Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE) kuingia mkataba na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Kufundisha wanafunzi

Zulu Man Tz

Member
Sep 23, 2020
73
99
Utangulizi
Chuo Cha Elimu Ya Biashara (CBE) kila baada ya miaka 5 inafanya Utafiti wa soko la Ajira ili kuboresha mitaala yake. Mwaka jana Mwezi March, 2022 CBE kilifanya Utafiti kwa Wahitimu waliomaliza chuoni apo.

Matokeo ya Utafiti
59.5% ya Wahitimu wameajiriwa katika Taasisi za Umma na Taasisi Binafsi.
20% ya Wahitimu pia wamejiajiri Kutokana na ujuzi na weledi walioupata kwenye safari yao ya kielimu chuoni hapo. Na 20.5% ya Wahitimu waliobakia bado wanatafuta ajira na hawajaweza kujiajiri.

Uboreshwaji Wa Mitaala Baada Ya Utafiti
Baada ya Utafiti huo chuo kimeanza mkakati wa kubadili mitaala kwa kuanzia na sehemu hizi kuu tatu nazo ni Technology and Digital solution, Metrology and Standardization (Wakala wa Viwango na Mizani) na tatu ni Banking and Finance.
Ifikapo Mwezi October,2023 CBE itaanzisha mtaala mpya wa Digital and Technology Solution kuanzia ngazi ya certificate, diploma, bachelor mpaka masters degree.

Program ya Uanagenzi
program hii wezeshi itatumika kwa wanafunzi wa bachelor degree watakaochukua shahada ya Digital and Technology Solution. Program hii ni ya miaka 3 ambayo mwanafunzi kila Mwaka wa masomo, semister moja atasoma CBE na nyingne atajifunza kwa Mwajiri kwa vitendo ambaye ni e-GA.

Chuo Cha Elimu Ya Biashara (CBE) kimeshasaini MOU na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) ili kusaidia mafunzo kwa vitendo zaidi kwa wanafunzi hao. Hali hii naona itachagiza kuongezeka kwa ujuzi na uzoefu kwa wanafunzi ili waweze kukabiliana na ukosefu wa Ajira, Ni maoni yangu.

NB; kwenye hizo picha hapo chini, mama aliyekaa peke yake ndiye Kaimu Mkuu Wa Chuo Cha Elimu Ya Biashara (CBE) Prof. Edda Tandi Lwoga.

DSC_0334-copy-950x634.jpg
rector.png

20230321_235647.jpg
 
Back
Top Bottom