Dar es salaam wamelala

Kwanini watu mnataka watu wafanye vitu kwa mtazamo wenu? Kama umechagua CUF, CDM, TLP is good for you. Waachieni wenzenu watumie haki zao za kikatiba na kiraia.
 
oh, ndo maana ilala na temeke mbunge lazime awe born hiahia die hiahia siyo!..Poleni bandugu

OK, Ni MOSHI peke yake ndio wanaweza kuchagua mbunge Mmakonde na kumuacha Mchaga. Si unaona wabunge wao huko ni wakutoka mikoa ya kusini na .....

Mawazo ya kufikirika.....Shaaban Robert
 
wana jf
kwa mtazamo wangu naona watu wa mikoani wamejitambua muda mrefu na hata kuchagua wabunge kutoka vyama vya upinzani tokea mabunge yaliyopita(ukiacha kawe na ubungo 2010),ukiangalia msukumo uliopo arusha,mara,mbeya ,kigoma,songea,kagera,mwanza nk utaliona hilo.je ni kwanini wana dar hawana mwamko sana wa kimapinduzi na ukizingatia wajanja wengi wapo hapo?
nawasilisha ukumbini
wewe unaishi wapi???? Dar au nje????
 
Ndio maana wamemchagua DR fake Didas Masuburi eti kuwa MEYA !What a shame kwa hawa WASWAHILI!
 
Watz wa dsm wako chini ya vigezo vingi mno. Kubwa lao ni maisha. Wengi wao ni wajasilia mali. Hawa ni wale, bila chapaa basi kila kitu hakiendi, wafanyakazi nao mshahara hautoshi. Omba omba ni wengi mno, mateja ni kabisa. Hapa asilimia kubwa ni wale waliokata tamaa na kuridhika na matatizo yao ukizingatia kwamba wengi ni wakuja. Inashangaza sana utakuta kwamba hata mambo ya jamii inakua ni mtu mmoja mmoja. Je mambo ya uchaguzi siitakuwa zaidi ya hapo?. Wapenda mabadiriko tupo wengi lakini tumezingirwa na roho ya kukata tamaa. Fikiria temeke, watu wake ni wale wa hali ya chini mno. Ilala pia wale wale tu. Tofauti na kinondoni imejazwa na watu wa kutoka AR,MS,MZ,TARIME n.k. Watu hawa ni wale wasiopenda ujinga katika mstakabari mzima wa haki na maisha.

Mkuu,

Temeke walishahi kumchagua Mrema kuwa mbunge wao. Waliwahi kuchagua mbunge kutoka CUF. Na wakati wa mfumo wa chama kimoja walikuwa mbunge mpemba ambaye aliipa taabu serikali kuhusu Kigamboni.

Watu hawajalala hila unataka wafanya vile unavyofikiri wewe.
 
Dar es Salaam hawajalal kama unvyofikiria. Hawana sababu ya kuwachaguwa wakuja. Utakuta hata hao wabunge wawili ni wakuja tu na wamechaguliwa na wakuja. Na madhara yake yataonekana baada ya muda si mrefu.

Si kwamba wamelala issue ni kwamba wengi wako busy for nothing. Of course wengi wao wana assume kuna mtu atafanya kitu badala yao. huu ni ujinga tuamke.
 
Baada ya kufikiri kodogo, naona huyu jamaa aliosema Dar Es Salaam wamelala ana point.

Nyerere, alikaribishwa na vijana wa Dar. Hata suruali alikuwa hajawahi kuvaa, kwani alikuja hapa na kaptura. Akawazidi ujanja akaukwaa uRais halafu akawageuka vibaya sana.

Katika siku hizo Nyerere alikuwa akivaa kaptura na soksi ndefu, mavazi yaliyopendwa na walimu wa shule na hasa kivazi kilichopendwa na wale waliojiona wameelimika, hususan watu wenye asili ya bara. Nyerere amenukuliwa akisema kuwa ilikuwa Dossa Aziz ndiye aliyemtahadharisha kuwa maadam sasa anachanganyika na wazee haitakuwa vyema kwake kuonekana amevaa kaptura.

soma zaidi: http://www.king.igs.net/~kassim/an-nuur3/291/291-7.htm
 
Enzi za wakati huo(mfumo wa vyama vingi bado mchanga) zimepitwa na wakati, huwezi kulinganisha na sasa. Kwa kweli wote tufike mahali tutambue kwamba ni sisi wenyewe ni chanzo cha yote. Tukitaka mabadiriko inawezekana kabisa. Kwani ccm ni kitu gani? Sasa angalia hapo mwanzo wa kampeni, mtemvu aliahidi mambo mengi tu ndani ya 5years, kubwa ni kuifanya hospitari ya temeke iwe ya rufaa, hii ni ahadi kubwa sana na hata kipofu haiwezi kumuingia akilini. Na inasubiriwa hiyo itekelezwe. Utashangaa ni sisi wenyewe na kukata tamaa kwetu, tutapiga debe arudi, tunasubiri mstari utakaochorwa jimbo la ubungo na kawe ndipo 2o15 maamuzi ya busara yafikiwe. Temeke, ukonga n.k.
 
Suala si wakuja wewe, zomba. Watz wa dsm tuamke bado asubuhi. Na kama ni kada wa hao ccm, basi elimu ya uraia uipate ya kutosha ili unapotoa hoja iwe yenye nguvu. Wakati umefika tz ibadirike kiuongozi.
 
