Computer programing na ma-software jamani!

Wakuu naomba na mimi nafasi japo nipate kuchangia kidogo, Programming kwa hapa kwet Tanzania ni Janga la kitaifa kama ilivyo kwa masoma ya Hisabati.Kwani kiukweli hakuna chuo cha serikali labda kama vipo vya binafsi vyenye waalimu ambao ni competent kwenye maeneo hayo.Si hivyo tu bali bado syllubus za vyuo vyetu havimuandai mwanafunzi kua programmer zaidi ya kufundishwa Introduction ya programming languages kama C++,Pascal,Visual Basic, etc, na jinsi ya kutengeneza very miner programas kam kujumlisha moja na mbili, with alote of blah blah katika masuala ya msingi kama arrays, linkers etc, Mitaala ya vyuo vyetu hakuna inaposisitiza katika masuala haya na wala serikali zetu na mashirika yetu ya binafsi ama hata costech wamekua hawaweki msisitizo wowote wa kuwafanya vijana wetu waconsentrate katika fani hiyo. Kwani katika kila mradi tumekua tukitafuta consultants kutoka nchi za nje,tukinunu software kutoka nje kwa kisingizia kuwa proffessionals katika eneo hilo hakuna wakati tunaruhusu certifications kam OCA,MCSTP etc, na kuwaita watu wenye vyeti hivyo kuwa eti ndo MaICT gurus.

Sijui tutafika wapi na changamoto mpya ya CLOUD computing ambapo watu wote waliosoma IT watakua ni watazamaji kwa sababu maanalist na maprogrammer wa MArekani, India, Uingereza na kwingineko wataweza kutoa support hukohuko walipo kwa kutumia clremote login.
 
  • Thanks
Reactions: KXY
Kutengeneza software sio kazi ngumu kabisa, ukitaka kujifunza kutengeneza software mwenyewe unaweza kama uko tayari kuweka muda kidogo kwa ajili ya kujifunza huko, personally ninekushauri kununua kitabu nenda maduka ya bongo angalia wana vitabu gani vya beginners kisha nenda Amazon.com checki review zake nunua kizuri, ningekushauri kuanza na kati ya Java/C#/Python kama lugha ya kwanza. Kama hauwezi kununua kitabu kuna vitabu vya bure kibao mfano C Sharp Programming Course kuna list ya vitabu vya bure hapa free - List of freely available programming books - Stack Overflow.

Pia siku hizi kuna video course kibao za bure unaweza kufanya tena kutoka university bora duniani Stanford/MIT/IIT etc.

Introduction to Computer Science I | Harvard Video Course

Computer Science I: Programming Methodology | Stanford Video Course

Introduction to Computer Science and Programming | MIT Video Course

NPTEL PHASE 2 - Courses

Zaidi ya hapo search YouTube au Google tutorial za programming yoyote utapata.
 
Kwani katika kila mradi tumekua tukitafuta consultants kutoka nchi za nje,tukinunu software kutoka nje kwa kisingizia kuwa proffessionals katika eneo hilo hakuna wakati tunaruhusu certifications kam OCA,MCSTP etc, na kuwaita watu wenye vyeti hivyo kuwa eti ndo MaICT gurus. Sijui tutafika wapi na changamoto mpya ya CLOUD computing ambapo watu wote waliosoma IT watakua ni watazamaji kwa sababu maanalist na maprogrammer wa MArekani, India, Uingereza na kwingineko wataweza kutoa support hukohuko walipo kwa kutumia clremote login.
Umeongea kitu cha maana sana kuhusu Cloud Computing mkuu. Wasiwasi wangu ni kwamba taasisi zinazoendeshwa kifisadi hazitakuwa tayari kuhamia huko maana watu wateweza hack nyaraka nyeti. lakini 10 to 15yrs to come nafikiri itakuwa hakuna jinsi lazima tuelekee huko
 
Ahsante bro! Katika course ninazosoma Mathematics imo, katika kozi za Math tumesoma introduction za kozi kama (C++ na Numerical Analysis)! Nahisi nitafikia malengo yangu...........!
 
