meningitis
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 8,349
- 4,674
wakati umefika wa kusema ukweli kuwa huduma za afya haziwezi kuwa bure!
Amefanya vizuri kuondoka. Ni afadhali aondoke wabaki watu wenye wito na moyo kuliko kubaki kunyanyasa wananchi wenye matatizo.
Kuondoka kwake kutaisaidia serikali kupeleka wasomi zaidi wakasomee hiyo area yake kama ni kweli yupo peke yake.
Ila kwa Tanzania ya leo hatuna eneo ambao tuna mtaalam mmoja.
Naamini kwa dhati kabisa kuwa Kikwete hakufikiria kwa kina madhara ya kauli yake kuwa asiyeridhika na malipo ya serikali aondoke. Naamini aliitoa kauli hii bila kufikiria kuwa kwa muda mrefu madaktari, na wataalamu wengine wengi tu, wamekuwa wakifanya kazi wkamoyo wa kuipenda nchi yao. Ingawa wanakatishwa tamaa na malipo dunui, lakini watu hawa wanatiwa moyo na uzalendo wao ambao hutiwa moyo zaidi na kauli chanya za viongozi wao. Inapotokea kiongozi, tena kiongozi mkuu, kutoa kauli kama hii ya Kikwete, kwa kweli inawakatisha tamaa sana.Katika kuonyesha kuitika mwito wa Rais kikwete aliyetangaza kuwa Madaktari wasioridhika na malipo kiduchu na mazingira mabaya wanayofanyia kazi hapa nchini waondoke, Daktari pekee bingwa wa upasuaji wa vitoto vichanga (paediatric surgeon) ameondoka muhimbili na kuhamia hospitali moja ya binafsi mikoa ya kaskazini.
Hili ni pigo kubwa sana kwa watoto wachanga na sisi wazazi. Sasa mtoto akiwa na tatizo la upasuaji sasa hana tumaini tena la kuishi maana daktari huyu alikuwa anawafanyaia upasuaji watoto wote kutoka nchi nzima.
Ubinafsi huu wa wanasiasa kujineemesha huku wakitukana na kuadharau wataalamu utatumaliza.
Imagine mwanao anazaliwa bila njia ya haja kubwa halafu anakosa kufanyiwa upasuaji wa kuifungua! Mungu atusaidie!
atapatikana mwingine kwa njia hizo hizo alizopatikana yeye.
Anaitwa Daktari Bingwa wa Watoto.
kuna madaktari wanaotembeza cv zao wanatafuta kazi,haya sasa mambo hayo.inaitwa bandua,bandika
Njia ni hizi: S/Msingi 7, Sekondari 6, Shahada ya kwanza 6, kuwa wa watoto 4 na kuwa mpasuaji 4 jumla ni miaka 27 hao watanzania watazaliwa kweli waweje? Tusichukue majibu mepesi kujibu hoja nzito, kumtayarisha daktari bingwa inachukua muda mrefu na bado kumfanya awe mzoefu inachukua muda mrefu zaidi kwa hiyo labda kama wewe umeshamaliza kuzaa na watoto wako ni wazee lakini hata hivyo wajukuu wako watazaa watoto watakaokuwa kama waliolishwa dawa ya 'thalidomide' ukitaka google upate undani wake zaidi maana unashabikia kitu usichokijua naona!
Sure ni paediatric surgeon, ila sina hakika kama yupo pekeyake, ila kuna Dr. Sayi, mara nyingi alikuwa anafanya operation za watoto sina hakika kama ni paediatric surgeon au la.Anaitwa Dr. Mng'ong'o ..hapana, uliowataja mkuu ni Pediatricians ( Pediatric Physicians), na aliyeondoka ni Pediatric Surgeon...so hawawezi fanya upsauaji kwani si speciality yao...ila aliondoka zamani mkuu yapata miezi miwili sasa.
Sure ni paediatric surgeon, ila sina hakika kama yupo pekeyake, ila kuna Dr. Sayi, mara nyingi alikuwa anafanya operation za watoto sina hakika kama ni paediatric surgeon au la.
Huyo mama alikuja muhimbili nadhani kati ya 2006 au 2007 akitoke KCMC. nadhan ameonja machungu ya kufanya kazi na serikali isiyojali na kuthamini michango ya wataalam. Nenda mama kapumzike, uilinde heshima yako dhidi ya kashfa za huyo Dk. ambaye hana sifa za kupewa hizo PhD
huu ni uongo,KCMC kuna madaktari bingwa wanaopasua watoto kila kukicha
kama aliweza kufuatwa Muhimbili, atafatwa huko huko kaskazini hata kama ni Seriani au KCMC
Kama kuna muhusika anasoma thread hii anisikilize kwa makini, Namfahamu vyema Dr Catherine Mng'ong'o alimfanyia oparesheni mtoto wangu.
Sasa nawashauri Serikali kuna daktari wenu huku mtaani anaitwa Dr Kabote mlimdisco KCMC wakati anachukuwa mafunzo yake ili awe daktari Bingwa wa huo upasuaji weni, mimi si mtaalamu wa hayo majina.
Dr Kabote mkamfukuza kazi na kodi zetu tulizomsomesha zimegeuka useless, yuko mtaani anakunywa pombe tu 24/7. pls namfamu huyu Dr Kabote kweli ni mlevi lakini pls hebu mrudisheni huyu mtu afanye kazi, kwani nilimjuwa Dr Catherine kupitia Dr Kabote na Dr Catherine akasema Kabote ni sinior sana kwake kwenye hayo mambo ya upasuaji, na ilibidi Dr Kabote ndio aanze kuwa Daktari Bingwa kabla ya Catherine.
Pls nyinyi serikali dhaifu hebu njooni mumtowe huyu Dr huku mtaani analewa tu wakati tumemsomesha kwa gharama kubwa sana.