Watoto mapacha waliofanyiwa upasuaji wa kutenganishwa waruhusiwa kutoka Muhimbili

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) umeishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na uwekezaji uliofanyika hospitalini hapa ambao umewezesha huduma mbalimbali za kibingwa na ubingwa bobezi kufanyika ikiwemo upasuaji mkubwa wa kutenganisha watoto pacha.

WhatsApp Image 2024-02-27 at 18.12.55_d7dcdb3f.jpg

WhatsApp Image 2024-02-27 at 18.12.26_81b8fb07.jpg
Akizungumza na waandishi wa habari Februari 27, 2024 wakati wa kuwaruhusu watoto pacha waliozaliwa kwa nje wakiwa wameungana tumbo na kifua, ndani waliungana ini na mfupa wa kidari, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Mohamed Janabi, amesema uwekezaji wa kusomesha watalaam, kuboresha miundombinu na ununuzi wa vifaa vya uchunguzi vya kisasa umeiwezesha hospitali hiyo kutoa huduma zinazolingana na hadhi yake.
WhatsApp Image 2024-02-27 at 18.12.14_4c45ea70.jpg
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto MNH, Dkt. Victor Ngota ameeleza kuwa upasuaji wa kuwatenganisha watoto hao, ulichukua saa sita na kuhusisha jopo la wazawa lenye utaalam mchanganyiko wa hali ya juu wa madaktari bingwa wa upasuaji watoto, upasuaji rekebishi, usingizi na ganzi, watalaam wa lishe pamoja na radiolojia.

“Tuliwapokea watoto hawa tarehe 11 Machi 2023 wakiwa na jumla ya kilo nne hivyo tulianza mchakato wa kuwahusisha wataalam ambao wanahusika na huduma hizi, ilituchukua takribani muda wa miezi kumi kuangalia mwenendo wao wa afya kwa ujumla kabla ya kuwatenganisha ili kuweza kupata dira ya namna watakavyoishi mara baada ya kutenganishwa ambapo hadi wanatenganishwa walikua na kilo 16 sawa na kilo nane kwa kila mmoja” amefafanua Dkt. Ngota.

Mzazi wa watoto hawa Bi. Mariam Shabani, mkazi wa Kigamboni Jijini Dar es Salaam, ameishukuru Serikali na watoa huduma wote wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na jinsi alivyohudumiwa katika kipindi chote alichokuwa hapo.
 
Pongezi kwa Samia lakini tukumbuke Kikwete alifanya jitihada kubwa sana kuwekeza kwenye maarifa na Elimu Ili tuweze kuhudumia wagonjwa na magonjwa ambayo hapo awali walipelekwa India kwa gharama kubwa. Aliwekeza kiasi kikubwa kwenye miundo mbinu wezeshi.
 
Nawaza tu, badala ya fedha nyingi kutumika kwa madaktari wa aina hiii ili wajengewe uwezo na vifaa vya kutosha kufanya tafiti nyingi tiba nyingi zifanyike nchini kama hivi, wao wanapeleka kwa wagonga meza na kusinzia
 
Hii si mara ya kwanza Muhimbili kufanya upasuaji wa kutenganisha mapacha...

Lakini sasa soma maneno ya ndugu yangu Dr. Janabi yalivyojaa siasa...
Sio mara ya kwanza lakin hii ndio imekua ya mafanikio, kuna wale wengine walipoteza maisha
 
Pongezi kwa Samia lakini tukumbuke Kikwete alifanya jitihada kubwa sana kuwekeza kwenye maarifa na Elimu Ili tuweze kuhudumia wagonjwa na magonjwa ambayo hapo awali walipelekwa India kwa gharama kubwa. Aliwekeza kiasi kikubwa kwenye miundo mbinu wezeshi.
Hapa Samia au Kikwete wanaingiaje boss? Au uchawa kama kawaida?
 
Wameunganika INI alafu wametenganishwa????

Hapo nilitamaji pata ufafanuzi zaid manahicho kiungo kukitenganisha sijui kwakweli.
 
Lengo ni kuwapatia motisha hao waliofanya kazi zilizoshindikana kwa wengine. Kuwa na jengo wakati chakula huna, ni sawa na kazi bure.
Sasa si ndio wanapata motisha kwa kutengenezewa Legacy itakayo dumu milele hata wao wakifaa inabak kwamba chuo hiki kilijengwa kwasababu ya watu flan waliofanya mambo flan. Heshima yao na shukran za watanzania zitabaki milele kuwahusu wao
 
Back
Top Bottom