Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Usimjaribu bwana Mungu wako.... Kama njia ni kusali tu mbona unaenda kazini kila siku... Why don't you stay at home pray for the bread on your table....
It's obvious gathering zinasambaza ugonjwa and yet Kariakoo is full of people just like a normal day... What do you expect??


Sent using Jamii Forums mobile app
Biblia huwa unasoma?
Watu waliobahatika kulishwa na Mungu moja kwa moja Ni wana wa Israel..hao walibahatika kushushiwa chakula toka mbinguni ..hii ilikuwa katika safari yao kutoka misri nchi ya utumwa kwenda kaanani nchi ya ahadi.

Mungu alimwambia Adam atakula kwa jasho.. lazima ujishughulishe..amekupa uwezo wa kupambanua mambo,amekupa Nguvu,amekupa akili,amekuweka katika ardhi,amekupa kutawala juu ya wanyama na ndege wote.
Mungu anakubariki kupitia kazi unazofanya

Soma comment yangu ya mwanzo utaelewa Nini naongea.
Mwanzo nimesema hivi inabidi tuombe Toba kwa Mungu maana ni Kama tulifanya uzembe hadi ugonjwa huu ukatufikia.. Mungu alitupa akili na mamlaka tuzitumie..sisi hatukutumia vyema.

Kuhusu kujazana ni swala jingine, Watu wanakusanyika kutokana na sababu mbalimbali,wengi wao Ni ugumu wa maisha kutafuta hela mkono uende kinywani..usilichukue hilo kumdiscredit Mungu tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi naomba unifundishe kuhusu sadaka kwa wahitaji(yatima na watumishi wa Mungu - ingawa hawa wanaoitwa watumishi wa Mungu siwaelewi hawa kabisa maana wengi siku hizi wamekua wababaishaji sana)..

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli wengi Ni wababaishaji
Hata katika maandiko Mungu anasema nasi kuhusu Hawa Watumishi wa uongo..
Anasema kwamba tuangalie Kuna wengi watatokea wakitaja Jina lake wakijivisha ngozi ya kondoo Kumbe ndani Ni mbwa mwitu..

Swali:unawajuaje? Unawajua kwa kuwajaribu,si kila roho inatokana na Mungu.. nyingine zatoka kuzimu

Unawajaribuje? Lazima kwanza uwe na uhusiano mzuri na Mungu
Lazima utengeneze na Yesu.

Lazima Roho mtakatifu akae ndani yako,umpe nafasi,umsikilize na ukubali kutenda anayokuelekeza.

Na ili Roho mtakatifu akae ndani yako ni lazima uwe msafi,usome Neno maana Neno ndiyo taa yako.

Lazima uishi maisha matakatifu.. Roho mtakatifu huwa hakai mahali pachafu.
Lazima ukubali kwamba u dhaifu na unahitaji msaada wake sawa na Rum8:26

Unafanikiwaje: Kuna gharama,lazima ukubali kutoa muda wako kwa ajili ya kujifunza Neno,kusali, kufanya mazoezi ya kumkaribisha na kumsikiliza Roho mtakatifu,utulivu wa ndani na nje. Kuna vitu lazima uviache/vikupite ili ujiimarishe kiroho

Wakristo wengi wanashindwa kutambua Watumishi wa kweli ni wapi na waongo ni wapi kwa sababu hawataki kujitesa kwa kusoma Neno,kuomba, kutengeneza na Mungu.
Watu wanapenda vitu vya mkato matokeo yake wengi wanalizwa hovyo.

Mtumishi anayekwambia umpe pesa kwanza ndipo akuombee Huyo si mtumishi wa Mungu, na Kama Ni Wake basi amekengeuka.

Mungu hugawa karama kwa watu wake kadri apendavyo mwenyewe
Anasema mmepewa bure toeni Bure. Anayeponya Ni Mungu na wala si mtumishi.
Watu wasivyopenda kujitesa kusoma maandiko wanajikuta wanapelekwa kokote.

Hawahangaiki kumtafuta Mungu mwenye nguvu ila wanazitafuta tu Nguvu za Mungu.
Neno linasema mtakeni Bwana na Nguvu zake Mtakeni Bwana kwanza.

Sadaka juu ya wahitaji nitakufundisha kesho Mungu akipenda. Nitaomba unitafute sehemu nzuri.. sidhani Kama hapa panafaa sana kwa Mimi kuweza kukufundisha

Barikiwa Sana na karibu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna atakayekujibj hili. Dini ililetwa na wazungu wakati wa ukoloni leo wameitema sisi tunajifanya tunaijua kuliko wao haha hata wakituona wanatucheka sishangai wakituita nyani kwa ujinga uliowajaa waafrika wengi. Non sense kabisa
 
Maombi yamefanya madaktari toka Cuba waende kusaidia Italy
😂 maombi ya nani? Una uhakika?
Dini ka bangi, tatizo dini inakaa mwilini tu muda mrefu unakua high miaka.Nyie watu hua mnajifanya mna solution ya kila jambo 😂 😂 ovyo kabisa
 
Watanzania wamepewa siku tatu kuomba Mungu alisamehe taifa nakutuponya na gonjwa baya la Covid 19.

Wakati hayo yakiendelea ni dhahiri shahiri katika ofisi ya mkuu wa taifa lenye ukwasi wa mali ktk ardhi yake kuna mtu mmoja tu anaitajika fanya maamuzi magumu kwa Taifa lake. Nimaamuzi yatakayo kwenda gharimu kidogo tulicho nacho na kusababisha mtikisiko katika kila sector.

Hesabu ngumu kuliko zote ni maamuzi hayo yataligharimu taifa kwa muda gani? Hesabu hii inamkosesha mkuu wa taifa letu usingizi. Maana anakumbuka maumivu ya vita Kagera na hawez sahau watu walivyopata shida hata mpaka leo.

Kiukweli viatu vya mkuu ni vizito kama gunia la cement ndio maana wapo viongozi wa mataifa fulani wanapiga gambe kupoteza mawazo.

Hatima yetu ipo mikononi mwa sign ya mkuu wa taifa. Baba tukumbuke. Amen
 
mr mkiki,
Ukitka kupata reasoned jibu kwa swali lako, lazima ujibu kwanza swali hili: Je Mungu yupo? Hii ni kwasababu tunaaminishwa tu bila proof kuwa Mungu yupo. Huwezi ku assign duties kwa kitu ambacho hakipi. Tujiridhishe scientifically kama Mungu yupo.
 
Back
Top Bottom