Muhimbili yasema upasuaji wa watoto pacha umefanyika kwa mafanikio

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,462
Pacha.jpg

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imetangaza kuwa upasuaji wa kutenganisha watoto waliokuwa wameungana umefanyika kwa mafanikio.

Watoto hao Rehema na Neema walikuwa wameungana kifuani na upasuaji huo umefanyika leo Julai Mosi, 2022 chini ya Wataalam wa Afya 31.

Awali, Mtaalam wa Magonjwa ya Watoto-Muhimbili, Dkt. Petronila Ngiloi alisema watoto hao walikuwa na muunganiko mkubwa wa Ini na kuna uwazi mkubwa katika Kitovu wanachotumia pamoja.

Pia soma > Watoto pacha walioungana kufanyiwa upasuaji Muhimbili, leo Julai 1, 2022
 
Najivunia Tanzania yangu. Huduma kama hizi zilizoeleka kusikika toka ughaibuni na uhindini.

Wabarikiwe waasisi waliowezesha haya matokeo. Tuwatukane, tuwaveze lakini kuna mengi mazuri tukiweka siasa pembeni wamepambana sana.

Heko Tanzania.
 
Ni jambo jema ila waendelee kua chini ya uangalizi maalum ili kuona kama kutakua na reaction yeyote kutoka kwao wote wawili,

Mungu aendelee kuwasimamia In sha Allah.
 
Ni jambo la kujivunia sana kwa tulipofikia kwenye idara ya afya,.. Wananchi hupata matumaini mapya ya maisha yao.. Hongereni madaktari
 
mm nitawapongeza pale nitakapoona hao wtt wazuri wanaishi buheri wa afya, maana kutenganisha na kuishi ni vitu 2 tofauti. wengi huwa wanafanikisha kuwatenganisha lkn baada ya muda fulani tunapewa taarifa za majonzi. Inshallah ,Allah awaepushie mbali na hili watt wazuri.
 
Back
Top Bottom