Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

CORONA:
TUOMBE, TUSIOMBEOMBE
Vita dhidi ya Corona haiepukiki. Napendekeza haya:
1. Mungu haongei nasi kutumia Corona. Tunaalikwa kuongea na Mungu kwa tishio la Corona.

2. Katika vita kuna kujilinda na kushambulia adui. Tumesikia mbinu nyingi za kujilinda na chache za kushambulia Corona. Tuanze kushambulia. Kinachohitajika ni mikakati, vifaa, umoja wa kitaifa na makamanda imara.

3. Tutangaze tunapofunga goli na tunapofungwa. Hofu ya kufungwa inaongeza mbinu za kujilinda. Watu wakiona na kusikia habari za watu wanaowajua, wataelewa kirahisi hatari inayotukabili. TUSIFICHE CHOCHOTE.

4. Tuwalinde wachezaji wetu kwa gharama. Watumishi wa afya nchini kote, wapewe vifaa vya kujilinda na watengewe maeneo ya kukaa. Wasirudi majumbani.
5. Vifaa vipatikane na vijulikane viko wapi. Wenye uwezo wajinunulie na wawanunulie wasio na uwezo.

6. Visivyopatikana nchini viagizwe. Msamaha wa kodi utangazwe na ukiritimba wa kuviingiza uondolewe haraka. Mashirika yahanasishwe kuagiza haraka.

7. Tusitishe vyombo vya usafiri kutoka mkoa kwenda mkoa. Hivi sasa kirusi chaweza kuwa Ubungo asubuhi na jioni kikawa Kahama. Barabara nzuri na Bombadier hazisafirishi bidhaa tu. Hata virusi vinapata lifti.

8. Mashine za kupima virusi zipelekwe kila mkoa. Kupeleka sample DsM ni usumbufu na inaongeza uwezekano wa kuharakisha maambukizi wakati wa kusubiri matokeo. Tumejifunza kwa NIDA na Passport mpya.

9. Elimu isisitizwe kuliko adhabu. Usugu wa adhabu utaongeza kasi ya maambukizi. Polisi wapige virusi, wasipige watu.

10. Tufunge na kuomba lakini tukumbuke CORONA NI TATIZO LA KISAYANSI ZAIDI KULIKO KUWA TATIZO LA KIROHO. Tuombe, tusiombeombe
 
Mimi sio mzuri sana kwenye historia na biblia!!! Ni ugonjwa gani duniani umewahi kuondoshwa kwa maombi?.
.
Nadhani hata ukoma ulipatiwa dawa!!

Maombi isiwe sln coz daily tunaomba b4 corona,now we need things like Stimulus package,Tax reduction,Reduced income tax.

Suspension of all the projects now, Reduced banking rate, Suspension of payment of all loans for at least 3 months.

Umeme na maji viwe bure hata kwa miezi mitatu.

mr mkiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mr mkiki, Kwa hiyo huamini katika maombi?
Magonjwa mengi yanaondoshwa kwa maombi. Kwa sisi tz tungeanza kwanza na Toba maana Ni Kama tulizembea kuchukua tahadhari mapema.

Mungu anaweza jibu moja kwa moja au kwa kupitia kwa wataalam wetu wa afya.
Hayo Mambo unayosema tax reduction si suluhisho la ugonjwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo huamini katika maombi?
Magonjwa mengi yanaondoshwa kwa maombi
Kwa sisi tz tungeanza kwanza na Toba maana Ni Kama tulizembea kuchukua tahadhari mapema
Mungu anaweza jibu moja kwa moja au kwa kupitia kwa wataalam wetu wa afya.
Hayo Mambo unayosema tax reduction si suluhisho la ugonjwa

Sent using Jamii Forums mobile app
We unaamini katika maombi?

Nyie ndio mnaosema tumjengee mchungaji apate sehemu pa kukaa ili atuombee na sisi tujenge

Kwanini mchungaji akipata shida anawaomba nyinyi mumchangie halafu wewe ukipata shida anakuambia funga na kusali mungu atakupa??

Kama makanisa huko italia yamefungwa kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu, nini kinachokufanya uone makanisa na habari za maombi zinamsaada katika kuokoa maisha ya watu???
 
Back
Top Bottom