  • Thanks
Reactions: KXY
Ukweli ni kwamba kutengeneza commercial software kwa viwango vinavyokubalika kimataifa ni jambo gumu. unaweza tengeneza software inayofanya a b c kwa kampuni au taasis A. its ok, kwa sababu its unlikely kwamba itaonwa na kutumiwa nje ya hiyo taasisi A. lakini kutengeneza ambayo inauzwa kibiashara its not a joke my friend. There are a lot of things that need to be considered and handled accordingly eg multi user support, session handling, security, easy of use, modularization etc. Haya mambo yote hatafundishwa universities za Tz. Kimsingi mwanafunzi anayemaliza chuo computer science au IT or Whats ever they call it, anakua amejifunza introduction tu kumuwezesha kusomea kazi. Bahati mbaya hapa kwetu wakipata hicho ki degree ndo wanajiona wamefika. Software industry hapa bongo bado sana. We need to do something.
 
kwa ushauri wangu unaweza soma software engineering hapo utajifunza language mbalimbali za kompyuta na utakuwa jirani sana na mambo ya software japo utengenezaji wa software ni jambo gumu lakini ukiwa na bidii utafanikiwa, zaidi ya hapo mimi mwenyewe nasoma S.E ni mahali sahihi kwa mahitaji yako. lakini uctegemee wepesi hata kidgo.
 
Ukweli ni kwamba kutengeneza commercial software kwa viwango vinavyokubalika kimataifa ni jambo gumu. unaweza tengeneza software inayofanya a b c kwa kampuni au taasis A. its ok, kwa sababu its unlikely kwamba itaonwa na kutumiwa nje ya hiyo taasisi A. lakini kutengeneza ambayo inauzwa kibiashara its not a joke my friend. There are a lot of things that need to be considered and handled accordingly eg multi user support, session handling, security, easy of use, modularization etc. Haya mambo yote hatafundishwa universities za Tz. Kimsingi mwanafunzi anayemaliza chuo computer science au IT or Whats ever they call it, anakua amejifunza introduction tu kumuwezesha kusomea kazi. Bahati mbaya hapa kwetu wakipata hicho ki degree ndo wanajiona wamefika. Software industry hapa bongo bado sana. We need to do something.

Ni kweli aisee.
 
Nimeona watu wanataja hesabu. Je ni hesabu gani hizo unazohitaji kujua kuwa programmer mzuri. Is it Logic mathematics au trigonometry ?

Binasfi nilipass tu programming. NIna theoretical knowledge ya programming nzuri tu lakini practical applicatin na experince mhhhh. Na hili nadhni ndio tatizoletu wengi.

Kingine nilikuja kugundua material nzuri za programming online baada ya kumaliza kanmumbas college na kuichukia programming.

Nadhani kama una nia ,muda , internet na muongozo( mwalimu vitabu video). Cha mwisho baada ya hayo yote ni kujaribu na kufanya coding kwa language yeyote.
 
Naunga mkono hoja lakini kwa maoni yangu graduate wa CS ana basics nzuri sana za software development, tatizo mi naliona linahusu industry nzima sio tu hao wanafunzi.

Kwenye Software development life cycle (SDLC) kuna mambo huwa hatutilii maanani aidha kwa kuepuka gharama ama kukosa wataalamu au vyote, watu wengi wanakazania hatua ya implementation na maintenance ndio maana tunashindwa kutengeneza commercial Software. Kila hatua katika SDLC inahitaji timu ya kufanikisha majukumu ya hiyo hatua, hapa ndio unakutana na tatizo maana kama requirements analysis haijafanyika kwa kina kazi zinazofuata zote hazitaenda sawa sababu plan yenyewe haiko sawa.

