Dada yangu ananipa hasira, alikimbia ndoa baada ya mwaka sasa yupo kwa wazazi

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Ni dada yangu wa tumbo moja.

Baada ya muda mrefu huku miaka ya kuplewa ikiwa ukingoni, alipata bahati ya kuolewa na kijana msataarabu kabisa, hakika ilikuwa kama muujiza ila dada akakimbia huku ndoa kwa sababu ambazo hadi leo zinaonyesha alimsingizia tu mme wake wazi wazi ilomradi aondoke.

Alipata mtoto akiwa kwenye ndoa , mtindo wa maisha yake tangu ana miaka 15 ulichangia sana kupata mimba kwa shida, wazazi waligharamika sana ili kutetea ndoa yake, Ilifanyika mipango daktari alikuwa anatoka Asia anakuja hapa bongo, gharama yake ya kumweka hapa bongo ilikuwa kama milioni 1 na nusu kila siku, Jumla ya gharama zake zilifika takriban milioni 60 na zaidi ili akamate mimba na isiharibike (Imebidi niweke kiasi ili mjue uchungu nilio nao), haya yalikuwa mapenzi ya wazazi kwa mtoto wakijua kabisa bila mtoto kwenye ndoa ni changamoto na ndoa inaweza kuvunjika. ilibidi Mashamba, viwanja, n.k viuzwe ili kugharamia.

Kapata mtoto wakiwa kwenye ndoa, baada ya miezi minne mtu karudi nyumbani kwa wazazi, kumuuliza vipi anasema ananyanyaswa, tulishangaa maana huyo mme wake ni mtu mstaarabu kabisa japo ninamjua dada yangu yeye ndie mwenye tatizo maana huwa ana kiburi flani hivi tangu namjua, ikawa wazi anamsingizia tu labda kachoka ndoa.

Sasa kuna wiki flani nlienda home nashangaa sista kajiachia kabisa, ka relax , Chakula anapika jumapili tu siku nyingine wanapika house girl, Nguo anazovaa akitoka hazina staha ni taiti nyepesi, jeans zinazombana utafkiri hana lengo hata tone la kurudisha ndoa, Mtoto kaletewa house girl mpya wa kumlea na gharama ni juu ya wazazi, kiukweli nilikuwa najisemea huyu kabla sijaondoka lazima nimtie mambata mazito,

Mme wake hana tatizo anatuma pesa ya malezi kila mwezi, nyumbani karibia kila kitu kipo, Jitihada ziliwahi kufanyika kurejesha ndoa ila sista nikawa namuona kabisa kama haonyeshi ushirikiano wowote, Yani kawa mzigo tu nyumbani nae ame relax kabisa
 
Dada zetu hawa kuna muda unataman hata Wazaz wakose hela ili dunia imtie adabu. Hapo anachoringia ni hizo mali za wazaz wenu na ukimchekea hata ndoa zenu kama mmeoa atazivuruga.

Waambie wazazi wako wampe amri achague kurudi kwa mumewe au atafute pa kwenda, akichagua kwenda mtaani mpeni miezi 6 atarudi kashachoshwa na wahuni na hilo ndio fundisho mtakuwa mmempatia.
 
Ni dada yangu wa tumbo moja.

Baada ya muda mrefu huku miaka ya kuplewa ikiwa ukingoni, alipata bahati ya kuolewa na kijana msataarabu kabisa, hakoka ilikuwa kama muujiza ila dada akakimbia huku ndoa kwa sababu ambazo hadi leo zinaonyesha alimsingizia tu mme wake wazi wazi ilomradi aondoke.
Mke akishazoea kulala bila ya ndani halafu ghafla meza ipinduke aanze kulala nayo madhara yake huwa mengi na makubwa
 
Dada zetu hawa kuna muda unataman hata Wazaz wakose hela ili dunia imtie adabu. Hapo anachoringia ni hizo mali za wazaz wenu na ukimchekea hata ndoa zenu kama mmeoa atazivuruga.
Waambie wazaz wako wampe amri achague kurudi kwa mumewe au atafute pa kwenda, akichagua kwenda mtaani mpeni miezi 6 atarudi kashachoshwa na wahuni na hilo ndio fundisho mtakuwa mmempatia.
Hii ni fact Bora kabisa
 
Ni dada yangu wa tumbo moja.

Baada ya muda mrefu huku miaka ya kuplewa ikiwa ukingoni, alipata bahati ya kuolewa na kijana msataarabu kabisa, hakoka ilikuwa kama muujiza ila dada akakimbia huku ndoa kwa sababu ambazo hadi leo zinaonyesha alimsingizia tu mme wake wazi wazi ilomradi aondoke.
Shida inaanzia kwa wazazi wako....
 
Dada zetu hawa kuna muda unataman hata Wazaz wakose hela ili dunia imtie adabu. Hapo anachoringia ni hizo mali za wazaz wenu na ukimchekea hata ndoa zenu kama mmeoa atazivuruga.
Waambie wazaz wako wampe amri achague kurudi kwa mumewe au atafute pa kwenda, akichagua kwenda mtaani mpeni miezi 6 atarudi kashachoshwa na wahuni na hilo ndio fundisho mtakuwa mmempatia.

sky soldier hili ndio jibu, huyo mjinga anawachosha tu hao wazee, muda wa kufurahia uzee wao wanakaa wanalea mtoto na mjukuu. Fuata huo ushauri uone kama hajanyooka.
 
Ni dada yangu wa tumbo moja.

Baada ya muda mrefu huku miaka ya kuplewa ikiwa ukingoni, alipata bahati ya kuolewa na kijana msataarabu kabisa, hakoka ilikuwa kama muujiza ila dada akakimbia huku ndoa kwa sababu ambazo hadi leo zinaonyesha alimsingizia tu mme wake wazi wazi ilomradi aondoke.
Deka mwana deka...
Tatizo siyo dadako Bali ni Wazazi walvyomlea.
Solution: mhusika dadako lazima na haraka sana asimamishwe na kurekebishwa.
Pili, asomewe ruqya na Dua'a za hidaya aokoke na ujahili/ushetani huo.
Poleni ...
 
Hzo tarakimu za dolali nadhani anajarbu kuwasilisha uchungu alio nao .. jamaa kaweka kuonesha walivoingia gharama kubwa kutetea ndoa ya dada yake lakin
dada mtu Ni kichwa maji Yani Kuna washeli zinapungua.
Kiukweli ni gharama kubwa sana, tulitehemea ndoa itakaa muda mrefu maana kutakuwa na mtoto ila ikawa kinyume, inauma mnoo
 
Back
Top Bottom