Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,987
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linachunguza tukio la kuuwawa kwa mtoto wa miaka 7 mwanafunzi wa shule ya msingi Kibonde maji B, Mbagala na mwili wake kukutwa tarehe 13 Machi, 2024 kwenye msitu wa Jeshi karibu na Shule aliyokuwa anasoma.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Muliro J. Muliro amesema Mtoto huyo aliondoka nyumbani kwao na mtoto mwenzake tarehe 12 Machi 2024 majira ya 11:30 jioni.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Polisi Kilwa road kwa uchunguzi zaidi. Ufuatiliaji mkali unaendelea kumtafuta mtuhumiwa/ watuhumiwa waliohusika ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.