Udhaifu mwingine ni documentation, bila hili inakuwa vigumu sana ku enhance product yako maana huwezi kumbuka kila ulichokifanya kama hakijaandikwa na inakuwa vigumu kazi hiyo kuendelezwa na mtu mwingine kama wahusika wa mwanzo hawapo. Software hata iwe nzuri kiasi gani yenye ufanisi wa hali ya juu kwa mtumiaji kama haiko well documented haitakubalika kuwa kwenye kiwango cha kimataifa.

Mi naona kufanikisha vitu kama hivi inahitaji investment kubwa kwenye suala la kuwa na wataalamu wa kutosha na uwezo wa kuwahudumia mda wote ambao wanakuwa jikoni kutengeneza System. Ukifuata hatua zote na kufanya kazi iliyo kwenye standard ya kimataifa inatumia mda mrefu sana na hapa ndio napoona watu wanakimbia gharama.

Pia kwa upande wa programmers wetu inabidi kujizoesha kufuata utaratibu rasmi maana hata mini-projects ndogo tu watu wanalipua, ni mara chache sana utakuta kwenye project za wanafunzi wanaweka comments kwenye codes.

Tubadilike haya mambo yanawezekana jamani.
 
Ukitaka kuwa programmer mzuri inabidi uwe unaandika codes kila siku kwa muda wa miaka 10. Au ujifunze algorithims na uwe unacode kila siku for 2years!
 
Nimeona watu wanataja hesabu. Je ni hesabu gani hizo unazohitaji kujua kuwa programmer mzuri. Is it Logic mathematics au trigonometry ?

Binasfi nilipass tu programming. NIna theoretical knowledge ya programming nzuri tu lakini practical applicatin na experince mhhhh. Na hili nadhni ndio tatizoletu wengi.

Kingine nilikuja kugundua material nzuri za programming online baada ya kumaliza kanmumbas college na kuichukia programming.

Nadhani kama una nia ,muda , internet na muongozo( mwalimu vitabu video). Cha mwisho baada ya hayo yote ni kujaribu na kufanya coding kwa language yeyote.

Hii ni myth kwenye programming, kuwa unatakiwa kujua hesabu kuweza kuprogram. Of corse kuna sector za programming utahitaji hesabu lakini ni minority na hesabu hizo ni very specific ambazo mara nyingi unaweza kujifunza kama utazihitaji, vectors kwenye 3D kwa mfano.

Kwa kifupi 99% ya programming usiwe na wasiwasi kabisa kuhusu hesabu.
 
Ukweli ni kwamba kutengeneza commercial software kwa viwango vinavyokubalika kimataifa ni jambo gumu. unaweza tengeneza software inayofanya a b c kwa kampuni au taasis A. its ok, kwa sababu its unlikely kwamba itaonwa na kutumiwa nje ya hiyo taasisi A. lakini kutengeneza ambayo inauzwa kibiashara its not a joke my friend. There are a lot of things that need to be considered and handled accordingly eg multi user support, session handling, security, easy of use, modularization etc. Haya mambo yote hatafundishwa universities za Tz. Kimsingi mwanafunzi anayemaliza chuo computer science au IT or Whats ever they call it, anakua amejifunza introduction tu kumuwezesha kusomea kazi. Bahati mbaya hapa kwetu wakipata hicho ki degree ndo wanajiona wamefika. Software industry hapa bongo bado sana. We need to do something.

Umeongea point nzuri sana
kila sku naongelea hii kitu,Masharobaro wananiponda tu.ICT kwa bongo ni kwa ajili ya kutafutia kazi tu.hakuna jipya
 
Heshima yako ndugu Rutunga M,
Hakuna kinachoshindikana, tatizo ni watu wenye mawazo kama yako.. Kama havijawahi fanyika, haimaanishi havitafanyika.. Ingependeza kumshauri hatua anazotakiwa chukua..

Binafsi ni Programmer though bado ni medium programmer.. Wakati naanza kusoma Computer science, nilipata changamoto kadhaa, baada ya watu kunishauri kuwa Programming ni ngumu.. Kutokana na Syllabus ya chuo changu, kulikua na mambo ya Programming kibao.. Automatically nimejikuta nimeipenda Programming sana tena sana, kutokana na the way walimu wangu walivonifundisha, na interest niliyo nayo katika Programming.. Sio maeneo hayo tu, hata katika maeneo mengine ya System Analysis, System & Database design and Implementation..

