Napenda sana mambo ya kutengeneza programe na software. Kozi gani nisome na Chuo gani? Niko University (PCM A-level) ila nasomea ishu nyingine tofauti na hiyo.Ningependa kuanzia ngazi ya Diploma au Degree.
Kwa kuwa bado uko A -Level tambua kuwa program na software ni kitu kile kile na ili kutengeneza hii kitu itakubidi ufanye kazi kubwa katika masomo yako,ngazi ya diploma sidhani kama unaweza.
Hii kazi ni ngumu sana lakini inayolipa kwa kiwango cha kutisha.Hapa bongo unaweza husipate waliowahi kufanya hii kitu.
kule South Africa wameweza kutengeneza Opetating software ya Ubuntu .wengine mikwara tu.
Napenda kuwaasa jamaa zangu wanaopenda kuwakatisha wengine tamaa. Ndugu zangu,mimi naamini hakuna somo gumu, ila determination ya anayesoma. Tuondokane na tabia hii.
Ushauri ambao ni + ni huo wa kujiendeleza. Mimi nilisoma arts ila napenda computers, rafiki zangu wananisaidia, nimefika mbali.
No No.Haya mambo ya kutokupenda kuelezwa ukweli ndiyo yanayotuharibu wabongo,mnapenda maelezo matamu matamu ya kutia moyo wakati hali iko tofauti.
ninaposema kuwa kutengeneza software ni kazi NGUMUUUUUU sana na inabidi uwe mzuri sana katika lugha za computer.
Kama unabisha nitajie software 5 tu zilizotengenezwa na wabongo tangu kuumbwa kwa hii dunia na zinatum,iwa na nani.Je si kwamba wataalam wa ICT wanasoma kila kukicha? huo ndiyo ukweli hata kama unaumwa.
unaowaona humu na mikwara yao yoooooote,waambie kuhusu kutengeneza software watatoa maelezo mpaska mwakani.
Mkuu labda tuelimishane kidogo kuhusu Software.
Software kwa lugha rahisi ni mfumo wa kompyuta ambao umeandikwa kwa lugha ambayo inaeleweka kwa kompyuta kwa ajili ya kuiambia kompyuta nini cha kufanya na kifanyike wakati gani.(kwa maneno yangu)
Kuna aina mbalimbali za software kutokana na vigezo vitakavyo tumika kuzigawa lakini aina mbili ndio zinazofahamika na kutumika zaidi nazo ni System Software na Application Software.
Kwa maelezo yako hapo juu unaongelea aina ya kwanza yani System Software ambazo zinajumuisha operating Systems kama Windows na Ubuntu.
Tukija aina ya pili, Application Software hizi zinatengenezwa kukidhi mahitaji ya sehemu husika kwa mfano hospitali wanaweza kuwa na Hospital Management System, Supermarket zinapatikana na katika ofisi mbali mbali. Aina hii ya Software tuna vijana wetu wa kitanzania wanatengeneza na mfano wa kampuni ni data vision, cats, dflex na nyinginezo kwa kiasi flani wahindi ndio walifungua milango katika kutengeneza hizi software.
Kwa maelezo hayo kwa kifupi nataka kumshauri mtoa mada kwamba 'impossible is nothing', watu wanafanya haya mambo naamini na wewe utaweza ukiamua.
coming soon!Uko sawa kwa asilimia 100 unachosema.
Lakini mkuu kumbuka kuwa hapa bongo wanachofanya ni Development tu siyo Creation ya software...hivyo kwa ufupi hakuna application software unayoweza kunieleza kuwa imekuwa created na wabongo labda kufanya developments.
labda nipatie elimu kwa kunitajia hiyo software.
Uko sawa kwa asilimia 100 unachosema.
Lakini mkuu kumbuka kuwa hapa bongo wanachofanya ni Development tu siyo Creation ya software mfano hizo dflex ,data visio ni development tu !
Ebu tazama
1: Unasema datavision soma hapa
2:Unasema dflexsoma hapa
3:Unasema cats somahapa
hivyo kwa ufupi hakuna application software unayoweza kunieleza kuwa imekuwa created na wabongo labda kufanya developments.
labda nipatie elimu kwa kunitajia hiyo software.
Umenichanganya kidogo.
unamaanisha development inayofanyika ni re-engineering tu na hamna new product au?
1. www.datavision.co.tz
2. www.dflex.co.tz
3. www.cats-net.com
coming soon!
No No.Haya mambo ya kutokupenda kuelezwa ukweli ndiyo yanayotuharibu wabongo,mnapenda maelezo matamu matamu ya kutia moyo wakati hali iko tofauti.
ninaposema kuwa kutengeneza software ni kazi NGUMUUUUUU sana na inabidi uwe mzuri sana katika lugha za computer.
Kama unabisha nitajie software 5 tu zilizotengenezwa na wabongo tangu kuumbwa kwa hii dunia na zinatum,iwa na nani.Je si kwamba wataalam wa ICT wanasoma kila kukicha? huo ndiyo ukweli hata kama unaumwa.
unaowaona humu na mikwara yao yoooooote,waambie kuhusu kutengeneza software watatoa maelezo mpaska mwakani.
Eagery waiting for HT software solutions.
Rutunga M. Mpe ndugu yako moyo kujua wapia aanze, mwenyewe atajipima kama kweli dream yake ya kuwa software developer inawezekana.
Pia sioni ajabu ya software kuwa configurable, kwani kuna njia nyingi tu za kudevelop software, a closed software au open software...
Kama mteja anahitaji kudevelop a given solution, developers wake wataangalia development environments ambazo zipo sokoni na kujua ni ipi/zipi zitaweza kutumika for the solution, hapo basi, huyu developer sio lazima aanze ukurasa wa kwanza kutengeneza the environment, na baadae ndio atengeneze software. Kutokuwepo na the "environment" as a solution iliyotengenezwa Tanzania sio hoja, kwani ki'biashara, haitii akili kuanza square one, katika hili. kutumia development framework/solution mbona is order of the day?!
Kweli Linux imetengenezwa South Africa, au na wenyewe wame-configure a linux variant into Ubuntu...?