaji wa wananchi kwa kufuatilia GPS iliyofungwa kwenye pikipiki hiyoiliwafikisha eneo la Pugu Kisumo ambapo waliwakuta watuhumiwa hao wote watatu wakiwa kwenye pikipiki iliyoporwa, wakawashambulia na kuwajeruhi sana. Jeshi lilifika eneo la tukio na kukuta watuhumiwa wakiwa tayari wameshapoteza maisha.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linachunguza kwa kina tukio hili na likibaini kuwepo kwa ukiukwaji wowote wa sheria, litachukua hatua.

Imetolewa na ;
Muliro J. MULIRO - SACP
Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam
 
Walijuaje kama ndo hao?
Kuna dogo mmoja Magomeni aliiba pikipiki akaenda nayo masikani kwao akaipaki akaenda dukani kuchukua sigara, kumbe ile pikipiki ina GPRS ile pikipiki alivyoicha pale kuna mshkaji akawa ameenda kuikalia, kule ilipoibiwa pikipiki wakawa wanaifatilia na wakafanikiwa kufika mpaka pale ilipo pikipiki na wakamkuta mwana wakajua ndo yeye aliyefanya tukio unaambiwa mwana alichezea kipigo mpaka kakata moto. Ili tukio limetokea Magomeni
 
Back
Top Bottom