Kuwa Best Programmer sio lazima uweze kutengeneza System softwares kama OS nk. Kuna mambo mengi yanaweza fanyika katika Programming..

Nilichokuja kukigundua katika Programming ni kwamba, inategemea na eneo husika la Programming.. Ila kitu cha msingi sana katika programming ni analytical,creative,Mathematics skills na Logic.. Especially kwenye designing and implementation of a system..

Pia tutambue kuwa, Programming zote zinahusiana.. Mfano ukiangalia Hardware Programming (Programming of Micro Processors), Games Programmings (C/C++ graphics), Robotics, Web Programming, Desktop apps Programming kuna vitu vinavyo bind hizi lugha pamoja... Logic za maeneo haya zinahusiana sana, cha msingi ni basic knowledge..

Dunia ya IT ya sasa, inajitahidi ku implement IDE's ili kuweza kuokoa muda wa ku code Programs (Component Technology, Pattern Technology) na pia sasa tuna-shift kwenda kwenye Distributed Network Objects (eg.. CORBA, etc).. Kwa hiyo ukiwa kwenye realtime, sio lazima uanze coding from the scratch.. IDE's zimetengenezwa, kwa ajili ya ku-implement kutengeneza softwares..

Programming is all about logic.. First, Believe kwambba Program flani inawezekana kutengenezwa... Kitachofata ni namna ya kufanya hicho kitu..

Kwa mtazamo wangu, Programmer wengi wa kibongo sio kwamba hawawezi kufanya mambo makubwa HAPANA, nasema HAPANA.. Shida yetu kubwa wengi tunasoma huku tukifikiria swala la ajira.. Unakuta mtu, anasoma huku akifikilia, je akimaliza shule yake ataweza kuwa placed katika kampuni itakayomlipa??

Kuna hizi wanazoziita Certifications kama (OCA,OCP,CCNA,CCNP) na nyingine kibao.. Kwa mtazamo wangu, zinachangia kwa namna moja nyingine kuua morali ya vijana katika maeneo kama haya ya Programming.. Kwa nini nasema hivi? Kampuni kama CISCO kwa sasa, wanaingiza pesa sana katika mitihani kama hiyo.. Ofcoz, kwa upande mwingine, hizi Certifications ni mhimu kwa sababu zinatumika kama Proof, ila kwa upande mwingine vijana wengine hawa concentrate kufanya vizuri katika maeneo yao kwa sababu wanawaza kufanya tu mitihani hii ili waweze pata kazi nzuri. Maana Kampuni nyingi zina imani kuwa mtu akiwa na certifications, ndio anafaa.. Binafsi sipingi Certifications, ila certification bila Ujuzi ni useless..

Wabongo wengi tunapenda maisha ya mkato katika mafanikio, so hatutaki kutumia skills zetu kufanya innovative activities, kwa sababu tunaona ni wastage of time.. Na hii ni kama nilivosema awali, wengi wanasoma ili wapate kazi, na si kusoma ili Ujue vitu.. But hakuna kinachoshindikana..

Kwa hiyo ndugu mwanzisha thread, kama u really like Programming, ni wewe tu.. Cha msingi jipime kwanza..

Jiulize maswali yafuatayo:

1. Do you have Analytical skills? au je waweza fundishika Analytical skills?
2. Do you have Creative skills? au je waweza fundishika Creative l skills?
3. Do you know Mathematics and Logics??
4. Je, unataka kusoma ili upate kazi(Kwa ajili ya kipato) au unasoma Ujue vitu??
Hoja hujibiwa kwa hoja. Nimeupenda uchambuzi wako.
 
Chamalama umefikia wapi ktk ndoto yako? Je umeisha master basics zote au bado unajifikiria? Weka mrejesho huu mwaka wa saba sasa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom