Clouds FM na unazi wao kwa CCM

kibonde alipewaga kasuti na jk nayeye akawa magamba hakuwaga hivyo pomba ni hando na pj tuu.wengine wote magambaziii!!!

mkuu wote ni magamba kwa lazima. Hando huwa anajaribu kujitutumua lakini anashindwa maana anaogpa kupotea kitumbua chake . PJ yeye alishakubaliana na amri na kutii, yeye ndo huwa hata anamzuia hando akitaka kufatilia habari za kuiponda ccm. Wamewekewa tonge mdomoni wakita kusema kitu juu ya gamba wanaambiwa mng'unyeni hilo tonge na wanashindwa kuongea.
Mimi naamini hawa jamaa ni njaa tu ila wote ni full charge chadema!
 
Clouds itakuwa inafanya makosa makuwa sana kuonesha inakuwa affiliated na political party fulani. Maana yake ni kwamba una eliminate segment fulani ya wasikilizaji. Mimi huwa ninamuheshimu sana mwanamuziki JD, huyu dada aliisha liona hilo na hata akialikwa kwenye kutumbuiza kwenye vyama huwa anajiweka neutral sana na kwamba yupo pale kikazi zaidi ya kisiasa.

Wanasiasa ni kama kupe, huwa wanapenda kuji-attach pale ambapo wanaona kuwa ustawi wao ni mkubwa pindi wakiisha kuona hauna la maana wanakuacha na kukusahau na hili ninawaonya si tu wasanii wa Tanzania bali pia hata vyombo binafsi vya habari. Unless umehakikishiwa subsides na serikali kuwa watakufidia kwenye lost revenues usikubali ku-contaminate your goodwill and reputation uliyoijenga kwa muda mrefu bila usaidizi wa serikali. Ukiwa juu ya mawe nobody will think about you again. Wamiliki wasikubali watendaji kufanya vyombo vyao kama ngazi za kupandia katika siasa.
 
Lakini mbona wametoa mchango mkubwa sana katika kuhamasisha uchangiaji wa CHADEMA kule ausha katika tangazo lao?
Sio tangazo lao, lile ni tangazo la CDM. Ile ni biashara, unapeleka tangazo lako unalipia linatangazwa kama lilivyo.
 
Hawa wanajulikana wazi wanavyojikomba kwa magamba, hata Nape alishawaambia anawashukuru sana kwa mapenzi waliyonayo kwa ccm wakati wa kipindi cha jahazi mwezi wa Januari.
Si mnakumbuka mwaka jana ndio waliomwandalia jk bonge ya pati ya birth day yake?
 
Jaribuni kumsikiliza Masoud Kipanya na timu yake times fm kwenye sunrise ni mbadala pb!
 
Vipi Cloud ingetoa hotuba ya Vincent Nyerere na Mgombea Nasari kisha ikasema gazeti lililopatikana ni Tanzania Daima pekee. Ungekuja kulaumu kwa kuipendelea CDM? bila shaka sivyo ndivyo.

Mimi ningekuwa wa kwanza. Chombo cha Habari kinachovutia upande mmoja kinapoteza mvuto haraka kuliko unavyotegemea. Kusikia propaganda za chama kimoja kwenye redio ambayo ulitegemea kusikia pande zote inakera!!!! Kama nikitaka kujua ya Ngoswe nitamfwata Ngoswe atanipa habari zake siku nzima. Kwa hili la clouds FM a.k.a peoples Stations LINABOA (EMBARRASSING)
 
Nilikuwa busy usiku kucha. nikalala saa kumi na nusu alfajiri kushtuka nikakuta PB on saturday ambayo wanapitia mambo yote muhimu ya wiki.Nilipoamka ili kusikiliza & nikakuta wameipa coverage hotuba ya merry Nagu kwenye kampeni za arumeru mashariki. Merry anavyojinadi kwa mambo aliyoyawezesha wakati akiwa waziri wa viwanda na biashara.

Baadae wakampa coverage Sioyi Sumari akajinadi nikategemea kumsikia Nasari na Vicent wapewe nao ola. Labda kama walianza nao ndipo nitawaelewa! Sasa nilipojua kwamba sio bahati mbaya kwenye mapitio ya magazeti wakadai wamepata matatu tu! JAMBO LEO, MAJIRA na MTANZANIA! sasa Jambo leo si ni la magamba! habari iliyosomwa kwa kirefu ni propaganda za jambo leo!Kwamba CCM wameshamaliza kazi!

My take:
Kwanini tunailalamikia clouds? kwa miaka mingi tumekuwa tunaiheshimu kwa uwezo wao wa kutoa burudani na ubunifu. Leo Peoples station mtakubalije kuwa CCM Station? Hivi kweli SUPER BRAND mnaweza kuamua kutuvunja moyo vijana kiasi hiki? Tunajua magamba wanaweza kuwavamia kwa kuwa wanajua mnainfluence ya vijana lakini kwani si wote tunajua vijana wa sasa hawataki kufanywa wajinga?

AU MMEJISAHAU?

Badala ya CLOUDS FM waitwe CLOUDS CCM.
 
Back
Top Bottom