Wananchi tuna haki kufahamu alipo Makamu wa Rais Philip Mpango

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,755
Tulimpoteza Magufuli kwa sababu kuumwa hadi kuzidiwa kulifanywa National Bigly Secret ambapo wananchi hatukujulishwa iwapo anaumwa ama amezidiwa zaidi ya kustuliwa na taarifa ya kifo chake mnamo 17 March 2021.

Rais ni wa Jamhuri ijulikane kuwa anamilikiwa na wananchi wote bila kujali itikadi, imani wala kabila. Nasema anamilikiwa ni kwa sababu shughuli zake zote zinamhusu kila raia awe mdogo au mkubwa kwa jinsia zote.

Rais anamilikiwa na wananchi ndo maana analindwa na wananchi na kutunzwa na kodi za wananchi. Ingawa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wanadhani wao pekee ndo wenye dhamana ya kumtunza na kumlinda Rais. Wananchi watasali kwa miungu yao, watatambika kwa mahoka wao na kadhalika ilimradi Rais aweze kufikia matarajio na matamanio yao. Wenye Mungu nao watamuombea ili awe salama na aweze kutekeleza majukumu yake vyema.

Inaelekea tukio la marehemu JPM halijatupa funzo lolote. Zimeanza tetesi kupitia wale wale walioeneza uvumi kuhusu hatma ya JPM na sasa wanamtaja Makamu wa Rais. Tetesi hizi zimeendelea kupata mwangwi mkubwa kupitia mitandao ya kijamii kuhusu afya na uhai wa Makamu wa Rais.

Serikali, imeendelea kupuuza uvumi huo kama ilivyopuuza uvumi (uliokuwa siyo uvumi) enzi Mwendazake wakati anapigania uhai wake vyumba vya afya. Tuliona viongozi wakubwa akiwemo Waziri Mkuu wakitoa matamko ya kubeza tetesi hizo kwa kuuaminisha Umma kwamba Rais wao anachapakazi yupo gado kabisa.

Jana, serikali ilisambaza bango mitandaoni kumuonesha Makamu wa Rais atakuwa mgeni rasmi kwenye Mkutano wa TAWIRI unaoanza tarehe 06 Desemba 2023..... sisi tunaochoshwa na tetesi za vifo vya wakubwa tukanyenya mikono juu kumshukuru Mungu kuwa tetesi kuhusu hali ya Mhe. Mpango ni uzushi na upotofu. Lakini aliyefika mkutanoni ni mwakilishi (Mhe. Kairuki) na siyo mgeni mlengwa.

Tumepatwa na msiba wa kitaifa kule Hanang kwa kuondokewa na ndugu zetu kutokana na mafuriko makubwa. Tumeona mfariji wa Taifa ambaye ni Rais ameshajitokeza na kusimama na wananchi wote na hata Waziri Mkuu na viongozi wengine wa Serikali wanafanya kila linalowezekana ili kuwanasua waliokwama chini ya tope zito la mlima Hanang. Lakini hatujamsikia popote Makamu wetu wa Rais akitoa pole kama ilivyo kawaida yake kwa matukio aina hii.

Kwa niaba ya Watanzania, naleta ombi kwa serikali ituondoe kizani kuhusu alipo makamu wa Rais. Hizi tetesi zinazoendelea hazina afya kwa Taifa.

Endapo kweli hatunaye na hatukutangaziwa kuumwa kwake ni wazi hatutazuiwa kuwaza kwamba serikalini kuna hila nyingi dhidi ya viongozi wa Kitaifa na hakika tutaamini kwamba vyombo vyetu vya ulinzi na usalama pamoja na mamlaka zingine zina muunganiko usio na afya kwa Taifa letu.

Naomba tujulishwe

========= UPDATE ==========


Makamu wa Rais Mhr. Dkt. Philip Isdori Mpango hatimaye alijitokeza mbele ya umma siku ya jumapili tarehe 10 Desemba 2023. Alihudhuria ibada ya jumapili na kuzungumza na Taifa akishukuru kwa maombi na kusema alikuwa nje kwa kazi maalum ambayo hakuitaja.


Tumewaza memgi
Tumesema mengi
Tukasikia mengi.


yote ya heri ama shari lengo lilikuwa kufahamu alipo kiongozi wetu namba mbili wa Serikali yetu.

ssuti zetu zimesikika
Sauti zetu zimeleta chachu.


Ahsante jukwaa la JamiiForums
 
Tulimpoteza Magufuli kwa sababu kuumwa hadi kuzidiwa kulifanywa National Bigly Secret ambapo wananchi hatukujulishwa iwapo anaumwa ama amezidiwa zaidi ya kustuliwa na taarifa ya kifo chake mnamo 17 March 2021.
...
Sidhani hata kama wanajali hizi dukuduku za wananchi. Nimesikia habari nzito kuhusu mwamba huyu lakini siwezi kuisema hapa kama ilivyokuwa vigumu kusema ya Magufuli aliyesemekana kufariki lakini serikali ikaja kutoa taarifa baada ya wiki moja hivyo kusogeza mbele tarehe ya kifo chake.

Ngoja pia waendelee kuficha ugonjwa wa Mpango lakini kifo kitawaumbua kama kilipowaumbua kwa Magufuli. Wakati ukuta.
 
Ndugu zangu watanzania tuchangie chama chetu

20231206_144636.jpg
 
Tulimpoteza Magufuli kwa sababu kuumwa hadi kuzidiwa kulifanywa National Bigly Secret ambapo wananchi hatukujulishwa iwapo anaumwa ama amezidiwa zaidi ya kustuliwa na taarifa ya kifo chake mnamo 17 March 2021.
Hata kipindi mkulu anakufa tuliambiwa ni mzima wa afya anawasalimia na kuwasisitiza mchape kazi hivyo hata huyu ni suala la muda tu ukweli utajulikana japo nasikiaga eti lisemwalo lipo acha tuone hii week nayo iishe
 
Na huu ndio ukweli, watu wanamjia juu waziri mkuu utadhani yeye anaongea tuu bila kupewa kauli, ni mara ngapi rais hata awamu zilizopita anamuapisha mtu ambaye sio sahihi, lawama zinaenda kwa rais wakati sio kila mtu anapitishwa na rais
Viongozi wetu wote ikifika ni muda wa kuongea na wananchi lazima waandaliwe maelezo. Hua hawajipangii tuache kumlaumu PM
 
Back
Top Bottom