CUF: Wabunge 10 kufukuzwa; Maalim Seif adaiwa kudidimiza chama!

Mod ondoa hii habari ni ya uongo. Nimefuatilia kote mpaka makao makuu na kukutana na Prof Lipumba, Sheikh Sharif na Hamad wote wamethibitisha kuwa hizo zote ni propaganda za uongo tu. Kuwa hakuna aliyeandika hiyo barua, hivyo hiyo ni barua ya kupikwa tu. Hebu ichunguze hakuna hata mahala pamoja alipohojiwa Sheikh Sharif au Prf Lipumba. Hilo ni gazeti au uchwala. Mod hii taarifa itakugharimu ni bora uifutilie mbali.
Mkuu mbona nasikia kuwa Lipumba hayuko Tanzania?
 
Danganya toto tu hiyo, hao CCM B hawana ubavu wa kumfukuza Mbunge yeyote yule.
 
Danganya toto tu hiyo, hao CCM B hawana ubavu wa kumfukuza Mbunge yeyote yule.

Mkuu BAK,

Uko sahihi kabisa kwamba CUF hawawezi kufukuza mbunge maana sidhani kama wako tayari kuingia kwenye kasheshe za uchaguzi na kuhatarisha kupoteza jimbo.

Nilichokiona kwenye hiyo habari ni sarakasi za uongozi ndani ya chama. Kuna mtu anataka ulaji ndani ya chama na hivyo ameanza kulia lia mapema ili apate wafuasi wa kumtetea. Ni Hamad Rashid huyu huyu alileta choko choko iliyopelekea kubadilishwa kwa tafsiri ya kanuni za Bunge kuhusiana Kambi ya Upinzani. Kwa hiyo unaposoma habari za kumhusu inabidi kuwa na kumbukumbu kwamba Hamad ni mtu ambaye ana-mind sana mafao (ulaji) na anaweza kwenda an extra mile ili kufanikisha agenda yake.

Kuanika siri za chama hadharani ni hatari kubwa sana na kwa mwendo huo wapinzani hawawezi kufika mbali. Nikisoma habari hiyo yote ni kwamba mwandishi amepewa kama ilivyo na yeye akaiweka gazetini. Lengo ni kuanza kujenga mazingira ya kupewa u-Katibu Mkuu.

Ngoja tusubiri majibu ya Maalim, Jussa na Prof. Lipumba kwamba watajitetea nini kuhusiana na hilo. Maana hizi ni tuhuma nzito sana ambazo zinalenga kukiua chama au kukivunja mapande mapande. Kwa uzito wa tuhuma zenyewe ninategemea hao watu watatu wajitokeze kujibu na wasipojibu ndo wanaizika CUF taratibu hata huko kwenye ngome yao ya Pemba.

Ndoa ya CUF na CCM inaweza kuzaa matunda kwa CCM kwa kuwa kuna uwezekano wa hii mifarakano mdogo midogo ikaenda mpaka kwenye uteuzi wa wagombea na baada ya hapo ukasikia jimbo limeenda CCM. Yangu macho!
 
Sasa hapa natoa ushauri wangu,Chadema kwa sasa hivi bado hakijapata nguvu zanzibar,hivyo basi kinachotakiwa sasa hivi wafanye kile kinachoitwa vita vya panzi furaha ya kunguru,watafute wabunge wazuri kutoka CUF,wawachukue ili wawezeshe kuijenga chadema upande huo wa zanzibar.kwa hiyo wakati ugomvi unafukuta moto ukiwaka vizuri CDM waanze kuwavuta taratibu angalao CDM ipate mwakilishi hata mmoja kutoka Zanzibar.
 
CUF sio chama cha upinzani wala sio chama twawala. Mguu moja huku mguu moja kule,sasa mnategemea nani awape kura? Jirekebisheni kwanza mjipambanue mko upande gani.
 