Dsm wanajua haki zao hawawezi kuingizwa mkenge wa kijinga kama wengine wa huko mikoani. Jimbo kama la Ilala linachangia 80% ya mapato ya serikali ya kila mwezi, sasa unafikiri wa kuja anaweza kulishika hilo jimbo? Hata CHADEMA japokuwa makao makuu yao yapo hapa dar waliogopa kuliingia hilo jimbo

Wewe ni Empty Brain kweli, kumbe sekta ya Utalii inaingiza ngapi, Madini na Kilimo je? Utalii ulioko Ilala unashinda wa Arusha na mbuga zake? Madini ya Kanda ya Ziwa na Samaki zake. Kilimo cha nchi nzima, kuanzia kahawa, pamba, tumbaku, korosho za Lindi na Mtwara na Mazao ya Chakula ya mikoa ya Big 5 yanashindwa na kilimo cha Ilala. Ama kweli wewe ndo Bongo Lala wa Ilala!
 
Baada ya kufikiri kodogo, naona huyu jamaa aliosema Dar Es Salaam wamelala ana point.

Nyerere, alikaribishwa na vijana wa Dar. Hata suruali alikuwa hajawahi kuvaa, kwani alikuja hapa na kaptura. Akawazidi ujanja akaukwaa uRais halafu akawageuka vibaya sana.

Katika siku hizo Nyerere alikuwa akivaa kaptura na soksi ndefu, mavazi yaliyopendwa na walimu wa shule na hasa kivazi kilichopendwa na wale waliojiona wameelimika, hususan watu wenye asili ya bara. Nyerere amenukuliwa akisema kuwa ilikuwa Dossa Aziz ndiye aliyemtahadharisha kuwa maadam sasa anachanganyika na wazee haitakuwa vyema kwake kuonekana amevaa kaptura.

soma zaidi: An-nuur Na. 291

Wewe ulitaka avae kanzu na nusu koti? Waswahili wa Dar walikuwa waoga kupambana na Mkoloni, maneno mengi ya kwenye kahawa lakini hawawezi kujieleza mbele ya mkoloni. Wakaona wamtangulize JK wa Ukweli kwa vile ana asili ya ujasiri toka Mara. Lakini baada ya kupewa nchi na wakoloni si alimkabidhi nchi Kawawa yeye akaenda kuimarisha chama? Mwacheni Baba wa Taifa apumzike kwa amani huko aliko.
 
Wajanja wengi au wezi wengi ndio wapo dar.
Dar wizi mtupu kuanzia kwenye ngazi ya umachinga hadi mainvestors wakubwa.
Watu wa dar wanaangalia nafsi zao na mapinduzi ya kweli unatakiwa uangalie nafsi za wengine.

Na wezi na majambazi wenyewe ni hawa mashabiki wa chama fulani cha upinzani ambacho uwizi na ujambazi ni asili yao huko wanakotoka ktk mikoa ya Kaskazini!!!
Dar lilikuwa jiji salama kiasili lakini baada ya kuvamiwa na hawa jamaa toka huko kaskazini, yaani uwizi, ukahaba, uzinzi, rushwa, ukabila ndio ulipopamba moto!
 
Wewe ulitaka avae kanzu na nusu koti? Waswahili wa Dar walikuwa waoga kupambana na Mkoloni, maneno mengi ya kwenye kahawa lakini hawawezi kujieleza mbele ya mkoloni. Wakaona wamtangulize JK wa Ukweli kwa vile ana asili ya ujasiri toka Mara. Lakini baada ya kupewa nchi na wakoloni si alimkabidhi nchi Kawawa yeye akaenda kuimarisha chama? Mwacheni Baba wa Taifa apumzike kwa amani huko aliko.

Baadae alianza kuvaa kofia aina ya kibarakashehe!!
 
Baada ya kufikiri kodogo, naona huyu jamaa aliosema Dar Es Salaam wamelala ana point.

Nyerere, alikaribishwa na vijana wa Dar. Hata suruali alikuwa hajawahi kuvaa, kwani alikuja hapa na kaptura. Akawazidi ujanja akaukwaa uRais halafu akawageuka vibaya sana.

Katika siku hizo Nyerere alikuwa akivaa kaptura na soksi ndefu, mavazi yaliyopendwa na walimu wa shule na hasa kivazi kilichopendwa na wale waliojiona wameelimika, hususan watu wenye asili ya bara. Nyerere amenukuliwa akisema kuwa ilikuwa Dossa Aziz ndiye aliyemtahadharisha kuwa maadam sasa anachanganyika na wazee haitakuwa vyema kwake kuonekana amevaa kaptura.

soma zaidi: An-nuur Na. 291
wallah naapa kumsikia (System at w0rk) (ZOMBA)anasapot thread japo with -ve perception

wallah naapa kumsikia (System at w0rk) (ZOMBA)anasapot thread japo with -ve perception
mkuu hiyo gazeti uliyoiquote inasomwa na na nyinyi walengwa tu,haiwezi kuuza hata kopi 1000 kwa wiki hapa dar kwenye population ya watu 5,000,000 lakini kwa kuwa mnajua kuongea sana vijiweni na kwenye daladala wapo wanaowasikiliza..humu JF ni community iliyoelimika japo sauti yao haisikiki mbali kwani ni watanzania wachache wenye uwezo wa kumiliki pc na mtandao au kufanya kazi ofisi zenye kuwa na uwezo huo.pia ni wachache wenye kumiliki simu zenye uwezo wa kubrowse na pia wenye uthubutu wa kunena kilichopo mioyoni mwao.
anyway tunakusikiliza na kukupembua
ukitaka kusikilizwa na kukubaliwa basi uwe unachangia Annur na pia mgawe nakala nchi nzima bure kwa wale wasomi wenu wa madrasa
Siku njema Cocroach!!
 
Yaani hata huyo mbunge wa Ukonga na Segerea sijamsikia wala kumuona akitoa pole kwa waathirika wa mabomu ambao ni wapiga kura wake!...yupo Dodoma anakula nyama choma tu
 
Back
Top Bottom