Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
- Thread starter
- #21
Katika ku--peruse thread zilizoingia baada ya kutoingia humu JF kwa muda nimeikuta hii thread ambayo kusema kweli imenivunja mbavu, na pia kusikitisha. Mwaka 2000 mkutano wa CUF wa Jangwani wa kumalizia kampeni ulikuwa na umati mkubwa ambao hadi sasa haujawahi kuonekana katika eneo hilo hadi leo hii.
Lakini leo hii hawa jamaa zangu CUIF wanafanya mikutano vichochoroni!! Wanaogopa kuitisha mkutano mkubwa pale Jangwani kwa sababu utapwaya sana kwani ni dhahiri chama hicho siyo cha upinzani tena.
Na tatizo liko kwa viongozi wawili tu -- Profesa na HRM. Hebu muone Profesa anamkumbatia Mbatia Jukwaani wakati mwaka 2004 katika uchaguzi wa marudio huko Pemba alikisaliti CUf kwa kuwekea pingamizi wagombea wake na hivyo kufanya CCM izoe majimbo yote kule.
Mbatia alijichimbia huko Pemba wakati wa kampeni kwa shughuli hiyo maalum aliyopewa na CCM dhidi ya CUF hadi alikuwa tayari kupoteza Mbvunge huko Kigoma Kusini katika uchaguzi mdogo wakati huo huo -- maana hakwenda Kigoma kumfanya kampeni.
Nawashauri CUF kwamba akina Profesa wakiachwa kuendelea kukikumbatia chama tawala na vibaraka wake basi watakuwa wanakimaliza kabisa -- hata vichochoroni watu watakuwa wanawazomea au kuwapiga mawe. Lazima CUF wachukuwe hatua kukinusuru chama hasa huku Bara.