Hiyo hali kwa watz wengi ipo. yaani tunakumbatia zaidi uovu kuliko uzuri. Ukifanya kitu kizuri kama Hamad lazima uonekane mwovu kwa asiyekukubali. USIFE MOYO RASHID
 
Sasa siasa imeshika hatamu, hii ndo ile wanaita ngoma ngondoigwa yaani '"nifitini nikufitini".........tihii tihii hiii.....:focus:
 
kilichobakia ni muungano kamili wa ccm + cuf kuzalisha chama kipya cjui watakiitaje, vinginevyo hakuna cuf tena tz. tuacheni cdm tuendelee kulisongesha cufccm mtaona vumbi 2. “vita vya panzi furaha kwa kunguru”
Haswa, tuachane na hao Cuf sisi tusonge mbele na cdm yetu mwisho wa siku tutafika tu
 
Itawagharimu vipi wakati wandishi yupo na jina lake limetolewa. Kwa nini wewe usimfuate mwandishi ukamhoji habari hii kaipata wapi pengine anao ushahidi dhidi ya maneno ya Lipumba au Seif S. Hamad ambao wametaka kukutolea nje..Mtafuta huyo Khamis Mkotya upate uhakika toka pande zote mbili..

Huyo Khamis Mkotya ndie nilianza nae, Hana jibu lolote la maana alichosema eti kama nataka uhakika niwaulize wahusika 'Viongozi wa CUF' Kwani yeye barua kaianika. Hilo ndio jibu lake.

Swali: Kwanini niiamini hiyo barua ambayo haina muhuli wala sahihi, si mtu yeyote anaweza kuiandika. Hapo ndipo nikamuona huyo mwandishi ni Tapeli, isitoshe hakuwaeza kuwahoji wahusika, Prf Lipumba, sheikh Sharif, Jussa na wqbunge hao kumi. Yaani taarifa imekaa kimtaani mtaani tu.

NI UONGO NA HAKUNA KITU KAMA HICHO. M,OD FUTILIA MBALI HII TAARIFA
 
Nimewashika pazuri, mbona hamjibu. Kuna wasomaji 60 na wanachama 9 mnaosoma uongo usiojibika.

Naelewa mtu unaweza kufanya propaganda lakini angalau iwe na miguu.

Uongo! Mod futa hii habari itakugharimu.
 
MMh hiyo ni balaa kweli. Sasa CCM A inaelekea kufa, CCM B nayo iko njia hiyo hiyo.....Nafikiri option waliyobaki nayo na kuua CCM A na B na kuunda CCCUFM..teh...teh.
 
na bado hizo ni rasharasha tu mamboyanakuja. Kaka yangu Mtatiro tumekuimbia sana wimbo wa wewe kuhama hicho chama, nenda chadema kwenye watu makini, huko wamebaki na upemba wao tu hakuna la maana, ondoka huko nenda cdm.

jamani chadema nako kunafuka moshi ukabila udugu na udini unakimaliza cdm haf mtatiro aende kunakofuka moshi acheni hizo
 
vyama vyote vina matatizo hakuna anayejidai kuwa chama chake kiko salama kwani vyama vyote vinaongozwa na watanzania wenye tabia inayoendana. Hivyo matatizo ya vyama vyetu yanafanana. Ni afadhali hata Cuf. Unaweza baki salama ukafanya shughuli zako kama ulikuwa tishio ndani ya uongozi haswa unapoitaka nafasi ya mwenyekiti nyote mashuhuda prof safari yupo salama ila amehamachama. Lakini cdm tumeshuhudia chacha wangwe amepotezwa sababu alitishia nafasi ya mwenyekiti mungu mbowe wa cdm na kutaka kutoa siri ya chama ama moyo wachama.
 
Huyo Khamis Mkotya ndie nilianza nae, Hana jibu lolote la maana alichosema eti kama nataka uhakika niwaulize wahusika 'Viongozi wa CUF' Kwani yeye barua kaianika. Hilo ndio jibu lake.

Swali: Kwanini niiamini hiyo barua ambayo haina muhuli wala sahihi, si mtu yeyote anaweza kuiandika. Hapo ndipo nikamuona huyo mwandishi ni Tapeli, isitoshe hakuwaeza kuwahoji wahusika, Prf Lipumba, sheikh Sharif, Jussa na wqbunge hao kumi. Yaani taarifa imekaa kimtaani mtaani tu.

NI UONGO NA HAKUNA KITU KAMA HICHO. M,OD FUTILIA MBALI HII TAARIFA

Kama barua ni ya uongo kwanini uongozi wa CUF wasilichukulie hatua gazeti na/au mwandishi wa habari hiyo? Maana hilo ni kosa la jinai ya kughushi. Tuhuma kama hizi zikiachwa bila ya kujibiwa ndio mwanzo wa kuisambaratisha CUF. Kuendelea kukanusha hapa hapa JF kwamba ni uongo haisaidii, kitakachosaidia ni kukanusha kwenye gazeti hilo hilo lililoandika habari hiyo.

