Mganga aliyedaiwa kuwalewesha na kisha kuwaibia watu 16 akamatwa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,978
141,994
Kijana mmoja aliyefahamika kwa Jina la Lucas ametiwa mbaroni na police kwa kutapeli Watu akijifanya ni Mganga wa Kienyeji

Kamanda Muliro amesema Lucas atafikishwa mahakamani kesho

Source: Upendo TV

Mlale Unono 😀😀😀🔥

=====
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limemkamata na kumuhoji kwa kina Mtu aliyejifanya Mganga wa jadi Lucas Salumu Baswege(42), Mkazi wa Kisemvule, Mkuranga kwa tuhuma za kuwanywesha dawa Watu zaidi ya 16 maeneo tofautitofauti dawa inayodhaniwa kuwa ni sumu na kuwaibia.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Muliro Jumanne amesema “Uchunguzi wa awali umebaini Mtuhumiwa huyo alifanya matukio kama hayo maeneo ya Mjimwema Kigamboni, Tuangoma , Kilungule na Ubungo, vitu alivyoiba tayari vimekamatwa na Polisi ikiwemo pikipiki iliyoibwa Tuangoma na simu za mkoni 10 ambazo tayari zimetambuliwa na wenye nazo”

“Jeshi la Polisi pia limemkamata Thomas Mhagama (35) Fundi simu wa Temeke Sandali ambaye amekuwa akishirikiana na Mganga huyo wa jadi kwa kupokea simu za wizi na kuziuza kwa Watu, Watuhumiwa wote watafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo”

Pia soma: Dar: Polisi wamsaka Mganga aliyelewesha Watu 16 wa familia moja kisha kuwaibia
 
Naagiza wamuachie mara moja huyo kijana muadilifu aliyekuwa anajitafutia mkate wake!

Muliro mwenyewe jambazi tu, wamuachie Lucas haraka sana.
 
Kwani ukiwa mganga wa kienyeji lazima uwe na diploma ya D MBILI?

Analaghai vipi watu?

Mtu akiamua kuwa mganga wa kienyeji, na watu wakamuamini, shida iko wapi?
 
Kijana mmoja aliyefahamika kwa Jina la Lucas ametiwa mbaroni na police kwa kutapeli Watu akijifanya ni Mganga wa Kienyeji

Kamanda Muliro amesema Lucas atafikishwa mahakamani kesho

Source: Upendo TV

Mlale Unono 😀😀😀🔥

=====
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limemkamata na kumuhoji kwa kina Mtu aliyejifanya Mganga wa jadi Lucas Salumu Baswege(42), Mkazi wa Kisemvule, Mkuranga kwa tuhuma za kuwanywesha dawa Watu zaidi ya 16 maeneo tofautitofauti dawa inayodhaniwa kuwa ni sumu na kuwaibia.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Muliro Jumanne amesema “Uchunguzi wa awali umebaini Mtuhumiwa huyo alifanya matukio kama hayo maeneo ya Mjimwema Kigamboni, Tuangoma , Kilungule na Ubungo, vitu alivyoiba tayari vimekamatwa na Polisi ikiwemo pikipiki iliyoibwa Tuangoma na simu za mkoni 10 ambazo tayari zimetambuliwa na wenye nazo”

“Jeshi la Polisi pia limemkamata Thomas Mhagama (35) Fundi simu wa Temeke Sandali ambaye amekuwa akishirikiana na Mganga huyo wa jadi kwa kupokea simu za wizi na kuziuza kwa Watu, Watuhumiwa wote watafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo”

Pia soma: Dar: Polisi wamsaka Mganga aliyelewesha Watu 16 wa familia moja kisha kuwaibia
Lucas mwashambwa au Luka Kani huyo
 
Waganga akili zao huwa low sana

Dah huwa naamini wanaoenda kwao pia akili zao huwa ni ndogo hata awe amesomaje?
 
Back
Top Bottom