Ushuhuda wa dada yangu: Ukioa mdada wa chuoni ambae kwao anaweza kurudi kirahisi tegemea kusingiziwa unamfanyia ubaya akiona majukumu ya ndoa magumu

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,081
Sina maana ya kuwa mmbea ama kumkandia dada yangu ila hii ndio hali halisi ya matatizo haya ya sasa yanayofanya ndoa nyingi kubomoka, mimi nimeleta case study.

Mifano ipo mingi sana juu ya wanawake wasomi wa vyuoni kuwa wasumbufu kwenye ndoa ila wacha niweke kisa cha mtu naemjua kabisa wala si wa kihadithiwa.

Ni dada yangu huyu kabisa, aliitafuta sana ndoa na akaipata kimbebe kikawa kwenye maisha halisi ya ndoa.

Dada alikuwa kakariri sana maisha ya miss independent, haki sawa, ndoa za kitamthilia, n.k kwa bahati mbaya ama nzuri mme wake alikuwa hawezi vumilia haya mambo, kapata kazi hapa mjini na ni msomi ila kakulia sana maisha ya kijijini.

Dada alianza kuleta kiburi kumfulia mme wake nguo akashauri watafte house girl, mme wake akamwambia hata wakimleta house girl bado nguo zake haziwezi fuliwa na house girl, hilo ni jukumu la mwanamke wa ndoa.

Dada alianza kiburi kuamka asubuhi kumpashia mme wake maji, anamwambia mme wake apashe, walikuwa wanakorofishana sana.

Uvivu wa kupika, kuna muda anamwambia mme wake ale huko huko, yeye kachoka kupika.

Dada alikuwa bado hana kazi anashinda nyumbani, anaachiwa hela kila siku nje ya matumizi.

Vitimbwi vilikuwa ni vingi sana ila kwa ustaarabu wa kipekee wa yule bwana dada hakuwahi kupigwa hata kibao.

Baada ya miezi minne ya ndoa nikaanza kuona dada anapost status za kimafumbo za taasisi za kukemea uonevu kwenye ndoa, haki sawa kwenye ndoa, n.k.nikimpigia anadai anateswa na vitu vingine kibao, hio ilikuwa ni mbinu ya kupata tundu la kuchomoka / exit strategy, vitu vingi alikuwa anadanganya.

Alirudi nyumbani na mpaka sasa yupo nyumbani, mzazi hawakuwa na tatizo lolote kwa yeye kuridi na hata anavyoondoka chumba chake kilifungwa asilale mti mwengine.

vikao kama viwili hivi haonyeshi nia ya kurudi, nyumbani karudi na mtoto kuna house girl, anapikiwa, n.k.

Bwana yule anatoa laki 3 ya kumtunza mtoto kila mwezi lakini dada hakuwahi kusema hili, tulikuja gundua baadae, hapa nikaona kabisa sista alikuwa anataka atuvute upande wake tumuone mme wake hafai.

Pia napata stori pale nyumbani kwamba yule bwana akienda kumuona mtoto kuna mchezo mchafu unachezwa, dada anamwambia house girl ampeleke mtoto mtaa wa pili washinde huko hadi baba yake akiondoka, ni dada yangu lakini kwa kuwa nami pia ni baba, nikiona mwanaume mwenzangu anafanyiwa haya inaniuma.

Majukumu ya ndoa kwa mabinti wengi wa vyuoni ni tatizo, wanataka kuendelea na lifestyle za vyuoni ambazo haziwezi kuendana na maisha ya ndoa, wanataka haki sawa bila kutekeleza majukumu yao, wamekuwa brain washed na tamthilia, n.k.
 
Ni dada yangu huyi kabisa, aliitafuta sana ndoa na akaipata kimbebe kikawa kwenye maisha halisi ya ndoa.

Dada alikuwa kakariri sana maisha ya ndoa za kitamthilia ila mme wake alikuwa hawezi vumilia huu upuuzi.

Dada alianza kuchoka kumfulia mme wake nguo akashauri watafte house girl, mme wake akamwambia nguo zake haziwezi fuliwa na house girl inabidi afue dada maana ni majukumu yake.

Dada alianza kuchoka kuamka asubuhi kumpashia mme wake maji, anamwambia mme wake apashe, walikuwa wanakorofishana sana.

Dada alitaka kuendelea tabia zake za kukutana na kutoka out na anaowaita marafiki zake wa kiume, mme wake alikataa hii.

Vitimbwi vilikuwa ni vingi sana

Baada ya miezi minne ya ndoa nikaanza kuona dada anapost status za kimafumbo kuashiria anateswa, nikimpigia anadaibanatishiwa maisha lakini kwa akili yake navyomjua ni rahisi kumjua anaposema uwongo, nikawa kimya tu. Yule mme wake wala hana tatizo na ni mtu mstaarabu sana hakuwahi hata kumpiga japo dada kuna kipindi alifeki kapigwa.