Mhusika mkuu wa habari hiyo ni Hamad Rashid, na ndiye aliyetoa taarifa hiyo kwa kuwa nina amini kwamba uongozi wa CUF hauwezi kutoa barua kama hiyo kwa waandishi wa habari na ndiyo maana kabla mwandishi hajaanza ku-quote barua ameweka utangulizi wa kile alichokuwa anakijua (kama alikuwa anakijua kweli) na baada ya hapo akaenda kumhoji Hamad Rashid na mwishoni aka-quote barua hiyo.

MOD hawezi kufutilia mbali habari ambayo imetoka kwenye gazeti maana whoever aliye-post habari hiyo hajaiandika mwenyewe bali ameinyofoa kwenye gazeti. So, mwenye kosa ni gazeti/mwandishi/mchapaji/mhariri na wengineo. Bado tunasubiri kauli ya uongozi wa CUF waseme kama hii habari ni ya kizushi au la. Wakikaa kimya tutajua ni ya kweli na ndio maana wamekaa kimya bila kujibu madai ya Hamad Rashid!
 
Kama magamba walifanikiwa kumtumia mrema kuivuruga NCCR. Nirahisi sana kuvuruga cuf ukizingatia wapo kitanda kimoja mia.
 
Taarifa kutoka Kwa Watu Walio Karibu na Maalimu Seif Katibu Mkuu CUF zinaonyesha kuwa ,tuhuma alizotoa Hamadi Rashid zimemuudhi Maalim Seif na sasa anataka kujibu Mabigo Kwa Kutumia Nguvu Yake ya pesa.

Katika Hatua ya Kwanza ametenga kiasi Cha Tshs 180,000,000/= ambazo zitasambazwa kweye ofisi za Wilaya 100 za CUF nchi zima kwa nyakati Tofauti ikiwa kama semehu ya Malipo ya Ruzuku kwa Miezi Sita.

Watafiki wanasema CUF ina Wilaya 100 na kwamba Ruzuku kwa Kila wilaya kwa Mwezi ni Tshs 300,000/=. Hivyo CUF huwa Wanatenga Tshs 30,000,000/= Kila Mwezi Kwa Wilaya 100.
Sasa Tangia Seif awe Makamu wa Kwanza Zanzibar Kumekuwa hakutolewi Kiasi hicho cha pesa Mpka Hamadi Rashid alipoeleza nia yake ya kugombea nafasi ya Katibu Mkuu Taifa.

Chanzo kutoka ofisi ya Uhasibu CUF kinasema Tsh 30,000,000 kwa mwezi mmoja zimeshatumwa na pesa zingine zinafuata!!! Baadhi ya Watendaji Makao Wanashangaa hizo pesa zilikuwa wapi??
Mkakati mwingine uliowekwa ni Maalimu seifu Kufanya ziara nchi zima ambapo amelenga kuonana kwa siri na viongozi wa Cuf Wilaya na Matawi na kuwapa Rushwa kati ya 50,000/= na 100,000/- kwa mufumo wa posho na kumusema vibaya Hamadi Rashidi ili asipate Wafuasi!!!

Utafiti unaonyesha kuwa kati ya tarehe 23/11/1011 n1 24/11/2011 vikao vya mtandao wa Maalimu Seif Vimefanyika Star Light Hotel ambapo wanaelekeza kufanya mikakati hiyo Mikoa ya Kusini Mtwara, Lindi, ambapo inahisiwa Mh Barwani amekuwa anahamasisha harakati za kumutoa Seif Madarakani!!!

Mtu wa Karibu na Maalimu Seif anayeitwa Hamadi MMuManga (0777416630) ndiye anayetajwa kuratibu Ziara za Maalimu Seif Lind amabapo Maalim Sef amepanga kwenda huko Tarehe 2/12/2011

Mgogoro uliopo CUF ni Kwamba Seif hataki Kuachia Ukatibu Mkuu Kwa njia ya Uchaguzi bali Kwa Njia ya Ufalme ambapo yeye anataka kumuweka mtu wake ambaye ni ISMAIL JUSSA.

 
Back
Top Bottom