Paparazi Muwazi
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 310
- 79
Kambi rasmi ya upinzani kuvunjika hivi karibuni. Hatua hiyo inatokana na msuguano kati ya CHADEMA na CUF. Wadadisi wa mambo wanasema kwamba kwa kanuni za bunge zinasema kwamba chama au ushirikiano wa vyama utaunda kambi rasmi bungeni ikiwa una zaidi ya asilimia 12 ya wabunge. Vyama vya CUF na CHADEMA vyote vina chini ya asilimia 12 kila kimoja ingawa kupitia umoja huo wameweza kutimiza sharti hilo na hivyo kuwa na kambi rasmi. Habari toka ushirikiano wa vyama hivyo bungeni zinaeleza kuwa Dr Slaa kama makamu wa upinzani aliitisha kikao cha Wenyeviti wa vyama hivyo kilichofanyika nyumbani kwa kiongozi wa upinzani Hamad Rashid ili kuepusha hali hiyo. Katika kikao hicho inaelezwa kwamba CHADEMA waliwapatia wenzao wa CUF ushahidi wa mikanda ya video iliyoonyesha viongozi wa NCCR na TLP wanavyotumiwa na baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi kuhujumu harakati za vyama hivyo. Katika kikao hicho inaelezwa kwamba CHADEMA waliwaomba wenzao wa CUF kuvunja rasmi ushirikiano na vyama hivyo na kubakisha ushirikiano kati ya CUF na CHADEMA ambao upo pia bungeni. Chanzo chetu kinaeleza kuwa Prof Lipumba alimweleza Mbowe kukabiliana na msimamo huo, hata hivyo alimjulisha kuwa chama cha CUF kingependa kupata muda wa mwezi mmmoja kuweza kufanya maamuzi hayo. Hata hivyo, mara baada ya kikao hicho kilichofanyikwa mwezi Septemba 2008, Lipumba alikaa kikao na Mbatia na Mrema na kuwaeleza mambo yote yaliyojadiliwa. Katika kikao hicho cha viongozi watatu ambacho hakikumhusisha Mbowe iliamuliwa kwamba vyama hivyo vimuunge mkono mgombea wa NCCR katika uchaguzi wa Tarime. Mwezi mmoja baada ya uchaguzi huo wa Tarime ambapo CHADEMA iliibuka mshindi, palifanyika kikao kingine kati ya Hamad Rashid, Dr Slaa na wabunge wengine wenye ushirikiano bungeni kujadili suala hili na kupokea maamuzi kutoka chama cha CUF hata hivyo chama hicho kilijulisha kuwa Baraza Kuu la chama hicho limeelekeza wapewe muda zaidi kuweza kutafakari kabla ya kufikia maamuzi ya mwisho. Na kwamba CUF iliijulisha CHADEMA kuwa katika kipindi hicho cha subira chama hicho kitasitisha ushirikiano na vyama vya TLP na NCCR. Hata hivyo, uamuzi wa CUF kurejea kuwa na ushirikiano na vyama hivyo wa karibu katika uchaguzi wa Mbeya Vijijini umefanya majadiliano ya dharura kati ya Dr Slaa na Hamad Rashid kuweza kufanyika kuhusu hatima ya ushirikiano bungeni. Kama majadiliano hayo yatafikia hitimisho la kuvunja ushirikiano baina ya vyama hivyo, ni wazi kwamba kambi rasmi ya upinzani itavunjika bungeni. Hali hii itaathiri nguvu ya pamoja katika kupambana na ufisadi. Wachambuzi wa mambo walishabashiri toka mwaka 2008 kwamba watuhumiwa wa ufisadi wangepenyeza nguvu yao katika ushirikiano wa vyama hivyo hali ambayo inaelezwa kuweza kuanza kujitokeza.
PM
PM