Alirudi nyumbani na mpaka sasa yupo nyumbani, vikao kama viwili hivi haonyeshi nia ya kurudi, nyumbani karudi na mtoto kuna house girl, anapikiwa, n.k.
Wewe naye ni lijinga sana sasa mambo ya dada yako yanakuhusu nini ?

Tafuta demu uende uoe ili ujue ukweli wa mambo sio kuishi kwenye nadharia mshenzi .

Mkuu nisamehe tu ila ni vile sipendi watu wambea kama wewe .

Vipi lakini Yanga atashinda kweli ?
 
Epuka sana kuingilia mambo ya ndoa za watu, hasa ndoa ya dada yako.
Inaelekea una ukaribu sana na mambo ya ndani ya dada yako kiasi cha kujua visa vyote. Haifai kwa mtoto wa kiume.

Kama shemeji ni mtu pisi kama ulivyosimulia basi wewe endelea kuwa na urafiki nae kama mshkaji. Ila usiwe mshauri wa ndoa, ipo siku kibao kitakugeukia uonekane wewe ndio ulikuwa mfitinishaji.
 
Lijamaa ni limbea sana yaani limekalia kuwaza eti dada kaachika nakumsifia shemeji yake .

Yawezekana lilikuwa linaishi huko sasa limetimuliwa na dada yake sio bure
unataka kusema alikua ana lala sebuleni kwa shemeji yake...yaani wa mwisho kulala wa kwanza kuamka
 
Sina maana ya kuwa mmbea ama kumkandia dada yangu ila hii ndio hali halisi ya matatizo haya ya sasa yanayofanya ndoa nyingi kubomoka, mimi nimeleta case study.

Mifano ipo mingi sana juu ya wanawake wasomi wa vyuoni kuwa wasumbufu kwenye ndoa ila wacha niweke kisa cha mtu naemjua kabisa wala si wa kihadithiwa.

Ni dada yangu huyu kabisa, aliitafuta sana ndoa na akaipata kimbebe kikawa kwenye maisha halisi ya ndoa.

Dada alikuwa kakariri sana maisha ya miss independent, haki sawa, ndoa za kitamthilia, n.k kwa bahati mbaya ama nzuri mme wake alikuwa hawezi vumilia haya mambo, kapata kazi hapa mjini na ni msomi ila kakulia sana maisha ya kijijini.

Dada alianza kuchoka kumfulia mme wake nguo akashauri watafte house girl, mme wake akamwambia hata wakimleta house girl bado nguo zake haziwezi fuliwa na house girl inabidi afue dada maana ni majukumu yake.

Dada alianza kuchoka kuamka asubuhi kumpashia mme wake maji, anamwambia mme wake apashe, walikuwa wanakorofishana sana.

Dada alitaka kuendelea tabia zake za kukutana na kutoka out na anaowaita marafiki zake wa kiume, mme wake alikataa hii hasa pale alipokuwa anaona ni kama vile bado hajui nini maana ya ndoa.

Vitimbwi vilikuwa ni vingi sana ila kwa moyo wa kipekee wa yule bwana, dada hakuwahi kupigwa hata kibao, ingekuwa hata mimi angekuwa ashachezea sana tu.

Baada ya miezi minne ya ndoa nikaanza kuona dada anapost status za kimafumbo kuashiria anateswa, nikimpigia anadai anatishiwa maisha lakini kwa akili yake navyomjua ni rahisi kumjua anaposema uwongo, nikawa kimya tu.

Alirudi nyumbani na mpaka sasa yupo nyumbani, mzazi hawakuwa na tatizo lolote kwa yeye kuridi na hata anavyoondoka chumba chake kilifungwa asilale mti mwengine.

vikao kama viwili hivi haonyeshi nia ya kurudi, nyumbani karudi na mtoto kuna house girl, anapikiwa, n.k.

Bwana yule anatoa laki 3 ya kumtunza mtoto kila mwezi lakini dada hakuwahi kusema hili alikuwa anasema hapewi chochote, na hii nikaja kugundua ni mbinu ya kumfanya aliekuwa mme wake tumuone ni mkatili nae apate points za kujitetea.

Majukumu ya ndoa kwa mabinti wengi wa vyuoni ni tatizo, wanataka kuendelea na lifestyle za vyuoni ambazo haziwezi kuendana na maisha ya ndoa, wanataka haki sawa bila kutekeleza majukumu yao, wamekuwa brain washed na tamthilia, n.k.
Hiyo ni reflection ya aina ya malezi aliyopata. Nitarudi
 
Back
Top Bottom