Chuo Kikuu Muhimbili chasitisha masomo kwa kukosa chakula

drgeorge

Member
Jun 22, 2009
99
23
Leo ni siku ya pili wanafunzi wa chuo kikuu cha Muhimbili (IHAS) hawajaingia madarasani au wodini kufundishwa kwa kile kinachodaiwa kuwa chuo hakina chakula kwa ajili ya wanafunzi. Chuo kilifunguliwa jana Jumatatu lakini hakuna kusoma kwa wasababu hakuna chakula.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ndiyo yenye wajibu wa kutoa fedha kwa ajili ya chakula. Mkurugenzi wa IHAS alifika Wizarani (MoHSW) jana na haijafahamika mara moja aliambiwa nini ila hakuna matumaini kwa sasa, Wizara haina fedha.

Uongozi wa chuo unakwepa hata kukutana na wanafunzi na hakuna kinachoelezwa. Wanafunzi hao wanaosoma kozi mbalimbali za afya, kama uuguzi, ufamasia, elimu ya mionzi, sayansi ya baabara n.k hawajui nini cha kufanya huku wanaoishi jijini Dar wakirudi majumbani.

Hali si shwari kwa baadhi yao hasa wanaotoka nje ya Dar kwani wanaishi kwa kuwaomba wenzao wanaishi jijini au angalau wenye vijipesa kuwasaidia kupata chakula.

Waziri na Naibu Waziri wake, sijui wanalipi la kutueleza kwa sasa.

Taarifa hizi zinatoka ndani ya chuo hicho kwa wanafunzi wenyewe na baadhi ya viongozi wa chuo kwa sharti lakutotajwa majina au nyadhifa zao wenye uchungu na mateso wanayopata wanafunzi pamoja na kuzorotehwa kwa elimu nchini.

Binafsi niombe muhimili wa nne wa Taifa yaani Waandishi wa habari kufika chuoni hapo Muhimbi Institute ya Allied Sciences (IHAS) kudodosa na kuwapatia watanzania habari hizi.

Inaniuma sana...
 
Guess ni MTC,POLENI serikali imefilisika sijui kodi inaenda wapi,postgraduate MUHAS imeahidi nkutotoa results za Univery examination hadi school fees zilipwe,mgomo kesho ndo maisha sijui yanaelekea wapi,Gadaffi alionewa sana.
 
Haiwezekani kupoteza mawaziri wawili kwa sababu ya maumivu ya mamilioni ya watanzania. (mtazamo wa viongozi wetu)
 
Muhimbili Technical College (MTC) ndio walio katika athari ya moja kwa moja ya ukata huu, sababu wao hupikiwa chakula moja kwa moja kutoka kantini za college na hukatwa kwenye ada zao. Wanafunzi wetu wa Muhimbili University wao wanaendelea na mafunzo kama kawaida, na hujilipia chakula wenyewe kantini. Ila ukata huu ukiendelea naamini nao wataathirika, maana wanategemea boom ambalo halijaingia mpaka sasa na bodi haijatoa taarifa zozote na wala haijibu tukijaribu kuwasiliana nao.
 
Hivi MUHAS chakula wanapewa kawa shule za bweni au wananunua wenyewe kama vyuo vingine? Au ndio tuseme HESLB wamekuwa Wizara ya Afya?
 
badala ya madaktari kugoma wangeona na wengine wanahitaji kusikilizwa kama hawa wanafunzi
 
Muhimbili Technical College (MTC) ndio walio katika athari ya moja kwa moja ya ukata huu, sababu wao hupikiwa chakula moja kwa moja kutoka kantini za college na hukatwa kwenye ada zao. Wanafunzi wetu wa Muhimbili University wao wanaendelea na mafunzo kama kawaida, na hujilipia chakula wenyewe kantini. Ila ukata huu ukiendelea naamini nao wataathirika, maana wanategemea boom ambalo halijaingia mpaka sasa na bodi haijatoa taarifa zozote na wala haijibu tukijaribu kuwasiliana nao.

Wewe yaonyesha ni mwanajamii wa MUHAS lakini tatizo lako hujui mazingira wala taasisi zilizopo hapo kwenu. Je! Umetoka shule za kata?

Mwenzako hapo juv kafafanua vizuri tu.

Si kweli MTC ni Muhimbili Technical College (ulikuwa mvivu kufikiri hata kwenye kuangalia ulinganifu wa kimaana)

MTC ni Muhimbili Training Centre.
 
mhh kaz kwelikwel wizara haina pesa au? Maana sasa hv hata mfumo wa maombi ya kujiunga na koz mbal mbal za afya umebadilika kabisa bila ya kulipia 4m ya maombi kias cha sh. 15,000 ndo maomb yako yafike sehemu husika.
Kwa hal hii 2tafika ss wa2 wa vijijin kwel?
 
Kuna watu ni Freemasons. Hawachukui hatua, na wenzao wakichukua hatua nzuri za kuokoa jahazi wao wanazuia............... nina hasira hivyo siongei sana
 
Back
Top Bottom